THE JAGGERS
JF-Expert Member
- Apr 3, 2023
- 545
- 410
Bomba xana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Link mkuu tukashibishe akiliNdio tumefikia final Leo!
Link mkuu tukashibishe akili
Nilimekamilisha hakika nayo hii imetulia,kazi safi mkuu!MADAM PRESIDENT - FINAL EPISODE
Tulimzika Janet na kusahau kabisa,
Niliomba likizo ya mwezi mmoja na nikaenda kijijini Mlandizi nilienda maalum kwa ajili ya kusalimia ndugu na jamaa lakini kikubwa nilienda kuweka sawa utaratibu wa Mali zangu hususani nyumba,
Nilimkuta shemeji Aida akiwa pale kwake na kidogo alikuwa amefanya usafi nyumba yake imekaa Vizuri,
"Naona shemeji yake leo umetukumbuka, nikajua umekuwa mwanasiasa Hadi uchaguzi mwingine!"
Alisema shemeji Aida
"Hapana shemeji Aida, unajua Mimi siwezi kukusahau kabisa,
Sasa hebu fanya kwanza ugali samaki aisee"
Nilisema Huku nikikaa pale kwenye sofa,
Tulipiga stori mbali mbali baadae nilimwambia
"Shem nakumbuka Sana msaada wako, Nina zawadi yako kidogo naomba uikubali"
Nilisema Huku nikienda kwenye Gari na kutoa bahasha,
"Shemeji Ile nyumba ambayo mlikaa kule mabatini kuanzia Sasa hivi Ni yako,"
Nilisema Huku nikimpa Ile hati ya nyumba,
Shemeji Aida alifurahi Sana,
Niliona Ile ingeweza kumfaa kwa makazi na hii ya kwake kwakuwa ilikua mjini kabisa angeweza kuipatia wapangaji.
Nilitoka na kumtafuta Jose ambaye naye nilimpa Nyumba yangu nyingine pamoja na Gari dogo,
"Hivi bado Nini tena kwenye maisha kinahitajika?"
Nilijiuliza wakati narudi Dar,
Niliamua kumalizia likizo yangu kwa dada Tatu,
Mbezi
**************
Wakati namalizia likizo walikuja watangazaji Wa Dar TV kufanya mahojiano na Mimi ya kipindi Chao kipya Cha " Mapito"
"Labda wengi wanakufahamu Kama shemeji lakini Kuna mengi sana ambayo hawajui hususani mahusiano yako na marehem Madam President, hebu Leo tuambie ilikuwaje kuwaje yaani"
Alisema mtangazaji
Nilikunywa maji kidogo Kisha nikatabasamu na kuongea..
"Ni kweli Mimi mwenyewe nimetamani Sana kuiweka wazi hii story Sasa tuanze..
Madam President....02 (SOMA SEHEMU YA 1)
Juni 1998
Ilikua jioni nzuri kabisa ambapo sehemu mbali mbali za jiji la Tanga Kuna Hali ya baridi na mvua nyepesi zilikua zimeanza, nikiwa na Rafiki yangu Jacob tulikua mwisho kabisa ya mstari kuingia kwenye Basi la shule tayari kwenda Tanga mjini ambapo kesho yake mashindano ya mkoa umiseta yalikua yanaanza,
Mimi na Jacob Kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wengine tulikua na Furaha kabisa ya kutoka eneo la shule na kwenda kwenye mashindano hayo... Mimi nilikua nacheza mpira wa miguu na Jacob yeye alikua mchezaji mahiri wa mpira wa kikapu..
Tulipenda kumuita Joo tukikatisha jina la Jordan tukimfananisha na mchezaji mahiri Michael Jordan,
Hakika alifanya vizuri lakini pia umbo lake lilimbeba kwani alikua mrefu ...
Kwenye mpira wa miguu Mimi nilicheza Kama winga wa kulia namba 7, pamoja na Mambo mengine lakini nami nilipewa jina la Beckam kutokana na kuwa mahiri katika kucheza mipira iliyokufa,
Tulisogea kwenye basi huku tukishikilia mabegi yetu na Safari ikaanza ...
**************
Ni saa 3 tuliwasili Shule ya Tanga technical ambapo Kama ilivyo kawaida wanafunzi walipiga makelele na Furaha huku wakigombania kushuka,
Ilikua Ni Mara ya kwanza kufika eneo Hilo hivyo nilihakikisha kila kitu kimekaa vizuri kabisa Kisha nikashika begi langu na kusogea kuelekea kwenye mabweni ya wavulana ambayo tulikua tumeandaliwa...
"Dah mwanangu angalia watoto walivyo wazuri kweli hii ndio Tanga! Tutatoka kweli?"
