Hadithi: Mpangaji

MPANGAJI 07
Niliona watu watatu wakiwa wamefunika nyuso zao ila kwa muonekano mmojawapo alikuwa mwanamke, walikuwa wamemtoa mama yangu pamoja na daktari na mlinzi na dada wa kazi na kuwafunga kamba na kuwawekea vitambaa mdomoni ispokuwa mama yangu ambaye walikua wakimuuliza nilipo
“yuko wapi Gift?’ Alikuwa akiuliza Yule mwanamke akimpiga mateke mama
“Gift yupo na baba yake kwenye kampeni!”mama alijibu huku akilia,
Sitaki kukumbuka Esta, ila ni kwamba walimpiga mama risasi na wale wengine walifariki pale pale kisha wakatoka nje na kuchoma moto nyumba”
Sele sasa alikuwa Analia kama mtoto mdogo,
Esta nae alijikuta akilia kwa nguvu na na mara wakajikuta wamekumbatiana wote wakilia kama watoto wadogo
“inauma sana Esta, sasa kesho yake jambo baya zaidi likatokea, magazeti na vyombo vya habari walitangaza kuwa mama yangu, pamoja na mimi wote tulifariki katika ajali ya moto iliyotokea usiku ule,
“kwa maana hiyo ule mwili wa dokta ndio ukaonekana ni wewe au?” aliuliza Esta
“nilikuja kugungua baadae mama mkubwa ndio alimuua mama yangu mzazi na alifanya vile makusudi ili hata kama nikiwa hai nisiwe na namna yoyote ya kujitokeza kuwa mimi ni mtoto wa mzee Tupa kwakuwa tayari nilishafariki kwenye ule moto” alisema Sele
“loh kwanini lakini Binaadamu ni wanyama kiasi hiki,?”alisema Esta sasa huku akijifuta machozi
“Vipi sasa baada ya kutoka hapo ilikuwaje na ule usiku ulienda wapi na ikawaje sasa hadi ukaishi hivi unavyoishi leo Sele?”
“niligundua kwamba tayari nilishafika maeneo ya koko beach kwahiyo nilirudi kwenye gari na kwa bahati nilikuta pesa kama laki mbili hivi kwenye ile gari ya Dokta, nikaenda kutafuta chumba gest nikalipia siku tatu, ili nitafakari cha kufanya”
Nilifanya mawasiliano na dada Doreen ambaye hakuamini kama anaongea na mimi maana alijua nimeshafariki, kwahiyo akanisisitiza kuhakikisha waliofanya haya yote wanakuja kupata haki yao hapo baadae, nilisubiri usiku sana nikaenda kwenye nyumba yetu na kujaribu kutafuta kama nitapata kitu cha maana
Kitakachonisaidia, vitu vingi tayari vilikua vimeshachukuliwa na nadhani ilikua ni njia mojawapo ya kuficha siri, nilifanikiwa kuokota baadhi ya picha za mama na za kwangu na vitu kadhaa tu
“Sele kwahiyo hii ilikua ni mwaka 2000 sio?”
“yap, kipindi kile kile cha…” sele alikatishwa na sauti ya mhudumu ambaye alikuwa ameleta chakula kutokana na oda zao walizokuwa wameagiza, hakika walijikuta wamepiga story sana kwa muda mrefu na hata hawakusikia njaa mhudumu aliweka chakula mezani na kisha waliamua kula

