wao ni wao
JF-Expert Member
- Dec 23, 2022
- 1,179
- 2,807
Nimeona mkuu , nimereplywao ni wao nimekuPM mkuu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimeona mkuu , nimereplywao ni wao nimekuPM mkuu
ShunieeeeeAsante sana
Shukrani sana mkuu, umetutendea haki kabisaa Huna mbambaaKESI YA MZEE MNYOKA- MWISHO WA MWISHO (
Kwa udhamini wa mkuu Gily )
Baada ya wiki moja
Oscar alikua amejilaza kwenye sofa huku akiangalia vipindi mbali mbali kwenye televisheni yalikua ni matangazo ya moja kwa moja kutoka chuo kikuu cha dar es salaam ambapo waziri mkuu alikua akiwatunukia shahada ya uzamivu wanafunzi waliohitimu mafunzo maalum ya mifumo ya komputa , hawakuwa wengi sana, na kutokana na kozi yenyewe,
Na wanafunzi hao kuitwa mmoja mmoja,
‘Na huyu ni mwanafunzi aliyefanya vizuri zaidi na kupata GPA 4.9 anaitwa JOYCE TITUS KILIBIKA!
Alisema mc wa shughuli hiyo
“whaaaaat!” alisema oscar akiruka pale kwenye kochi na kuvaa haraka haraka kisha akawasha gari na kuwahi mwenge. Mlimani..
Kama bahati alikuta sherehe bado hazijakamilika na wahitimu bado walikua ndani
Ndugu jamaa na marafiki walikua wamezunguuka nje na zawadi zao huku wakisubiri kwa hamu wapendwa wao watoke nje!
Naam hatimaye walianza kutoka mmoja baada ya mwingine wakiwa na majoho yao,
Oscar alijitahidi kujipenyeza hadi akafanikiwa kuwa karibu na mlangoni kabisa, kwanza hakua na zawadi yoyote! Hivyo ilikua ni rahisi kufika mbele kabisa,
Hatimaye mtu wake alitoka! Oscar kama mshale alichomoka na kwenda kumkumbatia Joyce! Joyce nae hakuamini macho yake, machozi yalimtoka kwa furaha,
Bila kujali macho ya watu oscar alimbeba Joyce na kutokomea nae kwenye gari…..
‘oscar tunaenda wapi? Ujue ndugu zangu nimewaacha na mshangao wa haja” alisema Joyce huku akivua joho la kubaki na suruali na tisheti nyepesi , oscar hakujibu chochote alizidi kukanyaga mafuta kuelekea Tegeta,
Baada ya safari ya kutokuamini hatimaye walifika , oscar alishuka na kwenda kufungua geti na kuingiza gari ndani kisha akafunga tena geti na kumbeba tena joyce hadi ndani na kumtua kwenye sofa!
“oscar. Oscar..”
“shhhhh!” oscar aliweka kidole mdomoni kumuashiria asiseme kitu Joyce kisha akamsogeza karibu na kuanza kumtomasa na kumvua nguo moja baada ya nyingine mwishowe walijikuta katika mapenzi mazito hapo hapo sebuleni, na hivyo kuamua kuhamia chumbani na shughuli ikaanza upya,
Saa mbili Usiku walirudi sebuleni na joyce alikimbilia simu yake,
“yaani wamepiga mpaka wamekoma, nimetafutwa sana!’ alisema Joyce
“vipi nikupeleke !” aliluliza Oscar
“ah keshoo njaa inauma hatari’ alisema Joyce akitafuta jiko lilipo oscar nae alimfuata akiwa na bukta .
Kesho yake walienda hadi gereza la keko kumtembelea mzee Tito,
oscar alibeba kitabu cha hadithi kilichoitwa “MPANGAJI” ili kumpa mzee Tito asome akiwa lupango..
“hakika maisha ni hadithi ndefu sana” alisema Joyce wakiwa njiani kurudi,
“nakuachia binti yangu, muangalie, nakuamini Oscar, asije kulia machozi yanayotokana na wewe!” oscar alikumbuka maneno ya mzee Tito muda mfupi uliopita na kujikuta machozi yakimtoka,
Hakupendezwa na hali hii ya kuishi na Joyce wakti baba yake akiwa gerezani lakini hakuwa na namna yoyote,
Maisha lazima yaendelee
Aliwaza akikanyaga mafuta kurudi tegeta.
