SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Katika tathmini yangu ya Habib Kyombo, namuona ni mchezaji mzuri sana anayestahili kupewa nafasi zaidi.
Sitaongelea mikimbio yake wala mbwembwe zingine, ni mchezaji anayeonekana ana IQ nzuri ya soka halafu ni mpambanaji.
Changamoto kubwa ya Simba pale mbele ni kasi ndogo, Okrah akitaka kuwakimbiza, akigawa mpira tu wenzake wanapunguza kasi na kurudisha mipira nyuma. Kyombo anaweza kwenda na kasi hiyo pale mbele.
Pia ufupi wa safu ya mbele nalo ni tatizo. Mipira mingi ya juu, asilimia kubwa Simba wanapoteza. Kyombo pekee pale mbele anaweza kupambania hii mipira.