Hadithi: Kesi ya Mzee Mnyoka

KESI YA MZEE MNYOKA 27

Mzee Mnyoka aliwahi ofisini kesho yake mapema sana akiwa na lile daftari alilichanganya na mafaili mengine ya pale ofisini,

Kisha mtendaji alipofika alimuagiza kutafuta vijana ambao wangefanya usafi pale ofisini na kutoa kila kitu nje,

"Nataka tufanye usafi na kutoa mafaili yote na yale ambayo hayafai tuyachome Moto"

Mzee Mnyoka alimuambia mtendaji,

"We Mzee Basi unajiona umefika, umetaka Sana iyo nafasi ila baadae utajilaumu Sana"

Mtendaji aliongea,

"Sikiliza Bwana Mdogo hebu uliza historia yangu hapa kijijini kabla hujaongea utumbo wako"
Alisema Mzee Mnyoka huku akianza kutoa meza nje,


Mtendaji hakuwa na namna akatafuta vijana na kuanza kufanya usafi ,

Walitoa vitu vyote nje Kisha wakafagia na kudeki,


Mzee Mnyoka sasa alikua bize akipekua Nyaraka moja baada ya nyingine na mwishowe akamuita mtendaji,.


"Hivi daftari la kahawa sio hili kweli?"

Alisema Mzee Mnyoka akimuonyesha mtendaji,


"Dah Ni lenyewe aisee Asante Mungu"

Aliongea mtendaji huku macho yakimtoka kwa furaha,

Yeye mwenyewe alikua amekalia kuti kavu kutokana na kupotea kwa daftari Hilo,


Hatimaye baada ya muda habari zilisambaa kuwa daftari limepatikana, Mzee Mnyoka sasa aliwaambia wananchi kuwa malipo yatafanyika kesho kutwa,


"Kuna watu wasio waadilifu walijaribu kuficha hili daftari ili wadhulumu pesa, lakini tunashukuru limepatikana!"

Mzee Mnyoka aliongea huku wenzake wakimshangilia,

Mwenyekiti aliyefururushwa alijisikia vibaya Sana na aliamua kwenda kumuona katibu tarafa Mzee Mkude ili waone namna ya kumkomesha Mzee Mnyoka



*********"""

Tito hakwenda Bungeni siku hiyo, badala yake, alibaki hotelini akiwaza,
Alimuelewa vyema Bwana Shida, na kutokana na mapato aliyokua akipata pale mgodini milioni 500 isingekuwa tatizo kwa mwezi,


Hata hivyo alielewa kuwa Shija baadae atataka kitu kingine

"Once a cheater , always a cheater"


Alikuwa akiwaza,


Alimtumia naibu wake ujumbe kuwa anajisikia mafua mafua na kichwa kinauma, hivyo aendelee kumuwakilisha kwenye kipindi Cha maswali na Majibu, halafu jioni atafika kwenye kikao Cha jioni ,

"Nimfanyeje huyu Mwanaharamu?"

Tito aliendelea kuwaza,

Asingeweza kumueleza Bwana Johnson kuhusu Hilo kwani angemuona Kama mzembe mtu aliyezembea,

Na kingine kilichomtia wasi wasi, Ni namna gani Bwana Shija alijua hizi taarifa na je Ni Nani na nani wanajua hizi taarifa?


