Yaani ije itokee Watanzania wataingia Kenya bila kupimwa kisa kulialia kwenu huko, yaani Kenya ibadilishe kauli kwamba hawatapimwa, na wawe wanaingia tu kutuambukiza watakavyo, yaani kuanzia hiyo siku nabadilisha mtazamo wangu na kuwa hasi kwa kila kitu kitakachomhusu huyu rais wetu. Nitachukia sana.......nitatoa tamko humu hiyo siku.
Haiwezekani akayatia maisha yetu rehani na kuendana na upuzi wa kwenu wa kuogopa corona na kufukia vichwa ardhini kisa umaskini wenu. Lazima azingatie maisha ya Wakenya kwanza zaidi ya chochote kingine.
Yeye kumpigia rais wenu simu sioni cha ajabu maana ninavyomfahamu ni mwanadiplomasia wa hali ya juu, huwa hanyanyui mapumbu kwa kila kitu, atawakuna na kuwapa hizo hisia za utamu wa kukunwa ilmradi muache kulialia, lakini kipimo lazima kibaki pale pale, kama vipi waje mpakani wataalam wenu waungane na wa kwetu wawe wanapima wote pamoja.
Ninachojua na kutegema ni kwamba hawa madereva, wa kwetu na kwenu lazima waambukizwe corona wengi maana wanaishi maisha ya kulala kwenye magesti ambayo unakuta malazi na mashuka hufuliwa labda hata mara moja kwa wiki, unaingia gesti ukiwa mlevi haujali nani kalala humo jana, unajiachia na lichangudoa lako humo, maisha yao huwa yamo hatarini, hivyo sioni kikubwa kuskia wakitajwa wengi kuwa na corona.
Lakini lazima wapimwe na wapimwe tena na tena.