Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nishushe mwingine? 😂😂Safi...
Mgongano mkubwa unakuja...!
🔥🔥🔥
Bila shaka Kamanda...Nishushe mwingine? 😂😂
Kesho nayo sikuBila shaka Kamanda...
hongera sana aisee...wewe ni mwamba wa hizi vitu 👏👏Kesho nayo siku
I like itAisee ukishusha muendelezo nitag wa kwanza my friend...kazi nzuri sana 🤗😊😊
Leo tunakesha wote hapa😂😂😂
Ukimaliza semaLeo tunakesha wote hapa😂😂😂
Kazi nzuri...weka namba nikutumie ya soda na bundle 🤣🤗Mwisho
tunashukuru sana kwa ukarimu wenu bwana na bibi Gwakisa Mungu awazidishie baraka katika kazi zenu” alitoa shukrani za dhati Adam kwa niaba ya mke wake wa bandia (Bite).uchangamfu wake na wingi wa vituko ulifanya nyumba ya Gwakisa iwe iwe yenye shangwe na tabasamu kila siku,kitendo chake cha kuaga pale kilimsononesha Gwakisa na mkewe lakini hawakuwa na jinsi,kutoka mfukoni mwake aliwakabidhi shilingi laki mbili za kuanzia maisha yao huko waendako
Tayari Adam alianza kumpenda kwa dhati Bite uchapakazi wake na jinsi alivyomwokoa kutoka katika kifo ulichangia sana lakini kiunganishi cha mtoto Christian ndio ilikuwa chachu kubwa ya mapenzi yao.walivyohama katika nyumba yao ya kupanga walianza rasmi kuishi maisha ya mke na mume Adam hakuwa na amani hata kidogo na familia ya Reshmail hasa baada ya kukuta katika nyumba hiyo ndogo waliyohamia magazeti yaliyobandikwa kama mapambo likisema “imani za kishirikina zamwondoa mheshimiwa Manyama bungeni” alitamani sana kuisoma habari hiyo kiundani iliyotoka takribani miaka mitano iliyopita lakini ilikuwa imeandikwa inaendelea ukurasa wa pili anbao haukuwepo pale ukutani
“au walikuwa wanataka kunitoa kafara? Mungu wangu!! Niliwakosea nini mimi” alijiuliza Adam wakati wakiingiza yao ya Rambo ndani ya chumba hicho kimoja kilichotenganishwa na pazia kufanya sebule na chumba
Hisi hizo mbaya zikamfanya Adam aamue kuanzisha rasmi uhusiano na mwanamke ambaye amezaa naye mtoto pia aliyeokoa maisha yake bila kutarajia mwanamke ambaye hajawahi kumkwaza,mwanamke mpiganaji anayempa furaha tele kila siku
“Bite nataka uwe mke wangu”
“Mh!! Niwe mkeo mara ngapi mimi mkeo tayari jamani” alijibu Bite huku akichezea ndevu za Adam ikiwa ni siku ya pili tu tangia wahamie katika makazi hayo mapya
“una utani wewe mbona ulikuwa hujaniambia wala sijawahi kusikia ukiniita mume wako?
“sio lazima nikwambie tayari nina mtoto wako halafu humu ndani kuna kitanda kimoja tena kidogo tu,ulidhani chako mwenyewe!!!” aliuliza Bite kisha wote wakacheka huku wakikumbatiana na kuangukia kitandani
** *****
Maisha ya Reshmail jijini Dar-es-salaam yalikuwa yamebadilika sana akiwa anasubiri wakati baba yake akimtafutia kazi itakayompendeza alifurahia mara zote na Christian huku akiwa amewabadili watu wote wanaomfahamu kwa ukaribu kutokea kumwita Reshmail na sasa walimwita mama Christian na alikuwa amejivika pete ya ndoa katika kidole chake cha shahada ikwa na jina Adam na nyingine ndogo akiwa amemvisha Christian ikiwa imeandikwa Reshmail.