Hadithi ziliendelea mpaka jioni Tayari Sele alikua amemsimulia kila kitu ambacho alidhani alipaswa kumhadithia,
“sasa ulipata vipi tena vitambulisho vyako?” Esta aliuliza
“kutokana na vitambulisho vile havikuwa feki yaani vilitoka mamlaka husika, nilienda tu polisi nikachukua loss riport na kisha nikarudisha kimoja baada ya kingine” alisema Sele
“Sele nataka uniamini mimi, kwakweli hadithi yako inahuzunisha sana, kwa mtu yoyote Yule kama nilivyokuahidi Sele, kuanzia leo hii mimi nitakuwa upande wako katika kila jambo ambalo unapanga kulifanya, nipo Sele kwa ajili yako..’ alisema Esta akimkumbatia Sele kwa nguvu, Sele alijisikia msisimko wa ajabu pale matiti ya Esta yalipokuwa yakigusa kifua chake kipana cha wastani taratibu na yeye alianza kumshika Esta kwenye kiuno na kifuani, hatimaye wakaanza kupunguza nguo kwenye miili yao waliendelea kutomasana kama wapenzi waliokuwa hawajakutana muda mrefu na pole pole wakahamia kwenye mahaba mazito, hakika ilikua ni vurumai mle ndani kwa vita ile isiyoumiza hadi kila mmoja akabaki hoi kabisa.
“Esta wewe ni mwanamke Jasiri na nakushukuru kwa kunibadilisha leo hii najisikia Sele mpya kabisa!” alisema sele akiwa bado anachezea nywele za Esta
“Sele nakuahidi kuanzia siku hii sitakubali tena uishi maisha ya huzuni” tafadhali ngoja niende Lindi kesho halafu nasubiri uniambie nifanye utakachotaka Sele, chochote kile Sele” alisema Esta akiwa amelala juu ya kifua cha Sele.
Usiku ule ulikuwa wa furaha sana kwa wawili wale na ipofika asubuhi Esta alilipa Bili yote ya pale kisha safari ikaanza.
Esta alipata Gari ya Masasi kisha Sele alienda “kazini kwake” kwa siku zote kisha jioni akarejea kama kawaida

