MPANGAJI 13
by CK Allan
“dokta James , Yule ni Mtoto wa Dokta james ambaye ndio alikua daktari wa Yule mama Doreen,” Alisema Yule muuza duka na kumfanya Sele sasa atake kuzimia
“ni kweli tarifa hua zipo tu zinaelea, unaweza kupaa kuzifuata au utume chombo kukuletea” aliwaza
“ah kwahiyo Yule Bwana mdogo ni Jose si ndio!” aliuliza Sele
“ndio Jose Yule, Dogo tangu dingi yake avute amekuwa kama teja hivi anaropoka tu, unajua bhana wakati mwingine kuna watu hawana huruma,”
“basi broo mi nipo hapa kuna pisi imenielekeza ipo mitaa hii ila naona nimefika mpaka hapa hola na simu hapokei”
“ah pisi za sinza nyingi pasua kichwa broo, itakuwa umepigwa” alisema Yule muuza duka
Sele alijifanya kusoma sms kwenye simu yake na kuaga
“ah amesema yuko kule juu kijiweni’ alisema akilipa pesa ya soda na kuondoka
Aliwaza na kuwazua na hakuona namna ya kumsaidia Jose kwa wakati ule ingawa aliamini kuwa lazima atafuatiliwa, hata hivyo alijua hawezi kudhurika mapema maana watu wataunganisha doti kwa urahisi
Mzee Lukas sasa alikua alikua akiwasubiri kwa hamu vijana wake ambao walirejea baada ya kuhakikisha mke wake ameondoka sasa vijana wake walimpa habari zote
“Yule ni kijana wa dokta James, anaitwa Jose, kama unavyojua alikua na urafiki kiasi na Gift, kwahiyo mara nyingine dokta James alipokuwa anaenda kwa mama Doreen alikua anaenda nae na akawa anacheza michezo ya video na Gift, inaonekana wakati baba yake anaondoka siku ile alijua anakokwenda au kuna kitu dokta alikua amemueleza mwanae”
Alisema Joshua
“vipi mnadhani kijana wangu Gift yuko hai kama alivyosema?” aliuliza Mzee
‘hapa tuweke hamsini kwa hamsini uhakika tunao sana kwa dada yake Doreen,”
“achana na Doreen, Doreen yupo kwa mume wake huko Italy unadhani mimi nilishindwa kumpata Doreen? Lakini unadhani ningemtazama vipi usoni? Wakati anajua kabisa mama yake ameuawa na mimi sijafaanya kitu?” alisema Mzee Tuppa machozi yakimtoka
“nisikilizeni Yule shetani ataenda kumuua Yule Jose na mama yake masikini, ili kufuta ushahidi wa ushetani wake safari hii sitamsamehe yeyote endapo hilo litatokea” alisema Mzee Tuppa
‘tumelizingatia hilo na tunafanya utaratibu wa kuhakikisha wanakuwa salama mzee” alisema Joshua huku akiondoka na wenzake kwenda sehemu zao za kupumzika
“yaani kuwa mlinzi wa raisi ni heka heka mwanzo mwisho, sijui mwisho wangu utakuwaje yaani” alijiwazia Joshua
Upande wa pili Mama Joan nae alikua anaongea na walinzi wake na kuweka mikakati yao
“kwahiyo kumbe ni mtoto wa dokta James eeh, aah sasa naelewa kwanini alikua anampigia chapuo mke wa marehemu’ aliwaza mama Joan akikumbuka jinsi mke wa dokta James alivyolipwa mafao mengi na fidia kubwa na vitu vingine vingi! Kumbe alikuwa na mtoto wa kiume yue mshenzi
‘nataka wiki hii isiishe huyo mpuuzi awe amefariki” sitaki mfanye upuuzi wowote na hakikisheni kama kuna kiumbe chochote cha Lukas kinaishi, nataka nimalizie uzee wangu kwa amani mimi” alisema mama Joan
“Lukas , utajilaumu sana” aliwaza mama Joan huku akizunguusha zunguusha simu yake
Alitoa maagizo hayo kwa vijana wake kisha aktoka sehemu hiyo ya makutano na kuondoka haraka kurejea nyumbani, alairudi na kumkuta mume wake huyo nae akiwa katika Lindi la mawazo alijua fika mke wake alitoka wapi na alipanga nini , lakini wanasema aliyetangulia ametangulia tu, Mzee Lukas alikua hatua kadhaa mbele ya mke wake
Akili yake ilijua kabisa mwanae Gift atakuwa hai, kama ilivyo kwa dada Yake Doreen, mara kadhaa alijaribu kumpigia simu Doreen, lakini alipopokea simu hakuongea chochote, pamoja na kwamba alitangazwa kuwa amekufa lakini kijana yake mmoja ambaye alimpenyeza kwa siri kumchunguza mkewe, ndie aliyekuja kumpa taarifa kuwa aliyeuawawa usiku ule alikua ni mlinzi pamoja na daktari na sio mlinzi na Gift katika ile miili minne kwa miaka Yote hiyo Mzee Tuppa alijitahidi kumtafuta mwanae kwa siri lakini aliona kila anavyokaribia anaweza kumpa nafasi mkewe pia kujua mwanae huyo alipo na pengine kabla yake, wasi wasi huu ndio ulimfanya mzee Lukas kusubiri mpaka majukumu haya makubwa yapite kisha “aingie mzigoni” mwenyewe kutafuta namna ya kurejesha familia yake hii
Aliwaza haya sasa akimuangalia mkewe wake huyo
“kwanini umemsamehe? Nakuuliza Lukas, hivi unaona watu wanatuzungumziaje huko kwenye mitandao? Hebu amka Lukas wewe bado ni Rais ujue” alisema mama Joan akiingia ndani akimpita mume wake pale nje
