Swali lingine (sijui labda lahitaji thread yake)!
Mwanaume ambaye ameumizwa sana kwenye past relationship; akago thru councelling n what, je possibility ya kufanya revenge (kumuumiza mdada aliyenaye sasa hivi) ikoje?
Samahani nitazungumzia ulipizaji kisasi kwa jumla, kwa wote, mwanamke na mwanamme.
Kwa nini kulipiza kisasi, wakati mapenzi ni kama maisha yenyewe,
ni mchezo wa kushinda na kushindwa, wa kukimbia na kuanguka.
Unaposhindwa unajiweka sawa, unatafuta makosa yako,
unapoanguka unasimama, unajipangusa vumbi na matope......
unasonga mbele; kwa nini basi unapotendwa, usimshukuru
mtendaji wako kwa kukupa fursa ya kuanza upya bila ya yeye?
Badala yake mtu anakimbilia kulipiza kisasi! Nahisi hii zaidi ni
tabia ya mtu. Anayelipiza kisasi kwa sababu ametendwa katika
mapenzi, huyo atalipiza hata kwa bata wa jirani aliyeshit uwanjani
pake. Kulipiza kisasi ni wivu, ni chuki, ni husuda. Na watu wa namna
hii daima hawaishi kwa amani, kwani maishani mwao mote
wanapoteza wakati kwa kuandaa visasi vipya hata kabla ya kutendwa.