Hadi kufikia Novemba 24, 2024, Idadi ya watu waliopaswa kuondoka Marekani ni 1,445,549, wamo watanzania 301

Heparin

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2021
Posts
242
Reaction score
1,141
Rais wa 47 wa Marekani, Donald Trump, ameendelea kuonesha msimamo mkali kuhusu suala la wahamiaji. Katika sera zake, amesisitiza kuimarisha usalama wa mipaka, ikiwemo ujenzi wa ukuta mpakani na Mexico, pamoja na kuimarisha sheria za uhamiaji ili kupunguza wahamiaji wasio na vibali halali. Trump pia amependekeza sera za kuwaondoa wahamiaji haramu nchini na kubana vigezo vya kupata uraia kwa wahamiaji.

Hata hivyo, sera zake zimepokelewa kwa mitazamo tofauti: wafuasi wake wakiona juhudi hizo kama njia ya kulinda maslahi ya Marekani, huku wakosoaji wakizitaja kuwa za kibaguzi na zisizofuata haki za binadamu.

Katika mwendelezo wa sakata hili, nyaraka ya idara ya Uhamiaji ya Novemba 24, 2024 imeonekana mtandaoni ikiwa na orodha ya watu 1,445,549 wenye amri ya kuondoka nchini humo, huku watanzania wakiwa 301 kati yao.

Tutegemee kuona idadi hii ikiongezeka zaidi?
 
Attachments

Kenya 1,282
 
Idadi ya watanzania wanao ondolewa katika ardhi ya Marekani na kurudishwa nyumbani imetolewa leo na mamlakani ya kudhibiti wahamiaji haramu nchini humo (ICE) chini ya Utawala mpya wa rais Trump.

Hapo jana idara ya ICE ilikamata wahamiaji 957 huku waziri wa mambo ya ndani akijiunga hivi leo katika operation hiyo mjini New York

Karibuni nyumbani sana watanzania

USSR
 
Back
Top Bottom