*********************************
Wiki mbili zilikatika na taratibu Sele alianza kubadilika, alikua amenyoa nywele zake na kuchonga ndevu zake vizuri , siku hiyo alienda mpaka kwenye kaburi la mama yake maeneo ya sinza akiwa na shada la maua, Sele aliweka yale maua kisha akapiga magoti pale
“mama najua umeona mwanao nimesimama tena, mama nimampata mwanamke anaitwa Esta Chilambo, ni mwanamke mzuri mama ana upendo kama wewe, anasema ananipenda mama, kama ulivyokuwa unanipenda mama, baada ya kuwakamata wale washenzi wote waliofanya ukatili huu mama, basi nitamuoa mama, angalia mama mwanao nimebadilika kabisa mama hata naomba mama niombee msamaha kwa dada Doreen, nimekua kaka mbaya” alisema sele sasa akilia machozi pale kaburini
Alikaa zaidi ya nusu saa kisha akasimama na kujifuta machozi na kusimama na kuondoka,
Sele alikumbuka jinsi alivyokuwa amezinguana na dada yake baada ya kumtaka asichukue hatua kwanza za kulipiza kisasi mpaka pale wakati ukifika
“haiwezekani Gift, huwezi kufanya sasa, watakuua , Wataniua na mimi, jifiche hivyo hivyo mdogo wangu vuta subra kidogo tuu!” alikumbuka maneno ya dada yake huyo, lakini Gift hakukubali, Gift hawezi kusahau siku hiyo akiwa maeneo ya mwenge alimuona mama yake mkubwa huyo mke wa Raisi akiwa katika matembezi yake, alikua amejiandaa kwa siku kadhaa akiwa na bastola yake kuwa popote atakapomuona Yule mama basi angempiga risasi ili kumlipizia kisasi mama yake, wakati msafara unakaribia mama yake mkubwa alishuka huku akiwa amezunguukwa na walinzi alielekea kituo cha watoto yatima kilichokuwa karibu ili agawe misaada Gift alijichanganya kati kati ya watu huku bastola yake ikiwa kiunoni tayari kufanya mauaji, wakati anakaribia kabisa alishtuka kuhisi mikono iliyokua na nguvu zaidi yake ikimshika vizuri kiunoni na bastola yake ikachukuliwa! Halafu akavutwa pole pole kuelekea kwenye gari
Alitupiwa kwenye gari na safari ikaanza aliwekwa kati kati ya watu wawili na watu wengine wawili walikua mbele ambao hawakugeuka na hivyo hakuona sura zao gari ilishika kasi kuelekea nje ya mji na baadae gari ilisimama kisha wakashuka watu wote na Yule mmoja aliyekuwa mbele akarudi sasa Siti ya nyuma na kukaa na Gift akiwa na ile bastola
“nisikilize Gift” alisema Yule jamaa ambaye Gift alikua hamjui kabisa
“unafanya jambo la kipuuzi kuliko upuuzi wenyewe! Usifanye tena huu upuuzi kama unataka kulipa kisasi cha mama yako!”
“wewe ni nani na umejuaje haya yote?” aliuliza Gift
“mimi ni mjomba wako!” alisema
‘lakini mama yangu hajawahi kuniambia chochote kuhusu kuwa na mjomba mwingine!” alisema Gift
“ni kweli , iko hivi Unakumbuka siku ile ukiwa pale Mlimani city na wenzako na ikatokea vurugu?”
“ah nakumbuka ndio kuna mtu akaja haraka na kutuingiza kwenye gari kisha akatupeleka kila mtu nyumbani kwao na akakataa kuchukua pesa?’ sasa Gift alianza kumbuka Yule jamaa
‘ulipomaliza tu kidato cha sita mama yako aliniajiri niwe mlinzi wako kuhakikisha unakuwa Salama, nasikitika sana maana siku ile pengine badala ya kukufuatilia ulipoenda kutafuta dawa ningebaki pale nyumbani!” pengine wasingemuua mama yako
Alisema na yeye sasa akifuta machozi
“najua una hasira lakini nataka kukuhakikishia kuwa siku ukitoa bastola yako tu mbele ya mama yako mkubwa bila hata hujafyatua watakuwa wameshakuwahi na habari za mama yako zitakuwa zimeishia hapo!” alisema
Kuanzia siku ile Gift alilikubali rasmi jina la Sele na kisha akaanza kuishi maisha yake, alikata mawasiliano na dada yake Doreen kabisa kwani alijua ingeweza kuwa njia rahisi ya kumkamata yeye, jambo ambalo alilifanya alimtumia Yule jamaa kusimamia miradi ya mama yake na kisha faida ya ziada alimuingizia Gift katika akaunti zake za Sele, na kama kulikua na ulazima basi walikutana kwa siri nyumbani kwa Yule jamaa,
Sele alifanikiwa kutojiingiza katika ulevi na wanawake, kwani kwa pesa alizokuwa nazo angeweza kuishi maisha ya pombe na kubadili wanawake atakavyo lakini alijua kuwa siku ambayo angeanza kuishi maisha ya kujulikana basi ndio siku ya kukamatwa kwake, kwahiyo Sele alitoka kwenye jumba lao zuri kule mbezi beach akalitafutia mpangaji kwa msaada wa Yule jamaa kisha yeye akaenda kuishi uswazi katika maisha ya chini kabisa ili kusubiri Uraisi huu wa baba yake upite, hata hivyo wakiwa mwishoni kabisa kumaliza mhula wa mwisho wa urasi
Mzee Tuppa alinogewa na madaraka na kubadili katiba kisha akaongezewa tena miaka 10!
Sele alishindwa kuvumilia zaidi na ndipo kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu wakakutana Nairobi yeye na dada Yake Doreen, ambapo dada yake alisema wasubiri miaka hiyo 10 iishe na Gift akasema walianzishe tuu kwa kutumia vyombo vya kimataifa, walipingana na kutoleana maneno makali na kikao chao kikaishia hapo!
Kila mmoja akaenda njia yake na hawakusalimiana wala kuwasiliana tena!
Miaka zaidi ya 7 ilipita wakati leo hii Sele akikumbuka haya akitoka makaburini kwa mama yake
 
