Hadithi: Mpangaji

MPANGAJI 03

Sele hakukaa hata kidogo aliondoka zake mara tu baada ya kumuacha Ester pale kwao,
Sasa Ester alizunguukwa na wapangaji wote waliokuwepo wakitaka awaeleze kuhusu Sele,
“hivi anaongea kabisa, halafu anacheka?” aisha alidakia
“jamani Sele ni mwanaume mzuri tu kama walivyo wanaume wote, yaani sijui nisemeje ni binadamu kabisa!” alisema ester sasa alishachoka kufanya mahojiano ambayo kwa uono wake yeye haukuwa na kichwa wala miguu,
“haya tuambie mlikula nini, kawhiyo Sele pia anakula kabisa!” aliuliza mama Mwajuma!
“hahahaha jamani mama, eti anakula, kwahiyo bado mnaamini Sele ni Zimwi, sijui jini huko..” alisema ester akiingia ndani
“na mizigo yote hii mwanangu umemaliza mshahara wako huko!” alisema mama mwajuma
“hapo vitu vingi kaninunulia Sele” alisema Ester sasa akiangalia hotpot lilipo ili achukue chakula
“mh makubwa haya jamani!”alisema mama Mwajuma sasa akimtafutia maji ya kunawa mwanae

Ndani ya muda mfupi Sele alizoeana kabisa na Ester na sasa unaweza kuwakuta wamekaa nyuma ya nyumba usiku wakipiga soga huku wakicheka kabisa, hata hivyo Sele alikataa kata kata kumueleza chochote kuhusu maisha yake pamoja na Ester kujinasibu kumuelezea hadithi zake za mahusiano yaliyopita na maisha ya shule kwa ujumla , Sele hakuthubutu kumueleza chochote,
Na sasa waliweza kubadilishana namba za simu na siku nyingine wangechati mpaka usiku wa manane,
Baada ya sikukuu ya Pasaka sasa Ester alipaswa kuondoka kurudi kazini kwake lindi , Tayari mkuu wake wa shule alishampigia kumkumbusha umuhimu wa kurejea mapema,
Hivyo siku hiyo Ester alitumia muda wake kwenda kariakoo kununua vitu baadhi alivyodhani vingemfaa , aliwaza na kuwazua akaona atafute zawadi ndogo kwa ajili ya Sele na hivyo akaingia duka moja la kuuza simu na kununua simu janja aina ya Tecno F2.

“bila shaka Sele atafurahi kuwa na simu hii janja, na nitakuwa namtumia picha zangu nay eye ananitumia zake nikiwa Lindi” aliwaza Ester.
Alirudi nyumbani na kuandaa mizigo yake tayari kwa safari kesho yake, baada ya kumaliza alitoka nje kwenda kumsubiri rafiki yake Sele ambaye alifika kwa wakati kabisa,
“yaani umejuaje kunisubiri hapa!” alisema Sele akiwa na bashasha kweli kweli,
“ah yaani acha tu wewe mwanaume una kismati maana hata sijui kwanini nimekuzoea hivi” alisema Ester bila kujielewa
“nisubiri basi hapa nikaweke mizigo then nitakukuta hapa nje!” alisema Sele akiingia ndani
“mh yaani mpaka naondoka sijaingia chumbani kwako Kaka sele Jamani!” alisema Ester akipiga hatua kumfuata Sele,
“HAPANAA!!” alifoka Sele , mpaka mwenyewe akashangaa na kurudi nyuma kwa ester kuomba radhi,
“nisamehe Ester, kwakweli hakuna mtu ataingia chumbani kwangu , nasikitika nimekufokea nisubiri tu nakuja” alisema Sele akiingia ndani haraka
“nitaingia hiki chumba Sele, kama sio leo basi kesho!” alijisemea Ester akimsubiri Sele atoke
Sele alitoka baada ya dakika chache tu kisha wakasogea kwenye msingi wa nyumba ambao ulikua haujaisha na kukaa kupiga Story,
“yeah kama nilivyokuambia kesho nasepa Sele nitakumisi sana!” alisema Ester kwa uchungu kidogo
“yeah, ndio hivyo kazi ni muhimu sana Ester inabidi uende mimi mwenyewe nitakumisi ujue, wengine wananitenga mara waniite zimwi, siijui jinni.. hahahaha!” alisema sele akimalizia na kicheko
“hahaha yaani nakuambia kabla hatujaonana nilikua naambiwa sana habari zako , ila kumbe mtu mwenyewe wala hata hauko hivyo,” alisema Ester akilala kwenye mabega ya Sele
“hahaha mawazo yao tu, sema unajua maisha ya Dar kila mtu na hamsini zake kwahiyo nadhani watu wako bize sana kutafuta riziki ndio maana wananifikiria vibaya!” alisema Sele
“kaka Sele nimekuletea Zawadi hii” alisema akitoa ile simu kwenye box lake na kumkabidhi Sele,

