. . . . . .nilihisi kuona nyota nyota kutokana na kipigo.
Nilikuta nikiishiwa nguvu,mwili mzima ulinilegea,nilitamani kumsemesha askari lakini nilijihisi mdomo kuwa mzito,nililala chini pole pole.
Nilijikuta nimeingia kwenye ulimwengu mwingine,na kuiona dunia nyingine.
Niliona watu wamevaa mavazi meupe.
Watu hao walikuwa wakinitaza bila ya kuniongelesha.
Walikuwa wamesimama mistari miwili kulikuwa na watoto,watu wazima,vijana na wazee.
Ghafla alitokea mtu mwenye ambae sikuweza kuiona sura yake kutokana na ilivyokuwa iking'aa kama mwanga wa jua.
Mtu huyo alinipa ishara kuwa nimfuate,nami sikusita nilikuta nikimfuata mpaka tulipofika sehemu kulipokuwa na watu wengine.
Watu hao walikuwa wanatisha,manywele marefu zaidi ya sharubu za simba,menu na kucha zao zilirefuka na kuonekana kali kama kisu kilichonolewa kwa ajili ya kuchinjia mnyama.
Mtu niliekwenda nae alipotea ghafla na kuniacha mimi na watu wale.
Watu hao wakutisha walianza kunisogelea,nyuso zao zilionekana kuwa watu wa shari na makatili.
Waliponikarabia,nilianza kukimbia huku nikipiga kelele za kuomba msaada.
Hakuna aliesikia,kwa bahati mbaya nilikutana na shimo moja refu ambalo lilikuwa halionekani mwisho wake,nilidumbukia ndani ya shimo hilo na kupiga makelele.
Nilishtuka na kujikuta bado nipo kituo cha polisi tena nikiwa nimefungwa kamba kwenye kiti huku mwili wangu umeloana kwa maji.
. . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
Baada ya kudondoka chini nilipoteza fahamu.
Askari yule aliwaamuru mahabusu wawili wanibebe ambapo walinipeleka chumba maalamu cha mahojiano
nilifungwa kamba kwenye kiti cha chuma na ndipo nilipomwagiwa maji na kuzinduka.
Nilina askari wawili wakiwa mbele yangu. . . .