Hadithi: Mpangaji

Hadithi: Mpangaji

MPANGAJI 21
By CK Allan
“baada ya muda tuliondolewa kwenye nyumba ile na kuhamia kwenye nyumba ambayo tunaishi hadi leo” alimalizia Jose huku ajifuta machozi
“je mlipata mafao yoyote ?” aliuliza Rapha
“hapana, hakuna malipo yoyote tuliyopata na hata baba yetu mkubwa ambaye ndie alikuwa anafuatilia yale mafao alifariki mwaka jana na hivyo tulishindwa tena kufuatilia”
“pole sana Jose, ni kwanini unahisi kifo cha baba yako kilitokana na kuuwawa?” aliuliza Rapha
“kuna siku moja ya wikiendi nilienda kule mikocheni kwa akina Doreen wakati tunacheza michezo hii ya kwenye computa mimi na Gift, kwa bahati mbaya niliangusha glass ya maji, yakamwagika kwenye waya wa umeme na cheche za moto zikatokea lakini umeme ulijizima ghafla nyumba nzima na kengele ya tahadhari ikalia, wote tukatoka ndani ya nyumba wakati tunatetemeka na kuogopa mama yake Gift alitoka nje akiwa na viti viwili alikuwa anatabasamu nakumbuka alikua anacheka halafu akasema kuwa kwanini sisi wanaume tunakimbia alarm tu Gift alimwambia mama yake kuwa tulisababisha shoti ndio maana tukakimbilia nje, mama yake akasema kuwa shoti ya umeme isingeweza kutokea kutokana na vifaa vilivyokuwa vimefungwa na zaidi sana umeme utajizima tu na alam inapolia basi inatoa taarifa moja kwa moja kwa kampuni yao ya ulinzi ambayo hufika ndani ya dakika 10 tu, na kweli kabla ya mama hajamaliza kuongea tulisikia honi nje na kweli walinzi na mafundi walikua wamefika ambapo dakika chache tu walimaliza na sisi tukarudi ndani kuendelea na game letu”
Alimalizia Jose
“hii ina maanisha nini Jose?” aliuliza Rapha
“toka siku ile nilifuatilia zaidi kujua ulinzi huo wa mfumo wa umeme na ni kugundua ni kweli, kama ni kweli kulikua na shoti ya umeme kama walivyodai basi mafundi wale wangeweza kuthibitisha, lakini hadi leo wale mafundi na ile kampuni ya ulinzi sijwahi kuona taarifa zao tena, kitu ambacho sio kawaida na kingine tulikuta geti likiwa wazi na tuliona gari inatoka nje ya nyumba” alisema Jose akilia
“mheshimiwa hakimu kwanza nataka kusema kuwa shahidi anatoa ushahidi wa uongo
Ni miaka zaidi ya 17 sasa toka tukio hilo litokee, shahidi alikuwa mtoto mdogo tu anawezaje kukumbuka taarifa kiasi hicho? Hizi ni taarifa za kupangwa tu kumchafua mteja wangu!”
Mteja wangu hakufanya mauaji yoyote ambayo anasingiziwa kuyafanya! Alisema wakili

