Hadithi: Mpangaji

Hadithi: Mpangaji

Kuna uzi humu jf wameweka pdf za adithi kibao. Sema sijui unaitwaje huo uzi

huu apa mkuu

Sent from my SM-C9000 using JamiiForums mobile app
 
Karibuni Tena katika story hii
Kama kawaida ni mwanzo mpaka mwisho hakuna kuishia njiani

Kutoka "madam president" na ",kesi ya Mzee Mnyoka"

Ssa Leo tunaanza kisa kingine Cha Mpangaji
Mtunzi ni Mimi mwenyewe CK Allan

(0746 Mia mbili sitini na sita mia mbili sitini na Saba)

MPANGAJI 01
Hakuna mpangaji yoyote ambaye alikuwa anafahamu asili ya Yule mpangaji mwenzao, hata jina lake la ‘sele’ wapo waliosema halikua jina lake halisi, lakini yote kwa yote Sele kama unavyoweza kusema alikua mpangaji wa kudumu wa mzee Mhina, miaka ilikatika na sio mzee Mhina wala wapangaji ama watoto wake walijua kazi halisi ya Sele,
Wapo waliosema sele alijihusisha na kazi ya kuzibua vyoo huko mjini mbali na hapo, wengine walisema sele Alikuwa mtu wa ‘kitengo” na kama ilivyo kawaida ya wabongo basi wengine walizua kuwa sele ni jahili mzoefu,
Kwanza Sele asingetoka nje ya chumba chake bila kuitwa, na kwakuwa chumba chake kilikua ni selfu basi huwezi kujua kama sele yupo ndani au ametoka,
Mama mwajuma hawezi kusahau yeye na wapangaji wenzake walivyoumbuka siku hiyo walitumia masaa zaidi ya mawili kumsengenya sele kwa sauti ya juu kabisa
“tena nakuambia huyu Sele itakuwa anafuga majini, mwanaume gani huwezi kumkuta yuko nje na wenzake, nyumba haina redio wala tivii halo halooo!”
“halafu hata siku moja sio mwanaume wala mwanamke aliwahi kuingia hicho chumba!”
“hakuna hata ndugu yake mmoja aliyewahi kuja hapa nakuambia mwaka wa sita huu mimi niko hapa!” wapangaji wenzake walikua wakiendelea kumzodoa sele,
Mama Mwajuma alikua amekazana kuongoza maongezi hayo bila kujua sele alikua ndani akiwasikiliza tu,
Ni mpaka pale waliongea hadi wakachoka ndipo Sele alitoka akiwa na mkoba wake
Alimsalimia mama Mwajuma kwa heshima kama ilivyokuwa kawaida yake kisha akatoa elfu tano na kumpa mama mwajuma ambaye alishikwa na kigugumizi
“hii hela ya umeme utampa kaka Efraimu hapo tutaonana baadae” alisema Sele akitoka zake..
Huku nyuma wale wanawake waliangua kicheko
“tumeumbuka shoga, umbea huuu”
Alisema aisha akirudi ndani kwake..

****************************
Kama kawaida siku hiyo saa tatu usiku Sele alirejea zake nyumbani kwake aliwapita wanawake kadhaa waliokuwa bado hawajamaliza kupika vyakula vyao vya usiku, aliwasalimia kana kwamba hakuna chochote kilichotokea asubuhi ile kisha akafungua mlango na kujitosa ndani,
Huku nyuma vicheko vilisikika kama kawaida lakini aliwapotezea, hakuwa na muda wa kubishana nao kwanza ukimtoa Ephraim , wapangaji wengine walimkuta akiwa pale, kwanini ahangaike nao,
Usiku wa manane Sele alistushwa na kelele za wapangaji huko nje ya chumba chake alijaribu kutega sikio kusikiliza vizuri na kugundua ulikua ugomvi wa mke na mume tu, kama kawaida hakujishughulisha na ugomvi usiomhusu akavuta shuka lake na kulala.
Alfajiri alistuka mlango wake ukigongwa kwa nguvu na Ephraim , alimtambua sauti yake
“labda ni pesa ya umeme” aliwaza akitoka akivaa “malapa” yake na tisheti kisha akafungua mlango na kutoka
‘OI, broo’ alisema Sele
‘kuna kikao mshkaj njoo chap ‘ alisema Ephraim akirudi zake, kwa muda wote aliokaa pale hakuwahi kumuelewa Sele, kuna wakati alijaribu kumzoea lakini alijikuta akishindwa na hakuna hata siku moja alifanikiwa kukaa nae zaidi ya dakika tano,
Hata kwenye vikao vya usafi, umeme na maji, Sele hakuchangia chochote alisubiri makubaliano tu kisha alitoa pesa yoyote itakayokubaliwa,
Hata mzee Mhina alikua akimtolea mfano kuhusu ulipaji kodi, haijawahi kutokea Sele akapitisha mwezi bila kulipa kodi ya pango,
Tofauti na vikao vingine , siku hiyo mzee Mhina na balozi wa nyumba walikuwepo kweny kikao cha siku hiyo kidogo sele alistuka lakini hakuonyesha mshangao wake wazi akasogea na kukaa kwenye mkeka kama wenzake
“nadhani wotetupo sasa tuendelee ili wengine waende kutafuta riziki”
Alisema mzee Mhina. Wote waliitikia kisha Balozi akamkonyeza mzee Mhina kumuashiria atoe hoja kikao kianze
“ sasa ndugu zangu nimepata malalamiko kuhusu Bwana Sele hapa” alianza Mzee Mhina,