MWISHO.
Namba zangu ni 0746 mia mbili sitini na sita mia mbili sitini na Saba
Niwashukuru sana wadau,
Asanteni kwa support yenu!
Mpaka wakati mwingine kwenye "MPANGAJI AU MZAHA WA DAMU"
Story nzr sn ngoja nipunguze alosto[emoji39]KESI YA MZEE MNYOKA 09
"Ndio yule kijana alipoleta flash, sura yake haikua ngeni kabisa, Ila Sasa nilisahau wapi nilipomuona Mara ya kwanza, Ila hata akija hapa namkumbuka kabisa"
"Okay Sasa Mzee Mnyoka , kazi hii inaweza kuchukua muda wa wiki moja au mbili hivi mpaka kumalizika, kwasasa sikushauri urudi kule kwanza, hivyo unaweza kuendelea "kuumwa" hapa kwa siku kadhaa na nikihitaji chochote nitawasiliana na Dokta Kimei lakini pia ukiwa na taarifa nyingine ambazo unahisi zitasaidia Basi tutawasiliana, vinginevyo usimuambie mtu yoyote , na vile vile Mimi na wewe hatujawahi kuonana na hatujuani kabisa, Sasa kila la kheri"
Oscar alitoka na kuaga, dokta Kimei alimtoa mgeni wake Hadi nje ya hospital ,
"Kesho saa sita na nusu pitia kwenye dustbin lililo nje ya ofisi yako, utakuta chupa ya kibox kidogo kutakua na maelezo yako kuhusu hatua inayofuata, vinginevyo kila la kheri na mgonjwa wako, "
Alisema Oscar Kisha akapotelea zake gizani...
**********
Kesho yake asubuh dokta Kimei alifika kwa Mzee Mnyoka na kuweka mipango yao sawa,
Habari za Mzee Mnyoka kuumwa Sasa zilienea Kijiji kizima na watu Sasa walimiminika hospital kumjulia Hali Mzee Mnyoka,
Ni watu wawili pale hospital ndio walijua undani wa ugonjwa wa Mzee Mnyoka,
Dokta Kimei aliendelea na kazi zake Kama kawaida ambapo ilipofika saa sita na nusu alitoka nje kwenda Kwenye ndoo ya kutupia taka taka ambazo si hatarishi Sana,
Alivaa baada ya kutupa jicho huko na huko, ndipo akavaa gloves zake na kuingiza Mikono kwenye ndoo,
Alitabasamu baada ya kuona kibox kidogo hivi , akakitoa na kuweka kwenye mfuko wa koti lake Kisha akavua gloves na kuzitupia humo...
Alirudi ofisini kwake Kisha akakifungua
Ndani yake kulikua na kikaratasi kidogo tu
"Zoezi litaisha baada ya wiki moja,
Usiamini mtu , kwenye chumba Cha Mzee mnyoka ,
Na jiangalie wewe mwenyewe,.
Kwa chochote piga hii namba, "0002004006"
Unaitwa TEMBO
Dokta Kimei Sasa alikua ameingia kwenye majukumu mazito ambayo binafsi hakutarajia,
Aliamua kuweka utaratibu wake mzuri wa kumuhudumia Mzee Mnyoka,
Ambapo alimuandalia chakula kule ofisini kwake, na Kisha Mzee Mnyoka alikua analetwa anakula halafu anarudishwa Tena Kama mgonjwa mahututi!
*******
Siku mbili baadae
Kijijini Kinjeki... 8:34 asubuhi
Vijana wengi walikua kwenye foleni kwa ajili ya kupata vibarua kwenye mradi uliokua unaendelea pale kijijini,
Zipo kazi ambazo zilihitaji watu wanne, zingine watatu, na zingine mmoja,
Mnyapara Sasa alikua akitangaza kila kazi na idadi ya watu,
"Mtaro deep, wanne!"
Square round kuchimba wanne!"
"Kusogeza mabomba kumi na mbili!"
"Free role mmoja"
"Niko hapa boss" Kijana mmoja aliruka mbele kwa Kasi ya ajabu, Ni wazi kuwa alikua anasubiri hiyo nafasi ....
"Wa ndani sita"
Mnyapara aliendelea na mwishowe geti likafungwa,
Vijana hawa waliobahatika kupata kazi siku hiyo waliingia ndani kabisa ya uzio kwa ajili ya kuanza kazi...
