Hadi sasa Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) hawajakabidhi zawadi kwa washindi msimu wa 2017/2018. Zimetafunwa? Vodacom walishakabidhi

Hadi sasa Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) hawajakabidhi zawadi kwa washindi msimu wa 2017/2018. Zimetafunwa? Vodacom walishakabidhi

TataMadiba

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2014
Posts
9,866
Reaction score
5,747
Juni 23, 2018 zilifanyika tuzo za wachezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom(VPL) ukumbi wa Mlimani City, ambapo tuzo 16 zilitolewa mgeni rasmi akiwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe. Lakini washindi wa tuzo nne hadi sasa hawajapewa zawadi zao za fedha.

Washindi hao ni: 1. Nicholaus Akwitende (Tuzo ya Heshima sh,mil.4), 2. Shaaban Idd Chilunda (Goli Bora sh.mil.4), 3. Hellen Mduma (Mwamuzi Msaidizi Bora sh.mil.4) 4. Abuu Juma (Tuzo ya U20 sh. Mil.4). Tuzo nyingine zote wahusika walipata zawadi kwa vile zimetoka Vodacom isipokuwa tuzo hizo ambazo ziliongezwa.

Lakini TFF ilipata udhamini kwa ajili ya tuzo hizo kutoka Azam sh. Mil.25,KCB Bank sh.mil.13, Premium Bet sh.mil.8 jumla ya fedha za zawadi nje ya vodacom ni sh. Mil.43! Lakini wanamichezo hao wamekuwa wakihangaishwa kupata fedha zao na mwisho ilikuwa Ijumaa Septemba 21. TFF Wametafuna Fedha hizo?.
 
wasomali nuksi tupu,bora wangempa Ali uongozi.
 
Back
Top Bottom