Aliamua Bora amueleze mwenzake Majimbi,


Alitoa Simu yake ya kazi ambayo ilikua kwa ajili ya mambo yake ya Siri tu,

Kutokana na mazingira ya asubuhi hakuweza kujua askofu atakua mazingira gani hivyo alimtumia meseji Kwanza kwenye Simu yake ya kawaida,

"Askofu Mimi Ni waziri Tito nilikua nahitaji uniombee "


Askofu Majimbi alikua ofisini kwake, akitoa semina ya wanandoa ambao walitegemea kufunga ndoa jumamosi pale kanisani kwake, aliwahudumia Kisha akamwambia Katibu muhtasi wake asiruhusu mtu kwanza Ana maombi Binafsi,

Kisha akabonyeza kidude fulani sehemu ya ukuta ikafunguka akaingia na ikatokea sasa ofisi nyingine ambayo ilikua ya tofauti kabisa,


Alitoa Simu yake ya kazi nae akampigia Tito,


"Tito una nini asubuhi yote hii"

Alianza askofu Majimbi baada ya Simu kupokelewa,

"Kaka Kuna tuko matatizoni aisee"

Alisema Tito Kisha akamsimulia habari zote za waziri mwenzake Bwana Anthony shija,

"ah sasa hapo unakwama wapi jamaa yangu, huyo Ni kumpoteza tu kabla hili Jambo halijafika kwa Raisi"

Alisema Majimbi,

"Unajua kabisa ,yule Ni Waziri unadhani itakua simple kumpoteza bila kuacha alama?"

Aliuliza Tito,

"Sikiliza yeye si anataka millioni 500 kila mwezi?"

Aliuliza Majimbi
"Yeah"
Alijibu Tito,

"Sasa huyo tunaweza kutumia million 200 au 300 pekee kumpoteza huyo mjinga"


Alisema askofu Majimbi,

"Ninashangaa unaogopa eti, tumefanya kazi ngap? Hata kule mgodini tumeua wangapi? Sembuse mtoto mdogo tu huyo"


Alijitapa askofu Majimbi

"Tunamaliza kikao kesho, kwahiyo Mimi nitamjibu kuwa tutampa hizo pesa ila nikija Dar let's finish this son of bitch"
Alimalizia Tito Kisha akazima Simu halafu akachukua Simu yake nyingine,


Akampigia kimada wake mmoja Kisha akampigia dereva amfuate


"Nitakuonyesha kuwa Mimi Ni zaidi yako Shija"

Alijisemea sasa akijifunga taulo na kuelekea bafuni.


*************


"Sikiliza Mzee Mnyoka Hana ujanja mbele yetu, sisi tuliacha tu kumnyoosha kwahiyo tupe siku mbili ngoja amalizie malipo hizi siku mbili halafu siku ya tatu tunampoteza"


Aliongea Mzee Mkude

"Ila yule Mzee Ni mjanja mjanja hivi"

Aliongea mwenyekiti

"Hata Kama sisi Ni wajanja zaidi yake"

Wewe nenda kesho kutwa jioni hatuko nae Tena yule,"

Alisema Mzee Mkude,

Alishamchukia Mzee Mnyoka kabisa,


______ ___________


Mzee Mnyoka alishirikiana na kamati ya wilaya na alifanya malipo kwa wanakijiji na zoezi lilienda kwa weledi kabisa,

Ingawaje hakukuwa na maelewano mazuri na Mtendaji lakini zoezi lilikwenda vizuri,

Wakati Mzee Mnyoka anamalizia kufunga ofisi aliona gari dogo likiwa linajongea maeneo ya ofisini kwakuwa ofisi ilijitenga kidogo Mzee Mnyoka alijua bila Shaka ule Ni ugeni wa Kijiji,

Hivyo alisubiri bila kufunga mlango kwanza,

Gari ilisimama karibu Kisha mmoja wapo akashuka na kumueleza Mzee Mnyoka kuwa anaweza kufunga tu mlango hawana haraka,

Mzee Mnyoka alifunga mlango Kisha akaenda kuwasikiliza,


Wakati anainama alistuka kupigwa na kitu kizito akaanguka chini na kupoteza fahamu,

Kwa haraka jamaa walimuingiza ndani ya gari na kuondoka nae,


Baada ya masaa muda mwingi kupita Mzee Mnyoka alizinduka akiwa amelala sakafuni huku akiwa amefungwa kamba za mikono na miguu...
 