Kila mmoja alikua na hamasa kwani malipo si haba, Kibarua alilipwa 18,000 ama 15,000 Kama atakula chakula Cha mchana pale pale,
Oscar alikua miongoni mwa vijana hao ambaye kwa makusudi kabisa alichagua kuwa free role siku hiyo,
Oscar alifika Jana usiku akiwa full na ndipo alimtafuta Kijana mmoja na ndie aliyempa utaratibu mzima wa kupata kazi na Aina ya kazi pale "mgodini"
Oscar alipewa muongozo wa kazi yake ambaye kwa uzoefu wake aliokuwa nao ilikua Ni kazi simple sana kwake,
Kwanza ilikua Ni kupata sample, kwenye maji ya visima vimojawapo, na , na pia kujua mhusika au wahusika wanaongoza hiyo oparesheni ya kuibia nchi,
Hivyo asubuhi hii alivaa Kama vijana wengine , kaptura ya jeans, na raba, pamoja na shati lililokatwa Mikono,
Alichagua kitengo Cha kutokuwa na kazi maalumu kwanza,
Kutokana na maelezo ya yule Kijana kitengo kile kilikua na kazi nyingi na malipo yalikua Ni elf 10 kwa siku,..
"Siku nyingine unaweza kutumwa na mabosi uwapelekee sigara au maji"
Ndio maana Oscar alivyorukia iyo nafasi asubuhi Ile vijana wenzake walimshangaa!
Kazi iliendelea Kama kawaida, vijana waliendelea kufanya kazi Kama mchwa, kutokana na section zao,
Ni Oscar pekee yake ambaye alikua yupo "kazini" kivyake vyake, hata hivyo usingeweza kumdhania kwa namna alivyokuwa akipiga kazi Kama mzoefu, aliweza kufanya kazi zote alizotumwa kwa haraka na weledi mkubwa ,
Mpaka muda wa mchana Sasa, alianza kutabasamu baada ya kuona kazi yake inakwenda vizuri,
Mosi, aligundua kuwa sehemu Ile inalindwa Sana,
Kwa haraka alishapishana na walinzi zaidi ya ishirini, kwa namna wanavyotembea na kuongea na miili yao, Oscar Kama mpelelezi mzoefu alishaona, zaidi ya yote pia aliona CCTV camera zaidi ya nane, kwa maana hivyo kila tukio lilikua linaonekana mahali Fulani, na hivyo asingeweza kutoka na "sample" kirahisi kwa mchana ule,
Kitu pekee ambacho aliamini Ni kuwa kuna Ofisi mahali kubwa kuliko hii ambayo inaonekana hapa, kwa uzoefu wake alihisi lazima jengo Hili liwe Ni kiini macho tu,
"Oya baharia hatujaja kukaa kizembe hapa, nenda Pembe Ile ukamshikie mjomba pale ngazi"
Oscar alistuliwa na nyapara wakati akiwa katika fikra nzito,
"Poa poa bosi" Oscar alisema akinyanyuka haraka, na kuelekea kule...
***********
SAA 12 jioni ilikua Ni mwisho wa kazi ambapo vibarua walisogea kwa Nyapara wao na kupewa malipo yao,
Oscar alichukua elfu kumi yake nae na kutoka nje ya mgodi, ....
"Baadae kidogo tutaonana"
Alijisemea kisha akaingia zake mtaani kwenda mahali alipokua amejihifadhi,
*********
Hospital Kiomboi saa 1 usiku,
Dokta Kimei na Mzee Mnyoka Sasa walishaanza kuzoeana na ilifika mahali wa kupeana "huduma" Yale maongezi hayakuwa katika sauti ya chini Tena,
Mzee Mnyoka alitamani kumwambia mkewe, kuwa yeye Ni mzima wa afya tele, lakini aliogopa mkewe anaweza kutibua Mambo,
"Ah wanawake Ni wanawake tu, " Mzee Mnyoka alijisemea ,
Dokta Kimei aliendelea kumsisitiza mama Monica kuwa mgonjwa Sasa alikua na nafuu,
Wakati wakiendelea na story zao Kama kawaida baadhi ya manesi kutokana na haraka zao au kuzoeana na madaktari huwa hawapigi hodi,
Mzee Mnyoka na Dokta Kimei wakiwa wanaendelea na story zao Mara ghafla mlango unafunguliwa! Nesi Furaha alipigwa na butwa kumuona Mzee Mnyoka akiwa amekaa kitandani buheri wa afya! Lakini zaidi ya yote alisikia wazi wakiwa wanaongea, hata huu mshtuko anaona hapa Ni baada ya kuwafumania wakiwa wanaongea,
Hata hivyo alijifanya hajui kinachoendelea..
