Kwanza niwe muwaza kabisa kuwa sihafurahishwa na haya matokeo, tumecheza vizuri ila siwezi kujivunia sare mbele ya team isiyokuwa na malengo.
Israh Mwenda ameonyesha kukua kimpira na kama atalata muda wa kucheza zaidi, basi hatukuwa na wasiwasi juu ya mbadala wa Kapombe tena. Uongozi utafute mzawa wa kumsaidia Zimbwe pia.
Kyombo akipewa muda atakuja kuwa hatari sana, ni swala la kupewa muda tu kama jinsi ambavyo Israh kapewa, yani badala ya kuanza na Sakho ni bora tuwe tunaanza na Kyombo ili Sakho asugue benchi mpaka pale atakapojua kuwa yeye si mkubwa kama anavyodhani.
Tutafute mshambuliaji mwingine wa maana pale mbele atakaesaidiana na Phiri ili tuzitumie vizuri nafasi ambazo tumekuwa tukizitengeneza.
Hii mentality ya uchoyo inataka kukomaa sana na hili lipo sawa kwa Sakho, Banda na Okhra, itafutwe namna sahihi ya kuwashauri hawa jamaa, ni wachezaji wazuri ila wamejaa ubinafsi sana.
Vinginevyo team imekuwa vizuri sana kwa maoni yangu, na nampongeza sana Mgunda.
Sent using Jamii Forums mobile app