Hadithi: Mpangaji

Well
 
hadithi njoo utamu kolea
 
MPANGAJI 19
By CK Allan

“ndio niliwatuma vijana wangu na ndio maana muda mfupi tu alikamatwa” alisema mheshimiwa Kidude. Sasa Sele alikata tamaa ya kutoka salama katika kesi hii, kama alivyokuwa ametarajia, mke wa Raisi alikuwa amejipanga vilivyo kuhakikisha kuwa hachomoki katika kesi hii ,akili yake ilimwambia kuwa mheshimiwa kidude hakukamatwa bali alijikamatisha makusudi baada ya kupanga mikakati yake ipasavyo
Ilifika zamu yake akasomewa mashataka yake na hakutakiwa kujibu chochote na kesi ikaahirishwa tena

Doreen sasa aliona kama mbwai na iwe mbwai tu alishauriana na mumewe na kisha akaaomba likizo ya mwezi mmoja kazini kwake na kupanda ndege kuelekea Tanzania , Doreena asingeweza kukaa kimya huku mdogo wake akiozea gerezani hata hivyo alitaka kulifanya jambo hili bila kumshirikisha Sele, tayari alishakuwa na mawasiliano na mr K na sasa alimuomba msaada wa kupata mawasiliano ya mzee Tuppa, Mr K alijitahidi na mwishowe akapata namba ya mlinzi wake mmoja ambaye alimtumia Doreen haraka.
Doreen alishuka uwanja wa ndege wa Julias Nyerere na kuita tax iliyokuwa jirani na kumuelekeza ampeleke rombo hotel, ni miaka zaidi ya 15 sasa Doreen hajawahi kukanyaga ardhi hii
“hakika nchi imebadilika sana, lakini watu ni wale wale!” aliwaza akiweka miwani yake vizuri huku akitazama mazingira mazuri ya jiji la Dar
Alifika hotelini na kuchukua chumba chake kisha akafanya mawasiliano na mumewe na kisha akaanza kutoa vitu vyake na kuvipanga vizuri
“Gift, dada yako niko hapa pamoja na wewe”
Tayari alitoa laptop yake na kufungua fungua baadhi ya picha na video zilizokuwemo kisha akajilaza kitandani
Wakati huo Sele , Rapha na Mr K walikuwa katika kikao kizito cha kujadiliana namna ya kutoka kwenye kesi ile,
Kilichokuwa kinasumbua ni kesi ya rushwa, lakini kesi yao ya msingi ya kuwa mtoto wa Lukas walikuwa na ushahidi wa kutosha tu katika hilo
‘tuangalie namna ya kuwarudishia hii kesi , alisema Rapha huku macho yake yakiwa katika video ya ulinzi wa kamera katika nyumba ya Sele
“hebu rudisha nyuma hapo weka pause” alisema Rapha akisogea kwa makini
“mwangailieni huyu jamaa, huyu ,huyu!” alisema Rapha huku mr K na Sele wakimtazama tuu
“hii sura ya huyu jamaa hamjawahi kuiona kweli? Hebu fungua youtube niwaonyeshe kitu” alisema rapha na sele haraka akafungua tovuti iyo
‘andika msafara wa mke wa raisi mama Tuppa” alisema rapha sasa akiamini akili zake hazijamdanganya
“fungua hiyo video ya pili hapo” alisema akionyeshea
Na sasa wote walipigwa na mshangao , sura pamoja naumbo la mlinzi mmojawapo wa mama Joan lilifanana kabisa na Yule mtu alikuwa amesimama pale nje kwenye zile video za nyumbani kwa Sele, ambaye alikua amemteka Esta
‘kwahiyo hapa asilimia mia moja huu ni mkakati wa mama joan na huyu mzee Kidude” alisema Sele
“yeah na inavyoonekana hapa kuna kila dalili huyu mama amekusudia mambo makubwa huko mbele” alisema Mr K,
“ukishagundua mtu unayepambana nae hakuna shida” alisema Sele
Wakati wao wakiendelea kujadili huku mzee Tuppa sasa alikuwa amepumzika nje ya nyumba yake kwenye bustani za maua akicheza na ndege wake aina ya kanga wakati mlinzi wake Joshua alipomfuata na kumnong’oneza waliingia ndani kisha kama kawaida yao wakapitia mlango wa uani na kutokea nje na kuingia kwenye gari ya kawaida kabisa na kuondoka kwa kasi,
Mzee Tuppa alipenda kwenda sehemu mbali mbali na kufanya starehe zake kwa kupitia njia hii ya uani ili kuwakimbia walinzi wake, aliondoka na dereva wake na Joshua tu
“una uhakika yupo?” aliuliza tena mzee Tupa
“ndio mzee yupo anatusubiri” alisema Joshua sasa wakikata uchochoro na kutokea barabara ya moro goro kisha wakaiacha kimara mwisho na kuingia kimara temboni NA kuingia kwenye barabara ya vumbi na kisha wakapaki gari yao mbele ya kanisa la KKT
“vaa hii” alisema Joshua sasa akitoa kofia moja inayofunika masikio wengine walipenda kuiita pama mzee Tupa alitabasamu na kuivaa kisha wakazunguuka nyuma ya kanisa hilo na kutokea kwenye viti maalum vilivyotengenezwa kwa Zege na kukaa
“yuko wapi sasa?’ aliuliza mzee Tupa