Alisema Jacob akinisukuma bega kidogo,
"Hapana kaka Mimi siwezi kumsaliti Mary kabisa" nilisema huku nikionyesha dalili za kukasirika kidogo tulipanda ngazi na kuelekea vyumbani huku ratiba zingine zikifuata!
*************
MWISHO...[emoji3479]
Kwani mtunzi kasema ina uhalisia?km haikuvutii unafuatilia ya nini?si ufanye mambo mengine?Hii stori hainq uhalisia, ni ya kufukirika sana mpaka inatia uvivu kusoma
Sidhani kama kutoa maoni ni kosa hapa JF, don't take things too personal ndugu, life is to short to overeact on everyrthingKwani mtunzi kasema ina uhalisia?km haikuvutii unafuatilia ya nini?si ufanye mambo mengine?
Nice storyMADAM PRESIDENT 09
Roda alikuja na tukasaidiana kumbeba dada mpaka nje kwenye Gari, roda alienda kuangalia ufunguo kwa bahati akaupata tukaenda hospital mbezi ambapo madaktari walifanikiwa kumrudisha katika Hali yake ya kawaida ..
Ingawa hakuongea chochote alikua akilia tu,
Nilitoka nje huku nivaa kofia na miwani yangu vizuri ili kuepuka kutambulika,
Majira ya saa 5 tulirudi nyumbani
"Dada haya Mambo hayana ukweli na baada ya hapa utasikia Mambo mengi zaidi Ila unanijua mdogo wako sijawahi kuwa mwizi na siwezi kuwa"
Nilisema Kisha nikaenda chumbani...nilichukua kile kibegi changu na vitu vyangu vya muhimu, mfukoni nilibaki Kama na elf 30 hivi nikaondoka!
Sikutaka kuendelea kukaa na sister pale
Nilitoka huku Nikiwa sijui naenda wapi lakini niliona nirudi mlandizi nikachukue pesa na kadi zangu za benki kabla hawajazifunga....
Nilifika mbezi standi na nilipata Gari la mizigo lilikokuwa linaelekea chalinze, niliwapa elfu tano nikapanda na Safari ikaanza jamaa walikua wakipiga story kuhusu Allan
"Aisee Yule dogo noma Sana, millioni 50 usawa huu hata ingekuwa Mimi ningesepa nazo"
Alisema dereva
"Sio milioni 50 unaambiwa dogo alipiga hamsini keshi, Kisha akapiga ishirini za kwenye makaratasi yaani hizo anaenda kuzitoa mbele kwa mbele halafu akapiga na computer Kama tano hivi za ofisi"
Aliongezea mwenzake...
Nilijikuta nilitabasamu tu
Huku nikiendelea kufuatilia hizo stori zao..
"Unaambiwa dogo alikua anawasomea ramani tuu ,unaambiwa dogo hayupo Tena Tanzania yaani"
Dereva aliendelea kuongea..
"Ah huwez kaa bongo aisee, lakini huwez kujua pengine yupo hapa hapa nchini"
Tuliendelea na Safari Hadi tukafika mlandizi nikashuka zangu tayari ilikua saa 9 kasoro nikaingia uchochoroni nikavaa zile nguo za kike na nikatupia wigi juu na Ile miwani nikampigia Simu Jose
"Oya Niko mlandizi njoo hapa kwa msebene chap"
Ni kweli baada ya Muda mfupi Jose alitokea akiwa anaangaza macho huko na huko alifika mpaka pale niliposimama huku akiendelea kutafuta mwishowe alikuja
"Samahani sista hakuna jamaa alikua hapa dakika chache zimepita?"
Aliuliza
"Acha uboya Jose "
Nilisema huku nikitoa lile wigi..
"Hahaha aisee we Ni noma ushafkia kujigeuza demu?"
Jose alisema akiangalia huko na huko, tuliongozana na kupita vichochoro Hadi kwa Jose
Story zilikua zile zile..
Kwa bahati Jose alikua na piki piki tukaenda Hadi kwenye nyumba yangu nikazama ndani na kuchukua kadi zangu za benki kwenye akaunti yangu ya mshahara ilikua na pesa ambazo nilikua nimeomba mkopo Kama milioni 9 hivi na laki 3 ambazo ziliingia Ile siku ya tukio
Nilikua na akaunti yangu nyingine ambayo ndio nilikua naweka akiba zangu pamoja na Kodi za nyumba pamoja na pesa alizokuwa ananipa Janet,
Tulienda kwenye atm nikatoa pesa kwa kiwango kilichowezekana Kisha nikazigawa nilimuachia Ile atm yangu
"Sikiliza utakuwa unatoa kila siku milioni moja mpaka hizi pesa ziishe maana wataifungia siku sio nyingi weka kwenye hii akaunti yangu nyingine na endapo ukatokea umeshikwa nayo waambie mi nilikuachia kitambo hii kadi ulikua unanisimamia ujenzi wa nyumba wakikuuliza nyumba ipi wapeleke Ile misufini Ile ndogo anayokaa Ima,...