KESI YA MZEE MNYOKA 28

Mzee Mnyoka alijitingisha na taratibu kumbukumbu zikamrejea akakumbuka alikua anafunga ofisi Kisha akawaona watu wapo kwenye gari aliposogea ndio akapigwa kitu kizito,

Sasa alijisikia maumivu kichwani,

Mazingira Yale yalikua machafu na hali ya utulivu kiasi, alikuwa Peke yake chumbani, aliangalia mazingira ya pale na hakuona dalili za kuwepo watu, alijibingirisha kidogo na Mara mlango ukafunguliwa,

"Ah umeamka eeh"
Alisema sasa huyo mtu akiingia,


"Kwanini mmenikamata, Niko wapi?"

Mzee Mnyoka aliongea kwa Shida,

"Mzee usingeamka tu"

Alisema huku akimsogelea na kumuweka sawa kwenye kiti,

"Mnataka nini? Kwanini mmenikamata?"
Mzee Mnyoka aliuliza akihema,

Yule jamaa hakumjibu chochote zaidi ya kumkaza zaidi kamba zilizokua zimeonyesha kulegea,

Alimuweka vizuri Kisha akatoka nje na baada ya muda akarejea tena akiwa na mwenzake,

Mzee Mnyoka hakuweza kutambua sura zao, na akili yake ilimuambia hajawahi kuwaona popote vijana wale,

Hawakuongea nae chochote zaidi ya kumlinda tu huku wakiwa wamening'iza bunduki zao

***********

Kama ujuavyo msomaji wangu Mzee Mnyoka alikua na kawaida ya kuchelewa kurudi nyumbani, hivyo si mke wake mama Monica au mtoto wake Mary aliyekua na wasi wasi,


Pamoja na kuchelewa kurudi lakini Mzee Mnyoka asingeweza kulala nje ya nyumba yake hata Mara moja,


Baada ya kumaliza kula chakula Cha jioni mama Monica na mtoto wake sasa waliangalia tamthilia yao kwenye televisheni huku wakitegemea Mzee Mnyoka kuingia wakati wowote,


Mpaka saa 5 kamili usiku Mzee Mnyoka hakuonekana,

Sasa mama Monica alianza kukasirika

"Namuambia kila siku baba yako asichelewe kurudi lakini hanielewi, anajua jinsi anavyochukiwa lakini baba yako Ni mbishi, "
Mama Monica aliongea


"Ooh huyo ndio Mzee Mnyoka Bwana, mwenyewe anakuambia haogopi chochote"

Mary alisema huku akiingia chumbani kwake kulala,

"Mzee Mnyoka lakini kwanini unapenda kuchelewa kurudi?"

Mama Monica aliongea nae huku akiingia chumbani

************

Baada ya kumalizana na kimada wake Shania Tito alirudi bafuni Tena kuoga

Baada ya muda alikua tayari sasa kwenda kupata chakula Cha mchana na baadae kuhudhuria kikao Cha jioni Cha kuahirisha Bunge,

Alifika Bungeni mapema na akiwa na tabasamu kabisa alimsalimia Shija,


Baada ya kikao sasa wabunge walikumbatiana huku wakisalimiana na wengine waliagana sasa kwani wangekutana Tena baada ya mwezi mmoja ujao,


Tito alitoka akiwa na Shija mpaka nje kabisa ya viwanja vya Bunge,


"Yeah we have a deal"

Alimuambia Shija akimaanisha kuwa amekubaliana na kile alichosema Shija....

"Safi Sana Tito, unajua kizuri kula na mwenzako ndugu yako, hahahahahaha"

Alisema Shija huku akicheka

"Lakini lazima tukubaliane kuwa hutageuka huko mbele"

Alisema Tito huku akiwa sasa na hali ya umakini,

"Usijali Bwana Mdogo"

Alisema Shija Kisha wakaagana kila mmoja akapanda gari lake,

"Hupati hata 10 mbwa wewe!"