“anakuja mzee muda ….” Alikatishwa na mlio wa gari Joshua alitabasamu na kuzunguuka kule nyuma akiwa tayari kumpokea mgeni wake huyo
Baada ya dakika kadhaa alirudi akiwa ameongozana na mwanamke mmoja hivi aliyekuwa amejifunika mtandio
Sasa mzee Tupa alijikuta akisimama na kusogea hata kabla mgeni huyo hajafika mahali alipokuwepo
Doreen alivua miwani yake pamoja na kutoa ule mtandio wake kichwani na sasa alikua akitazamana uso kwa uso na binti yake huyo, ambaye hakukumbuka mara ya mwisho walionana lini
“dad!”
“daughter” alisema mzee Tupa akimkumbatia binti yake Yule walibaki wamekumbatiana kwa zaidi ya dakika tano huku kila mmoja akitoa machozi hatimaye waliachiana na kisha Doreena akamkumbatia uncle Joshua
Sasa waliketi chini na kuanza kuongea mzee Tupa alijieleza yote yaliyokuwa moyoni mwake huku akimtaka radhi binti yake huyo kwa mambo yote yaliyotokea
“Mungu ni shahidi sihusiki kabisa na yale yote na hata haya yanayoendelea kutokea katika jambo hili la Gift”
“Baba ni wakati wako wa kuonyesha Dunia kwamba wewe ni baba wa namna gani, vile vile ni wakati wako wa kutuonyeshea mimi na Gift kuwa ni kweli huhusiki kabisa na mambo yote haya yanayoendelea kutokea” alisema Doreen
“niambie mwanangu unataka mimi nifanyeje? Sema mwanangu?” aliuliza mzee Tuppa akimuangalia binti yake huyo
“turn yourself in” alisema Doreen
Mzee Tupa alikumbuka pia ushauri aliopata kutoka kwa rafiki yake jaji mstaafu kuwa ulikuwa sawa na huo huo kuwa ajiingize rasmi kwenye kesi hiyo
“nakuahidi nitafanya niwezavyo kuhakikisha mambo haya yanakwisha kabisa na kila mmoja atavuna alichopanda” alisema mzee Tupaa
“vizuri sasa mimi niondoke” alisema Doreena akiondoka
“Doreen, nakupenda mwanangu, nisameheni sana!” alisema akisimama na kuondoka
Doreen alisimama na kuondoka zake na kurudi kwenye Taksi iliyokuwa inamsubiri na kurudi hotelini kwake, sasa aliamini mambo yataisha kabisa katika kesi ile alifanya mawasiliano na mzee K kisha akakutana na Rapha na kuweka mikakati sawa namna ya kuweza kuweka ushahidi sawa, kulikua na ile video ya mauaji, pamoja na picha kadhaa za utotoni za akina Gift akiwa pamoja na mzee Lukas Tupa na ile picha maarufu ya familia ambayo walipiga wote wanne
“mzee ameonyesha nia?” aliuliza Rapha
“yeah lakini hatabiriki sana” alisema Doreen
“okay tujipange sisi kama Sisi, labda nikuulize swali moja, wakati unasoma Kenya kuna siku baba yako alishawahi kukutembelea na mkapiga walau picha ukiwa shuleni na walimu au wanafunzi wenzako?” aliuliza Rapha
“mzee alikuja kama mara tatu hivi, na siku zote alifika shuleni na kusema alikua anatembelea watanzania waliokuwa wanasoma nchi humo, nadhani tulikuwa kama wanne hivi wawili katika ile shule na wawili walikuwa katika shule nyingine, so alikua anatukusanya na kutupeleka lunch au dina, na nilishaambiwa kuwa nisiseme kuwa yeye ni baba yangu nikiwa kule Kenya, kwa ajili ya usalama wangu, nakumbuka mama aliniambia Kenya kuna magaidi na kama wakijua mimi ni mtoto wa waziri basi wataniteka” alisema Doreen akifuta machozi
“hakuna shida, sasa tuanze na hiki kilichopo halafu tubadili kesi na tumfungulie rasmi kesi ya mauaji madam” alisema Rapha
Hatimaye siku ya kesi ilifika na kama kawaida gift alipewa nafasi ya kujitetea na kama alivyofundishwa na wakili wake alikuwa sasa anatoa utetezi wake kabla ya hukumu kutolewa
‘tuliishi mikocheni na baadae tukahamia mbezi beach, wakati wote huo mama alikua anafanya kazi chuo kikuu cha Dar es Salaam, kwahiyo baba yetu mzee Lukas Tuppa alikua na kawaida ya kututembelea nyumbani kila…..” sasa Gift alikua akieleza maisha yake binafsi na ya dada yake na jinsi mpaka alivyofanikiwa kuona mama yake akiuwawa”
“sasa kwanini unahisi kuwa kesi hii imepangwa na watu wabaya wakati wewe umekamatwa na ushahidi ndugu yangu?’ alikua anauliza sasa wakili upande wa mashtaka
‘Pesa hiyo niliwekewa baada ya kutekwa kule na watu wa mzee Kidude ndio walioweka bahasha hiyo” alisema Gift
Waliendelea kuuliza maswali na sasa wakili wa Gift akaanza kuita mashahidi wake kwa mshangao wa wengi Shahidi wa kwanza alikua Doreen baada ya kuapa na kupanda kizimbani nae akatoa maelezo yake
 