********************************
Sele alikua bize akiweka mikakati yake tayari alikua na sehemu ya kuanzia, hata hivyo hakutaka kufanya haraka ya kwenda kwa Dokta James kwani alijua fika sasa ile nyumba itakuwa inapigwa jicho kali alijaribu kusoma taarifa kadhaa za dokta James kupitia mtandao lakini hakupata taarifa za kumfaa sana
Siku hiyo aliamua liwalo na liwe alipanga kwenda usiku nyumbani kwa dokta James na kuonana na familia yake alifika na kupaki gari hatua kidogo mbali na nyumba yao kisha akashuka na kusogea mlangoni na kubonyeza kengele ya mlangoni , baada ya muda geti lilifunguliwa na na msichana mmoja hivi umri kati ya miaka 17 hivi, na kumkaribisha ndani,
“bila shaka ni mgeni wa kaka Jose,” alisema akitabasamu
“ah Ndio Ndio kwani vipi!? Sele aliuliza
“ah yaani kuanzia asubuh kila mtu anakuja, sijui wa online Tv, redio magazeti n.k” alisema huku akionyesha nae amechoka kufungulia wageni
“ah yupo, ndani?” sele aliuliza
“ndio yupo, lakini kwakweli sidhani kama atakubali kutoka nje maana amesema hataki tena kuonana na waandishi wa habari yaani” Alisem
“mimi sio mwandishi wa habadari dadaangu nina shida binafsi nay eye, tafdhali sana” alisema huku akiweka mikono yake kifuani ishara ya kuomba
Hata hivyo baadae alitoka akiwa na uso wa kukata tama
“amekataa kabisa na hata mama amesema kwa leo inatosha Tadhali naomba nifunge geti”
Alisema Yule msichana na sele akatoka nje ya geti,
Aliangalia saa yake tayari ilikua ni saa tatu kasoro usiku, hakutarajia kuwa Jose alikuwa anapata wageni wengi kiasi hicho, lakini hata hivyo tayari ilishakuwa story kubwa na waandishi wasingependa kukosa kila hatua ya skendo hiyo
Alitoka nje na kusogea mahali alipokuwa amepaki gari lake aliingia na kuanza kuondoka taratibu mara ghafla akapishana na gari aina ya noah iliyokuwa na vioo vyeusi alipunguza mwendo na kuanza kupaki pembeni kisha akageuza kulifuatilia lile gari sasa watu wawili walishuka na kuanza kutembea kwa kasi kuelekea ilipokuwa nyumba ya akina Jose,
Aliamua kupitiliza kana kwamba hakuona chochote huku akitafuta upenyo wa kuzunguuka kurudi tena, wakati anajiuliza aliona gari nyingine ikiwa imepaki huku taa zimezimwa lakini kwa harakandani kulikuwa na watu,
“mmh hapa kuna kitu kinaendelea lazima” alisema akiipita na ile gari nyingine na kisha akatafuta upenyo na kuipaki gari kisha akarudi kwa miguu, wakati anakaribia kwenye ile gari aliona mtu mmoja akija kwa kasi na kuingia kwenye ile gari na kisha ikawashwa na kuondoka pale, bila kujiuliza mara mbili alirudi haraka na kuingia kwenye gari yake kujaribu kuwafuatilia, alipita pale kwa akina Sele na tayari watu walikua wameanza kukusanyika nje aliona kwa mbali Yule msichana aliyempokea muda mfupi akilia akiwa ameshikana na mama mmoja hivi
Aliongeza kasi na kweli kwa mbali aliona ile gari mbele yake,
Aliifuatilia na walipofika sinza kumekucha wakapinda kulia kuelekea mwenge Sele alizidi kufuatilia na mwishowe akawakaribia kabisa na sasa aliamini bila shaka gari iliyokuwa na Sele itakuwa mbele ya ile gari nyingine,
“vipi kama hawa ni kikosi kimoja nah ii gari moja ilikua kwa ajili yakuzuga tu?” aliwaza sele sasa akizidi kukanyaga mafuta, walipofika maeneo ya afrika sana, gari walielekea kushoto na kunyoosha hatimaye walitokea katika jengo moja la hoteli ambalo lilikuwa linajengwa na halikukamilika, lile gari likapunguza mwendo na kuingia, Sele kama kawaida alipitiliza na kisha akapaki gari na kuzima taa kisha akarudi mbio mbio kwa kunyata na kuingia kwenye lile jengo alizunguuka na kutafuta njia kwa mwanga hafifu na hatimaye akainama kwa kunyata huku akichungulia na akaanza kusikia sauti
“hamuendi popote na huyo dogo muacheni”
“bro nakuheshimu sana ondokeni hii misheni haiwahusu’
‘sikiliza T, unanijua vizuri, mzee hatawaacha salama amesema huyu dogo asiguswe”
“broo kama unatuchelewesha tupishe mama anamtaka huyu dogo ujue, hata hapa kupaki ni kwasababu ya heshima yako tuu”
“hebu kuwa muelewa wewe jamaa, mnazidi kumchafulia mzee hamjui tu wewe na huyo bi mkubwa wenu sasa hivi kesho magazeti na vyombo vyote vya habari watatangaza dogo amepotea unadhani nani wa kwanza kulaumiwa? Mmelifikiria hilo wewe na huyo mama yenu Shetani?”
Sasa sele akili zake zilikaa sawa alielewa kabisa haya ni makundi tofauti mama dhidi ya baba na mama yake ndie aliagiza Jose auwawe lakini baba yake ndie ameagiza kundi linguine kuzuia
Wakati akitafakari mara ghafla ukatokea mwanga mkali na kuwamulika pale