Hakuwa mtu wa kulialia tena wala msongo wa mawazo haukumsumbua tena aliamini nafasi ya Adam ilikuwa imezibwa vyema na Christian ambaye alikuwa Adam mpya kwake. Walilala wote,walicheza wote na kusimuliana mambo mbalimbali.alipoenda kusalimia rafiki zake walienda wote Christian mkono wa kulia. Harakaharaka Christian alijikuta akimpenda mno Reshmail kuliko hata ilivyokuwa kwa mama yake mzazi,maisha ya kifahari ya kwao Reshmail yalimfanya Christian anawiri sana ungewakuta wakicheza bustanini kama vile wanalingana umri walibembea pamoja na kupigana kiuongouongo,kwa ufupi waliishi maisha ya kusisimua kwa kila aliyewaona. Akiugua Reshmail ni Christian atamuuguza kwa kukaa pembeni yake bila kutoka nje hadi apone hivyo hivyo kwa Reshmail abaye alimwogesha na kumlisha. Wakati huo Reshmail ndio alikuwa mwalimu wa Christian akimfundisha kusoma na kuandika jambo ambalo hata baba yake alilipenda na Christian alikuwa mtu anayeelewa haraka akifundishwa ,reshmail alifurahia sana.
Baada ya kukaa na Christian mwezi sita reshmail kwa mara nyingine Iringa kwa rafiki yake jambo kubwa lililompeleka huko ni harusi ya rafiki yahe huyo ambapo alitarajiwa kuwa matron wa kipenzi chake hicho.
“shoga shughuli kesho kutwa hata haujaonekana jamani au ndio mambo yetu yale haja ya kufanyiwa make up….”aliuliza kiutsni .Eve katika simu alipokuwa anaongea na Reshmail.
“Kesho asubuhi na mapema nakujua ,mume wangu alikuwa na mafua ndio tatizo si unajua tena.”alijibu Reshmail.
Haya mume huyo anavyoringiwa shauriro “alijibu Eve .Christian alikuwa amependekezwa kuwa bwana harusi mdogo pamoja na Loyce (mtoto wa kaka yake Benny).
“He unatoka mume wangu asiuze sura,na jinsi alivyoandaliwa huku Dar es salaam ,utachoka mwenyewe na simtoi mpaka siku ya shughuli,atakayeruhusiwa kumuona ni bibi harusi mdogo(Loyce) peke yake wakati wa kujifunza,sitaki mwingine amuone mpaka siku yenyewe”alijibu Reshmail kwa furaha.
“Haya umeshindwa ambao hatuna waume tunalo,alijibu Eve kisha wakaagana.
Asubuhi ya siku iliyofuata majira ya saa nne asubuhi tayari Reshmail,Christian,mpambaji pamoja na dereva walikuwa ndani ya gari la baba yake (Resh)taratibu safari ya Iringa ikaanza.
“Usitupeleke kwa kasi sawa eeh,alitoa malekezo Reshmail na kukubaliwa na dereva kwa sababu hawakuwa na haraka yeyote ila mbele yao yalikuwa bado masaa mengi sana kabla ya harusi kufanyika.
Kwa mwendo wa kinyonga kabisa gar lilifika mbele ya nyumba ya Eve majira ya saa nne usiku na hakuna aliyekuwa ameschoka sana.Shamrashamra zilikuwa kubwa sana maeneo ya pale kwa Eve kelele zilizidi alipofika Reshmail, na kama alivyoaahidi kweli alishuka yeye peke yake kutoka katika gari akifuatiwa na dereva,urembo wake utadhani alikuwa amepembwa tayari kuingia ukumbini.
“Shoga tabia gain hiyo kupendeza kuliko bibi harusi?”aliuliza eve kiutani baada ya Reshmail kuingia katika chumba ambacho Eve alikuwa amehifadhiwa akiwa na wapambaji wake.
“Hebu acha utani wako,kila mara unadhani tuko shuleni?mwone,”alijibu Reshmail,Eve akajiziba mdomo kwa aibu huku akiwatazama wapambaji wake waliokuwa wamejizuia kucheka lakini uvumulivu ukawashinda wakacheka kwa nguvu.
Chumba kile kikageuka kijiwa cha story kati ya Reshmail na Eve ,stori zingine zilikuwa juu ya mume wa Reshmail (Christian),shoga hadi pete?
“Sina utani mie mbona”?alijibu Resh huku wapambaji wakiwa hawajui hata kinachoongelewa.
“Mama kuna mtu anataka kukuona,ilikuwa ni sauti ya kike ikimueleza Eve.