MPANGAJI 20
By CK Allan

“Tuliishi kwa furaha mpaka siku ile ambapo baba alikuja kutuambia anataka kujiingiza kwenye mbio za uraisi, na kusema kuwa hatakuja tena pale nyumbani, baba yetu alitupenda sana na kulikua na kila dalili alikua anampenda mama yetu zaidi kuliko mama Joan na ndio maana mama Joan akamuua mama yetu mzazi…”
“haaaaaaaaaaaaa” sasa kulikuwa na mguno mkubwa pale mahakamani na minong’ono ilikua dhahiri na ikabidi mwendesha mashtaka kuingilia kati
“binti, hizo tuhuma za mauji ni kubwa sana, unaweza kuthibitisha?” aliuliza mwendesha mashataka kwa utulivu
“ndio, tulifanikiwa kuondoka na kipande kidogo cha video kutoka kwenye nyumba yetu kabla vitu vinginme havijachukuliwa na mheshimiwa hakimu ushahidi huo unaonesha wazi wazi mama Joan akiwa na watu wake wakimshambulia mama kwa risasi” alisema Doreen
“haaaaaaaaaaaaaaa” miguno iliendelea tena pale mahakamani
“sio hivyo tu, nyumba yetu haikuwa na uthibitisho wowote wa kuwa na tatizo lililosababisha shoti ya umeme, ama gesi ama chochote kile, badala yake moto ule uliwashwa makusudi kupoteza ushahidi” alisema Doreen
“tunaomba hiyo video tafadhali” alisema mwendesha mashtaka na kisha wakaingia kwenye chumba maalum pamoja na mawakili wa pande zote mbili na kuangalia sasa ile video huku kila mmoja akiandika vitu muhimu
Na baadae walirudi tena mahakamani na Doreen akatoa ushahidi wa picha na vitu kadhaa vingine
“kwakuwa tayari tumeshapata mtuhumiwa mwingine naagiza sasa mama joan, aletwe hapa mahakamani kwani tayari hatuwezi tena kuendelea kusikiliza mashahidi wengine na kuendelea na kesi hii bila mtuhumiwa kuwepo” alisema hakimu huku akiahirisha kesi tena
Gift na dada yake walibaki nyuma huku wakikumbatiana na kuongea kwa fuaraha
“asante kwa kuja dada” alisema Gift
“asante sana mdogo wangu siwezi kukuacha nyuma” alisema Doreen
“haya tupite njia hii” alisema Mr K akiwaongoza kupita njia ya pembeni kwani tayari waandishi walikuwa wanawasubiri nje na wasingeweza kuwakwepa bila kupitia mlango wa nyuma