Hakikisha hakuna anayejua kuhusu nyumba nyingine zilipo na kule wife alipo,....
Tumia pesa vizuri tutakua tunawasiliana "
Nitajua namna ya kusolve hii kesi,
Sasa kachukue lile box kule mtafute Jacob"
Mimi napotea Broo"
Nilisema huku nikirudishia Lile wigi
Niliingia kwenye uchochoro mmoja Kisha nikavua Lile wigi na zile nguo za kike nikaweka jeans yangu moja hivi na raba Kisha nikatoa wigi lingine ambalo Sasa lilikua na nywele fupi ambazo Ni nyeusi Kama mwanaume tu aliyefuga nywele zake vizuri... nikatupia na miwani nyingine ndogo ingawa sikujitazama kwenye kioo Ila nilijiambia bila shaka naonekana Kama mtalii fulani hivi kutoka Jamaica...
Sasa nilitembea bila Shida kuelekea stand kuu ya magari ilikua Ni saa kumi na moja na dakika kadhaa Pilika Pilika za Maisha zilishaanza
Nilifika stand na kukata tiketi ya kwenda Dar kwa bas la mapema kabisa,
Niliongea Kingereza kibovu Ila walau tuliweza kuelewana na hakika wengi walijua Mimi Ni mtalii kutoka nje ya nchi....
Tulipanda kwenye Basi safari kwenda Dar ikawadia
SAA mbili na nusu tulikuwa kimara kutokana na foleni kidogo saa 3 na dakika kadhaa tulifika ubungo,
Nilishuka haraka kutoka nje ya stendi nikaenda kujichanganya na wapita njia..
Nilifika wanapouza magazeti nikachukua matatu nikayakunja na kuweka kwenye begi...
Nilinunua kofia kadhaa nguo na raba pear nyingine...
Nilipanga kwenda kutafuta sehemu ya mbali kabisa nje ya jiji niishi kwa kuruka ruka mpaka nitakapohakikisha Jacob na Jose wamepata lile box...
*****************
Niliishi kwa siku tatu Huku nikilala sehemu tofauti tofauti..
Vyombo vya habari vilizidi kuripoti habari zangu..
Siku hiyo nikiwa kwenye katika nyumba moja ya kulala wageni nilimuona Janet akiwa anafungua kongamano la kipolisi Kanda maalum ya Dar es saalam katika hotuba yake alikua akiwashambulia polisi kwa kushindwa kukamata wahalifu,
"Mtu kaiba mamilioni ya pesa na vifaa vya ofisini , lakini Hadi Leo IGP hakuna taarifa zozote, huyu mtu Yuko wapi...hii Ni aibu kwa Jeshi la polisi"
Aliongezea Janet
Alisisitiza ndani ya siku tatu niwe nimepatikana..
Bila shaka Janet alikua Ana hofu baada ya Mimi kuwatoroka vijana wake, alikua na hofu kuu,
Lakini zaidi ya yote alikua na hasira ya "kunikosa"
Labda hii ndio lilikua linamuumiza Sana,
"Aliwazalo mjinga ndilo linalomtokea, soon Janet mama utajua mziki wangu"
Sikutaka kuwasiliana na Jose hata kidogo niliwaza pengine atanipa taarifa za mke wangu sikutaka kuonana na mke wangu katika hali hii..
Nilienda dukani na kununua lap top pamoja na modemu Kisha nikaweka Ile laini nyingine nikaanza kufungua jumbe zangu...
Nilipata ujumbe mwingine kutoka kwa mtu niliyehisi atakua Jacob,
"1/5"
Ujumbe ulikua na maandishi kidogo "moja juu ya 5?"
Nilijaribu kuwaza lakini sikuelewa chochote nikaamua kuendelea na kusoma habari mbali mbali na Sasa niliangalia namna nilivyokua nikisakwa na polisi
Hadi wakati nilishalala sehemu tofauti na zote niliingia kwa mawigi tofauti....
Hata hivyo nilijua hii haitadumu muda mrefu haswa Kama Jose akikamatwa au mke wangu akijulikana alipo...