“Heh!!ushazaa na wewe?”aliuliza kiutani Reshmail.Mh!!niringe huyu ni msaidizi wangu tu wa kazi anaitwa Bite,nampenda naye ananipenda pia.
“Sio kama mimi na Christian “alidakia Reshmail ambaye tangu aingie chumba kilitawaliwa na vicheko.
“Bite humuwezi huyu anaitwa mam Christian ni rafiki yangu tangu utotoni.
“Nafurahi kukufahamu mama Christian hata mimi.alitaka kuondelea kuongea Bite akakatishwa na Eve.”Anayetaka kuniona nani huyo tena?,mwambie nina mgeni Bite akajiondokea bila kumalizia kauli yake.
Sherehe ilifana kuanzi kanisani lakini mambo yote yalikuwa saa mbili usiku maharusi wadogo walipokuwa wametangulia mbele wakifuatiwa na wana ndoa wenyewe(Eveline na Benjamin)huku nyuma yao Reshmail na Fredrick wakifunika kila kitu kwa pale mbele Christian aliteka macho ya watu huku kamera zimemulika yeye. Tabasamu lake pana la wakati wote lililoonyesha vishimo katika mashavu yake yote lilisababisha watu wengine wahisi huenda sio kutoka Tanzania , suti yake iliyoendana kabisa na mwili wake na viatu vyake pia jinsi mkono wake ulivyokuwa umemshika kiustadi Loyce (bi harusi mdogo) ulimfanya MC ashindwe kukaa kimya “nani mwenyewe harusi,wa mbele,nyuma au kati” aliuliza kwa mbwembwe
“mbeleeeeeeeee!!!.......nyumaaaaa!!!!” ndio majibu yaliyosikika kutoka kwa wengi
“hayaa wageni waalikwa wanasema maharusi wa katikati wamefunika sana” alidanganya MC aliyefahamu wazi Christian na Reshmail wameteka macho ya watu wengi pengine kuliko maharusi wenyewe.
Picha zilipigwa kwa wingi lakini Christian hakuonyesha wasiwasi wowote “mh!! Katoto kazuri halafu kajanja hako” wanawake walikuwa wakinon’gonezana huku wakimtazama Christian anavyozidi kusonga mbele
“wamekatoa nje,baba yake ni mreno” alidakia mama aliyesifika kwa umbea pale mtaani aliyejulikana zaidi kwa jina la mama mwingi.hata hawakuhangaika kujibishana nae kwani walishamzoea
Taratibu kabisa kwa mwendo wa kunyata jozi hizi tatu za kuvutia ziligawanyika huku jozi mbili za wakubwa zikienda katika meza kubwa kabisa na watoto wakienda katika meza yao ndogo iliyokuwa akimeremeta soda na vinywaji vingine baridi,”kusema ukweli sherehe imependeza,siongei kama MC bali kama ndugu Kidagaa Peter Kubalunga wengi wananiita MC K.P” alichombeza Msema Chochote (MC) na kushangiliwa sana na umati mkubwa uliohudhuria sherehe hiyo
********** ************ ********
“dah!! Umependeza kweli sitaibiwa huko na wajanja,hebu ona ona mgongo wako utadhani huna mamba ulivyopendeza,ona kifua chako mpenzi wangu hapana nitaibiwa mke mie” Adam alikuwa akimtania Bite huku akim funga zipu yake ya mgongoni
“acha wivu mwanaume wewe,kaa ndani usubirie ya kwako aniibe nani wataishia kutamani tu!!” alijibu Bite huku akimun’gunya midomo yake ili lipstick aliyopakaa ikae vizuri zaidi na kioo kikiwa mbele yake
“nakupenda sana mke wangu,tambua hilo niliamua toka moyoni mwangu na wala sijutii hata kidogo najionamwenye bahati sana” Adam kwa sauti ya chini iliyomaanisha anachokisema alimwambia Bite ambaye alitulia tuli akamtazama Adam kisha akamkumbatia na kumbusu.
