MPANGAJI 04
Asubuh na mapema Sele aliamka na kufanya mazoezi kiasi kama ilivyokuwa kawaida yake, akitumia vifaa kadhaa alivyokuwa navyo, alipiga push up za kutosha na mazoezi mengine kisha akaenda bafuni na kuoga na siku hiyo aliamua kuvaa nguo za kawaida kabisa, alivaa pensi na raba kisha akavaa na kofia moja matata iliyokua na herufi chache tu “CK” kisha alifungua kwenye begi lake na kutoa kiasi cha pesa na kuhesabu noti kadhaa na kuzitia kwenye waleti yake halafu akatoa simu yake na kukuta missed calls mbili za Esta,
“la haulaa!” alijisemea sasa akivuta begi lake na kuchukua ufunguo mezani na kutokomea nje
Alimkuta Esta akiwa mlangoni na begi lake tayri kwa safari..
Mama Mwajuma nae alikuwepo kumsindikiza mwanae
Baada ya Salamu sele alichukua begi la Esta na kulivuta taratibu kutokea nje Mama Mwajuma tayari alishahisi kuna jambo linaendelea kati ya watu hawa wawili hata hivyo kwa upande mwingine alifurahi kwani pamoja na mambo mengine ya Sele, alikua ni kijana mtanashati, mwenye adabu na asiyekuwa na makuu, kuhusu anafanya kazi gani mama mwajuma hilo halikumuumiza sana kichwa isipokuwa ni namna ambavyo uhusiano huu utaishia
“potelea pote hawa ni watu wazima” aliwaza mama Mwajuma sasa wakipiga hatua kutoka nje ya nyumba, tayari wapangaji wengine waliokuwepo walishaagana na Ester na wengine tayari walikua wameshamzoea
“sasa Mama wewe ishia hapa mimi nitamsindikiza Esta mpaka ubungo na kuhakikisha anapanda basi la Lindi kabisa mama!” alisema Sele huku akitabasamu,
“itakuwa vizuri kabisa Basi mimi niishie hapa, Sasa Esta, nikuage Mwanangu alisema mama Mwajuma huku akipunguza mwendo kidogo Sele alikuwa ameshaelewa hapa ni “mausia” ndio ambayo yanafuata
“Mwanangu usinifiche kitu mimi ni mtu mzima, niambie una uhusiano na Sele?” mama Mwajuma aliuliza huku akimtazama mwanae usoni
“hapana mama, Ni tumezoeana tu yaani, hivyoo tu!” alisema Esta huku akiwa kama anataka kusitisha mzungumzo
“ila Sele anakupenda maana hajawahi kuwa na ukaribu na mtu yoyote , sasa mpaka anafikia hatua ya kukusindikiza hadi stendi?” alisema mama Mwajuma
“ungejua sio kunisindikiza tu, kanaipa hadi laptop!” alijisemea moyoni Esta
“haya mama uwe makini huko shuleni, kaa vizuri na walimu wenzako, na mkuu wako wa shule na usisahau kuniletea mzigo wangu likizo ya mwezi wa 6” alisema mama Mwajuma akimuaga mtoto wake kwa mbali alimnyooshea mkono Sele ambaye alikua sasa ameweka begi chini akimsubiri Esta ambaye alifika na kisha safari ikaanza. Hawakupiga hadithi sana kwani kila mtu alikua anawaza mambo yake kichwani, walipofika Kimara Mwisho Esta alilalamika kuwa kuna kitu aliagizwa na shoga yake amnunulie na alisahau kununua,
“yaani Nikifika bila hicho kitu Shoga yangu hatanielewa kabisa yaani” alisema Esta akimweleza Sele
“okay tushuke kwanza unaweza kukipata hapo nje hicho unachokitafuta halafu tukachukua bajaji tu kwenda stendi bado ni mapema” alisema Sele huku akisogea mlangoni
Walishuka pale Kimara mwisho ambapo wengine walipenda kuita darajani
Na kuvuka upande wa pili
sele alijua bila shaka ni vitu vya wanawake ambavyo shoga yake huyo alimuagiza
“wanawake wana vitu vingi sana yaani!” alijisemea sele huku sasa akivuta begi la Esta
Walisogea kabisa pembeni ya barabara na kuingia mtaani walikaribia sehemu kulikua na bajaji kadhaa zimepaki Esta akamwambia Sele asubiri yeye aende kuuliza hicho kitu
Alisogea pale na kabla hajafika alishadakwa na madereva kadhaa alichagua mmoja kisha wakaongea halafu baada ya muda kidogo Esta alimnyoshea mkono Sele amfuate
Sele alimfuata na kuingia kwenye bajaji ya Yule kijana
“vipi tena?” aliuliza Sele akiwa ameduwaa
“nakumbuka wakati nakuja nilikuambia unizunguushe nione mji kwahiyo leo ni zamu yako kaa utulie mwanaume wewe na usiongee kitu!” alisema Esta kwa utani
“haya langu jicho Esta, ila kwa hali safari labda kesho unapajua Lindi wewe?” Sele aliongea sasa akiwa haelewi nini kinatokea
