Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,187
- Thread starter
- #61
No, genetic origins haiangalii mtu mmoja ama familia pekee, inaweza ikachukua hadi ukoo ama kabila. Unaweza kukuta wazazi wako hawakuwa na akili but ukawa na akili kwa sababu utakuwa umechukua aidha kwa wajomba ama shangazi.Nmekuelewa ndugu yangu, lakini tukijikita kwenye hiyo hoja inamaanisha jamii zile ambazo zinasemekana kuwa nyuma kuliko zingine hazina uwezo mkubwa wa kuendelea kwasababu ni matatizo ya vizazi. Hata wewe na mimi kama tumerithi Akili za wazazi halafu bahati mbaya wawe na akili za kawaida na sisi tukaefeli basi siyo makosa yetu kabisa.
NB: Wachina wanafanya vizuri darasani kwasababu wana sera Bora za Elimu kuliko wazungu. Prof Ian Morris kwenye kitabu chake cha WHY THE WEST RULES FOR NOW anasema kwamba Uchina ni jamii ambayo tokea miaka 5000 iliyopita ilikuwa inatilia mkazo sana kwemye Elimu. Kupenda kusoma na kuendelea iko kwenye Utamaduni wa wachina. Bunduki ya Kwanza kabisa kuonekana dunia ilionekana karne ya 11 uchina.
Zheng He ambaye alikuwa ni Baharia wa Kichina alifika Zanzibar na Pwani ya Africa Mashariki miaka 90 kabla ya Vasco Da Gama. Hiyo ni karne ya 15 mzee, na walikuwa ndiyo wanaongoza kwa teknolojia ya maji (Maritime Technology) miaka hiyo walijenga hadi Ubalozi hapa Afrika. Baada ya kuzembea walijikuta wanakuja kupigwa na mataifa ya Ulaya pamoja na wao kuwa wa kwanza hapa duniani kwa zaidi ya miaka 5000
Vilevile, wazazi wanaweza kuwa na akili nyingi ila mtoto akawa kilaza kwa sababu genes zinaweza kuwa determined na ndugu wa wazazi wa mmoja wa wazazi wako ambaye hakuwa na akili na hivyo kuathiri akili yako pia.