Alijisemea Tito nae huku akifunga mkanda kurudi zake Dar jioni hiyo hiyo....



**************************************

Mzee Mnyoka wasi wasi ulianza kumjia , lakini hata hivyo alihisi Hawa watu yupo wanayemsubiria isingewezekana kuwa wameshindwa kumuua , kulikua na mwanga hafifu pale ndani


Ni baada ya muda kidogo mngurumo wa gari ulisikika nje na mmojawapo wa wale jamaa akatoka nje Kisha baada ya muda akaingia mtu mzee Mkude!

Mzee Mnyoka alipigwa na butwaa Ni kweli alikua na ugomvi wa muda mrefu na mzee Mkude, ila sasa hakutegemea ingefikia hatua ya kutekana kabisa

"We Mwanaharamu niue tu sasa unasubiri nini?"

Mzee Mnyoka aliongea,

"Mzee Mnyoka mbona una haraka ya kufa, hebu subiri tu utakufa ndugu mwenyekiti,"

Alisema Mzee Mkude huku akimsogelea..


"Mzee Mnyoka hebu angalia maisha yangu sasa hivi! Ni tofauti kabisa na yako! Lakini si unajua tulikua Kijiji kimoja, tukiwinda sungura wote, sasa badala uniulize niliwezaje kuwa na maisha mazuri wewe kazi yako Ni kuleta majungu na fitina tu!"

Alisema Mzee Mkude


"Kwahiyo umekuja kuniambia hayo yote?"

Mzee Mnyoka aliongea..

"Sikiliza Mzee Mnyoka, baada ya wewe kufa maisha yangu yatabadilika kabisa, sitakuwa Kama hivi unavyoniona leo, ujue Kijiji chetu kina Mali nyingi na Ni sisi wachache tuliofanikiwa kuzifaidi, wewe endelea na majungu yako ambayo Leo ndio mwisho wake"

Aliongea Mzee Mkude

*************


Mama Monica alizinduka usiku wa manane akidhani mumewe atakua amerudi lakini Hali haikua hivyo, alienda kumuamsha mwanae Mary na usiku huo huo wakaenda nyumba ya jirani,

Sasa waliongozana na kupitia maeneo yote ambayo walihisi Mzee Mnyoka atakuwepo lakini hawakumuona,

Sasa watu waliendelea kumiminika nyumbani kwa mzee Mnyoka na wanaume wakaanza msako usiku huo huo kumtafuta Mzee Mnyoka,


*****************


Tito alifika Dar usiku Sana hakutaka kwenda kwake alinyoosha mpaka kwa askofu Majimbi ambapo walifanya kikao kizito usiku huo huo walijaribu kupanga mipango yao huku wakiangalia tahadhari zote,


Lengo likiwa kummaliza Shija bila kuacha alama yoyote,


Hatimaye walitoka na mpango mmoja madhubuti na Kisha Tito akaenda kutafuta chumba hotelini kumalizia usingizi wake,

Sasa alilala vizuri kabisa kwani mpango ambao waliupanga ulikua unatoa uhai wa Shija huku wao wakiwa salama kabisa...
 
KESI YA MZEE MNYOKA 29

Msako uliendelea kila Kona ya Kijiji na walijaribu kwenda mpaka shambani kwake lakini hakukuwa na dalili zozote za kumuona Mzee Mnyoka,

Mpaka asubuhi inafika sasa Mbiu ilipigwa na Mtendaji wa Kijiji akaripoti kituo Cha polisi,

Kuhusu kupotea kwa mwenyekiti wa Kijiji,

Polisi walifika na kuchukua maelezo,

"Ndio wakati Mimi narudi niliona gari Aina ya Noah ikiwa imepaki karibu na ofisi Mimi sikuangalia nikaendelea na Safari yangu na baadae niliona ile gari ikiwa inakata Kona kama inaenda njia ya wilayani"

Alisema shuhuda mmoja ambaye alikua akitoa maelezo kwa polisi,

"Ulimuona Mzee Mnyoka?"