“mheshimiwa hakimu bado nina shahidi mwingine! Alisema Rapha ambapo aliingia mtu mwingine ambaye baada ya kuapa nae alipanda kizimbani
“iambie mahakama hii tukufu unafanya kazi gani na umeifanya kwa muda gani!” alikua ni Rapha akimhoji shahidi huyo
“naitwa Musa Kiangi ni fundi umeme na vifaa vya umeme katika kampuni ya UGO electricity nimefanya kazi hii kwa takribani miaka 20 sasa kwa ujumla ndio kazi yangu inayoniingizia kipato”alisema
“bwana Musa tuambie je inawezekana kufunga vifaa vya kuzuia moto kwenye majumba hususani moto wa kusababishwa na hitilafu ya umeme?” aliuliza Rapha
“Mwanzoni ilikuwa ni umeme tu lakini kwa jinsi teknlojia inavyokwenda kasi unaweza pia kufunga vifaa ambavyo vitatambua vifaa vyote vya ndani ya nyumba kama vile majiko, gesi , vifaa vya umeme n.k”
“hebu tuambie vinafanyaje kazi?” aliuliza Rapha
“mteja atafunga vifaa vyake ktika mfumo wa komputa vikiwa katika hali ya kawaida yaani Normal na pia atauambia mfumo kuwa utoe taarifa ikiwa kifaa Fulani kitakuwa hakipo katika hali ya kawaida kwa mfano kama joto litazidi, umeme utazidi kiasi au kupungua kiasi, kisha mfumo huo utamjulisha mtumiaji kwa kupiga kelele msisitizo yaani alamu kisha mtumiaji akichelewa kufanya uamuzi basi mfumo huo utajizima na kuzima hicho kifaa husika kama ni jiko, feni, friji n.k” alisema Fundi Musa
“ni hayo tu mheshimwa sina swali tena!”alimalizia Rapha na kisha ikawa zamu ya wakili wa mshtakiwa kuuliza maswali
“Bwana Musa, uhakika wa vifaa hivi ni asilimia ngapi? Maana tunajua hakuna kitu ambacho hakikosi kasoro!”
“ni kweli lakini huu mfumo kazi yake ni kutambua tu vifaa vyako ambavyo umeshavinganisha na kama vitaenda tofauti basi mfumo unakujulisha wewe mmiliki” alisema fundi
“hujanielewa, nauliza hivi inakuwaje endapo mfumo ukatoa taarifa za uongo? Mfano ikakuambia fridge ni bovu kumbe sio bovu? Huu mfumo hauwezi kukosea?” aliuliza wakili
‘kama umenisilikiza mfumo kazi yake ni kutoa taarifa tu kwa mmiliki, mmiliki ndie ataenda kwenye kifaa husika na kukikagua ndani ya dakika tano tu, vinginevyo kwa ajili ya tahadhari mfumo utajizima, kwahiyo mfumo hautengenezi kifaa bali mmiliki!” alisema Musa
“basi mheshimiwa sina swali jingine” alisema wakili
Kwa hivi
Mawakili wa pande zote mbili walikuwa bize kuhakikisha wateja wao wanakuwa salama kabisa na kuondokana na madhila hayo ya kesi mama Joan aliikana ile video huku akisema sio yeye na wala hakumtambua mwanamke Yule kwenye video ile wala wale watu waliokuwa pale kwenye ile video!
Video ile ilirudiwa rudiwa na mwishowe ilimuonyesha mama joan akiingia kwenye gari na watu wake wakati nyumba ikiwa inateketea kwa moto hata hivyo alikanusha kabisa ni wakati wanataka kuahirisha tena kwa muda ndipo mwendesha mashtaka alienda kumnong’oneza hakimu jambo na kisha akasema yupo shahidi mwingine wa kujitolea katika kesi hiyo, kila mmoja aligeuka kutazama mlangoni ambapo nusura mama Joan aanguke baada ya kumuona Fred dereva wake akiapa na kupanda kizimbani
“haya iambie mahakama wewe ni nani na upo hapa kufanya nini?” aliuliza mwendesha mashtaka na kuwafanya sasa watu wote kuduwaa akiwemo Gift ambaye alimkumbuka Fred baada ya miaka kadhaa kupita
“naomba muweke ile video pale mwishoni” alisema Fred na kisha mwendesha mashataka kwa kutumia rimoti ndogo akawa anaipeleka mbele hadi wakati wa gari ianondoka
“simamisha hapo” alisema Fred akinyoosha mkono
“mimi ndio nilikuwa dereva wa hilo gari! Mheshimiwa hakimu!” alisema Fred
“haaaaaaaaaaaa” sasa mguno mkubwa ulisikika pale mahakamani
“umesikia ulichokisema wewe kijana?” mwendesha mashtaka aliuliza
“namaanisha mimi ndio nilikuwa nimewapeleka kwenye hiyo nyumba kwakuwa mimi ni dereva wake madam hata sasa hivi mimi ndio nimemleta hapa mahakamani” alisema Fred akiweka vizuri koti lake la suti ya bluu aliyokuwa ametupia siku hiyo
Alikumbuka jana jinsi mzee Lukas alivyokuwa ameongea nae kwa upole akimsihi afanye jambo
“wewe ndio unaweza kunisaidia Fred, sisemi kwamba unanilipa fadhila, lakini angalia watu wasio na hatia wanaenda kuhukumiwa, zaidi sana naweza kwenda kutengana na wanangu niliowapenda kwasababu ya huyu shetani!,Fred nakuomba kijana wangu, usipofanya hivi mimi nitaenda mwenyewe kufanya hivyo!!” Fred alikumbuka maneno hayo na sasa akaamua kama mbwai na iwe mbwai