Niliweka Mipango yangu sawa na hatimaye nikaenda benki Nikiwa na wigi langu ambalo nililipachika jina la kijamaika,
Niliangalia salio na kukuta pesa bado za kutosha na kwa Maisha Yale ningeweza kukaa Hata miezi mitatu, Hata hivyo niliona ili niwe huru zaidi nitafute nyumba na kwa akili za haraka nikaona nisiende nje ya mji Sana Ila nitafute uswazi kabisa lakini nyumba itakayokuwa na kila kitu ndani,
Changamoto ilitokea namna ya kupata nyumba,
Mara nilitabasamu baada ya kupata wazo mujarabu kabisa,
Nilitoka pale benki nikiwa na kiasi Cha pesa nilinunua vocha za kutosha nikatafuta gesti nikalala ...
Uzuri wa Dar watu Ni wengi Sana na Kila mmoja alikua na hamsini zake,
Hivyo nilifika na kuomba chumba kwa Kiswahili Cha kuunga unga nikalala huku nikisubiri usiku nifanye dili langu nililopanga...
Majira ya saa Nne na nusu nilivaa begi langu ambalo lilishaanza kuwa zito kutokana na kuendelea kuongeza mizigo..
Nilichukua boda boda mpaka buguruni.
Kisha nikatembea kuelekea wanakosimama madada poa,
Niliangalia angalia mwenye sifa ambazo nilikua nazitaka kutokana na kazi yangu tukapatana Bei nikachukua tax tukaondoka!
*****************
Anasimulia Aida,
Baada ya Jose kuondoka amani ilijereja na alituletea vitu vingi Sana kesho yake asubuhi tulijaribu kumpigia Tena Allan hakupatikana,
Tulimpigia simu Jose akasema tusiwe na wasi wasi,
Mary aligoma kula chakula Cha mchana kabisa na mwishowe aliamua kujifungia ndani,
Nilijikuta naishiwa pozi hatimaye ikafika usiku kwa bahati nzuri Mary alikua chumbani wakati wanatangaza kwenye taarifa ya habari, hivyo Mara baada ya kuona Ile habari, sikujua naanza vipi kumueleza Mary,
Kwa asilimia 50 niliamini zile habari kwanza kutokana na zile nyumba Allan alizokuwa akijenga lakini pia pesa alizokuwa nazo, ingawa Sasa sikujua Kwanini anifiche Jambo Kama Lile au amfiche mkewe,
Ni wakati nawaza ndipo mama Yake Mary akampigia Simu,
Mary alitoka haraka akaja Hadi sebuleni huku akilia..
"Wanamsingizia mume wangu! Wanamsingizia, Allan hawezi kufanya vile jamani..."
Aliendelea kulia
Alilia Sana na ndipo tukaelewa kwanini Jose alikua anatudanganya..
Nilijaribu kumtia moyo Mary
"Angalia kwanza afya yako mpenzi, Sasa hivi tayari Kuna tatizo hebu usiongeze tatizo lingine kwanza"
Nilimwambia,
Tuliendelea kujadili usiku kucha na Mary akakubali kujivika ujasiri..
Mtunzi ni CK Allan
Madam President
Juni 1998
Ilikua jioni nzuri kabisa ambapo sehemu mbali mbali za jiji la Tanga Kuna Hali ya baridi na mvua nyepesi zilikua zimeanza, nikiwa na Rafiki yangu Jacob tulikua mwisho kabisa ya mstari kuingia kwenye Basi la shule tayari kwenda Tanga mjini ambapo kesho yake mashindano ya mkoa umiseta yalikua yanaanza,
Mimi na Jacob Kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wengine tulikua na Furaha kabisa ya kutoka eneo la shule na kwenda kwenye mashindano hayo... Mimi nilikua nacheza mpira wa miguu na Jacob yeye alikua mchezaji mahiri wa mpira wa kikapu..
Tulipenda kumuita Joo tukikatisha jina la Jordan tukimfananisha na mchezaji mahiri Michael Jordan,
Hakika alifanya vizuri lakini pia umbo lake lilimbeba kwani alikua mrefu ...
Kwenye mpira wa miguu Mimi nilicheza Kama winga wa kulia namba 7, pamoja na Mambo mengine lakini nami nilipewa jina la Beckam kutokana na kuwa mahiri katika kucheza mipira iliyokufa,
Tulisogea kwenye basi huku tukishikilia mabegi yetu na Safari ikaanza ...
**************
Ni saa 3 tuliwasili Shule ya Tanga technical ambapo Kama ilivyo kawaida wanafunzi walipiga makelele na Furaha huku wakigombania kushuka,
Ilikua Ni Mara ya kwanza kufika eneo Hilo hivyo nilihakikisha kila kitu kimekaa vizuri kabisa Kisha nikashika begi langu na kusogea kuelekea kwenye mabweni ya wavulana ambayo tulikua tumeandaliwa...
