Hadithi: Mpangaji

Hadithi: Mpangaji

MPANGAJI 11

By CK Allan
Esta sasa alishatembelea karibia miradi yote na kuona kila kitu ambacho kinaendelea
siku hiyo usiku walikuwa wanajadiliana namna ya kurudi kwa kasi katika kuhakikisha kisasi kinalipwa ipasavyo
“nina wazo Sele”alisema Esta
“tutengeneze historia ya Sele Selemani Sele” alianza Esta
“sijakuelewa’
“Sikiliza Sele, kwanza tutengeneze uhuru wako kwanza, uwe huru kutembea popote wakati wowote na saa yoyote, halafu ujikite katika biashara mojawapo ambayo utaichagua uindeleze ukue nayo kabisa na kutambulika duniani kote, halafu ukishajulikana sasa ndio itakuwa rahisi wewe kuongea chochote na kikasikilizwa na Dunia, kuliko ilivyo sasa”
“mhh una mpango gani?” aliuliza sele
“kwasasa una vitambulisho vyote, lakini huna shule ya msingi wala sekondari wala chuo ulichosoma, nina wazo kwanza tutafute shule ya msingi, baadae Sekondari halafu huko juu tutajua” alisema Esta
“bonge la wazo ila kumbuka tunakimbizana na Muda, na inabidi mzee akimaliza tu muda wake kesi iishe, kwasababu kama ujuavyo sasa hivi hakuna mahakama itakubali kupokea kesi yoyote ya mke wa Raisi aliye madarakani, hakuna hata sehemu moja unaweza kufungua kesi” alisema Sele huku akichukua simu yake,
“uncle, huna mtu unafahamiana nae pale wizarani au baraza?” alisema baada ya simu kupokelewa
“nina kijana pale nilishawahi kufanya nae kazi kipindi Fulani ila naweza kuipata namba yake baada ya nusu saa, vipi?” alisema mr K
“basi fanya mpanga kesho tukutane nae”
Waliweka miadi vizuri nakesho wakakutana na mtu huyo wa baraza na kuweka nae utaratibu
‘inawezekana sana kwahiyo umri wa sele inabidi awe amemaliza shule kati ya mwaka 1997-1999 hivi, mnapendekeza awe amemaliza mkoa gani,
“hapa dar s salaam” walisema kwa pamoja

“okay sasa hii kazi itachukua wiki mbili kwasababu inahitaji umakini tusije kumpa shule ambayo kipindi hicho ilikua hata haipo, kama unavyojua ni kizazi cha google hiki” alisema Yule jamaa aliyeonekana kuwa mtaalamu wa “dili” kama hizo
“sasa kuhusu cheti cha form four inabidi kutafuta shule ambayo mkuu wake wa shule amefariki, yaani hayupo kabisa hapa duniani! Ili tunapochomeka jina basi mambo yote yatakuwa vizuri kabisa!” alisema Yule jamaa huku akipiga funda la juice
“sikia lengo letu sisi tunataka mtu anapotafuta taarifa hizi za mfanyabiashara maarufu Sele basi aweze kuona alisoma wapi hivyo tu, tunakutegemea sana ndugu yetu, si unajua wakati mwingine tunakosa Dili kutokana na Vyeti tuu” alisema Mr K akitabasamu
“sikilizeni hapa ndio kwenyewe ndugu zangu, siwezi kuwaangusha sema tu kama mjuavyo kazi hii sifanyi mwenyewe niko na wenzangu kwahiyo sijajua mmejipanga vipi!’ alisema Yule jamaa sasa akiweka miwani yake vizuri
“wewe unataka tukupe ngap?” aliuliza Sele ambaye alikua kimya muda wote
“kwa primary kikubwa ni matokeo ya mwisho na vyeti vya primary ni rahisi tu, cheti cha form four ndio kidogo kina mlolongo kwasababu inabidi kuonyesha pia matokeo ya form two kwahiyo kuna kamzunguuko kidogo kuwapoza watu hapa na pale n.k, sasa kwasababu najua sisi sote tunatafuta, toeni million 6 hii nimewasaidia sana ndugu zangu” alisema Yule jamaa
“na kazi yote inaweza kukamilika kwa lini?’ aliuliza Mr k
“haizidi wiki mbili kama kila kitu kikiwa sawa!”
“basi jioni utapata milioni 4 na ukimaliza kazi tutakupa iliyobaki tunakushuru sana tukiamini mambo yatakaa sawa!”
Waliagana kisha wakaendelea na mazungumzo yao huku Nyuma kati ya Mr K na Sele
“ ni wazo zuri sana, baada ya kupata vyeti hivi na kila mtu akijiaminisha Sele ndio Sele, na mheshimiwa atakuwa ameshamaliza muda wake wa kukaa madarakani na sisi tutaibuka pale juu” alisema Mr K akimgeukia Sele
“sasa ni biashara gani ambayo unataka kupanda nayo!” aliuliza Mr K
“ kwakuwa tayari nilishasomea mambo ya mifumo, tufungue kamupuni ndogo ya mifumo ya ulinzi wa kiteknolojia ambapo tutadeal na kufunga mifumo kwenye majengo, hotel, benk, n.k pamoja na kuuza vifaa vya ulinzi nadhani kwa Tanzania bado hakuna kampuni maalum ya kudeal na vitu hivi” alisema Sele na mr k alikubalina na wazo lake na sasa kampuni ikawa tayari imeanzishwa kwenye makaratasi