“nakupenda pia nakupenda sana” Bite akamwambia Adam halafu akatoka nje na kupanda teksi iliyokuwa inamsubiri kwa nje na kuondoka,Adam hakuthubutu kutoa hata pua yake nje kwani bado alikuwa na uoga wa kurejea mikononi mwa watu wabaya
Majira ya saa tatu na nusu Bite tayari alikuwa mlangoni akionyesha kadi yake ya mwaliko kwa watu wa ulinzi kisha mwanadada kutoka kamati ya maandalizi akamwongoza Bite kuelekea katika upande ambao ndugu zake na mwanamke walikuwa wamekaa,eneo la chini ya meza ya bwana na bibi harusi mdogo.Bite alikuwa tayari kama ndugu wa damu kwa Eveline walitokea kuheshimiana sana na hawakuwahi kuingia katika malumbano makubwa sana.
Amani ilitoweka katika meza ya bwana na bibi harusi wadogo,Christian alikuwa amekosa utulivu mara kwa mara alikuwa ananyanyua shingo yake aweze kuona kitu Fulani ambacho hakuna aliyefahamu ni nini kimemsibu
“au kanaumwa tumbo?” alijiuliza matron huku akienda kwenye ile meza kumsikiliza Chriss ana shida gain
“Chriss ni nini baba umekuwaje?” alimuuliza baada ya kumfikia
“nataka kwenda kwa mama” alijibu kwa sauti iliyojaa manun’guniko sana
“subiri kidogo mtoto mzuri nitakupeleka sawa” matron alimdanganya Chriss huku akiamini shida yake ilikuwa kwenda kwa Reshmail,kidogo Chriss alitulia japo bado hakuwa na katika hali ya uchangamfu kama awali
Muda wa kutoa zawadi ulipofika maharusi wote katika jozi tatu walitakiwa kuwa mbele ya umati kwa ajili ya kupokea zawadi zao.Christian na Loyce waliwekewa viti wakakaa wakati Eve,Benny,Reshmail na Fredrick walisimama wima kupokea heshima hizo
“he! We mtoto vipi? Jamani huyu mtoto kulikoni” yule mwanamke aliuliza baada ya kushikwa gauni lake na Christian alipotaka kuondoka baaba ya kutoa zawadi. Bahati mbaya muziki ulikuwa umezimwa hivyo ukumbi mzima ulishuhudia tukio hili la kushangaza
“mamaaaa!! Mamaaaa!!” Chriss alimpigia kelele alipotaka kuondoka
“Chriss…….Christian……Christian wanguuuu!!! Jamani ni mwanangu..ni mwanangu huyu” alipiga kelele mwanamke huyu,alikuwa ni Bite na tayari akili yake imemgundu Christian,watu wote waliamini amechanganyikiwa lakini alikuwa anasisitiza bado kwa maneno hayohayo. Hakika mbele yake alikuwepo mwanaye waliyepotezana zaidi ya nusu mwaka sasa na dalili za kumpata zilikuwa zimeanza kufifia. Mayowe yake yalivyozidi yakapoteza usikivu pale ukumbini na kila mtu kuanza kujiuliza kulikoni eneo lile
“mama mama mama,huyu ni mwanangu…..Christian jamani” Bite kwa sauti ya juu sana akaanza kumwambia Eveline ambaye alikuwa amekodoa macho kuangalia anachofanya Bite pale mbele
“kuna nini jamani” Reshmail alishindwa kujiuliza akamvagaa Eve na kumuuliza
“huyu ni Christian,mtoto wangu jamani mtoto wangu kabisa” alisisitiza Bite. Nguvu zilimwisha Reshmail japokuwa hakuzimia lakini alianguka chini,alishuhudia kila kitu lakini hakuweza kuzungumza,ulikuwa mshtuko wa hali ya juu sana haikuwa sherehe tena bali kasheshe,huku Bite na mayowe yake huku Reshmail akiwa chini. Wapiga picha hawakuwa mbali walilichukua hili tukio kikamilifu tayari kwa kuuza katika vyombo vya habari.