"Dah mwanangu angalia watoto walivyo wazuri kweli hii ndio Tanga! Tutatoka kweli?"
Alisema Jacob akinisukuma bega kidogo,
"Hapana kaka Mimi siwezi kumsaliti Mary kabisa" nilisema huku nikionyesha dalili za kukasirika kidogo tulipanda ngazi na kuelekea vyumbani huku ratiba zingine zikifuata!
*************
Mechi ziliendelea huku Timu yetu ya wilaya ya Korogwe ikiwa kwenye nafasi ya pili baada ya Tanga jiji kwenye mpira wa miguu huku mpira wa kikapu tukiwa tunaongoza kwenye kundi letu,
Tanga jiji walikuwa mbele kwa points mbili dhidi yetu na mechi ya mwisho ndio ambayo ilikua na ushindani Kwani ndio ambayo ingetoa mshindi wa kundi, kwa kuzingatia Hilo mechi yetu ambayo tulicheza dhidi ya Muheza Mimi, Joackim , Abdi na Musa Mwalimu alitupumzisha ili tusipate majeraha kusudi tucheze mechi ya mwisho dhidi ya Tanga jiji,
Kutokana na presha na ushindani wa Timu zote mbili mechi ilibidi kuhamishiwa kwenye uwanja wa mkwakwani na mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa mkoa,
Ilikuwa Ni Mara yangu ya kwanza kucheza kwenye umati mkubwa namna Ile,
Mechi ilianza kwa utulivu na umakini mkubwa huku kila Timu ikiepuka kufanya makosa, hata hivyo kwenye dakika ya 34 hivi wenyeji tanga jiji walipata penati baada ya beki wetu Abdi kucheza rafu ..
Mchezaji wa tanga jiji alicheza penati kwa ufundi wa Hali ya juu na kupelekea Hadi mapumziko tukiwa nyuma kwa goli moja...
Wakati tukiwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo Mwalimu alituambia kuwa tuna nafasi kubwa ya kushinda mchezo hususani Kama tutatumia nafasi za pembeni nakumbuka kocha alinifokea Sana kwa kushindwa kuwasoma mabeki wa Timu pinzani kuwa walikuwa wazito kufanya maamuzi ..
" Allan tumia zile nafasi, wanapoanza kupasiana golini hebu kimbia kwa spidi wanyang'anye mpira usisubiri kuletewa..." Mwalimu James aliongea huku akinitolea macho yake makali...
Nilijikuta natamani turudi uwanjani sekunde Ile ile ..
Wakati tunarudi uwanjani Jacob alikuja pia akinitakia kila la kheri tukarudi uwanjani...
****************
Tulibaki tumetazamana na kuduwaa maana wakati tanga jiji wanaanza mpira moja kwa moja wakapiga mpira mrefu na winga wao wa pembeni akakimbia na kuachia krosi nzuri na wakati Abdi anataka kuokoa akajifunga!
Hakika nilijikuta nakaa chini, macho yangu yalishindwa kutazama jukwaani hata hivyo kapteni wetu Joackim alichukua mpira haraka na kuupeleka katikati Kisha akatupigia makofi ya kututia Moyo,
Hatimaye niliona kocha wetu Mr James nae akitabasamu! Kana kwamba hakuna kitu kilichotokea
Nakumbuka baada ya kuanza mpira Joackim alirudisha nyuma kwa Abdi Tena ambaye alituliza Kisha akapiga shuti kubwa kwenda langoni kwa Tanga jiji,
Wakati beki wa tanga jiji anatuliza mpira
Nilikumbuka maneno ya kocha na hivyo nikakimbia kwa spidi Kali na kumpoka ule mpira Yule beki....nilisikia uwanja mzima ukizizima wakati naelekea golini na kipa aliposogea nikaubetua na kutumbukiza wavuni!
Uwanja mzima ulizizima kwa furaha nilikimbilia mpira golini na kuuweka Kati Kati ya uwanja...
Nilimtazama kocha wangu ambaye alionyesha Hali ya kukasirika naam Mr James ama Mzee wa vise versa tulipenda kumuita alikuwa sio mtu wa kutabirika anaweza kukupongeza unapokosea na akakufokea unapofanya vizuri!
Hatimaye dakika ya 60 tukapata Kona upande wa kulia na nikaenda kuicheza wakati nasogea Abdi alinionyeshea mkono kuwa nimpelekee pale alipo,
Nami bila kusita nikapiga shuti Kali kuelekea langoni na Abdi akaruka kichwa Safi kabisa na kuweka mpira wavuni ..