Hatimaye baada ya mwezi mmoja kampuni ilifunguliwa na kupata usajili wa awali kampuni illitwa “WE4U” ambapo ilihusika na kufunga vifaa vya ulinzi kwenye majengo na vile vile kuuza spea za vifaa vya ulinzi wa kiteknlojia,
kutokana na uhitaji wa vitu hivyo haikuchukua muda mrefu kampuni yake ikaanza kufahamika na kuanza kutumika kufunga vifaa katika majengo mbali mbali. Sasa ungeweza kukuta wakipokea oda nyingi kutoka sehemu tofauti, kama isingekuwa kufunga mifumo basi kuuza vifaa ,
pamoja na kuwa ilikua ni sehemu ya kupandia tu kufikia ndoto zao lakini na Faida kubwa pia Sele aliipata kwani alitanua wigo na kufanya kazi na makampuni mengine ya vifaa ndani na nje ya nchi
kila ambavyo mama Mwajuma alikua akitaka kumtembelea mwanae Esta, walikwepesha na wao wakaamua kumtembelea, hawakutaka kabisa mama Mwajuma ajue maisha halisi ya Sele kabla hawajaweka sawa hivyo baada ya kila kitu kukamilika siku hiyo walitaka kumfanyia mama Mwajuma Saprise sasa
“nadhani ni wakati sahihi sasa tumkaribishe mama!” alisema Esta maana kila siku anataka kuona tunapokaa!
“haha ni kweli ni mwaka kasoro sasa nadhani inabidi tufanye hivyo!” alisema Sele huku akimalizia kuvaa viatu vyake,
“sikia kuna mchoro mmoja wa benki ya Acb tawi la mwenge naenda kuchukua wanataka tuwafungie cctv camera, nikitoka hapo nitaenda ofisini nitapitia Sokoni pia, wewe mfuate mama si ushazoea sasa hivi kwenye mataa!” alisema Sele akitabasamu
“haha hakuna shida kabisa sasa hivi napiga gia hatari!” alisema Esta kwani tayari nae alikua na gari yake aina ya “vitz”
Baada ya Sele kuondoka Esta nae alimalizia kuandaa chakula na kukihifadhi vizuri kisha akamfuata mama mwajuma, kwa muda wa saa 4 asubuhi foleni haikua kubwa sana na masaa mawili tu yalitosha yeye kufika mwananyamala na kisha kuingia vichochoroni mpaka nyumbani kwao kwa zamani, alipaki gari yake nje kisha akaingia ndani na kumkuta mama yake na wapangaji wengine kama kawaida, aliwasalimia na eye akasogea kukaa kwenye mkeka
“we mwanamke nikajua umeshajiandaa jamani, kumbe tunaongea kwenye simu nikajua umeshamaliza!” Esta alianza kulalamika
“sasa mimi nikajua utakuja jioni ngoja nijiandae haraka’ alisema mama Mwajuma akinyanyuka na kujiandaa
‘haya sasa na hili wigi mpaka tutembee mpaka steni si nitakuwa nimeloa jasho mama Mwajuma mimi!” alisema
“mama utembee wapi jamani nimekuja na Gari!” alisema Esta
“kha! Gari, wewe umekuja na Gari?” alisema mama Mwajuma sasa huku akitoka mbio nje , ilibidi wapangaji wengine watoke kuchungulia
“jamani mke wa Sele, amekuja na gari loh!”
Esta sasa alikua anajizuia kucheka lakini alijikaza na kufungua mlango wa gari
“huu mkanda unafungwa hivi, halafu unavuta hapa!” alisema Esta akimfunga mkanda mama Mwajuma na safari ikaanza
“kwahiyo huyo mumeo Sele amekununulia gari na wewe unajua kuendesha gari? Mbona kama niko ndotoni mimi mama Mwajuma!”
“mama bhana hujaacha tu vituko vyako” alisema Esta sasa wakiingia kwenye barabara kubwa ya lami

