Hadithi: Mpangaji

Hadithi: Mpangaji

"MPANGAJI 01
Hakuna mpangaji yoyote ambaye alikuwa anafahamu asili ya Yule mpangaji mwenzao, hata jina lake la ā€˜sele’ wapo waliosema halikua jina lake halisi, lakini yote kwa yote Sele kama unavyoweza kusema alikua mpangaji wa kudumu wa mzee Mhina, miaka ilikatika na sio mzee Mhina wala wapangaji ama watoto wake walijua kazi halisi ya Sele,
Wapo waliosema sele alijihusisha na kazi ya kuzibua vyoo huko mjini mbali na hapo, wengine walisema sele Alikuwa mtu wa ā€˜kitengoā€ na kama ilivyo kawaida ya wabongo basi wengine walizua kuwa sele ni jahili mzoefu,
Kwanza Sele asingetoka nje ya chumba chake bila kuitwa, na kwakuwa chumba chake kilikua ni selfu basi huwezi kujua kama sele yupo ndani au ametoka,"


Nimekumbuka Mwanzo wa story ya Bigi ya Steve.....


Naweka kambi rasmi hapaa!!

Wapii Tayukwa Lovelovie Bantu Lady Kalpana baby zu Kigi Makasi Tyrone Kaijage mmash Restless Hustler Unforgettable Mafian cartel mtzmweusi mshaisoma hii storee???
Tumeshawasili dyadya...
 
MPANGAJI 03

Sele hakukaa hata kidogo aliondoka zake mara tu baada ya kumuacha Ester pale kwao,
Sasa Ester alizunguukwa na wapangaji wote waliokuwepo wakitaka awaeleze kuhusu Sele,
ā€œhivi anaongea kabisa, halafu anacheka?ā€ aisha alidakia
ā€œjamani Sele ni mwanaume mzuri tu kama walivyo wanaume wote, yaani sijui nisemeje ni binadamu kabisa!ā€ alisema ester sasa alishachoka kufanya mahojiano ambayo kwa uono wake yeye haukuwa na kichwa wala miguu,
ā€œhaya tuambie mlikula nini, kawhiyo Sele pia anakula kabisa!ā€ aliuliza mama Mwajuma!
ā€œhahahaha jamani mama, eti anakula, kwahiyo bado mnaamini Sele ni Zimwi, sijui jini huko..ā€ alisema ester akiingia ndani
ā€œna mizigo yote hii mwanangu umemaliza mshahara wako huko!ā€ alisema mama mwajuma
ā€œhapo vitu vingi kaninunulia Seleā€ alisema Ester sasa akiangalia hotpot lilipo ili achukue chakula
ā€œmh makubwa haya jamani!ā€alisema mama Mwajuma sasa akimtafutia maji ya kunawa mwanae

Ndani ya muda mfupi Sele alizoeana kabisa na Ester na sasa unaweza kuwakuta wamekaa nyuma ya nyumba usiku wakipiga soga huku wakicheka kabisa, hata hivyo Sele alikataa kata kata kumueleza chochote kuhusu maisha yake pamoja na Ester kujinasibu kumuelezea hadithi zake za mahusiano yaliyopita na maisha ya shule kwa ujumla , Sele hakuthubutu kumueleza chochote,
Na sasa waliweza kubadilishana namba za simu na siku nyingine wangechati mpaka usiku wa manane,
Baada ya sikukuu ya Pasaka sasa Ester alipaswa kuondoka kurudi kazini kwake lindi , Tayari mkuu wake wa shule alishampigia kumkumbusha umuhimu wa kurejea mapema,
Hivyo siku hiyo Ester alitumia muda wake kwenda kariakoo kununua vitu baadhi alivyodhani vingemfaa , aliwaza na kuwazua akaona atafute zawadi ndogo kwa ajili ya Sele na hivyo akaingia duka moja la kuuza simu na kununua simu janja aina ya Tecno F2.