“hata hapa Dar nasikia kuna sehemu inaitwa Lindi” alisema Esta Sele hakua na namna isipokuwa kucheka tu walipita sehemu kadhaa na baadae wakatokea mbele ya jengo moja zuri sana “LOTHA EXECUTIVE LODGE & RESTAURANT” maandishi makubwa yalisomeka kwenye kibao cha jengo hilo
*************************
‘pacheki sista kama hapafai nikupeleke nyingine ipo kati hapo nayo barida tu kama hii!” alisema Yule kijana wa bajaji akiwa amesimama tayari kutoa mizigo
Esta alishuka kwa kujiamini huku Sele akiwa hajui kama anatakiwa kupiga kelele za shangwe au kilio ama anatakiwa kufanya nini,
Esta alifika ndani na baada ya muda alirudi
“asante kaka pako vizuri bei gani vile ulisema?” alisema Esta kifungua pochi yake na kutoa elfu tano
“ah buku mbili tu sista, kama vipi chukua minamba nini ili kama niaje niaje nini fresh tuu!” alisema Yule kijana mpaka Esta alicheka
“hahaha usijali, sasa namba yako nitaisave niaje niaje bajaji” aliongea huku Sele sasa akishuka kwenye bajaji na mizigo
“kiuhalisia nataka niende Lindi nikiwa sina deni na mtu Sele”
Alisema Esta huku akiwa anatangulia ndani, Sele alifuata kama kondoo aliyekuwa mafichoni walipita mapokezi na mhudumu akawapokea na kuwapeleka kwenye chumba ambacho tayari Esta alishachagua, kilikua ni chumba kizuri sana, Esta alitua mizigo yake na kuipanga vizuri sele alikaa kwenye sofa lililokuwa pale chumbani na kukunja nne huku akimkodolea macho Esta kama mtu anayesubiri kupewa muongozo
“sele nikuambie kitu!” alianza Esta kwa upole sana, yeye kama mwalimu alijua namna ya kuweza kueleza somo lake likaeleweka kwa mwanafunzi wake huyu aliyekuwa mbele yake
“mimi nina miaka 26 sasa hivi, nina vitambulisho vyote kuanzia cha kupigia kura cha kazi hadi cha Taifa” alianza Esta
“unataka kusemaje?” aliuliza Sele
“naona kama mwenzangu umejaa hofu kana kwamba umeingia na mwanafunzi wa form one hapa kwahiyo muda wowote utakamatwa!” alisema Esta huku akicheka
“Hapana mwalimu mimi sijawa na hofu, ila nashangaa tu, ubungo imekuwa hii, sasa sijui hicho kitanda ndio basi au!” alisema Sele kwa utani
“kwahiyo huna hofu kabisa?” aliuliza Esta
“kwahiyo nikuogope wewe au!” aliuliza Sele
Esta hakujibu alisogea mpaka kwenye meza na kupiga simu mapokezi ambapo aliagiza supu ya kuku na chapati
‘ Sele safari yangu ni kesho, kwahiyo leo nimeamua rasmi nibaki na wewe hapa, kuna mambo inabidi nikuambie Sele ka aujuavyo kule nyumbani hakuna uhuru sana na tusingeweza kuongea” alisema Esta
“ kwakuwa leo ni siku ndefu kwanza nikushukuru sana kwa zawadi Sele yaani nikifika pale shule nitaosha kweli!” alisema Esta akiitoa ile komputa kwenye begi lake
“ooh usijali Esta” alisema Sele
“nielekeze elekeze basi ujue mimi sio mtundu sana kwenye komputa” alisema Esta akienda pale kwenye Sofa alipokaa sele,
“ooh, wewe mwalimu tena si mmespma ICT chuoni jamani!” alisema Sele
“tumesoma lakini theory nyingiii!” alisema
“mh tuanze na nini…” sele alikatishwa na sauti ya mhudumu aliyekuwa anagonga mlango na alifungua , na mhudumu akaweka mizigo mezani,
“karibuni” alisema mhudumu
“tuletee maji makubwa ya Kilimanjaro na glass mbili” alisema Esta sasa akisogea pale mezani na kuanza kupiga msosi…
Walimaliza kula na kisha Sele akamuelekeza vitu kadhaa kwenye komputa katika hali ambayo Esta alishikwa na bumbuwazi,
“sele mbona unaijua komputa hivi? Na wakati huo umesema hutumii kabisa mitandao ya kijamii?” aliuliza esta akiwa ameduwaa
“ah kumbe nilikua sijakuambia kazi yangu hadi leo! Hahaha alisema Sele akicheka”
“Mimi ni IT nimejiajiri binafsi, kazi yangu ni kufunga mifumo mbali mbali katika ofisi, majengo ya watu binafsi n. kama vile kuweka software za cctv camera, ama za ulinzi n.k, mwakani inshallah Mungu akipenda nitakuwa na ofisi yangu rasmi sasa hivi nafanya deiwaka tu na kampuni moja hivi inaitwa TAA” alisema Sele huku akiwa ametulia kabisa
“waooh kumbe, niko na IT hapa, kwahiyo kumbe ninyi ndio mnahack akaunti za watu insta, eeh?” aliuliza Esta kwa utani na sasa muda wa kubadili mada uliwadia ‘leo afe kipa afe beki” aliwaza