Mbili mbili!! Tulikumbatiana na kushangilia kwa nguvu huko nje ilikua Ni makelele na polisi ikawalazimu kufanya kazi ya ziada kuweka Hali sawa...
Tuliendelea kushambuliana kwa zamu na wakati zimeongezwa dakika mbili kocha wetu alisema tupande wote kushambulia kwenye dakika ya mwisho kabisa nilipokea mpira nikiwa katikati ya uwanja nikatoa pasi kwa Joackim Kisha nikasogea Tena wakati napokea mpira nikachungulia golini na kumuona kipa wa Tanga jiji amesogea mbele bila kujiuliza maswali nilivuta pumzi ndefu Kisha nikajivuta na kuachia shuti Kali la juu ambalo lilimshinda goli kipa wa Tanga jiji na kutinga moja kwa moja wavuni!
Nilikimbilia nje kwa furaha na wenzangu wakanifuata huku Mwalimu wetu akishangilia kwa nguvu hakika ilikua Ni furaha kubwa Sana,
Hatimaye mechi ikamalizika na tukaibuka washindi kwa goli 3-2,
Bila hiyana nikachaguliwa kuwa mchezaji Bora wa mechi ,
Wakati tunatoka upande wa getini Mkuu wa mkoa alikuja kutusalimia huku akinipongeza Binafsi kwa kunipa mkono
"Hongera Sana Allan"
Sauti nyingine ya kike ilisikika
"Ooh huyu Ni binti yangu Janet, amevutiwa Sana na uchezaji wako"
Alisema Mr Kibwana Mkuu wa mkoa..
"Asante dada Janet" nilisema huku nikimpa mkono
Hata hivyo nilishangaa anashikilia mkono wangu zaidi...
"Uko form ngap?" Aliniuliza
"Form 5" nilijibu
" Ah Mimi Niko form 6" alisema , nimependa unavyocheza unajituma Sana nitakuwa na zawadi yako kesho !
Alisema huku akiniachia mkono wangu,
Tuliondoka Hadi bwenini ambapo ilikua Ni furaha Sana kwetu...
**************
Kesho yake kwenye majira ya saa 4 asubuhi nilipata ujumbe kuwa Kuna mgeni alikuja Jacob..
"Kaka una bonge la zali yaani Yule demu kaja"
"Demu yupi?"
Nilisema
"Ah kaka Yule mtoto wa Mkuu wa mkoa"
Alisema Jacob
"Ah, anasemaje kwani?"
Nilisema nikivaa Kanda mbili zilizokuwepo pale ndani Kisha tukatoka na Jacob
Wakati tunakaribia Janeth alinikimbilia Kisha akanikumbatia
Nilipigwa na mshangao mno huku vijana wengine wakipiga kelele za shangwe pale...
Ni Kama Janet alistuka hivi kwa kuona aibu kidogo Kisha akasema twende nje tukaongee .
"Nimekuletea zawadi yako iko hapo nje" alisema akinivuta mkono Jacob alibaki kuduwaa Kama afuate ama abaki...
Tulitoka nje ya geti Kisha Janet akaenda kwenye Gari akatoka na mfuko mmoja wa Rambo hivi,
'Hii hapa zawadi yako Allan' alisema
"Asante Sana Janet"
Nilisema nikipokea mfuko huo
Tulisogea mpaka uwanjani ambapo wanafunzi wengine walikua wanaendelea na mazoezi mbali mbali Kisha tukakaa chini,
Nakumbuka Janet aliniambia wazi wazi kuwa ananipenda Sana na anatamani tuwe wapenzi...
Hata Hivyo kiuhalisia sikuwa na upendo wowote kwake nikilinganisha na jinsi nilivyokuwa nikimpenda Mary mpenzi wangu ambaye nae alikua kidato Cha 5 pale mombo sekondari nilimlinganisha na Janet nikaona Janet akiachwa mbali Sana, nilitamani kumueleza Janet kuwa hanivutii hata kidogo Ila nilijikuta nashindwa nikabaki kimya tu..
"Tafadhali niambie unanipenda Allan" Janet alinistua katika mawazo yangu hayo...