"Dokta nilikua naomba maelekezo ya contrimazole mg 200 kwa yule mtoto wa miaka 12"
Nesi Furaha aliongea..
"Hiyo ni antibiotics kwahiyo unaweza kumpa moja Mara mbili, au umpe amoxicillin mbili Mara mbili" dokta Kimei alijibu nesi Furaha akaondoka,
"Mzee Mnyoka endelea bhana na story ya Uganda , Ehh kwahyo mkafika kwenye nyumba aliyokuwemo Idd Amini"
Dokta Kimei Sasa alikua anainjoy story za Mzee Mnyoka huko vitani Uganda mwaka 1978..
"Mimi na Meja Msuguri, ndio tulikua na kamisheni 23 c,
Kwanza wenzetu wa kamisheni 19 kombaini walifika mapema Ila hawakuingia,. Ile tunashuka tu kwenye Gari ya jeshi meja Msuguri akapiga kelele dauuuniiii! Basi wote tukalala chini huku tukiwa tumeilenga nyumba ya Nduli!"
Dokta Kimei sasa alikua amekaukia kwa kicheko jinsi Mzee Mnyoka alivyokua anasimulia kwa vitendo,
"Haki ya Mungu we Mzee Ni hatari sana,. Walahi natamani ukae hapa mwezi mzima"
Dokta Kimei aliongea machozi yakimtoka kwa kucheka
*********
SAA 5:30 usiku "mgodini"
Oscar alitega vifaa vyake vizuri Kisha akavaa nguo zake za kazi, huku akimalizia na gloves zake ,
Mdogo mdogo alisogea kuelekea mgodini,
Kulikua na ukimya wa Hali ya juu mazingira ya Kijijini hakukua na pilika nyingi zaidi ya kelele kadhaa za ngoma na walevi kadhaa waliokua kilabuni.....
"We Mzee ,haya Sasa niambie umewezaje kuruka pale?"[emoji23]KESI YA MZEE MNYOKA 14
Mnyoka alikua amelala kitandani huku mawazo yake yakiwa mbali kiasi,
Aliona Kama misheni hii inachukua muda mno, alishachoka kukaa pale kitandani,
Mzee Omari alikua Sasa akikoroma kwenye kitanda kingine pembeni yake, Mzee Mnyoka alimhurumia sana Rafiki yake huyo kwa kupata kazi ya kulala na mgonjwa fake,
Ni wakati anatafakari tafakari ndipo taa zikazimika ghafla,
Mzee Mnyoka alihisi umeme umekata tu Na dakika si nyingi genereta litawaka,
Kama inavyokua siku zote, hata hivyo dakika tatu zilipita na Sasa Hali ya taharuki pale hospitali ilianza, Mzee Mnyoka Sasa "machale yalimcheza"
Akashuka Kitandani na kuvaa viatu vyake, Kisha akafungua mlango wa chooni, akafungulia maji yatiririke
*********
Frank alipaki Gari kidogo na hospitali upande wa nyuma Kisha akavaa nguo zake za kidaktari, alishasoma mazingira asubuh Ile na kurekodi Baadhi ya maeneo nyeti ikiwemo sehemu ya kuunganishia umeme kwa jengo zima, alipita kwa kujiamini Kama daktari akapita nyuma ya maabara na kutokea kwenye sehemu ya mfumo wa umeme, hivyo alifungua kwenye box Kisha akatupia kitu Kama kigololi hivi Kisha akapiga hatua kuelekea wodi ya wanaume, Ni baada ya hatua kadhaa mlipuko mdogo ukatokea kwenye lile box na kukawa na giza Totoro,.....