“loh asante sana Ester kwa smartphone hii” alisema Sele akiichukua
“ooh asante kwa kushukuru, ndio sasa nikiwa Lindi nitakuwa nakupigia video call, nakutumia picha na video zangu Sele!” alisema Ester kwa furaha
“sikiliza ester mimi situmii mtandao wowote wa kijamii” alisema Sele kwa upole huku mkono mmoja akiwa ameuweka begani kwa Ester
“sele unasema kweli?” Ester alihamaki akimtazama Sele machoni hakuamini kabisa maneno haya yanatoka kwa kijana mwenye umri wa miaka 30-33 hivi
“yaani hutumii facebook, insta, whatsapp?” aliuliza Ester na Sele aliatingisha kichwa tu kuashiria anakubaliana nae..
“basi ni kweli kuna tatizo Sele!” alisema Ester sasa akitoa kitambaa chake kwenye suruali aliyokua amevaa akifuta machozi na kisha akasimama na kuondoka kurudi ndani
“rudi ester” Sele alijaribu kumuita lakini tayari Esta alishawahi kulifikia geti kurudi ndani
“nilijua tu atachemka, mimi ni Zimwi kweli!” alijisemea Sele akipiga ngumi kwenye mchanga kwa hasira alijisikia vibaya sana kuagana na esta katika hali ile esta alirudi ndani na kukimbilia Chumbani kwake alijikuta akilia bila sababu mpaka yeye mwenyewe akawa anajishangaa
“Triiiiia” simu yake ilitingishika kuashiria ujumbe mfupi uliingia
Aliufungua na kusoma ulitoka kwa sele
“NINA ZAWADI YAKO PIA TAFADHALI UJE UICHUKUE”
Esta aliwaza kama aende ama abaki lakini baadae alijiona mpumbavu kulia mbele ya mtu ambaye hata hakuwa na mahusiano yoyote
Alijikaza kisabuni na kutoka nje na kumkuta sele akiwa ameshikilia begi dogo hivi la wastani
“hii zawadi yako Esta” alisema akimkabidhi kisha akageuka kurudi chumbani kwake!
“na hili begi, mbona kama kuna uzito humu?” aliuliza esta,
“bhana ni zawadi yako vyote pamoja na begi” alisema Sele akitabasamu kisha akaendelea na hatua zake kadhaa kuingia kwake,
Esta bado alikua na shauku ya kujua ndani ya begi kulikua na nini, hivyo aliangalia huko na huko kuhakikisha hakuna mtu pale nje kisha akaingia ndani na kufungua lile begi..
Ndani kulikua na komputa mpakato mpya kabisa aina ya apple ikiwa katika makaratasi yake
“whaaat” Esta aliweka ile komputa kitandani huku akiwa haamini, hakujua kama afurahi ama la, haraka alichukua Simu yake ana kuingia mtandaoni na kwenda kwenye google kisha akatafuta “apple sx400 min series price” bila hiyana google wakamletea $1,100 , alijaribu kubadili pesa hizo na kuweka kwenye pesa ya Tanzania na kukuta ni zaidi ya million mbili!
“yaani huyu Sele ananinulia mimi zawadi ya million mbili?, sele huyu katika nyumba ya kupanga ya kawaida tu?” Sasa akili yake ilimwambia huyu “sele” sio mtu wa kawaida kama alivyokuwa anamchukulia,
Aliwaza na kuwazua kisha akaona ngoja acheze huu mchezo
Alichuchukua simu yake na kuandika ujumbe mfupi kwa sele
“asante sana kwa zawadi dear ila nina ombi moja”
Kisha akutuma kwa sele , baada ya muda mfupi yake simu yake ilitoa ishara kuwa ujumbe ule umepokelewa na hivyo akasubiri jibu
“yap karibu” sele alijibu
“naomba sana kesho unisindikize hadi ubungo tafadhali sana, naomba sana kesho usiende kabisa kazini” aliutuma ujumbe huo kwa sele
“Esta nilishapanga hilo nisingekuacha uende mwenyewe best” alijibu sele kisha wakaagana
Kila mmoja aliwaza kuhusu mwenzake
Badala ya furaha Sele alijikuta machozi yakimtoka, alienda kwenye sanduku lake ambalo alikuwa ameliweka kwenye kabati ya nguo,
Alitoa bahasha kadhaa kisha akatoa picha mbili aliziangalia muda mrefu huku machozi yakimtoka
‘nipe Baraka zako , nipe Baraka zako!” alisema huku machozi yakimtoka akiwa ameshikilia zile picha,
Sele sasa hakuweza kutazama zile picha zaidi alizirudisha na na kisha akaenda bafuni alifungulia maji tu yakimwagikia mwilini na mwishowe akagundua kuwa alikuwa hajavua nguo zake kumbe
 