Walifika nyumbani kwa Sele na mama Mwajuma alishikwa na kigugumizi baada ya kuona nyumba nzuri vile ya sele
Alikua na maswali mengi kuliko majibu alikaa pale hadi Sele alipowasili na kuingia ndani ambapo alimsalimia kwa ufupi kisha akaingia chumbani na kubadili nguo na kisha akarudi tena Sebuleni
“aah mama Mama karibu sana sisi tupo hapa jamani, mambo yalikua mengi na kazi kila tukisema uje tunajikuta wote tuko bize, sasa tulipopata hii nafasi ndio tukaona uje upaone nyumbani mama” alisema sele baada ya kukaa kwenye Sofa
“sasa mwanangu maisha haya mmeyapata lini kwa haraka hivi mwanangu? Eeh, mbona hujawahi kusema unaishi vizuri hivi mpaka watu wakawa wanakudharau sele!” alisema mama mwajuma kama kwa kufoka hivi!
“mama Kwakweli namshukuru sana Esta, unajua kipindi kile nilikua nafanya biashara ndogo ndogo za kuuza vifaa vya komputa, sasa nilipokua na mwenzangu huyu kama unavyojua
 
MPANGAJI 12
wenzetu hawa walimu wanakopeshwa basi akaenda huko akachukua mkopo na tukaingiza kwenye biashara zetu basi Mungu akajalia mama!”alisema Sele
“ooh kwakweli mwanangu hongereni sana kwakweli umetutoa kimaso maso kwakweli” alisema mama Mwajuma
Sele aliingia zake chumbani akiwaacha mama na mwanae hapo ambapo jioni walimsindikiza tena mpaka nyumbani
Sasa mama Mwajuma hakutaka kulala usiku ule aliwakusanya wapangaji wenzake na kuwaelezea huko nyumbani kwa Esta
“nakuambia ni Ikulu, ni ikulu!” alisema mama mwajuma akikazia “umbea” wake kama ilivyokuwa kawaida yake
----------------------------------------------------------------
BAADA YA MIAKA KADHAA
Uchaguzi nchini Tanzania ulimalizika salama na Mzee Lukas Tuppa akakabidhi kijiti kwa aliyekuwa waziri Mkuu wake Bwana Jeremiah Mdee,
Mara baada ya kustaafu Mzee Tuppa tofauti na watangulizi wake, aliamua kubaki jijini Dar es salaam, tayari Joan na Jesca walishakuwa mawaziri katika serikali yake huku wakitajwa kama mawaziri wadogo zaidi kuwahi kutokea Tanzania, Bwana Tuppa aliongoza kwa miaka 20 , tofauti kabisa na watangulizi wake, tetesi zilikua zilisambaa kuwa mkewe mama Joan ndie aliyekuwa akimlazimisha Mzee kuendelea kubaki madarakani
Alirudi nyumbani kwake Masaki na familia akijinasibu kuwa anaenda kuwa mfugaji wa kuku kumalizia wakati wake wa kuishi hapa duniani pamoja na “kucheza na wajukuu” kama viongozi wengi walivyopenda kuongezea hayo maneno wanapohojiwa
Mzee Tuppa alitengana na mkewe Rasmi siku alipogundua alimuua mke mke mwenzake mama Doreen,
Kilichoonekana kwa nje ilikua ni maigizo tu na kamwe hawakuwahi kulala tena chumba kimoja toka siku ile
Kila mmoja alikua na chumba chake au tuseme ‘nyumba yake” walinzi wake wa karibu walikua wanajua hayo yote lakini wakati walipokuwa wakitoka kwenda kwenye ziara za kikazi Mzee Tuppa na mkewe walikuwa wakishikana mikono na kutabasamu
Mara kadhaa mama Joan alijaribu kumuomba msamaha mume wake huyo lakini mzee Tuppa alikataa kata kata