ā€œbila shaka Sele atafurahi kuwa na simu hii janja, na nitakuwa namtumia picha zangu nay eye ananitumia zake nikiwa Lindiā€ aliwaza Ester.
Alirudi nyumbani na kuandaa mizigo yake tayari kwa safari kesho yake, baada ya kumaliza alitoka nje kwenda kumsubiri rafiki yake Sele ambaye alifika kwa wakati kabisa,
ā€œyaani umejuaje kunisubiri hapa!ā€ alisema Sele akiwa na bashasha kweli kweli,
ā€œah yaani acha tu wewe mwanaume una kismati maana hata sijui kwanini nimekuzoea hiviā€ alisema Ester bila kujielewa
ā€œnisubiri basi hapa nikaweke mizigo then nitakukuta hapa nje!ā€ alisema Sele akiingia ndani
ā€œmh yaani mpaka naondoka sijaingia chumbani kwako Kaka sele Jamani!ā€ alisema Ester akipiga hatua kumfuata Sele,
ā€œHAPANAA!!ā€ alifoka Sele , mpaka mwenyewe akashangaa na kurudi nyuma kwa ester kuomba radhi,
ā€œnisamehe Ester, kwakweli hakuna mtu ataingia chumbani kwangu , nasikitika nimekufokea nisubiri tu nakujaā€ alisema Sele akiingia ndani haraka
ā€œnitaingia hiki chumba Sele, kama sio leo basi kesho!ā€ alijisemea Ester akimsubiri Sele atoke
Sele alitoka baada ya dakika chache tu kisha wakasogea kwenye msingi wa nyumba ambao ulikua haujaisha na kukaa kupiga Story,
ā€œyeah kama nilivyokuambia kesho nasepa Sele nitakumisi sana!ā€ alisema Ester kwa uchungu kidogo
ā€œyeah, ndio hivyo kazi ni muhimu sana Ester inabidi uende mimi mwenyewe nitakumisi ujue, wengine wananitenga mara waniite zimwi, siijui jinni.. hahahaha!ā€ alisema sele akimalizia na kicheko
ā€œhahaha yaani nakuambia kabla hatujaonana nilikua naambiwa sana habari zako , ila kumbe mtu mwenyewe wala hata hauko hivyo,ā€ alisema Ester akilala kwenye mabega ya Sele
ā€œhahaha mawazo yao tu, sema unajua maisha ya Dar kila mtu na hamsini zake kwahiyo nadhani watu wako bize sana kutafuta riziki ndio maana wananifikiria vibaya!ā€ alisema Sele
ā€œkaka Sele nimekuletea Zawadi hiiā€ alisema akitoa ile simu kwenye box lake na kumkabidhi Sele,