MPANGAJI 04
Asubuh na mapema Sele aliamka na kufanya mazoezi kiasi kama ilivyokuwa kawaida yake, akitumia vifaa kadhaa alivyokuwa navyo, alipiga push up za kutosha na mazoezi mengine kisha akaenda bafuni na kuoga na siku hiyo aliamua kuvaa nguo za kawaida kabisa, alivaa pensi na raba kisha akavaa na kofia moja matata iliyokua na herufi chache tu “CK” kisha alifungua kwenye begi lake na kutoa kiasi cha pesa na kuhesabu noti kadhaa na kuzitia kwenye waleti yake halafu akatoa simu yake na kukuta missed calls mbili za Esta,
“la haulaa!” alijisemea sasa akivuta begi lake na kuchukua ufunguo mezani na kutokomea nje
Alimkuta Esta akiwa mlangoni na begi lake tayri kwa safari..
Mama Mwajuma nae alikuwepo kumsindikiza mwanae
Baada ya Salamu sele alichukua begi la Esta na kulivuta taratibu kutokea nje Mama Mwajuma tayari alishahisi kuna jambo linaendelea kati ya watu hawa wawili hata hivyo kwa upande mwingine alifurahi kwani pamoja na mambo mengine ya Sele, alikua ni kijana mtanashati, mwenye adabu na asiyekuwa na makuu, kuhusu anafanya kazi gani mama mwajuma hilo halikumuumiza sana kichwa isipokuwa ni namna ambavyo uhusiano huu utaishia
“potelea pote hawa ni watu wazima” aliwaza mama Mwajuma sasa wakipiga hatua kutoka nje ya nyumba, tayari wapangaji wengine waliokuwepo walishaagana na Ester na wengine tayari walikua wameshamzoea
“sasa Mama wewe ishia hapa mimi nitamsindikiza Esta mpaka ubungo na kuhakikisha anapanda basi la Lindi kabisa mama!” alisema Sele huku akitabasamu,
“itakuwa vizuri kabisa Basi mimi niishie hapa, Sasa Esta, nikuage Mwanangu alisema mama Mwajuma huku akipunguza mwendo kidogo Sele alikuwa ameshaelewa hapa ni “mausia” ndio ambayo yanafuata
“Mwanangu usinifiche kitu mimi ni mtu mzima, niambie una uhusiano na Sele?” mama Mwajuma aliuliza huku akimtazama mwanae usoni
“hapana mama, Ni tumezoeana tu yaani, hivyoo tu!” alisema Esta huku akiwa kama anataka kusitisha mzungumzo
“ila Sele anakupenda maana hajawahi kuwa na ukaribu na mtu yoyote , sasa mpaka anafikia hatua ya kukusindikiza hadi stendi?” alisema mama Mwajuma
“ungejua sio kunisindikiza tu, kanaipa hadi laptop!” alijisemea moyoni Esta