“wewe ni muuaji Janet!, unathubutuje kumuua mama na mtoto kinyama kiasi kile kwa sababu za kijinga kama zile?” alikua anafoka mzee Tupa
“wangefanya nini wale eeh? Wangeweza kuzuia mimi kuwa Raisi? Ningekuwa tu! Walishaelewa ona umekatisha ndoto za kijana wangu! Mimi nitamtazama vipi huko kuzimu? Nakuuliza wewe?” Sasa Mr Tuppa alikuwa akikumbuka hayo yote akiwa ameshika picha ya mke wake mama Doreen waliyopiga wakati akiwa mhadhiri pale UDSM
“ twende mzee muda wa kipindi” ilikua ni sauti ya mlinzi wake Joshua ambaye sasa alikua akimsindikiza katika Televisheni ya Taifa ambapo kulikua na kipindi maalum cha “JIFUNZE KWAKE” ambacho kilikua maalum kuwahoji watu maarufu na kisha kupoke maswali machache kutoka kwa watazamaji mubashara baada ya kuwasili na ukaguzi kufanyanyika sasa mzee Tuppa alivalishwa kifaa maalum cha kukuzia sauti na kisha akaenda kukaa kwenye sofa kubwa iliyokuwa pembeni ya kamera nyingi nyingi
“habari mtazamajij wetu wa Televisheni yako ya taifa kama tulivyokuwa tukikujuza wiki hii nzima kuwa tutakuwa na Raisi mstaafu mheshimiwa Lukas Kaijage Tuppa, basi tayari ameshafika hapa studio tayari kabisa kukuletea mahojiano haya ya masaa mawili mimi ni mtangazaji wako Faraja Walter, na tutarejea baada ya muda mfupi!’
Kipindi hiki kilikua kipindi pendwa sana tayari watu wengi walikua wakifuatilia mahojiano hayo Sele akiwa nyumbani kwake na mke wake nao waliacha kula na kukodoa macho kwenye tv kuhakikisha wanasikia kila neno kutoka kwa mzee
“hebu sasa tuambie mheshimiwa unaona tofauti gani kati ya kuwa ofisini na ulivyo sasa nyumbani ukicheza na wajukuu?” aliuliza mtangazaji
“tofauti ipo kubwa sana, kwakweli ukiwa Raisi unapangiwa nini ufanye, nini ule, mpaka kitu gani uangalie kwenye Tv , tofauti na sasa hivi naweza kulala muda ninaotaka na hata kuamka pia, lakini pia naweza kula sasa hata vile vyakula ambavyo nisingekula kipindi nikiwa Raisi”
Waliendelea na mahojiano mpaka pale walipomaliza kisha wakaruhusu simu
Simu nyingi zilikua za kawaida na kupongeza mpaka baadae ilipopigwa simu moja hivi ambayo ilibadili kabisa mjadala
“mheshimiwa Raisi , kulikua na tetesi kuwa ulikua na mke mdogo ambaye alikua mwalimu pale chuo kikuu cha Dar, na mlijaliwa kuwa na watoto wawili,
nataka kujua kama je ni kweli na je baada ya kifo cha mke wako huyo katika ajali ya moto ulijisikiaje na huyo mtoto mwingine yuko wapi?
“tafadhali tutajie tena jina lako na unapiga simu ukiwa wapi?’ Faraja alijaribu kumkatisha Yule jamaa lakini tayari swali lilikua limeshasikika
‘basi tuendelee kuuliza maswali halafu mheshimiwa atayajibu kwa pamoja” alisema mtangazaji kwani tayari alishaona uso wa mzee Tuppa ukibadilika
“kama muuliza swali nimemsikia vizuri yeye amesema anawajua hao watoto kwahiyo nishauri jeshi la polisi lichukue hatua kwakuwa namba yake hii imeonekana basi ataeleza zaidi niwashi ndugu zangu watanzania tuachane na tetesi na habari za mitandao!” alimaliza mheshimiwa Raisi