“Nashauri tusitumie gari moja” alisema rapha
“na mimi naona hivyo pia” alisema Gift
“Sele na Mr K Mtatumia gari langu, mimi na Doreen tutatumia gari la Mr K , halafu gari la Sele liwe backup na james na Ali wakitufanyia backup” alisema Rapha na kisha wakatoka nje ya jengo
“mtanifuata mimi kila kichochoro ninachopita” alisema Mr K na sasa safari ikaanza mara moja wakitoka mahakamni kisutu na kuelekea huko Mr K alipokusudia
Waliendelea kuwa kuwasiliana kwenye magari yote matatu
“mbona tunaenda ofisini” aliuliza Sele
“ndio tunaenda huko ila kuna kitu nataka ukaone” alisema Mr K
Walifika mpaka ofisini kwao na kumkuta Esta ambaye alikua amekaa kwa muda akishikilia majukumu ya Sele kutokana na yeye kuwa katika ubize wa kesi walipitiliza na kuingia kwenye ofisi ya Mr K
“Mr K sidhani kama mahali hapa ni salama sana” alisema Rapha
‘subirini muone” alisema sasa akichukua simu iliyokuwa pale mezani
“Njoo” alisema kisha akakata simu akina Sele walikua wakimtazama tu sasa Mr K
Baada ya muda aliingia katibu muhtasi wake, Aisha
“tuna kikao kirefu sana kwa siku mbili mfululizo kutokana na jambo ambalo unalijua kwahiyo mtu yoyote akiulizia huduma basi muone namna ya kumsaidia na usimruhusu yoyote , narudia yeyote, kuja ofisini kwangu, nipigie simu yangu ya mkononi tu ikibidi sana” alisema.
Baada ya Aisha kuondoka sasa Gift alishindwa kuvumilia
“mr K Hapa hatuwezi kukaa angalia kwanza ni ofisini chumba kidogo na inabidi sehemu ya kupumzika bhana” alisema Sele ,
Mr K hakujibu alisimama na kwenda kuufunga mlango kabisa kisha akasogelea kwenye shelfu kubwa la vitabu na mafaili na kusogeza mafaili kadhaa kisha akatumbukiza mkono na kubonyeza kidude Fulani na sasa lile shelu likaanza kupanda juu pole pole na hatimaye mlango mkubwa ukatokea mbele yao
“haya njooni huku!” alisema Mr K Na sasa wote wakasimama wakiwa wamepigwa na butwaa