Mwanamama mwenye nguo nyeusi alikuwa anapambana kupenya katika msitu mkubwa wa watu pale ukumbini,mwanzoni hakuwemo kwenye sherehe “vimama vya Kiswahili navyo,hapo umbea tu ndo amefata humu,akipigwa hapo au akikanyagwa atamlalamikia nani” mwanaume mmoja aliyekuwa amevaa suti aliwaambia wenzake huku wakimtazama mama huyo mwenye baibui iliyovaliwa kwa staili ya ninja hasa hasa kwa waumini wa dini ya uislamu anavyopambana kwa juhudi ili apenye. Watu kwa huruma wakampisha,moja kwa moja akiwa anakimbia kwa kasi alifika mbele ya ukumbi akaanza kuzubaa na mara ghafla akakimbilia alipolala Reshmail na kuanza kutikisa
“huyu maza vipi mwehu nini? Yaani mtu ameachiwa hewa impige yeye anaenda kuweka usiku tena na manguo yake” kijana mmoja aliyekuwa amevaa jinsi kwa staili ya mlegezo aliwaambia wenzake
“tulia wewe huenda ni mamake huyo” alijibiwa na wenzake
“reshmail amka amka mpenzi” alimwambia kwa sauti ya chini.
** ** *
Wivu wa utani utani aliouonyesha mbele ya mke wake ulukuwa unatoka moyoni mwake,Adam alihisi huko nje labda kuna mjanja anamchukulia mke wake.”ngoja nikamfumanie mtu leo” alijiwazia Adam huku akipekua pekua nguo gani anaweza kuvaa iweze kumziba sura yake asiweze kufahamika kwa urahisi mbele za watu,’baibui’ ndio jibu alilopata,harakaharaka akajitanda kwa ustadi,alifahamu vyema pesa ya mkewe ilipokuwa inahifadhiwa akajichotea kiasi kilichotosheleza kwa nauli “Mountain view” alijikumbusha jina la hotel ambayo sherehe ilikua inafanyika,ni jina alilolikariri kwenye kadi ya mwaliko.
Akiwa na baibui lake alipanda teksi ikamfikisha moja kwa moja eneo la tukio,kukuru kakara aliyoikuta pale ilimtia hofu kubwa sana aliamini lazima kuna kitu kimeharibika eneo lile hakuwaza kitu kingine bali usalama wa mkewe (Bite) moja kwa moja naye alijichanganya humo ndani n
Tofauti ya malengo yake ya kumjulia hali mkewe,macho yake yanakutana na Reshmail akiwa sakafuni na vazi lake zuri la harusi,sura yake bado ilikuwa haijasahaulika katika kumbukumbu za Adam.
Nguvu zilizokuwa zimemwisha Resh pale chini zilirejea kwa kasi kutokana na kusikia sauti ya kiume kutoka katika nguo za kike “mamaaaaaaaaaaa!!!!” alipiga kelele kwa sauti ya juu huku tayari akiwa amesimama wima akijaribu kukimbia,kamera zikageukia eneo lao tena nyingi zikimmulika mwanamke mwenye baibui (Adam). Kabla hajakimbia Reshmail alidakwa mkono wake.”Adaam……Adaaaam!!!” alipiga kelele kali zaidi wakati huuu Reshmail. Adam alikuwa amejivua baibui kwa upande wa usoni,akiwa hajapewa jibu lolote reshmail palepale alifika Bite,”Adam! Umefikaje hapa mume wangu…si ulisema hauji…” Bite aliuliza
“nini? Nani? Umemwitaje? Na huyu ni…….” Hakuweza kumaliziankauli yake wakati huu,mawazo yakauzidi nguvu ubongo wake akazimia palepale.Wakati huo Chriss alikuwa analia tu hgajui kinachoendelea,Eve na Benny walikuwa wanahaha huku na huko bila kukumbuka kwamba alikuwa na shera safi kabisa tena ya gharama za juu kabisa,Benny ndio alikuwa kama tahira hajui hata pa kuanzia alikuwa ameshtuka sana. Ilikuwa kama vita vile lakini hakuna hata aliyejeruhiwa wala aliyekuwa anapigana vilikuwa si vita vya risasi bali vita vya mapenzi. Wgeni waalikwa waligeuza tukio hilo kuwa kama filamu ya kusisimua lakini waliyokuwa wameianzia katikati bila kujua ilianzia wapi na inaenda wapi.,nani nyota wa filamu na nani adui.