MPANGAJI 08
“uncle naomba simu yako kubwa” Sele alisema alipokuwa nyumbani kwa jamaa yake huyo Mr Kibwana ambaye sasa alikuwa ndiye baba na mama yake
“vipi kuna nini leo!” alisema kibwana akimtolea password
“kwakweli nataka kuongea na Dada nimmemmis sana” alisema Sele
“loh, hakika umebadilika sana Gift, wiki hizi nakuona unarudi kabisa katika yule Gift ninayemjua Mimi oooh Asante Mungu!” alisema Mr Kibwana akiwa anamwangalia Gift
“ni kweli umemmis sana dada yako, hebu angalia ushasahau kuwa sasa hivi ni saa 8 usiku huko Italy na kwahiyo huna budi kusubiri” alisema Mr K
Sele waliongea mambo mengi na ndipo Sele amkagusia kuhusu Esta, Mr K alifurahi kwani hii ndio ilikua ndoto yake ya kila siku kuhakikisha kuwa Gift anapata mke, kwani ingemsadidia kupunguza mawazo yake aliyo nayo lakini kusahau kabisa kuhusu kesi, ilikua ni ndoto ya Mr K Kuwa siku moja waachane na harakati hizi,
Mara kadhaa alimshauri Gift aachane na hay mambo na badala yake atafute mwanamke aoe na afurahie maisha yake,
“ona kwasasa una kila kitu Sele, lakini hata hufuarhii chochote, utaishi maisha ya huzuni hadi lini? Ni kweli mama yako amefariki, lakini maisha lazima yaendelee sele!” alisema akimshika bega,
“Naona ni wakati wa mimi kurejea katika maisha halisi” alisema Sele
“nataka ufanye finishing ya ile nyumba kule mbweni, mwezi ujao nihamie!” alisema Sele akiondoka na kuaga, kwa hali Fulani alijisikia amekuwa mwepesi hivi alitoka na kupita kwa jamaa mmoja anayesajili line na kumvuta pembeni
“E bwana nina shida na line ya Halotel” alisema
“ah poa broo utatoa buku mbili, buku ya line buku ya vocha” alisema Yule kijana akisogea
“sasa shida nimepoteza vitambulisho vyagu vyote na nina shida sana ya mawasiliano!” alisema Sele
“una hela?”
“shilingi ngap?”

“utatoa elfu 10 au unipe elf 20 nikutengenezee Royal kabisa kiongozi”
“inachukua muda gani?”
“ah royal ni robo saa tu ukiweka 10 inafunguka menu na uzuri wa hii huna haja ya kujiunga inajiunga automatic na unapata magb ya kutosha” alisema
“okay fanya mishe” alisema sele huku wakisogea sasa kurudi pale kwenye ule mwamvuli
Baada ya dakika 20 line yake ilikuwa tayari kabisa na aliichukua na kulipa kisha akaenda mlimani city kutafuta simu, alitafuta simu moja nzuri sana na kuweka ile line na kutengeneza akaunti kwenye mitandao ya kijamii lakini hakuweka picha yake kisha akarudi zake geto kwake

Usiku huo Sele akiwa nyumbani kwake aliingia facebook na kutafuta akaunti ya dada yake Doreen alimuona dada yake huyo na tayari alishakuwa na familia aliziangalia picha hizo huku machozi yakitaka kumtoka, mara ya mwisho kukutana na dada yake huyo ilikua nchini Kenya zaidi ya miaka 8 iliyopita, pamoja na jitihada za dada yake kumtafuta lakini Gift alikua amekataa kabisa kufanya mwasiliano nae dada yake hakusita kumtumia barua pepe mara kwa mara, na kumueleza maendeleo yake na barua ya mwisho alituma akimtaka Sele aachane na kulipiza kisasi atafute mke aoe na maisha yaendelee
Alitafuta kwenye sanduku yake na kuchukua notebook moja ambayo ilikua na namba ya simu ya Doreen na anuani yake kwa ujumla, kisha akaingiza namba hiyo kwenye simu yake na kuihifadhi baadae akafungua whatsapp na kuikuta ile namba tayari alishapiga mahesabu kama siku zote kwa muda huo huko Italy ingekuwa saa kumi na moja jioni,
Alituma ujumbe mfupi
“dada”
Na hatimaye ujumbe huo ukaonyesha tiki mbili kuwa umepokelewa na bila kupoteza muda alipiga video call
Kwa dakika mbili nzima walitazamana tu huku wakitokwa machozi kila mmoja akilia,
“gift mdogo wangu!, gift mdogo wangu!” alisema Doreen
“Dada!” alisema Gift sasa aliweka ile simu mezani na kukaa vizuri
Waliongea kwa zaidi ya nusu saa na hakika damu ni nzito kuliko maji kwani Hata Gift mwenyewe alikua amemkumbuka dada yake huyo

Waliendelea na mawasiliano na Dada Yake huyo siku baada ya siku, huku mawasiliano yake na Esta yakizidi kuimarika
Sasa nyumba ya kule mbweni ilikamilika kabisa na siku hiyo sele aliondoka na lile sanduku lake ambalo lilikuwa na vitu vyake vya thamani sana, na kupeleka kwenye nyumba yake ya Mbweni