“watamkamata huyo mtu” alisema Sele
“huyu mtu ni nani lakini? Amejuaje haya yote?” Aliuliza Esta
“sijui kwakweli” alisema sasa tayari alikua ameshaanza kuhisi kuna watu wengi tu wanajua sakata lake “ngoja tuone kesho wakimkamata nitafanya niwezalo kumuona” aliwaza sele
Ni kweli haikuchukua muda jeshi la polisi lilitangaza kumshikilia kijana huyo mapema sana kesho yake mchana kwa tuhuma za kutunga uongo na kuusambaza kuhusu familia ya Raisi mstaafu
“tunataka kutoa sampo kwa kijana huyu ili kukomesha kabisa tabia ya kusingizia na kuchafua watu kwa sababu za kisiasa, tutaanza na huyu na wengine watafuata” alisema polisi Mamboleo
Wakati huo Sele alikua jirani na kituo cha polisi hicho akijaribu kupenya penya ili amuone kijana huyo ni wakati anapaki gari na kusogea ndipo simu yake ikaita aliangalia mpigaji na kuweka simu chap sikioni
“baby niko hapa najitahidi..”
“usihangaike mume wangu, wamemuachia, Raisi amemsamehe ameamuru aachiliwe mara moja angalia whatsap nimekutumia clip’ Alisema Esta
Sele alirudi kwenye gari kisha akfungua mlango na kufungua ile video
“hatuwezi kumkamata kila mtu anayetunga uongo tutawakamata wangapi? Nimeamua kumsamehe Yule kijana na naomba jeshi la polisi kijana huyo aachiliwe” ilikua ni sauti ya mzee Tupa akiongea
“noo nooo something is wrong!” alijisemea Sele pamoja na muda mrefu aliokuwa nao lakini alijua baba yake amekasirika na sio kweli kuwa kijana huyo amesamehewa bali kuna jambo baya litamkuta, Sele aliendesha agari kusogelea kituo cha polisi na kweli alishuhudia kijana huyo akitoka, alimtazama kijana huyo angalau aone sura yake lakini hakuweza, tayari kulikua na msongamano wa waandishi wa habari na wapiga picha kadhaa hatimaye ilipaki gari ndogo pembeni na akashuka mama mmoja hivi akikimbilia kule ulipokuwa mlango na hatimaye
Baada ya muda mfupi akarudi kwenye gari akiwa na yule kijana, na gari ikaondoka
“fuata hiyo gari sele!” alijiambia wakati sasa anawasha gari kuifukuzia walitembea kutoka kituo cha polisi na kutokea barabara ya Shekilango na sasa waliingia kushoto na kufuata barabara ya sinza, halafu walipofika Mugabe wakaingia bara bara ya vumbi kulia, na sasa Sele alitabasamu baada ya kuangalia kwenye kioo cha gari cha kutazamania nyuma,
Naam hakuwa peke yake kulikua na gari nyingine nyuma yake ambayo alihisi nao walikua wakimfuatilia Yule kijana
“kumekucha” aliwaza akiendelea kusogea na walipita shule ya Msingi Mugabe, na kutokea kwenye nyumba moja iliyokuwa na geti jeusi baada ya kupiga honi geti likafunguliwa, sele alipaki pembeni na kusogea kwenye duka lililokuwa pembeni na sasa lile gari lililokuwa nyuma yake nao walifika na kupunguza mwendo kidogo kwenya ie nyumba kisha wakapitiliza
“naomba mirinda nyeusi” sele alisema huku akikaa kwenye benchi lilikokuwa pale nje
“hivi kumbe Yule dogo anakaa pale eeh” sele alianza maongezi
“ah Yule dogo bhana kajisababishia msala sana, ujue braza ukweli unaweza kukuua hivi hivi, Yule dogo juzi tu nilikua namwambia aache huo upuuzi wake lakini hakutaka kunielewa, wamemuachia lakini sijui kama wataamuacha yule maana ujue dogo ana siri nyingi sana za baba yake!”
“unataka kuniambia na wewe unaamini hizo tetesi?” Sele aliuliza
“broo wewe uko dunia gani, hata mtoto mdogo anajua kabisa Mzee aliua mke na watoto wake ili aupate uraisi nani asiyejua?”
“kwani Yule dogo ndio mtoto wa mzee nanilii ah nani Yule alikua …” sele alijifanya sasa kusahahu kidogo
 