Alishaelewa mpaka mafundi wagundue tatizo Ni baada ya robo saa na Hadi kutatua tatizo Ni nusu saa nyingine au lisaa limoja, hivyo alijiwekea dakika 12 za kumaliza kazi yake ya "kuondoka na uhai" wa Mzee Mnyoka halafu apotee zake,
Dawa aliyompaka Furaha ingechukua masaa 5 mpaka sita kuamka, hivyo alitaka afanye mishe zake Kisha arudi kwa Furaha kulala,
************
Dokta Kimei Sasa aliondoka Haraka kwenda Hospitali, aliona potelea pote Ni Bora amtoroshe Mzee Mnyoka pale Hospitali kwanza alitaka amchukue pale kwake Kisha amhamishie mbali zaidi lakini kwa usiku ule hakuona Ni busara kumuacha hospitali..
Alitoka pole pole na Gari yake na Kisha akapaki nje ya Geti kuu, hakupata tabu yoyote kupita maana alikua anakwenda Mara nyingi usiku Kama kukiwa na wagonjwa wa dharula, Ni wakati anakaribia geti kuu Mara umeme ukakata! Dokta Kimei Sasa aligeuka nyuma kuangalia Kama umeme umekata "kote" na kuona Ni pale hospitali tu,..
"Shiiit" dokta Kimei Sasa aligeuka nyuma kupiga hatua za haraka kupitia njia ya mkato kwenda chumbani kwa Mzee Mnyoka,
Aliamua kupitia ule mlango wa dharula hata hivyo aliamua kwanza kusikilizia kwa kutegea sikio Kama kutakua na dalili zozote za fujo,..
Akiwa pale nyuma ya kile chumba ndio akasikia dirisha likifunguliwa na taratibu akaona miguu inatoka na hatimaye mtu akaruka dirishani akapepesuka kidogo Kisha akasimama sawa!
Ndipo Sasa Dokta Kimei akapigwa na mshangao,
Mzee Mnyoka!
Alikua anataka kucheka lakini mwishowe akatingisha kichwa tu,
"Mzee twende, Mimi Kimei!"
Alimshika mkono Mzee Mnyoka ambaye alikua amestuka kidogo Kisha wakatoka mbio kutokea kwenye geti kubwa na kuingia kwenye Gari,
Dokta Kimei Sasa hakujua aanzie wapi kumuuliza Mzee Mnyoka,
Hata hivyo aliendesha Gari mpaka kwake baada ya kufunga vizuri milango yote, Sasa Dokta Kimei akamuangalia Mzee Mnyoka Kisha akaanza kucheka,
"We Mzee ,haya Sasa niambie umewezaje kuruka pale?"
Dokta Kimei aliuliza huku akicheka,
"Na wewe ulikua unafanyaje nyuma ya chumba pale, ningejuangukia Sasa!"
Mzee Mnyoka alisema nae akicheka,
********
Frank alifungua mlango pole pole huku bastola ikiwa mkononi,
Kwa kutumia tochi yake ndogo alimulika pale kitandani kwa Mzee Mnyoka na kuona Hakuna mtu, alimulika kitanda kingine na kumuona Mzee Omari akikoroma tu, alisikia maji yakimwagika chooni, akahisi Mzee Mnyoka alikua huko,
Alisubiri dakika mbili akaona amfwate huko huko
Alifungua mlango kwa tahadhari
"Shit!"
Aliachia msonyo mkali baada ya kuona dirisha lipo wazi na Mzee Mnyoka hayupo Sasa hasira zilimjaa na akatoka nje kwa haraka,
: ********************************************
Saa 5: 40 usiku Kijijini Kinjeki
Oscar alikua karibu kabisa na geti la kuingilia Mgodini, kwa maelezo ya yule Kijana ilikua wazi kuwa kuna wageni watakuja na kutokana na "tukio" la juzi usiku Ni wazi kuwa kikao Cha dharula Cha Wenye Mali kingefanyika,
Alivuta subra na ndipo kwa mbali akaona magari mawili yakiingia, yalipitiliza moja kwa moja ndani ya geti na kwenda kupaki...
Oscar alizunguuka nyuma kabisa na Kunyata Kisha akasogea kuelekea zilipo Ofisi,..
Safari hii alitaka kuwajua tu hao wahusika, kwahiyo alizidi Kunyata na kusogea jirani kabisa na Ofisi hiyo,
Walinzi wengi walikua upande wa mbele wakipokea wageni, hivyo ilimsaidia kujongea karibu zaidi bila kuonekana, alitoa kisu huku akijibingirisha kwa namna ya kukwepa kamera na hatimaye akawa ukutani kabisa mwa jengo lile, aliona asuburi kwanza waheshimiwa waingie ndani ya jengo,
*********
"Jamani Mume wangu! Jamani Mume wangu!"