Baada ya mwezi mmoja sele alishamaliza kufunga vifaa vyote vya usalama katika nyumba yake hiyo na kuweka miundo mbinu yote ambayo aliona itafaa, tayari ilikuwa ni likizo ya mwezi wa 6 na alitegemea kumpokea Esta siku chache zijazo,
“safari hii akija harudi tena Lindi” aliwaza sele,
Baada ya siku chache Sele alikuwa stendi kuu ya mabasi ubungo akimsubiri Esta , tayari aliamua kuishi maisha ya kawaida na hivyo alinunua gari dogo la kutembelea,
Majira ya saa kumi jioni Esta alishuka kwenye Basi huku akiangaza macho huku na huku, Sele alimtazama tu wakati anahangaika kutoa simu yake ndipo sele akamsogelea na kumkumbatia!
“Hello baby!” alisema huku akipokea mizigo ya Esta, safari hii Esta alikua na mabegi mawili ya nguo makubwa na box dogo, hakika ilikua ni furaha sana kwa Esta kumuona tena mpenzi wake huyo, walichukua mtu wa kubeba mizigo mpaka pale ambapo Sele alikua amepaki gari yake
Na kufungua buti ya gari kuweka mizigo kisha wakaingia kwenye gari na kuondoka tararibu wakiiacha ubungo..
“so ukaamua kununua Gari mpenzi!” alisema Esta akitabasamu
“yeah, nakushukuru sana Esta bila wewe sijui ningekuwaje yaani” alisema Sele akinyonga usukukani kutafuta sehemu ya mgahawa.
Walifika na kupata chakula cha mchana kisha wakaendelea na safari,
‘mama Mwajuma anajua umekuja leo?” aliuliza Sele!
“anajua nakuja lakini sikumwambia siku!”alisema Esta
“ohh afadhali, sasa hapa Esta nataka twende kwangu leo!” alisema sele huku akifungulia mziki kidogo kwenye radio ya gari

“umehama pale?” aliuliza Esta
“hapana pale nipo ila kile chumba kina historia yangu tu kwahiyo kipo vile vile sema naenda mara chache sana!’ alisema
“okay kwahyo huko ni wapi!”
Kunaitwa mbweni ni kuzuri sana kumetulia sana alisema Sele huku akipeleka mkono mmoja kwenye paja la Esta
“Sele acha jamani usije kuleta ajali hapa!” alisema Esta huku nae akiwa ameanza kusisimka
Baada ya mwendo mrefu walifika kwenye nyumba moja nzuri iliyokua uzio na geti jeusi, Sele alitoa rimoti ndogo na kubonyeza geti lile likafunguka na kisha akaingia ndani mpaka kwenye sehemu maalum aliyotengeneza kuwekea gari lake kisha wakashuka akafungua buti na kuweka mizigo yote chini baadae akafunga geti na kubonyeza namba Fulani hivi kwenye mlango na kuufungua na kuingia ndani
“Sele una nyumba nzuri sana yaani! Yaani siamini kuwa kwenye mjengo kama huu!” alisema Esta
“hahaha usinichekeshe bhana, hata hivyo karibu sana huku kunaitwa mbweni, kwa pembeni hapo ndio kuna kambi ya jeshi, na sio mji mkubwa sana ndio kunaanza kuchangamka changamka”alisema Sele
“Sele ntaka nioge kwanza maana sio poa” alisema Esta akipunguza nguo zake
Sele alimpeleka chumbani na kisha akaipanga mizigo yake vizuri kwenye kabati
Esta aliingia bafuni Sele nae alivua nguo na kujifunga taulo kisha akamfuata Esta bafuni

Siku ya Pili Sele amlimpigia Mr K ambaye alifika kisha akamtambulisha kwa Esta,
Mr Kibwana alifurahi sana kumuona Esta na kisha akatoa nasaha zake kuwa Esta hana budi kushirikiana na Gift katika kuhakikisha haki yake inapatikana
“kwasasa fanya yote atakayokuambia Sele na kuwa nae bega kwa bega” sisi tutamaliza masuala yote muhimu tutakwenda kwa bibi yako Morogoro na kwa mama Mwajuma pale kumtambulisha Sele” alisema sasa Mr K akiaga
Sele alitoka nje kumsindikiza mgeni wake huyo
 
Kazi nzuri sana
Tupo pamoja
 
Kazi nzuri sana
Tupo pamoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…