MPANGAJI 11
By CK Allan
Esta sasa alishatembelea karibia miradi yote na kuona kila kitu ambacho kinaendelea
siku hiyo usiku walikuwa wanajadiliana namna ya kurudi kwa kasi katika kuhakikisha kisasi kinalipwa ipasavyo
βnina wazo Seleβalisema Esta
βtutengeneze historia ya Sele Selemani Seleβ alianza Esta
βsijakuelewaβ
βSikiliza Sele, kwanza tutengeneze uhuru wako kwanza, uwe huru kutembea popote wakati wowote na saa yoyote, halafu ujikite katika biashara mojawapo ambayo utaichagua uindeleze ukue nayo kabisa na kutambulika duniani kote, halafu ukishajulikana sasa ndio itakuwa rahisi wewe kuongea chochote na kikasikilizwa na Dunia, kuliko ilivyo sasaβ
βmhh una mpango gani?β aliuliza sele
βkwasasa una vitambulisho vyote, lakini huna shule ya msingi wala sekondari wala chuo ulichosoma, nina wazo kwanza tutafute shule ya msingi, baadae Sekondari halafu huko juu tutajuaβ alisema Esta
βbonge la wazo ila kumbuka tunakimbizana na Muda, na inabidi mzee akimaliza tu muda wake kesi iishe, kwasababu kama ujuavyo sasa hivi hakuna mahakama itakubali kupokea kesi yoyote ya mke wa Raisi aliye madarakani, hakuna hata sehemu moja unaweza kufungua kesiβ alisema Sele huku akichukua simu yake,
βuncle, huna mtu unafahamiana nae pale wizarani au baraza?β alisema baada ya simu kupokelewa
βnina kijana pale nilishawahi kufanya nae kazi kipindi Fulani ila naweza kuipata namba yake baada ya nusu saa, vipi?β alisema mr K
βbasi fanya mpanga kesho tukutane naeβ
Waliweka miadi vizuri nakesho wakakutana na mtu huyo wa baraza na kuweka nae utaratibu
βinawezekana sana kwahiyo umri wa sele inabidi awe amemaliza shule kati ya mwaka 1997-1999 hivi, mnapendekeza awe amemaliza mkoa gani,
βhapa dar s salaamβ walisema kwa pamoja
βokay sasa hii kazi itachukua wiki mbili kwasababu inahitaji umakini tusije kumpa shule ambayo kipindi hicho ilikua hata haipo, kama unavyojua ni kizazi cha google hikiβ alisema Yule jamaa aliyeonekana kuwa mtaalamu wa βdiliβ kama hizo
βsasa kuhusu cheti cha form four inabidi kutafuta shule ambayo mkuu wake wa shule amefariki, yaani hayupo kabisa hapa duniani! Ili tunapochomeka jina basi mambo yote yatakuwa vizuri kabisa!β alisema Yule jamaa huku akipiga funda la juice
βsikia lengo letu sisi tunataka mtu anapotafuta taarifa hizi za mfanyabiashara maarufu Sele basi aweze kuona alisoma wapi hivyo tu, tunakutegemea sana ndugu yetu, si unajua wakati mwingine tunakosa Dili kutokana na Vyeti tuuβ alisema Mr K akitabasamu
βsikilizeni hapa ndio kwenyewe ndugu zangu, siwezi kuwaangusha sema tu kama mjuavyo kazi hii sifanyi mwenyewe niko na wenzangu kwahiyo sijajua mmejipanga vipi!β alisema Yule jamaa sasa akiweka miwani yake vizuri
βwewe unataka tukupe ngap?β aliuliza Sele ambaye alikua kimya muda wote
βkwa primary kikubwa ni matokeo ya mwisho na vyeti vya primary ni rahisi tu, cheti cha form four ndio kidogo kina mlolongo kwasababu inabidi kuonyesha pia matokeo ya form two kwahiyo kuna kamzunguuko kidogo kuwapoza watu hapa na pale n.k, sasa kwasababu najua sisi sote tunatafuta, toeni million 6 hii nimewasaidia sana ndugu zanguβ alisema Yule jamaa
βna kazi yote inaweza kukamilika kwa lini?β aliuliza Mr k
βhaizidi wiki mbili kama kila kitu kikiwa sawa!β
βbasi jioni utapata milioni 4 na ukimaliza kazi tutakupa iliyobaki tunakushuru sana tukiamini mambo yatakaa sawa!β
Waliagana kisha wakaendelea na mazungumzo yao huku Nyuma kati ya Mr K na Sele
β ni wazo zuri sana, baada ya kupata vyeti hivi na kila mtu akijiaminisha Sele ndio Sele, na mheshimiwa atakuwa ameshamaliza muda wake wa kukaa madarakani na sisi tutaibuka pale juuβ alisema Mr K akimgeukia Sele
βsasa ni biashara gani ambayo unataka kupanda nayo!β aliuliza Mr K
β kwakuwa tayari nilishasomea mambo ya mifumo, tufungue kamupuni ndogo ya mifumo ya ulinzi wa kiteknolojia ambapo tutadeal na kufunga mifumo kwenye majengo, hotel, benk, n.k pamoja na kuuza vifaa vya ulinzi nadhani kwa Tanzania bado hakuna kampuni maalum ya kudeal na vitu hiviβ alisema Sele na mr k alikubalina na wazo lake na sasa kampuni ikawa tayari imeanzishwa kwenye makaratasi