‘jana usiku kulikua na ugomvi miongoni mwa wapangaji na walitoka na kupigana bado kidogo wauane, wapangaji wote walitoka kuamua na kusaidia lakini ndugu yetu sele yeye wala hakujisumbua kutoka, sio jana tu lakini hata wakati ule chumba cha mama Isa kilipopata hitilafu Bwana Sele pia hakutoka kabisa, nakumbuka pia hata wakati wa sherehe ambayo niliandaa mimi mwenyewe wakati binti yangu Rehema akifunga ndoa Bwana Sele pia hakuhudhuria hivyo kwa mazingira haya naona kabisa kuna kitu huyu mwenzetu anacho anajaribu kutuficha nikaona balozi uje kidogo utusaidie,” alimaliza Mzee Mhina huku wapangaji wote wakipiga jicho kwa Sele
‘ ooh Kijana wangu Sele, hebu niangalie, hivi kweli leo hii hata nikikuambia unitajie majina ya wapangaji wenzako utawajua kweli?’ aliuliza Balozi huku wapangaji wengine wakicheka..
“huyu anamjua Ephraim tu ndio mwenzake huyoo” alidakia mama Mwajuma
‘ Hapana nawajua wote!” alidakia Sele kisha akaendelea..
‘wewe ni mzee Lota, una watoto wanne , watatu wa kike na mdogo wa mwisho wa kiume, Yule ni Aisha na mumewe Mkude, Yule ni mama Mama Mwajuma na mume wake Ngoda, pale ni Isa , kule ni John na hapa ni kaka Ephraim na mke wake mama Joan’ alimaliza Sele huku akiwaacha wapangaji wote mdomo wazi , hususani huyu mpangaji John ambaye alikua na siku ya pili tu!
“ wewe mwana wewe, umejuaje mpaka hawa wapangaji wapya? Umeona sasa Balozi tukisema sisi tunaishi na zimwi.. zimwi..” alidakia mama Mwajuma huku wapangaji wote wakiangua kicheko,
“ Mama Mwajuma, tumalize kikao ili usichelewe kumuandalia mgeni wako Ester anayekuja leo kutoka Lindi!” alisema Sele akitoka zake kurudi chumbani!
‘bwana sele hatujamaliza lakini!” alisema Mzee Mhina lakini sele alirudi zake chumbani kumalizia usingizi wake,
“makubwa haya, makubwa haya sasa kuhusu Huyu Ester huyu Sele kajuaje jamani” alisema mama Mwajuma huku akiondoka. Kikao kile kilivuruga kabisa mtazamo wao kuhusu Sele, wapangaji waligawanyika huku wengine wakitaka afukuzwe, na wengine wakisema hawajaona kosa
“sasa afukuzwe kwa kosa gani? Bili zote analipa, usafi analipa, kodi ya watu analipa, hawajawahi kugombana na mtu kaka wa watu, muacheni bhana!”
Alisema Ngoda na kisha kikao kikaishia hapo

Inaendelea
braza una uandishi wa kipekee,hii inaonekana bonge la story
 
huu apa mkuu

Sent from my SM-C9000 using JamiiForums mobile app
APA tulishamaliza kaka
 
Ngoja tutililike nayo
 
Asante sana kaka mie mdau wako wa kimya kimya haswa kwa Mzee Mnyoka nilikuwa silali😁Mwenyeezi Mungu abariki kazi ya mikono yako ufike mbali zaidi 🙏
Loh! Asante sana,
Kuna mzigo mwingine unaitwa MZAHA WA DAMU,
Uko tayari sema miundombinu ndio haijakaa poa namsubiria TAJIRI MKUU WA MATAJIRI 🤣🤣🤣🤣
 