“haya mama uwe makini huko shuleni, kaa vizuri na walimu wenzako, na mkuu wako wa shule na usisahau kuniletea mzigo wangu likizo ya mwezi wa 6” alisema mama Mwajuma akimuaga mtoto wake kwa mbali alimnyooshea mkono Sele ambaye alikua sasa ameweka begi chini akimsubiri Esta ambaye alifika na kisha safari ikaanza. Hawakupiga hadithi sana kwani kila mtu alikua anawaza mambo yake kichwani, walipofika Kimara Mwisho Esta alilalamika kuwa kuna kitu aliagizwa na shoga yake amnunulie na alisahau kununua,
“yaani Nikifika bila hicho kitu Shoga yangu hatanielewa kabisa yaani” alisema Esta akimweleza Sele
“okay tushuke kwanza unaweza kukipata hapo nje hicho unachokitafuta halafu tukachukua bajaji tu kwenda stendi bado ni mapema” alisema Sele huku akisogea mlangoni
Walishuka pale Kimara mwisho ambapo wengine walipenda kuita darajani
Na kuvuka upande wa pili
sele alijua bila shaka ni vitu vya wanawake ambavyo shoga yake huyo alimuagiza
“wanawake wana vitu vingi sana yaani!” alijisemea sele huku sasa akivuta begi la Esta
Walisogea kabisa pembeni ya barabara na kuingia mtaani walikaribia sehemu kulikua na bajaji kadhaa zimepaki Esta akamwambia Sele asubiri yeye aende kuuliza hicho kitu
Alisogea pale na kabla hajafika alishadakwa na madereva kadhaa alichagua mmoja kisha wakaongea halafu baada ya muda kidogo Esta alimnyoshea mkono Sele amfuate
Sele alimfuata na kuingia kwenye bajaji ya Yule kijana
“vipi tena?” aliuliza Sele akiwa ameduwaa
“nakumbuka wakati nakuja nilikuambia unizunguushe nione mji kwahiyo leo ni zamu yako kaa utulie mwanaume wewe na usiongee kitu!” alisema Esta kwa utani
“haya langu jicho Esta, ila kwa hali safari labda kesho unapajua Lindi wewe?” Sele aliongea sasa akiwa haelewi nini kinatokea
“hata hapa Dar nasikia kuna sehemu inaitwa Lindi” alisema Esta Sele hakua na namna isipokuwa kucheka tu walipita sehemu kadhaa na baadae wakatokea mbele ya jengo moja zuri sana “LOTHA EXECUTIVE LODGE & RESTAURANT” maandishi makubwa yalisomeka kwenye kibao cha jengo hilo
*************************
‘pacheki sista kama hapafai nikupeleke nyingine ipo kati hapo nayo barida tu kama hii!” alisema Yule kijana wa bajaji akiwa amesimama tayari kutoa mizigo
Esta alishuka kwa kujiamini huku Sele akiwa hajui kama anatakiwa kupiga kelele za shangwe au kilio ama anatakiwa kufanya nini,
Esta alifika ndani na baada ya muda alirudi
“asante kaka pako vizuri bei gani vile ulisema?” alisema Esta kifungua pochi yake na kutoa elfu tano
“ah buku mbili tu sista, kama vipi chukua minamba nini ili kama niaje niaje nini fresh tuu!” alisema Yule kijana mpaka Esta alicheka
“hahaha usijali, sasa namba yako nitaisave niaje niaje bajaji” aliongea huku Sele sasa akishuka kwenye bajaji na mizigo
“kiuhalisia nataka niende Lindi nikiwa sina deni na mtu Sele”
Alisema Esta huku akiwa anatangulia ndani, Sele alifuata kama kondoo aliyekuwa mafichoni walipita mapokezi na mhudumu akawapokea na kuwapeleka kwenye chumba ambacho tayari Esta alishachagua, kilikua ni chumba kizuri sana, Esta alitua mizigo yake na kuipanga vizuri sele alikaa kwenye sofa lililokuwa pale chumbani na kukunja nne huku akimkodolea macho Esta kama mtu anayesubiri kupewa muongozo
“sele nikuambie kitu!” alianza Esta kwa upole sana, yeye kama mwalimu alijua namna ya kuweza kueleza somo lake likaeleweka kwa mwanafunzi wake huyu aliyekuwa mbele yake
“mimi nina miaka 26 sasa hivi, nina vitambulisho vyote kuanzia cha kupigia kura cha kazi hadi cha Taifa” alianza Esta
“unataka kusemaje?” aliuliza Sele
“naona kama mwenzangu umejaa hofu kana kwamba umeingia na mwanafunzi wa form one hapa kwahiyo muda wowote utakamatwa!” alisema Esta huku akicheka
“Hapana mwalimu mimi sijawa na hofu, ila nashangaa tu, ubungo imekuwa hii, sasa sijui hicho kitanda ndio basi au!” alisema Sele kwa utani
“kwahiyo huna hofu kabisa?” aliuliza Esta
“kwahiyo nikuogope wewe au!” aliuliza Sele

