Hadithi hii inakufundisha nini

Hadithi hii inakufundisha nini

BashiriOnline

Senior Member
Joined
Nov 5, 2012
Posts
127
Reaction score
44
Hadithi inayokuja, ni ya Sungura
sikia,
Hadithi uliyongoja, leo
ninakuletea,

Alitoka siku moja, njaa aliposikia,
Nja aliposikia, Sungura nakuambia
Siku ile akaenda, Porini
kutembelea,

Akayaona matunda, mtini
yameenea,
Sungura akayapenda, mtini
akasogea, Mtini akasogea, Sungura
nakuambia.

Sungura karukaruka, lakini
hakufikia,
Matunda hakuyashika, mikononihakutia,

Hakika alisumbuka, nguvuze
zikapungua, Nguvuze zikapungua Sungura
nakuambia.

Mtazame hapo juu Sungura
amelegea,
Mtazame na miguu, matunda
anarukia,

Atafanya sikukuu, matunda
akifikia, Matunda akifikia, Sungura
nakuambia.

Karuka tena karuka, matunda
akarukia,
Mwisho wake akachoka,kachoka
hata mkia,

Penye mti akatoka, pembeni
akasogea, Pembeni akasogea, Sungura
nakuambia.

“Sizitaki mbichi hizi” Sungura
akagumia,“
Naona nafanya kazi, bila faida
kujua”,

Yakamtoka machozi matunda
akalilia, Matunda akalilia, Sungura
nakuambia.

Sio kama hakutaka, sasa
nakupasulia,
Matunda aliyataka, ndiyo kisa
akalia,

Tunajua hakufika, alichoka
kurukia, Alichoka kurukia, Sungura
nakuambia.

Hadithi nimemaliza, nimekwisha
simulia,
Jambo moja sikiliza, rafiki yangu
sikia,

Usikose kujikaza, mazuri
kukazania, Utamshinda Sungura, utapata
mbivu hizi
 
Hadithi hii inatufundisha kuwa sasa, sasa, saaa ya kwenda kwetu, kwaheri mwalimu kwaheri, tutaonana keshooooooooooooooooooooooooooooo
 
Asante mdau umenikumbusha mbali sana.Natafuta ile ya darasa la saba nafikiri.Ilikua inazungumzia yule mzee aliye kufani;

Karudi baba mmoja ,tokasafari ya mbali;
kavimba yote mapaja ,nakutetemeka mwili,
akatamka mgojwa,ninaumwa kwelikweli:
hata kama nikichanjwa ,haitoki homa kali,
roho naona yachinjwa,kifo kimenikabili;
kama mnataka mali ,mtayapata shambani

sikumbuki mashairi mengine.
 
Back
Top Bottom