Wakili wa mama Joan alisimama kutaka kumhoji Fred lakini akajikuta anauliza maswali ya kawaida sana na hivyoa akarudi kukaa na sasa ikawa zamu ya Rapha
“Fred, umetenda jambo la ushujaa sana, lakini tuambie mlienda kufanya nini haswa kwenye ile nyumba?” Rapha aliuliza
“mojawapo ya masharti ya kazi yangu ni kutomuuliza Bosi wangu anaenda kufanya nini? Huwa swali langu ni kumuuliza tu natakiwa tu kumpelela mtaa gani ama wapi, kama sio zile ratiba za kawaida za ofisini” alisema Fred
“hapa inaonekana ni usiku, je ulikuwa wapi wakati unapewa taarifa ya kwenda kule mikocheni?” aliuliza Rapha
“mimi ofisi yangu ni kweny gari langu, kama mama hajaniambia nikalale huwa nakuwa kwenye gari mpaka nitakapoambiwa kwenda kulala ndio naenda na simu yangu inakuwa on muda wote”
Alisema Fred
“kwa maana hiyo uliipata taarifa hiyo kuwa muende mikocheni usiku ukiwa kwenye gari?”
“ndio alikuja mlinzi wa mama kwenye gari na tofauti na siku zote yeye ndio alikaa mbele kunielekeza njia ya kupita na mama alikaa nyuma na walinzi wengine wawili”
“je walikuwa wanaongea chochote labda kuhusu wanachoenda kufanya?” aliuliza Rapha
“hapana sikumbuki, na huwa sio kawaida yangu kufuatilia bosi anachoongea kwenye gari kama hakijanilenga mimi moja kwa moja!” alijibu Fred
“wakati mnafika mikocheni kwenye hiyo nyumba ilikuwaje?”
“mimi nilibaki kwenye gari wao wakaingia ndani na kisha wakatoka na ndio mama akaamuru niondoe gari kwa kasi kurudi nyumbani”
Alimalizia Fred
“asante Fred mheshimiwa hakimu sina maswali mengine tena” alikaa chini huku akitabasamu
Mama Joan alimuangalia sasa wakili wake kama mtu anayeuliza “imekuwaje” sasa hakuweza kumtazama Fredi ambaye aliondoka pale akisindikizwa na Polisi
“Mshtakiwa unaweza sasa kuiambia Mahakama hawa watu wengine ambao wanaonekana katika video hii?” mwendesha mashtaka alimuuliza mama Joan ambaye alikaa kimya baada ya kumuangalia wakili Wake na kumtingishia kichwa ishara kuwa akatae!
 
MPANGAJI 22
By CK Allan

“Mshtakiwa tafadhali jibu, unaweza kutaja majina ya hao watu waliokuwa kwenye hii video?” hakimu sasa aliingilia kati baada ya kuona ukimya usiokuwa wa kawaida kutoka kwa mama Joan
“aah mmmh ah sio mimi na hao watu siwajui!” alisema tena mama Joan na kupelekea watu pale mahakamani kuangua kicheko
“haya tuambie unamfahamu Yule pale?” Mwendesha mashtaka alisema sasa akimnyoshea mkono Fred
“ahhh ndio, Hapana!” alisema mama Joan kwa kusita sita
“Hapana au ndio ?” aliuliza tena
“aaaah, mmhhh” aliongea mama Joan kisha akaanguka chini, hakimu aliahirisha kesi tena na mama Joan akakimbizwa Hospitali huku akisisitiza Mzee Kidude na Sele wasitoke nje Ya jiji la Dar es salaam wakati wote kesi ikiwa inaendelea