Aliuliza polisi
"Sikufanikiwa kumuona maana nilipita kwa mbali tu"

Alisema yule kijana..

Polisi walichukua maelezo ya mtendaji wa Kijiji na Kisha walichukua maelezo ya mke wake ,

Hakukuwa na mtu wa kumtilia mashaka moja kwa moja kutokana na kupotea kwa mzee Mnyoka hivyo polisi waliendelea kuhimiza wananchi kuendelea kumtafuta Mzee Mnyoka, na wao waliahidi kushirikiana na vyombo vingine katika jitihada za kumpata Mzee Mnyoka..



*************

Mzee Mnyoka sasa alitulia kimya huku akiomba Mungu aweze kumuokoa mikononi mwa watesi wake,

"Mzee Mnyoka Mimi kabla ya kukuua nataka uelewe kuwa mpaka sasa Mimi sio yule Mzee Mkude unayemjua,

Nina Mali nyingi sana ambazo wewe hata ukae miaka elfu moja hapa duniani huwezi kuzipata, siku zote nataka ujue kuwa majungu hayalipi, kwa taarifa yako siku ile uliyoniona na yule ng'ombe ndio maisha yangu yalibadilika, ulitakiwa unifuate uniulize Mzee Mkude tufanye nini , eeh tungeyajenga tuu lakini wewe ukajifanya mjuaji,"


Sasa Mzee Mnyoka aliona Kama masikio yake yanataka kupasuka kwa kusikiliza "mahubiri" ya Mzee Mkude ambaye sasa alikua anabwabwaja tu

"Sikiliza Bwana Mkude, siku zote ubaya hauwezi kushinda haki, ukiniua wewe hutaishi milele, na wewe utakufa tu"

Alisema Mzee Mnyoka kwa upole,

"Hata Mimi sitaki kuua, nataka ufe mwenyewe tu hapa, sikiliza Mzee Mnyoka ,tungetaka kukuua tungekumaliza tu zamani ila sasa hatupendi kuua"

Mzee Mkude aliongea huku akiwageukia wale vijana na kutoa kicheko...


*****************

Afande Josephine sasa alikuwa kwenye Gari wakirudi kutoka Kinjeki,


Alijaribu kukumbuka Kama jina la Mzee Mnyoka
"Mh huyu Ndugai Msoka Mnyoka, sio yule mgonjwa wa kimei kweli?"

Aliwaza afande Josephine huku akitoa Simu yake

"Oya vipi Kuna majeruhi huko?"

Alisema kimei baada ya kupokea,

"Hapana ,hivi yule mgonjwa wako wa kipindi kile ndio alikua anaitwa Ndugai Msoka Mnyoka?"

Aliuliza Josephine.
"Yeah, Mzee Mnyoka, vipi kwani"?
Aliongea dokta kimei sasa akijiweka sawa.

**********



Oscar alikua akimalizia malizia kuweka mwili sawa baada ya mazoezi aliyokua ameyafanya asubuhi hiyo ya siku hiyo Ni wakati anamalizia malizia aliona sms kwenye Simu yake,

"Tembo mmoja aliyepotea njia hajulikani alipo"


Aliangalia ile sms Kisha akamalizia mazoezi yake akaenda bafuni kuoga....