Hatimaye baada ya mwezi mmoja kampuni ilifunguliwa na kupata usajili wa awali kampuni illitwa βWE4Uβ ambapo ilihusika na kufunga vifaa vya ulinzi kwenye majengo na vile vile kuuza spea za vifaa vya ulinzi wa kiteknlojia,
kutokana na uhitaji wa vitu hivyo haikuchukua muda mrefu kampuni yake ikaanza kufahamika na kuanza kutumika kufunga vifaa katika majengo mbali mbali. Sasa ungeweza kukuta wakipokea oda nyingi kutoka sehemu tofauti, kama isingekuwa kufunga mifumo basi kuuza vifaa ,
pamoja na kuwa ilikua ni sehemu ya kupandia tu kufikia ndoto zao lakini na Faida kubwa pia Sele aliipata kwani alitanua wigo na kufanya kazi na makampuni mengine ya vifaa ndani na nje ya nchi
kila ambavyo mama Mwajuma alikua akitaka kumtembelea mwanae Esta, walikwepesha na wao wakaamua kumtembelea, hawakutaka kabisa mama Mwajuma ajue maisha halisi ya Sele kabla hawajaweka sawa hivyo baada ya kila kitu kukamilika siku hiyo walitaka kumfanyia mama Mwajuma Saprise sasa
βnadhani ni wakati sahihi sasa tumkaribishe mama!β alisema Esta maana kila siku anataka kuona tunapokaa!
βhaha ni kweli ni mwaka kasoro sasa nadhani inabidi tufanye hivyo!β alisema Sele huku akimalizia kuvaa viatu vyake,
βsikia kuna mchoro mmoja wa benki ya Acb tawi la mwenge naenda kuchukua wanataka tuwafungie cctv camera, nikitoka hapo nitaenda ofisini nitapitia Sokoni pia, wewe mfuate mama si ushazoea sasa hivi kwenye mataa!β alisema Sele akitabasamu
βhaha hakuna shida kabisa sasa hivi napiga gia hatari!β alisema Esta kwani tayari nae alikua na gari yake aina ya βvitzβ
Baada ya Sele kuondoka Esta nae alimalizia kuandaa chakula na kukihifadhi vizuri kisha akamfuata mama mwajuma, kwa muda wa saa 4 asubuhi foleni haikua kubwa sana na masaa mawili tu yalitosha yeye kufika mwananyamala na kisha kuingia vichochoroni mpaka nyumbani kwao kwa zamani, alipaki gari yake nje kisha akaingia ndani na kumkuta mama yake na wapangaji wengine kama kawaida, aliwasalimia na eye akasogea kukaa kwenye mkeka
βwe mwanamke nikajua umeshajiandaa jamani, kumbe tunaongea kwenye simu nikajua umeshamaliza!β Esta alianza kulalamika
βsasa mimi nikajua utakuja jioni ngoja nijiandae harakaβ alisema mama Mwajuma akinyanyuka na kujiandaa
βhaya sasa na hili wigi mpaka tutembee mpaka steni si nitakuwa nimeloa jasho mama Mwajuma mimi!β alisema
βmama utembee wapi jamani nimekuja na Gari!β alisema Esta
βkha! Gari, wewe umekuja na Gari?β alisema mama Mwajuma sasa huku akitoka mbio nje , ilibidi wapangaji wengine watoke kuchungulia
βjamani mke wa Sele, amekuja na gari loh!β
Esta sasa alikua anajizuia kucheka lakini alijikaza na kufungua mlango wa gari
βhuu mkanda unafungwa hivi, halafu unavuta hapa!β alisema Esta akimfunga mkanda mama Mwajuma na safari ikaanza
βkwahiyo huyo mumeo Sele amekununulia gari na wewe unajua kuendesha gari? Mbona kama niko ndotoni mimi mama Mwajuma!β
βmama bhana hujaacha tu vituko vyakoβ alisema Esta sasa wakiingia kwenye barabara kubwa ya lami
Walifika nyumbani kwa Sele na mama Mwajuma alishikwa na kigugumizi baada ya kuona nyumba nzuri vile ya sele
Alikua na maswali mengi kuliko majibu alikaa pale hadi Sele alipowasili na kuingia ndani ambapo alimsalimia kwa ufupi kisha akaingia chumbani na kubadili nguo na kisha akarudi tena Sebuleni
βaah mama Mama karibu sana sisi tupo hapa jamani, mambo yalikua mengi na kazi kila tukisema uje tunajikuta wote tuko bize, sasa tulipopata hii nafasi ndio tukaona uje upaone nyumbani mamaβ alisema sele baada ya kukaa kwenye Sofa
βsasa mwanangu maisha haya mmeyapata lini kwa haraka hivi mwanangu? Eeh, mbona hujawahi kusema unaishi vizuri hivi mpaka watu wakawa wanakudharau sele!β alisema mama mwajuma kama kwa kufoka hivi!
βmama Kwakweli namshukuru sana Esta, unajua kipindi kile nilikua nafanya biashara ndogo ndogo za kuuza vifaa vya komputa, sasa nilipokua na mwenzangu huyu kama unavyojua