Kuhusu kujua mambo ya kisheria nilifuatilia sana
Kipindi kile Cha "kesi ya mbowe" na wenzake
Nilijua sana mambo mengi kupitia ule Uzi!!

Kwahiyo mtakuta episodes za mahakamani utadhani ni kibatala!!

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kongole sana .
 
Kuhusu kujua mambo ya kisheria nilifuatilia sana
Kipindi kile Cha "kesi ya mbowe" na wenzake
Nilijua sana mambo mengi kupitia ule Uzi!!

Kwahiyo mtakuta episodes za mahakamani utadhani ni kibatala!!

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Nimecheka jamani ,,hongera kwa kujifunza jambo
 
"MPANGAJI 01
Hakuna mpangaji yoyote ambaye alikuwa anafahamu asili ya Yule mpangaji mwenzao, hata jina lake la ‘sele’ wapo waliosema halikua jina lake halisi, lakini yote kwa yote Sele kama unavyoweza kusema alikua mpangaji wa kudumu wa mzee Mhina, miaka ilikatika na sio mzee Mhina wala wapangaji ama watoto wake walijua kazi halisi ya Sele,
Wapo waliosema sele alijihusisha na kazi ya kuzibua vyoo huko mjini mbali na hapo, wengine walisema sele Alikuwa mtu wa ‘kitengo” na kama ilivyo kawaida ya wabongo basi wengine walizua kuwa sele ni jahili mzoefu,
Kwanza Sele asingetoka nje ya chumba chake bila kuitwa, na kwakuwa chumba chake kilikua ni selfu basi huwezi kujua kama sele yupo ndani au ametoka,"


Nimekumbuka Mwanzo wa story ya Bigi ya Steve.....


Naweka kambi rasmi hapaa!!

Wapii Tayukwa Lovelovie Bantu Lady Kalpana baby zu Kigi Makasi Tyrone Kaijage mmash Restless Hustler Unforgettable Mafian cartel mtzmweusi mshaisoma hii storee???
Naweka kitanda kabisa hapa.
 
Back
Top Bottom