Oscar alivaa nguo zake Kisha akachukua Simu yake na kupiga mahali, aliongea kidogo Kisha akakata Simu, halafu akakaa kwenye Kochi kusubiria, baada ya muda mfupi Simu yake iliita Tena,

"Ndio tumempata, yupo kwenye nyumba moja msituni , hii nyumba alikua anakaa meneja wa msitu wa Kinjeki zamani kabla haujakabidhiwa kwa serikali kupisha mradi"

Alisikika mtu mmoja upande wa pili

"Siafu?" Oscar aliuliza Tena,


"Siaafu, ooh hapa naona wawili tu"

Alijibu upande wa pili,

"Okay, usimueleze mtu kwanza ngoja tuimalize chap
Nipe location zote muhimu"

Alisema Oscar huku akichukua notebook yake na kuandika mambo muhimu,


Alimaliza Kisha akatoa Simu yake na kumpigia afande Josephine,

"Oya sikiliza, Mzee Mnyoka yupo kwenye nyumba ya meneja wa zamani wa msitu wa Kinjeki,. Ni beta mkawahi asubuhi hii kabla hajadhurika zaidi"

Aliongea Oscar Kisha akakata Simu,

Josephine alikua anatoka zamu lakini kutokana na taarifa hizo alirudi ofisini na kumueleza Mkuu wa kituo ambae alitoa gari na piki piki mbili pamoja na silaha kwenda kumuokoa Mzee Mnyoka,

**************

"Mzee Mnyoka Kama nilivyosema hakuna mtu atakuua, walinzi watabaki hapa tu kuhakikisha kuwa Huli Wala hunywi, na hakuna mtu atakuja kukuokoa, kwahiyo utaamua mwenyewe unataka kufa lini, haya mzee Mnyoka kwaheri tutaonana huko kuzimu"

Alisema Mzee Mkude akitoka zake nje,

Walinzi nao walitoka nje na kumfungia Mzee Mnyoka,

Mzee Mnyoka sasa alitulia kwenye kiti chake tayari kabisa kusubiria kufa kwa njaa na kiu,

"Ee Mungu nisaidie"

Alijisemea Mzee Mnyoka akifumba macho


***************

Shija alirudi Dar na Tito alikamilisha mipango yake yote kisha akampigia Simu wakutane,

"Ndio njoo Rombo Hotel, hapa utanikuta"
Alisema Tito huku akiwa ameshawapanga vijana wake,

"Huyu boya anakuja na sitaki tukosee, na kumbuka tunaua kwa akili sio risasi sawa wajomba?"

Aliwaambia vijana wake,

Shija aliwasili baada ya nusu saa Tito alimpungia mkono akamuona alipokaa ilikua ni asubuhi kwahiyo waliagiza supu na kuanza kupata kifungua kinywa huku wakipiga story,

"Kwahiyo Broo mambo yatakuwa tayari ila tu, naomba Sana asijue mtu yoyote"

Tito alikua anaongea huku akiendelea kula,


"Hakuna shida kizuri kula na ndugu yako bhana, "
Alisema Shija,

Tito alikua anampigisha hadithi Shija ili vijana wake wapate muda wa kufanya "mambo"

Baada ya dakika 40,
Tito alipokea ujumbe mfupi,

"Tayari"

Aliangalia hiyo sms Kisha akatabasamu,
"Kaka ngoja kuna demu nikamcheki kwanza si unajua ugonjwa wa mdogo wako!"

Alisema huku akimalizia kinywaji chake,

"Ahh nakujua Sana, ukiona sketi unaishiwa nguvu, mheshimiwa Raisi Ana pengo kwakweli la waziri mmoja!"

Alisema Shija huku akicheka nae akisimama kuondoka,

Tito yeye aliingia hotelini na kupanda kwenye chumba namba 78 ambacho angeweza kutazama vizuri huko barabarani,


Shija aliingia kwenye Gari lake lakini Jambo la kushangaza hakumuona Rajab Dereva wake,

Alitoa Simu kumpigia lakini kabla haijaita Rajabu alitokea

"Samahani boss nilienda toilet kidogo"

Alisema Rajab huku akiondoa gari
" Aisee uwe makini Kaka, nchi siyo hii saa hii, kumbuka unamuendesha waziri"

Alisema Shija akivuta mkanda wake vizuri...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…