ā€œloh asante sana Ester kwa smartphone hiiā€ alisema Sele akiichukua
ā€œooh asante kwa kushukuru, ndio sasa nikiwa Lindi nitakuwa nakupigia video call, nakutumia picha na video zangu Sele!ā€ alisema Ester kwa furaha
ā€œsikiliza ester mimi situmii mtandao wowote wa kijamiiā€ alisema Sele kwa upole huku mkono mmoja akiwa ameuweka begani kwa Ester
ā€œsele unasema kweli?ā€ Ester alihamaki akimtazama Sele machoni hakuamini kabisa maneno haya yanatoka kwa kijana mwenye umri wa miaka 30-33 hivi
ā€œyaani hutumii facebook, insta, whatsapp?ā€ aliuliza Ester na Sele aliatingisha kichwa tu kuashiria anakubaliana nae..
ā€œbasi ni kweli kuna tatizo Sele!ā€ alisema Ester sasa akitoa kitambaa chake kwenye suruali aliyokua amevaa akifuta machozi na kisha akasimama na kuondoka kurudi ndani
ā€œrudi esterā€ Sele alijaribu kumuita lakini tayari Esta alishawahi kulifikia geti kurudi ndani
ā€œnilijua tu atachemka, mimi ni Zimwi kweli!ā€ alijisemea Sele akipiga ngumi kwenye mchanga kwa hasira alijisikia vibaya sana kuagana na esta katika hali ile esta alirudi ndani na kukimbilia Chumbani kwake alijikuta akilia bila sababu mpaka yeye mwenyewe akawa anajishangaa
ā€œTriiiiiaā€ simu yake ilitingishika kuashiria ujumbe mfupi uliingia
Aliufungua na kusoma ulitoka kwa sele
ā€œNINA ZAWADI YAKO PIA TAFADHALI UJE UICHUKUEā€
Esta aliwaza kama aende ama abaki lakini baadae alijiona mpumbavu kulia mbele ya mtu ambaye hata hakuwa na mahusiano yoyote
Alijikaza kisabuni na kutoka nje na kumkuta sele akiwa ameshikilia begi dogo hivi la wastani
ā€œhii zawadi yako Estaā€ alisema akimkabidhi kisha akageuka kurudi chumbani kwake!
ā€œna hili begi, mbona kama kuna uzito humu?ā€ aliuliza esta,
ā€œbhana ni zawadi yako vyote pamoja na begiā€ alisema Sele akitabasamu kisha akaendelea na hatua zake kadhaa kuingia kwake,
Esta bado alikua na shauku ya kujua ndani ya begi kulikua na nini, hivyo aliangalia huko na huko kuhakikisha hakuna mtu pale nje kisha akaingia ndani na kufungua lile begi..
Ndani kulikua na komputa mpakato mpya kabisa aina ya apple ikiwa katika makaratasi yake
ā€œwhaaatā€ Esta aliweka ile komputa kitandani huku akiwa haamini, hakujua kama afurahi ama la, haraka alichukua Simu yake ana kuingia mtandaoni na kwenda kwenye google kisha akatafuta ā€œapple sx400 min series priceā€ bila hiyana google wakamletea $1,100 , alijaribu kubadili pesa hizo na kuweka kwenye pesa ya Tanzania na kukuta ni zaidi ya million mbili!
ā€œyaani huyu Sele ananinulia mimi zawadi ya million mbili?, sele huyu katika nyumba ya kupanga ya kawaida tu?ā€ Sasa akili yake ilimwambia huyu ā€œseleā€ sio mtu wa kawaida kama alivyokuwa anamchukulia,
Aliwaza na kuwazua kisha akaona ngoja acheze huu mchezo
Alichuchukua simu yake na kuandika ujumbe mfupi kwa sele
ā€œasante sana kwa zawadi dear ila nina ombi mojaā€
Kisha akutuma kwa sele , baada ya muda mfupi yake simu yake ilitoa ishara kuwa ujumbe ule umepokelewa na hivyo akasubiri jibu
ā€œyap karibuā€ sele alijibu
ā€œnaomba sana kesho unisindikize hadi ubungo tafadhali sana, naomba sana kesho usiende kabisa kaziniā€ aliutuma ujumbe huo kwa sele
ā€œEsta nilishapanga hilo nisingekuacha uende mwenyewe bestā€ alijibu sele kisha wakaagana
Kila mmoja aliwaza kuhusu mwenzake
Badala ya furaha Sele alijikuta machozi yakimtoka, alienda kwenye sanduku lake ambalo alikuwa ameliweka kwenye kabati ya nguo,
Alitoa bahasha kadhaa kisha akatoa picha mbili aliziangalia muda mrefu huku machozi yakimtoka
ā€˜nipe Baraka zako , nipe Baraka zako!ā€ alisema huku machozi yakimtoka akiwa ameshikilia zile picha,
Sele sasa hakuweza kutazama zile picha zaidi alizirudisha na na kisha akaenda bafuni alifungulia maji tu yakimwagikia mwilini na mwishowe akagundua kuwa alikuwa hajavua nguo zake kumbe


Mambo yanazidi kunoga lol!!

Ester na Sele on the line 1 and 2!!

Ngoja tuone šŸ™‡
 
"women will always let you down"

Alisema mwamba mmoja kwenye movie ya Bag man
 
Nimeweka namba Hapo napokea ushauri, maoni, pongezi na hata "bando" pia kama alivyoshauri Mcheza Viduku
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Watu wa JF wabahili saaana. Cha kufanya ni kuhamishia mzigo Telegram. Watu walipie bukubuku.



Kama mtu unashindwa kuandika Pongezi, huyu anayeandika simlizi ndefu hivi unajua anatumia muda kiasi gani?? Uchovu wake??
 
"ā€˜wewe ni mzee Lota, una watoto wanne , watatu wa kike na mdogo wa mwisho wa kiume, Yule ni Aisha na mumewe Mkude, Yule ni mama Mama Mwajuma na mume wake Ngoda, pale ni Isa , kule ni John na hapa ni kaka Ephraim na mke wake mama Joan’"


Sele nyookkoo

Pozi lazima ziliwaisha hapa

Aaliyyah kuna story ya Sele hukuu!!
Kati ya sehemu zilizonifurahisha sana kwenye hadithi ni hapa....
 
Back
Top Bottom