"Yaani Janet nashindwa niseme Nini ngoja kwanza nirudi bwenini" nilisema Kisha nikasimama Janet aliahidi kuja Tena kesho asubuhi,
Nilirudi ndani kwa unyonge na kukuta Jacob akiwa na wanafunzi wengine wakinisubiri
Wote waliponiona walinikimbilia na kuninyang'anya ule mfuko
"Dah mwanangu umepata bonge la zali, mtoto wa Mkuu wa mkoa kakuganda, dah bonge la zali" walisema huku wakifungua ule mfuko na kutoa track suit nzuri Sana
"Kwahyo mnasemaje Sasa kuhusu huyu demu?" Niliwauliza
"Ohoooo ushaanza Tena kuuliza ujinga, huyo unatakiwa umalize we vipi?" Jacob alidakia huku wenzake wakiongezea , Kama ujuavyo msomaji Basi akili za wanafunzi wa kiume nikajikuta nalewa ujinga wao hivyo siku iliyofuata nilimkubalia Janet huku moyoni nikiwa Sina hata chembe ya upendo kwake,
***********************
Tulirudi shuleni na Janet alizidi kuniandikia barua na yeye alimaliza kidato Cha sita na akajiunga na chuo kikuu Cha Dar es salaam akisomea Mambo ya utawala,
Mimi nilimaliza kidato Cha sita na kujiunga na chuo Cha ualimu Marangu ,nikisomea stashahada ya ualimu...
Niliendelea kuwasiliana na Mary ambaye yeye alikua amejiunga na Masomo ya udaktari katika chuo Cha kcmc Moshi hivyo Mara nyingine siku za weekend tuliwasiliana na wakati mwingine yeye angefika chuoni au Mimi ningekwenda hospitalini hakika tulipendana Sana na tulishaweka Mipango ya kuoana..
Ni muda mrefu ulipita bila kuwa na mawasiliano na Janet , Mara ya mwisho alinitumia barua nikiwa namalizia kidato Cha sita na kwa makusudi sikujibu Ile barua yake ili kupoteza mawasiliano kabisa, kwa ufupi tuseme nilisahau kila kitu kuhusu Janet,
*****************
Novemba 2004
"Walimu Kama nilivyosema atakuja hapa waziri wa elimu na jopo lake hivyo tuhakikishe Mambo yanakuwa vizuri kabisa"
Mkuu wa Shule yetu Bwana Alfred alikua anatoa taarifa fupi kuhusu ugeni ambao ungefika shuleni kwetu Segera sekondari,
Ndio waziri wa elimu alikua na ziara ya kikazi mkoani Tanga na katika sehemu ambazo angepitia ilikua Ni kwenye shule yetu kuja kuzindua Jengo la maabara,
Ni miaka miwili Sasa ilikuwa imepita Tangu niajiriwe Rasmi kuwa Mwalimu katika shule hii ya segera Mara baada ya kumaliza mafunzo yangu ya ualimu chuo Cha Marangu Moshi,
Mary alikua na miezi mitatu Sasa akiwa ameajiriwa hospital ya Magunga wilayani Korogwe, na pia huu ilikuwa Ni mwaka wetu mmoja tukiwa ndani ya ndoa,
Tayari tulikua na mtoto mdogo wa miezi miwili
Mary alikua na likizo yake ya uzazi.
Msafara wa magari ulikua unaingia Sasa shuleni kwetu Mimi niliendelea na kipindi darasani Hadi pale tulipoitwa kukusanyika,
Ni wakati naangaza macho huku na kule ndipo macho yangu yakamuona Janet!
Ndio Ni yeye akiwa ananong'onezana Jambo na waziri wa Elimu nilirudi nyuma na kujichanganya na walimu wenzangu ili kusudi nisionekane ..
Waziri alitoa hotuba yake Kisha akawatambulisha aliongozana nao
"Huyu Ni madam Janet yupo ofisi ya Raisi akishughulika na Mambo ya utawala Bora, nadhani mlisikia kuhusu uteuzi wake hivi karibuni, na Yule Ni Bwana Joeli Ni mhasibu wa wizara na....."
Masikio yangu yalishindwa kuamini yanachokisikia
Ni kweli nilisikia kuhusu uteuzi katika ofisi ya Raisi , lakini hata sikuweza kuhisi kama ndie Yule Janet ninayemfahamu
Waliongea mengi na ilipofika zamu ya Janet aliongea Mambo machache lakini alipongeza Sana walimu kwa kazi nzuri ya kufundisha na kuwaongoza wanafunzi....wakati anamaliza aliomba Tena kuongea kitu alichokuwa amesahau...
"Jamani ngoja nisisahau nimeona kitu Cha tofauti kwenye hii shule, wakati napitia mazingira nimeona Kuna ubao mmoja hivi pale Kuna gazeti la shule na wanafunzi wanaandika Hadithi, wanachora vikatuni na kuandika makala mbali mbali, Ni kitu ambacho hatujakiona kabisa kwenye shule Nyingine hivyo kipekee kabisa nataka nimpongeze huyo Mwalimu aliyesimamia Hilo gazeti ,Mkuu wa Shule tafadhali niitie huyo Mwalimu" Janet alisema huku akifungua pochi yake,
"Mwalimu Allan tafadhali huku mbele"
Mkuu wangu Bwana Alfred aliniita kwa Mara ya kwanza nilitamani litokeee shimo ghafla niingie..