“asante sana Baba, sikujua utafanya hivyo! Alisema Doreen sasa walipokuwa nyumbani kwa Mr K kuangaliwa mwenendo wa kesi yao
“kwasasa kesi ya msingi tunakaribia kuimaliza, mzizi wa yote haya ni hii kesi ya msingi, kama mambo yakienda hivi tunashinda hii kesi asubuhi sana” alisema Rapha huku akimalizia soda yake kwenye glas
“unadhani wanaweza kuja na hoja gani?” aliuliza Sele
“hawana hoja zaidi watang’ang’ania validility tu” alisema Rapha
“ndio nini iyo validility?”aliuliza Doreen
“ni muda wa huu ushahidi , kuwa ulikaa muda mrefu bila kutolewa, lakini hoja hii inakufa kwa kuzingia sheria ya ushahidi namba 213 ya mwaka 2005 kuwa ushahidi utaendelea kutumika na kuhesabika ni hai kuanzia siku shauri lilipofunguliwa hadi mwisho wa kesi” alisema Rapha
“hivi kwasasa Mama Joan atakuwa chini ya ulinzi wa Polisi ama bado hajapatikana na hatia?” aliuliza Sele
“Yule ni mtuhumiwa na kutokana na kilichotokea pale lazima atakuwa chini ya ulinzi ili asiharibu upelelezi, lakini tu hatalazimika kutoa ushahidi mpaka daktari athibitishe kwa maandishi kuwa anaweza kufanya hivyo” alisema Rapha
‘oooohoo basi kama ni hivyo mambo ni tofauti na tunavyofikiria” alisema Sele akisimama huku wenzake wakimshangaa tu
“huyu mama anafanya mchezo hizo siku kadhaa za kuwa hospitali inaweza kuwa ni janja yake kufanya jambo Fulani” alisema Sele akijishika shika ndevu zake
“kwani yupo hospitali gani?” alisema Mr K
“Hatujui ngoja tupeleleze mpaka jioni tutakuwa tumepata jibu” alisema Rapha huku akisimama na kuaga wenzake na kutoka nje ya nyumba ya Mr K,
Ni kweli majira ya jioni Sele alipata kujua kuwa mama Joan alikuwa amelazwa katika hospitali ya Mtakatifu Emmaus iliyokuwa kigamboni, Sele alichukua simu yake kisha akaingia kwenye mtandao na kutafuta taarifa za hospitali hiyo pamoja na kuangalia mazingira yake jinsi yalivyo
“naona kuwa kuna jambo haliko sawa kuhusu mama Joan ni kama anaficha kitu Fulani hivi na hata kule kuumwa sidhani kama ni kwa kawaida” alisema Esta sasa akimstua Sele katika mawazo yake hayo
“ah Yule haumwi ninachofikiria ni kuwa anajaribu kwenda kupanga mikakati yake zaidi ili kwamba aweze kutoka katika kesi inayomkabili” alisema Sele
Hata hivyo baada ya siku kadhaa waliitwa tena mahakamani na kuelezwa kuwa kesi yao inaahirishwa tena kwakuwa mama Joan, bado alikua hayupo katika hali nzuri ya kiafya
Hata hivyo baada ya siku chache tu wakili wa utetezi wa mama Joan na mzee Kidude alijitoa kwenye Kesi! Na hivyo ikabidi mzee Kidude ajitafutie wakili wake,
Siku hiyo mzee Kidude akiwa anatoka hospitali kumjulia hali mama Joan akiwa na derava wake ghafla gari moja ilikatisha mbele yake na kusimama kwa ghafla, kitu ambacho kilisababisha kidude kushtuka ghafla na derava wake kufunga breki za papo kwa papo, wakati wakiwa wanashangaa walishuka watu wanne haraka haraka wakiwa na bunduki na kumtoa mzee kidude na kumuingiza kwenye gari yao halafu mmoja wao akaenda kuendesha ile gari na kutokomea, kilikuwa ni kitendo cha dakika mbili tu na sekunde kadhaa,
“semeni jamani mnataka kiasi gani cha pesa semeni jamani!” alisema mzee Kidude
“kaa kimya mzee” walisema wale vijana na sasa safari ikaendelea na kisha wakamfunika kitambaa na kuingia nae kwenye “nyumba yao” ya siku zote, baada ya dakika kadhaa sasa walimfungua kitambaa mzee Kidude