Mr K aliifungua ule mlango na sasa wakatokea kwenye sebule moja kubwa iliyokuwa na Tv kubwa mbili na samani nzuri za kisasa
“haya sasa hapa tupo nyumbani kwetu kabisa tunaweza kuendelea” alisema Mr K akiwakaribisha wageni wake hao
“hakika hii inapendeza sana sikujua kama Mr K unaweza kubuni kitu kama hiki, haya tunafanyaje sasa hapa kujua yanayoendelea huko nje!” alisema Sele na kama alivyotegemea aliwasha Tv mojawapo aliyohisi na kweli ilikua inaonyesha matukio kadhaa yaliyokuwa yakiendelea kule ofisini na nje kidogo ya ofisi na kuzunguuka jengo zima
“haya sasa wanaotaka kupumzika kwa muda wanaweza, kuna vyumba viwili vikubwa vinatosha kabisa na jiko dogo lipo hapa na nimeweka vyakula vya kutosha kwa wiki kadhaa, kwakweli niliweka hiki chumba maalum kabisa kipindi kile vugu vugu lilipoanza nikahisi chochote kinaweza kutokea sasa” alisema Mr K,
Sasa walikaa na kujadili mipango yao yote huku wakifuatilia kila kitu kilichokuwa kinaendelea pale ofisini ni mpaka jioni sana sasa Doreen aliondoka kurudi hotelini kwake akisindikizwa na Rapha huku sele Na Esta wakirudi nyumbani kwao na kumuacha Mr K ofisini kwake
Hatimaye Mama Joan aliamua kujipeleka Polisi huku mzee Lukas akigoma kata kata kumsindikiza
“kila mmoja apambane na hali yake Vivian!’ alipenda kutumia jina lake halisi alipokuwa akiongea na mke wake huyo
“nilikulinda wakati wote lakini sio sasa Vivian! Sio sasa!” alisema mzee Lukasi asubuhi hiyo wakati mke wake huyo akienda kituo cha polisi
Mama Joan alikua aliwakilishwa na wakili wake ambaye alimpa matumaini makubwa ya kushina kesi hiyo asubuh kabisa
Wakati kesi ikisomwa sasa wakili wake huyo alikua akisimama mara kadhaa na kupinga baadhi ya maelezo au ushahidi uliokuwa katika upande wa mashtaka
“mheshimiwa hakimu mdai katika kesi ya msingi ni mtaalamu wa Tehama, tena anamiliki kampuni ya kuuza vifaa vya ulinzi wa mifumo, ikiwemo kamera za ulinzi, je kwa weledi wake mkubwa huu pamoja na tuzo alizoshinda anashindwa kutengeneza video kama hii? Mheshimiwa hakimu, lakini pia tunajiuliza kwanini wakae na ushahidi wote huu wa mauaji kwa miaka yote hii kwa kigezo tu cha kumlinda baba yao?” aliuliza wakili wa mama Joan
“napinga mheshimiwa..napinga!” aliingilia kati Rapha
“kuwa na kampuni ya vifaa na kujua tehema hakuzuii mahakama hii tukufu kuchukua ushahidi huu, video hii inaonyesha muda mwaka na tarehe ya matukio halisi ya wakati ule mheshimiwa hakimu” alisema Rapha huku akiweka Joho lake vizuri na kurudi kukaa
“je unao mashahidi wengine tafadhali?” aliuliza hakimu
“ndio mheshimiwa,’ alisema Rapha akimkonyeza mwendesha mashtaka ambapo baada ya muda aliingia Jose
Baada ya kupanda kizimbani sasa alianza kutoa ushahidi wake
“naitwa Josep James Kimei, baba yangu alikuwa daktari katika hospitali ya taifa muhimbili na baadae akwa daktari Binafsi wa familia ya Mzee Lukas, mara nyingi alikuwa akienda kuwahudumia akina mama Doreen na watoto wake kule Mikochoni au mbezi Beach mara kadhaa nilikua nakwenda nae kule hususani wakati wa likizo, ama siku moja moja wakati wa Wikiendi”
“hebu sasa tuambie siku ambayo baba yako alikuwa anakwenda kwa marehemu mama Doreen na baadae na hakurudi tena ilikuwaje hiyo siku?’ Rapha alikuwa anamuuliza
“ilikua ni majira ya saa tatu kasoro na tulikua tunakula chakula cha usiku wakati baba alipopigiwa simu kuwa aende haraka kwa mama Doreen, nilitaka kwenda na baba Siku ile lakini baba alinisihi nimalizie kula chakula kwani hatachukua muda kurudi, ilikua ni siku moja kabla ambapo alituambia kuwa kuna uwezekano akabadilishiwa majukumu ya kazi yake na hivyo pengine kazi zake zikaongezeka zaidi , baada ya kumaliza kula tulikaa mpaka majira ya saa tano usiku lakini baba hakurudi , hivyo mama ayangu alijaribu mara kadhaa kupiga simu yake lakini haikupokelewa na kwakuwa hapakuwa na umbali mrefu tulitoka na kupanda bajaji kuelekea kule kwa mama Doreen, wakati tunakaribia pale kwenye nyumba yao tuliona gari ikitoka kwa kasi na kuacha geti likiwa wazi na hivyo tuliongeza mwendo lakini tayari moto ulikua ukiwaka karibia shemu zote za nyumba na tayari watu walikuwa wanatoka majumbani kusogea pale,tulikuwa wa kwanza kufika pale lakini ghafla mama yangu alianza kulalamika moyo na presha na akazimia, sikua na namna isipokuwa kumkimbiza hospitali haraka na kisha kurudi tena kwenye tukio ambapo polisi walikuwa wameshatoa miili na kuzima moto na kesho yake tulitangaziwa kuwa mama Doreen amefariki na mtoto wake na mlinzi, baada ya mama kutoka hospitali hakuwa sawa mpaka leo hii,
Tulijaribu kutoa taarifa polisi lakini hakukuwa na taarifa zozote hata pamoja na kueleza kuwa baba alikuwa kwa mama Doreen hakuna polisi aliyetilia maanani na baada ya siku chache tukasikia gari ya baba imeonekana karibu na bahari ikiwa imetelekezwa, na baba hakuwemo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…