Sasa mama Monica alikua akiendelea kulia mfulululizo,
Mzee Omari Sasa alikua Hana maelezo ya kutosha zaidi ya kusema yeye alipitiwa na usingizi na aliamshwa kutokana na makelele ya kukosekana kwa umeme na aliposhtuka hakumuona Mzee Mnyoka,
Sasa msako ulianza pale hospitali na taarifa Sasa zikafika kwa Mganga mkuu wa hospitali Kiomboi,
Ambaye Sasa aliwatumia madaktari wake ujumbe wa "kupotea ghafla" kwa mgonjwa,
Dokta Kimei Sasa alichanganyikiwa baada ya kupata taarifa hizo za "kutafutwa" kwa Mzee Mnyoka,
"Mzee Mnyoka unatafutwa kule hospitali! Sasa tunafanyeje?"
Dokta Kimei alimgeukia Mzee Mnyoka,
"Kumbuka kukaa kwako pale hospitali hata dokta mkuu alikua anauliza Mara nyingi Sana, hivyo kwa suala hili kuwa wewe ndio ulikua unatafutwa itakua shida"
Dokta Kimei alisema
**********
Oscar alipata wazo la kupitia kule stoo kwa makusudi kabisa asubuhi Ile alitegesha dirisha, hivyo Kama halikufungwa ingekua rahisi kwake kuingia,
Hivyo alijivuta taratibu mpaka kwenye dirisha la store, na Kama bahati lilikua vile vile alivyolitega,
Alilisukuma pole pole, Kisha akapita ndani,
Kulikua na giza Totoro ndani na kwa akili ya haraka alijua hao wageni watakua kwenye ukumbi wakifanya kikao chao,
Alipanda juu ya mabox kadhaa Kisha akatoa mfuniko wa kwenye dari akaingia, alipanda kuelekea usawa wa ukumbi kwa tahadhari kubwa,..
Alifika na kutega masikio lakini Hali ilkua kimya kabisa,..
"Watakua wapi?"
Alijiuliza Maswali
Alisogea kabisa na kutoa kisu chake Kisha pole pole akatengeneza shimo dogo hivi akafungua begi lake na kutoa waya mdogo hivi Kama USB akautumbukiza pale Kwenye shimo pole pole, Kisha akatoa kitu Kama simu janja , akachomeka ule waya,
Sasa alikiwasha kile kifaa na Sasa mazingira ya ukumbi yakawa kiganjani mwake,..
Hakukuwa na mtu!
Oscar alizidi kuduwaa, na Kisha akaamua liwalo na liwe akatoa mfuniko na kushuka chini ya ukumbi, alitembea kwa haraka pembezoni na mwishowe wazo lilimjia kusogea mbele zaidi mwisho wa ukumbi,
Ukumbi ulikua umewashwa taa moja tu mwanga ulipatikana kupitia taa za nje,
Oscar Sasa alijaribu kuwaza walipo hawa wageni katika jengo Hili,
"Labda watakua kwenye ofisi mojawapo"
Aliwaza akizidi kusogea Sasa kwenye mlango wa mbele...
**********
Frank alirudi na kujilaza Kama kawaida,...
Furaha alikua amelala fofofo,
Aliwaza Nani alimstua Mzee Mnyoka mpaka akaamua kutoroka....
Ni wazi kuwa mipango ya kumuua Mzee Mnyoka imevuja! Na bila shaka kule kule ofisini kwao Kuna mtu alipata taarifa au Kuna msaliti katikati yao,
Frank Sasa alizidi kuwaza huku akifikiria Jambo la kumuambia boss wake,.
Mr Bill kesho asubuhi..
Thanks. Pamoja mkuu...nilitoka kdg majukumu ya kazi yalinizidiaNawashukuru sana kwa kampan yenu
Hope tutakuwa pamoja Hadi mwisho..
Mchawi atakuwa bando tu [emoji23][emoji23][emoji23]
moneytalk kabwe katalii Kabwe Katali Kibunango Gormahia FOX21 Vitalis Msungwite Watu8 TAJIRI MKUU WA MATAJIRI Da Vinci XV Shunie Queen Kan wao ni wao Angel Nylon Gily manndungu wegero kwetu djsharifu Toto mol Mcheza Viduku holy holm