Hadi sasa Rais Samia ndiye bora zaidi, anafanya kila kitu kwa ustadi mkubwa

Hadi sasa Rais Samia ndiye bora zaidi, anafanya kila kitu kwa ustadi mkubwa

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Haongei sana bali Anatekeleza sana!

Hana papara Ila anafanya kila kitu Kwa ustadi mkubwa. Sio mtu wa kupanic Ila anaamini kwenye anachofanya

Amewekeza sana kwenye kupanga mikakati kabambe na kuhakikisha inatekelezwa ipasavyo Kwa utekelezaji madhubuti wa Serikali

Nimefuatilia katika hili suala la Tozo. Wakati limeanza wananchi waligawanyika, Baadhi tuliunga mkono kwa maendeleo ya haraka ya nchi yetu na wengine walipinga.

Sasa Naona baada ya serikali kuanza kutoa mrejesho wa kiasi gani wamekusanya na kinaenda kufanya kazi gani? Wananchi Kwa uwingi zaidi wameanza kuunga mkono Tozo mbalimbali zilizoanza kutozwa na serikali.

Tuliounga mkono suala la Tozo tulijua Tax base na nchi yetu ni ndogo sana na ni wananchi wachache sana wanaoumizwa ili kuiendesha nchi hasa daraja la wafanyakazi. Kilio chetu sasa kimesikika, Tozo zimeanza na Miradi kabambe ya maendeleo imeanza kupelekwa Kwa kasi.

Hongera Sana Rais Samia, naona unatumia zaidi Logic kuliko propaganda katika kubadili akili za watu

Hongereni serikali Kwa utaratibu huu mpya Kwa kuonesha fedha zilizokusanywa na kazi zinazoenda kufanya

623CD4CA-7D12-4A75-83D5-546825B6F5CC.jpeg
 
Wacha kuhangaika kumpigia promo mtu ambae dalili zote zinaonesha hajui anachofanya, nchi iko kwenye auto pilot hii, hope now yupo angani, hayo mapesa anayokusanya kila mahali kwa masikini hakuna ambae angeshindwa kujenga hivyo vituo.

Kuchukua tozo kwenye saluni ya kijana anayejiajiri toka chuo, bado ukamkamue mtu huyo tozo kwenye mafuta ya kupikia, akimtumia mama yake pesa kijijini umkate, bado akinunua luku umkate tozo ya jengo ambalo sio lake, hakuna anachofanya ni unyonyaji mtupu, nyie vibaraka mnatumwa kumsifia.
 
sahihi mkuu, Samia sio msemaji sana, ila idea zake ni nzuri sema wabongo ndio kujitia ujuaji na kulalamika ujinga tu, imagine unakuta jengo lina wapangaji sita ila wote wanalalamika kulipia buku kwa mwezi, muda huo huo wanataka wakienda hosppitali wapate huduma nzuri
 
Wameanza kuelewa taratibu. Nenda page ya Tamisemi facebook uone watu walivyoanza kuelewa somo
 
sahihi mkuu, Samia sio msemaji sana, ila idea zake ni nzuri sema wabongo ndio kujitia ujuaji na kulalamika ujinga tu, imagine unakuta jengo lina wapangaji sita ila wote wanalalamika kulipia buku kwa mwezi, muda huo huo wanataka wakienda hosppitali wapate huduma nzuri
Huko hospital hizo huduma wanapata bure? Lakini mbona maraisi wengine hawakufanya hayo?
 
Huko hospital hizo huduma wanapata bure? Lakini mbona maraisi wengine hawakufanya hayo?
Taratibu tutafika huko unakokusema. Acha tujenge hii miundombinu kwa kasi na kufanikisha haya
 
Huko hospital hizo huduma wanapata bure? Lakini mbona maraisi wengine hawakufanya hayo?
Sasa hao marais ambao hawakufanya hivyo mbona waliacha vituo vya afya vinavyojitosheleza? nyie sindio mnalalamikaga kwamba miaka 60 ya uhuru lakini dawa hakuna hospitalini? sasa mnataka dawa zitoke wapi na kodi hamtaki kulipa
 
Sio tu dawa, wanalalamika ubovu wa miundombinu, ukosefu wa Zahanati na Hospitali alafu hawataki kulipa kodi. Wanataka kodi walipe wafanyakazi na wafanyabiashara wachache wenye biashara rasmi.
 
Trickle down economics by Mw*** lu Nc*m PhD First class UDSM 🤣🤣🤣 Eti tunawapokonya ela kwA mfumo wa kodi Ili tuwamwagie mtaani.

This is "sekondari kila kata" waiting to happen again...much emphasis on buildings again,by the way inabidi watoe ripoti zinaendeleaje hizo shule.

I usually don't root for a president to fail,sababu akifeli yy ntaumia mm maskini,, but my God this is so stupid.

Kuna economic boom gani mpaka uongeZe miKodi,,,I am no economist but I Can see this epic fail from a mile away.

Natamani niwe proved wrong
 
Back
Top Bottom