Sasa mzee Kidude aliomba bora awe anaota kuliko kutazamana uso kwa uso na Yule mtu aliyekuwa mbele yake
“pole mzee Kidude naona vijana wamekusumbua kidogo, karibu tuketi rafiki yangu!” alisema mzee Tupa
“kumbe, kumbe, ku-mbe,ni, we-we,’ alisema Mzee Kidude kwa tabu
“usijali,” aliongea mzee Tupa huku akitabasamu kisha akakonyeza walinzi wake ambao waliondoka na kuwaacha wenyewe
“haya mbona hutaki kuniua, niue sasa” alisema mzee Kidude
“mimi sio muuaji , ningetaka kukuaa ningekuwa kule kule bagamoyo, tangu siku ile umelala na mke wangu!” alisema Mzee Tupa na kumuacha mzee Kidude akitapata kutafuta maneno
“usihangaike nisikilize” alianza mzee Tupa
“najua ni wewe unasababisha kesi isisomwe mpaka sasa ukidhani kwamba utaweza kuwanunua mahakimu na hivyo unamuambiaYule shetani mwenzako kuwa azidi kujifanyisha huko hsopitali, sasa nisikilize unatakiwa ufanye mambo mawili tu,
Jambo la kwanza
Upeleke taarifa rasmi kuwa mko tayari kwa kesi kesho kutwa, halafu jambo la pili eleza pesa za Gift ulitoa wapi, na eleza ukweli mahakamani, ni hayo tu, najua unajua nitakachokufanya endapo hutafanya kama ninavyokulekeza” alisema mzee Tupa sasa akimkonyeza Mlinzi wake ambaye alikua mbali kidogo na hapo
“haya warudisheni” aliwaambia
“mpaka kesho asubuhi nitaona uaminifu wako mzee Kidude” alisema mzee Tupa
Sasa mzee Kidude alijikuta akipagawa, kabisa sasa alianza kuamini akili zake zile za mwanzo wakati anatamani kujiingiza katika mchezo huyu, mara kadhaa alikua anajiambia kuwa anacheza na kifo chake mwenyewe “unacheza na mke wa raisi Kidude” ni maneno ambayo yalikua yanamjia mara kwa mara kichwani kwake kabla hajaanza huu ujasiri wake wa kipumbavu
“bossi uko sawa?’ sasa dereva wake alikua akijaribu kumuongelesha bosi wake huyo
“twende nyumbani” alisema tu bila kujibu swali

Walifika na moja kwa moja mzee Kidude alifungua friji na kutoa kilevi na kujimiminia
“kwa mara nyingine tena umalaya umeniponza” alijisemea kidude
Sasa alikua na saa 13 tu kuamua hatima yake,

Mzee tupa alikua amepata simu kutoka kwa Raisi , kama angehitaji msaada wake bila kutambulikana, Mzee Tupa hakutaka msaada uliopilitiliza zaidi tu alitaka kujua mwenendo wa kesi na jinsi mkewe anavyojaribu kujitoa , angekuwa na uwezo hata wa kuomba kesi hiyo ifutwe ama apangiwe hakimu yoyote amtakaye lakini mzee Tupa alisema haki itendeke kwa asilimia mia
Na hivyo siku hiyo ndipo alipopata taarifa kuwa mama Joan alikuwa haumwi bali alikua anavuta muda ili kununua mahakimu na kuweka mambo mengine sawa, na tayari mzee Kidude alipokuwa kule hospitali sasa aliweza kujulishwa kila hatua na kuamua kumchukua jioni ile, mzee Tupa alikuwa na video kadhaa na mauza uza ya mkewe na Bwana Kidude, hakutaka zisambae haraka kwani zilikua zinamchafua yeye pia na sasa akafikiri njia pekee ni kumkaanga mama Joan na mafuta yake mwenyewe, ilikua kazi ndogo tu kumshawishi wakili wake kujitoa na sasa ilikua ni zamu ya Mzee Kidude
Kesho yake hakimu alipokea taarifa kuwa mama Joan anaweza kuendelea na kesi baada ya kupona na hivyo ikapangwa wiki iliyofuata huku wote wakisisitizwa waje na vielelezo vya msingi
Siku hiyo ya hukumu,
Kama kawaida siku hiyo mahakama ilikua imefurika watu kutoka sehemu mbali mbali kwani tayari kesi hiyo ilikua miongoni mwa kesi maarufu sana zilizovutia
Upekee wa siku hiyo mzee Tupa pamoja na watoto wake walikuwepo kushuhudia hukumu ya kesi hiyo
Baada ya kusoma utangulizi na maelezo ya msingi sasa hakimu aliwapa tena nafasi ya pande zote mbili kutoa hoja zao za kuhitimisha na kisha mzee Kidude akapewa nafasi na kutoa ushahidi wake,
Wakati anaingia kizimbani macho yake yalitazamana na mzee Tupa ambaye alimkonyeza na yeye akamkonyeza kisha akaanza kutoa ushahidi wake
“mheshimiwa hakimu, zile pesa nilipewa na mama Joan kuwa niziweke kwenye Gari la Sele kusudi kwamba tumtengenezee kesi ya uhujumu uchumi na ndio nasikitika sana nimedanganya mahakama
 
Back
Top Bottom