Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Kama Dkt. Slaa amevuliwa hadhi ya ubalozi kwa kupigania rasilimali naamini yupo kwenye mwisho mwema wa maisha yake hapa Duniani. Kwamba ameanza kwa kupigania haki na amezeeka akiwa mtetezi wa haki; alianza kwa kuhubiri uzalendo na amezeeka akipigania haki.
Waliomvua Ubalozi ipo siku watasimama nakuhojiwa na watamtaja kwa wema na siyo ubaya kwa sababu naamini wanajua wazi kwamba kilichomvua ubalozi siyo kashfa ya ufisadi bali ni nguvu kubwa aliyonayo yakumtukuza Mwenyenzi kutumia ukweli na kuwa wazi pale ambapo anaona na kwa maarifa aliyopewa na Mwenyenzi Mungu kwamba hiki siyo sawa.
Hakuna balozi nchi hii ambaye amewahi kusimama kutetea haki; wote wapo kimya. Maana yake Dr. Slaa kuondolewa hadhi ya ubalozi ni kumwondoa kwa wasiotetea nchi na kumrejesha kwa watetezi wa nchi.
Kwa wapenda haki wanapaswa kushangilia kwamba Dkt. Slaa amekabidhi cheo alichopewa kwa kurubuniwa na ambacho hakupewa kwa sababu Mungu amepanga bali alipewa na wanadamu. Cheo kile kilikuwa ni mzigo kwake, sasa rasmi amekitua na yupo tayari kuzeeka akiwa hana madaraka yenye doa.