***
Ni katika nyumba ya Eveline.Reshmail akiwa mbele ya Beti amepiga magoti akilia kwa uchungu
“Bite wewe ni mwanamke mwenzangu nionee huruma kwa haya niliyopitia,nimeteseka sana,nimedhalilishwa kwa ajili ya Adam,ni kwa ajili yake hadi leo mimi ni bikra,kwa ajili yake familia yake imetuchukia,kwa ajili ya Adam baba yangu haeshimiki tena mtaani kwetu,Bite sitamani mwanaume yeyote yule,ukininyan’ganya Adam na Christian mimi nitakufa Bite,ni furaha gani utaipata kwa kifo changu kwa ajili ya upendo?,sitajali huyu mtoto uliyezaa nae wala sitaumizwa na ujauzito wake uliombebea,ninakuomba Bite niache na mimi nipate furaha japo kidogo tu katika siku zangu zilizobaki hapa ulimwenguni,nisaidie niweze kurudisha upendo uliogeuka chuki kati ya familia yangu na Adam.Bite uamuzi upo mikononi mwako,ukikataa utaniumiza sana na nina uhakika nitakufa na pendo langu kwa Adam” Kilio kilimzuia kuendelea kuongea,lakini nay eye mgongoni mwake alilowanishwa kwa machozi ya Bite yaliyokuwa yanatililika muda wote wakati Reshmail anaongea,kwa hali halisi alimwonea huruma lakini pia kwa dhati kabisa aliwapenda Adam na Christian.Eve na mumewe Benny walikuwa watazamaji,wenyewe hawakuwa na uwezo wa kutoa maamuzi yoyote yale. Christian alikuwa ametulia kwenye kochi,hali ya utulivu aliyokuwa nayo ilipita siku zote.
“Adam tulipokutana unapajua,yote tuliyofanya unayajua,upendo wangu kwako nadhani unautambua pia……labda sikupangwa kuwa wako milele ndio maana aliyepangwa amejitokeza wakati muafaka,asante kwa zawadi ya penzi lako,asante kwa mtoto na huu ujauzito hii ni heshima kubwa kwako milele,neno gumu ninaloweza kulisema sasa ni kuwa kwa moyo mmoja nakuruhusu uendelee na Reshmail,nayasema haya mbele ya mama yanngu Eveline” alizungumza Bite kisha akashindwa kujizuia kuangua kilio kikuu kilichoamsha hisia za kila mtu pale ndani wote wakadondosha machozi yao. Adam,Reshmail na Bite wote kwa pamoja wakakumbatiana huku machozi yao yakitua juu ya Christian aliyekuwa ktikati yao,ilikuwa ni picha ya kusisimua na kuumiza sana.
****** *****
Kilikuwa kikao kikubwa cha familia yao Reshmail,watu wote muhimu walikuwemo jasoro mama wa familia hiyo aliyesusia kikao,mzee Manyama,Reshmail,Eve,Benny,Bite,na Paskalina walikamilisha kikao hichi,Christian alikuwa bustanini akibembea.Reshmail alikuwa anatoa siri nzito nzito za kushangaza ambazo kwa namna kubwa kabisa zilitoa taswira ya mambo yaliyokuwa yamefichika kwa muda mrefu,uhusiano wa kimapenzi kati yake na mama yake mzazi ulimwacha kila mtu mdomo wazi,Reshmail aliomba msamaha kwa hilo na alieleweka na kusamehewa. Ni katika usimuliaji wa upande wa Bite kuhusu ngome ya vigogo iliyoleta fikra za mazingira ya kupotea kwa kadi yake ya benki katika mazingira ya utata mkubwa,Benny hakuongea neno kwani yeye alikuwa kama mgeni tu katika mkutano huo.Mzee Manyama alikuwa kimya akimtafakari mkewe kwa maovu aliyoifanyia familia yake,kwa mateso aliyompa Adam na kwa uvunjifu wa amani aliouleta baina ya familia hizi mbili,kwa fedheha aliyomletea na kumvunjia heshima yake bungeni na hata mtaani,akiwa mwingi wa hasira alisimama bila kuaga na kuelekea chumbani,kwa hali aliyokuwa nayo Reshmail aliamua kumfata kwa nyuma ili asije kufanya jambo baya huko anapoenda,hasira yake ilipokelewa na na mwili wa mkewe ukiwa sakafuni,tayari alikuwa maiti. “ulistahili hukumu hii” bila kushtuka alisema mzee Manyama huku akimpisha Reshmail aingie humo ndani.
* ***** *****
Mapema baada ya mazishi ya mama yake mzazi Reshmail akiongozana na Adam katika gari ya baba yake,dereva akiwa Adam walifunga safari ya kwenda Mwanza kwa wazazi wake (Adam).
