ukweli sasa siyo fair deal.......................kesho nitakuja na uongo wa kuwapendezeni. [MENTION]@Smile[/MENTION]
Hii long distance inatesa sana!
Bora mwaya; utudanganye jinsi gani mwanaume akisema Nakupenda anaamanisha anachosema! LOL
Lkn ukimtegemea sana mtu, ndipo unampa nafasi ya kukudisappoint!
chagua kusuka au kunyoa...................huwezi ukavuna kila mahali....[MENTION]@Kaunga[/MENTION]
So kama happiness yako inakuwa influenced na mpenzi; maana yake u can't be a caption but rather a co-captain of ur happiness!
A tough one; so unamaanisha nina chance kubwa ya kupewa mgongo nikishindwa kuchagua? Au nikijipa say a year or two?
waswahili husema mchelea mwana kulia hulia yeye.......................
Hao hao husema..... Mvumilivu hula mbivu, na pia..... kula nanasi kwahitaji nafasi.., na kama hiyo haitoshi wa siku hizi husema.......mambo mazuri hayataki haraka....
Damn waswahili! Very confusing!
siri ni kumjua mtu wako ni mtu wa namna gani na khalafu kujipanga kutokana na khali khalisi.......
That is the word!
The world of the DAY................[MENTION]@Kaunga[/MENTION]
Swali lingine (sijui labda lahitaji thread yake)!
Mwanaume ambaye ameumizwa sana kwenye past relationship; akago thru councelling n what, je possibility ya kufanya revenge (kumuumiza mdada aliyenaye sasa hivi) ikoje?
Kama uko kwenye mazingira ya namna hii usikhofu hakuna baya isipokuwa body chemistry yenu na personality jellying ..........au kinyume chake personality clashes... Kaunga
Swali lingine (sijui labda lahitaji thread yake)!
Mwanaume ambaye ameumizwa sana kwenye past relationship; akago thru councelling n what, je possibility ya kufanya revenge (kumuumiza mdada aliyenaye sasa hivi) ikoje?
Samahani nitazungumzia ulipizaji kisasi kwa jumla, kwa wote, mwanamke na mwanamme.
Kwa nini kulipiza kisasi, wakati mapenzi ni kama maisha yenyewe,
ni mchezo wa kushinda na kushindwa, wa kukimbia na kuanguka.
Unaposhindwa unajiweka sawa, unatafuta makosa yako,
unapoanguka unasimama, unajipangusa vumbi na matope......
unasonga mbele; kwa nini basi unapotendwa, usimshukuru
mtendaji wako kwa kukupa fursa ya kuanza upya bila ya yeye?
Badala yake mtu anakimbilia kulipiza kisasi! Nahisi hii zaidi ni
tabia ya mtu. Anayelipiza kisasi kwa sababu ametendwa katika
mapenzi, huyo atalipiza hata kwa bata wa jirani aliyeshit uwanjani
pake. Kulipiza kisasi ni wivu, ni chuki, ni husuda. Na watu wa namna
hii daima hawaishi kwa amani, kwani maishani mwao mote
wanapoteza wakati kwa kuandaa visasi vipya hata kabla ya kutendwa.