The Sunk Cost Fallacy
JF-Expert Member
- Dec 1, 2021
- 19,582
- 14,167
Kwanza Kukopa hakujawahi kuwa tatizo ikiwa uwezo wa kulipa upo na mikopo kuwekezwa kwenye productive sectors.Pili kuongezeka kwa deni hakutokani tuu na mikopo mipya bali madeni ya nyuma yaliyoiva na kuongezeka kwa riba ya mikopo.Moja ya vitu ambavyo watu wengi wanapuuzia ni hili suala la mikopo kwa nchi yetu.
Lakini hawajui kuwa mikopo hii ndio inayofanya miradi ya Maendeleo. Watu wanafurahia miradi Ila hawajui pesa inatoka wapi.
Utawala wa awamu ya 5 ulikopa na taarifa zilitolewa kila mwezi pale BOT lakini hakuna aliyejali, Leo tunakuja kuelezwa Deni lilipofikia watu wanakuwa wakali.
Hivyo ni vyema sasa tukawa tunakumbushana hali ya Deni linavyoendelea ili baadae tusije kusema hatukujua.
Kutokea April hadi November, Deni limeongezeka kwa Trillion 8
Hivyo kwa miezi 7 Tumekopa Trillion 8 ni wastani wa zaidi ya Trillion 1 kwa mwezi.
Nashauri speed hii ipungue kidogo.
Mama aajikite zaidi na kuongeza makusanyo maana kwa sasa watu hawatumii sana mashine za EFD, ni kama wameambia wafanye wanachotaka.
View attachment 2043640View attachment 2043641
Hata hivyo kama deni limeongezeka ni sawa kwa sababu Nchi ina sera za mikopo kwa kila mwaka.Kwa bajeti hii serikali ilipanga Kukopa til.10 hasa kutoka vyanzo vya nje.