“utabaki ndani ya gari nitatangulia mimi najua watakuwa wakali hao lakini wakikuona ndipo mzizi wa fitna utakapokuwa umekatwa” Reshmail alimpa maelekezo Adam ambaye alikubali kwa ishara ya kutikisa kichwa.
Gari ilipaki nje kidogo ya nyumba ya kina Adam,kama walivyoelewana akashuka Reshmail akiwa amependeza sana,akaifunga gari kwa kutumia rimoti aliyoshuka nayo na kwa mwendo wa kunyata akaanza kuusogelea mlango akausukuma akaingia ndani,kupitia kwenye kioo Adm lishuhudi Reshmail akitoweka machoni pake.
“umefata nini hapa we mchawi Adam hajakutosha unamtaka na Rosemary ngoja sasa….Rose!!!!” aliita mama Adam,Reshmail akiwa anatabasamu kwani alijua ni muda mfupi wote watakuwa na furaha kubwa. Akiwa bado hajaanza kuongea alishuhudia mama Adam akimfuata na kisu huku Rosemary akifika pale na mwiko mkubwa,wakati huu akili yake ilifanya kazi haraka akaanza kukimbia lakini nguo yake ndefu ilimsaliti baada ya kunasa kwenye geti la kutokea nje.
Kwa macho yake mawili Adam alishuhudia Reshmail akiwa chini huku watu wawili wakimshambulia kwa fujo,alijaribu kufungua mlango lakini ulikuwa umewekwa ‘loki’ sauti yake haikuweza kusikika nje alipigapiga vioo vya gari lakini hakuna aliyemsikia. Alishuhudia damu nyingi sana ikiruka juu. Kwa akili ya haraka haraka akakumbuka kushusha kioo akatokea dirishani
“mamaaaaaaaaaaaaaaa!!!” Adam akaita kwa nguvu palepale mama yake akageuka na kudondosha kisu alichokuwa nacho,”Adam mwanangu ni wewe!!!” alisema mama Reshmail huku aimfuata Adam ambaye hakumjali bali alifika alipokuwa Reshmail “Reshmail,Reshmail” “ mama na dada mmemuua mke wangu jamani mamaaaa!!” alilia Adam baada yakuona hajibiwi kitu.”A.d….am!! ninaku….fa mume wangu….ninakufa kwa furaha…..ni..meku..rudish…sha kwenu…naku…panda..sana” Reshmail aliongea kwa kujiumauma huku akivuja damu,raia wengine walikuwa katika harakati za kutafuta msaada lakini msaada mkubwa uliopatikana ni wa polisi waliowatia nguvuni mama Adam na mwanae Rosemary huku roho ya Reshmail ikimaliza muda wake palepale Igoma jijini Mwanza.kama usingekuwa ujasiri wa Adam basi tukio lile lingegharimu maisha yake,tayari mama mkwe amepotea,na sasa mpenzi wake Reshmail,mama na mdogo wake wakitupwa jela kwa kesi ya mauaji.
** ***
“mapenzi yamenipotezea muda wangu nimekuwa mfungwa miaka mitano,mapenzi yameivunja vunja familia yangu,mwanamke niliyempenda ametoweka tayari tena mbele ya macho yangu,ni heri niisome hii sheria vizuri zaidi ili ikiwezekana siku moja niwatetee ndugu zangu walioko gerezani hao pekee ndio furaha yangu,kamwe siwezi kuhangaika tena na watoto wa hapa chuoni hata siku moja sidhani kama wana maana sana kwangu nikithubutu tena huend yatakuwa makubwa zaidi ya awali,usiku mwema Mosenya.” Alimaliza simulizi yake Adam,wote tulikuwa tunatokwa machozi ya uchungu,lakini lengo langu likatimia na swali la muda mrefu likapata jawabu baada ya simulizi hii kuanza kuandikwa katika gazeti la chuo.
Nishamaliza my friend...nimeenjoy sana aisee 😊😊🙈Ukimaliza sema
Karib sanaNishamaliza my friend...nimeenjoy sana aisee 😊😊🙈
Asante...niko kusubiri hadithi nyingineKarib sana
Salute...
Usijali inakujaAsante...niko kusubiri hadithi nyingine
Karibu tena na tenaSalute...
Kazi nzuri, hakika nimeburudika