Esta hakujibu alisogea mpaka kwenye meza na kupiga simu mapokezi ambapo aliagiza supu ya kuku na chapati
‘ Sele safari yangu ni kesho, kwahiyo leo nimeamua rasmi nibaki na wewe hapa, kuna mambo inabidi nikuambie Sele ka aujuavyo kule nyumbani hakuna uhuru sana na tusingeweza kuongea” alisema Esta
“ kwakuwa leo ni siku ndefu kwanza nikushukuru sana kwa zawadi Sele yaani nikifika pale shule nitaosha kweli!” alisema Esta akiitoa ile komputa kwenye begi lake
“ooh usijali Esta” alisema Sele
“nielekeze elekeze basi ujue mimi sio mtundu sana kwenye komputa” alisema Esta akienda pale kwenye Sofa alipokaa sele,
“ooh, wewe mwalimu tena si mmespma ICT chuoni jamani!” alisema Sele
“tumesoma lakini theory nyingiii!” alisema
“mh tuanze na nini…” sele alikatishwa na sauti ya mhudumu aliyekuwa anagonga mlango na alifungua , na mhudumu akaweka mizigo mezani,
“karibuni” alisema mhudumu
“tuletee maji makubwa ya Kilimanjaro na glass mbili” alisema Esta sasa akisogea pale mezani na kuanza kupiga msosi…
Walimaliza kula na kisha Sele akamuelekeza vitu kadhaa kwenye komputa katika hali ambayo Esta alishikwa na bumbuwazi,
“sele mbona unaijua komputa hivi? Na wakati huo umesema hutumii kabisa mitandao ya kijamii?” aliuliza esta akiwa ameduwaa
“ah kumbe nilikua sijakuambia kazi yangu hadi leo! Hahaha alisema Sele akicheka”
“Mimi ni IT nimejiajiri binafsi, kazi yangu ni kufunga mifumo mbali mbali katika ofisi, majengo ya watu binafsi n. kama vile kuweka software za cctv camera, ama za ulinzi n.k, mwakani inshallah Mungu akipenda nitakuwa na ofisi yangu rasmi sasa hivi nafanya deiwaka tu na kampuni moja hivi inaitwa TAA” alisema Sele huku akiwa ametulia kabisa
“waooh kumbe, niko na IT hapa, kwahiyo kumbe ninyi ndio mnahack akaunti za watu insta, eeh?” aliuliza Esta kwa utani na sasa muda wa kubadili mada uliwadia ‘leo afe kipa afe beki” aliwaza
 
Shunie Numbisa Gily moneytalk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…