Hadi kufikia sasa, hakuna kituo cha runinga ama redio kilichocheza wimbo wa "Nipeni maua yangu"

Melki Wamatukio

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2022
Posts
6,156
Reaction score
10,974
Sawa, hauna video, lakini hata kwenye redio haukuchezwa pia

(a) Ni kwamba wamiliki wa redio zetu pamoja na watangazaji wao hawana uhakika na uhuru wa vyombo vya habari walionao?

(b) Au ndo kusema kuwa barua kutoka BASATA zilisambazwa sehemu husika kimya kimya pasi na taarifa kwa umma?

Wacha nikae kimya, nina familia inayonitegemea
 
Hiyo ndiyo taswira ya waTz, yaani kuufyata.

Kila mtu anajishuku na kujikosoa hata panapostahili!

Ukiuchochea huo wimbo "utanuniwa" na nchi nzima bila kuelezwa sababu ama waweza kudhuriwa bila ya maelekezo kutoka "popote"!

Matokeo ni kulaza njaa hiyo familia unayosema inakutegemea.

Kwa kuwa hakuna umoja wala mshikamano, tunaishi maisha ya nyumbu, mmoja anapoparamiwa na simba, wengine mnabaki pembeni mkishuhudia mwenzenu anavyotafunwa kwa kuwa nyie zamu yenu haijafika hivyo haiwahusu!
 
Wasafi unapigwa..Mawingu ndo usiseme EFM ndo balaa

Acha uongo wako! Hizi radio na television CHAWA hawana ubavu kwa kupiga nyimbo ile ya ROMA!! Wao Wote ni CHAWA wa ccm na ROMA kasema " KATI YA CCM NA ANDAZI" atachagua andazi!!! Utakua mwehu kama utategemea kuusikia wimbo ule toka kwenye hivyo vyombo.
 
Wimbo wa harakati upigwe na redio za biashara??how??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…