Nilitamani kumwambia Mkuu asinitaje Ila kwa ujasiri wa ajabu nikajikuta nasogea mbele,
"Liwalo na liwe" nilijisemea nikisogea mbele
kupiga hatua moja zaidi mpaka sehemu Mkuu wa shule aliponionyesha kusimama wanafunzi walipiga makofi nilitulia tuli na macho yetu yakagongana Mimi na Janet,
Ni Kama alishikwa na mshangao na kigugumizi Cha ghafla hivi,
"You?" Alisema akinipa Mkono
"Yeah, it's me" nilisema ,
"Mwalimu unafanya kazi nzuri Sana na kwakweli pokea hii zawadi," alisema huku akitoa laki moja kwenye mkoba wake,
Niliipokea Kisha nikarudi zangu kwa wenzangu,
Mapigo ya moyo yalikua yankwenda Kasi sikutegemea kuonana na hiki kiumbe kabisa,
Nilikumbuka barua yake ya mwisho Janet alisema hawezi kuolewa na mtu mwingine zaidi yangu , na japokuwa eti nimekaa kimya lakini atanitafuta na ole wangu anikute na mwanamke mwingine!
Wakati macho yetu yanakutana hakika Ni Kama alikua anasema "kumbuka Ile barua yangu kenge wewe!"
Tulitoka pale asembly na kwenda maabara ambako waziri alifungua Lile Jengo Kisha akapata nafasi ya kuongea na wajumbe wa bodi na walimu,
Janet Mara kwa Mara alikua akinitupia jicho huku akiendelea kuandika Mambo kadhaa kwenye notebook yake,
Baada ya kumaliza shughuli waziri na jopo lake waliaga na kuondoka ,
*****************
Miezi mitatu baadae
Nikiwa nimetoka kwenye kipindi nilikua nanawa mikono ili niingie kwenye ofisi ya walimu kupata chai ndipo Mkuu aliniita
Hivyo badala ya kuingia ofisi ya walimu nikatoka na kuzunguuka nyuma ya Jengo ambapo ndipo ilipokuwa ofisi ya Mkuu wa Shule,
"Sijui niseme Nini, lakini maisha ndivyo yalivyo, Sina namna" alianza Mkuu wa shule kwa sauti ya huzuni
"Mkuu mbona sielewi" nilisema nikikaa vizuri kwenye Kochi
Mr Alfred hakuongea zaidi alifungua faili moja pale mezani Kisha akatoa barua moja na kunikabidhi
Nilipokea na kuifungua haraka
Niliangalia kichwa Cha barua haraka
Yah : kuteuliwa kuwa afisa michezo na utamaduni wilaya ya Pwani
Niliifunga haraka kisha nikamwangalia Mkuu wa Shule ambaye nae aliniangalia tu,
"Ndio hivyo hongera Sana" alisema huku akitabasamu...
"Duh" nilisema huku nikichukua Ile barua na kutoka nje nilifika ofisini nikanywa chai Kisha nikatoka nje kwenye kivuli nikaagiza kiti nikakaa,
Nilipitia Ile barua Tena na ilionyesha wazi imetoka utumishi na nilitakiwa kuripoti kituo changu ndani ya siku 14 zijazo na nitagharamiwa kila kitu niliwaza na kuwazua na mwishowe nilibaini Lazima Janet atakuwa na mkono wake katika Hili Jambo.
Baada ya wiki moja nilifika Pwani kuripoti na nikaonyeshwa ofisi yangu pamoja na muongozo wa majukumu na zaidi ya yote Bwana Luda afisa michezo aliyekuwa hapo alinipokea na kunielekeza Mambo muhimu kwa ufupi kwani alipaswa kuondoka kesho yake kwenda kigoma ambapo ndipo alipangwa kituo kipya baada ya aliyekuwepo huko kustaafu.
Kwa ufupi hakukuwa na majukumu mengi Kama kufundisha darasani ilikua Ni kufuatilia masuala ya michezo wilayani hususani kwenye shule.
Nilirudi kuhamisha familia yangu na kuaga ndugu na jamaa Kisha nikahamia Rasmi Pwani Kama afisa michezo na utamaduni wilaya.
Itaendelea huko kwenye comment
Lakini bado umepita nayo shwaa hd mwisho,hakika story tamu sn[emoji23]Katika story yenye uhalisia wa chini niliyopata kuisoma jamii forum basi nii hii, story ya kijinga kabisa utorakaji wa kijinga na nguvu ya rais ya kijinga sana humu