MPANGAJI ----- MWISHO WA MWISHO

BY CK ALLAN
“ kwahiyo ninaomba sana mheshimiwa Hakimu mahakama inisamehe tu maana nilitishiwa maisha yangu, kuwa nisipofanya hivi maisha yangu yatakuwa hatarini”
Alimaliza kujieleza mzee Kidude huku wakili wake akipigwa na butwaa na kujaribu kuingilia kati
“Mheshimiwa Hakimu mteja wangu hayuko sawa kisaikolojia hivyo naiomba mahakama yako tukufu isitoe uamuzi leo hii” alisema wakili
“napinga mheshimiwa Hakimu” aliingia Kati Rapha
“ mahakama yako tukufu ikubali maelezo ya mshtakiwa kwakuwa hakuna vielelezo vya daktari kuwa ana tatizo la kisaikolojia” alisema Rapha akikaa
“nakubaliana na wewe, maelezo yake yamechukuliwa na mahakama” alisema Hakimu na kisha akajiweka sawa ili kutoa hukumu ya kesi,
Mwendesha mashtaka alisoma maelezo ya kesi na ushahidi wa maelezo ya pande zote mbili na kisha akatoa ushauri wake kuhusu mwenendo wa kesi kisha akamkaribisha hakimu ambaye alisoma tena maelezo na kurejea vifungu kadhaa vya sheria kisha akatoa hukumu yake
“kwahiyo basi, Mahakama imeona kwamba ndugu Sele Selemani Sele hana kesi ya kujibu na mahakama imemuachia huru, hata hivyo kuhusu kesi yake ya madai kuhusu kuwa na undugu na ndugu Lukas Tuppa, mahakama inaruhusu mdai kuleta vielelezo ikiwemo kupima vipimo vya nasaba na mdaiwa, hata hivyo mahakama imemuona kuwa na hatia mshtakiwa Janet Lukas Tuppa , na kutoa adhabu ya miaka 25 gerezani kwa kupanga na kutekeleza mauaji , na vile vile mahakama inamhukumu kifungo cha miaka 15 gerezani kwa kupanga na kutekeleza utakatishaji wa fedha na uhujumu uchumi, na vifungo hivi vinaenda kwa pamoja, vile vile Mahakama inamhukumu Kidude James Tito miaka 8 gerezani kwa kupanga na kutekeleza njama za uhalifu wa kifedha pamoja na kuidanganya mahakama..”
Sele alipiga magoti chini huku akimshukuru Mungu na kisha akatazama huko na huko na kukumbatiana na wakili wake kisha akakumbatiana na watu wengine huku akisogea sasa kumuelekea mama Joan
Wakati huo mama Joan alikuwa akilia huku askari wakiwa wamemzunguuka katika harakati za kumtia pingu, ni wakati akiwa amenyoosha mikono ili wamfunge pingu kwa haraka alichomoa bastola ya askari mmoja na kujiwekea kichwani, taharuki ilizuka kwa ghafla huku sasa polisi wakimsihi asifanye alichokuwa akitaka
Hata hivyo bila kusita alifyatua risasi na kumpasua kichwa na kuanguka chini..
BAADA YA WIKI MOJA
Doreen alirudi zake Italy huku akiwa amemaliza kabisa kuweka mambo yote sawa,
Siku hiyo Sele alikuwa nyumbani na mke wake wakicheza mchezo wa mpira wa miguu kwenye komputa huku wakitaniana wakati kengele ya mlangoni ilipolia kuashiria kuna ugeni Haraka Sele alifungua simu yake na kufungua program maalum na kuangalia kamera ya nje
“mmhhh mbona kazi ipo!”alisema Sele akimuonyesha mkewe hao wageni wenyewe
“loh, Lukas, waziri Joan, Na Jesca’ mh
Alisema huku akimuangalia mumuwe, wakati huo tayari mzee Lukas alikua akijiandaa kubonyeza kengele kwa mara ya pili, ndipo Sele alimshika mkono mke wake na kutoka nje kwenda kuwapokea,
Alifungua geti kisha akamsogelea mzee Lukas na kumkumbatia kisha akawasalimia Joan na Jesca na kuwakaribisha ndani,
Walitulia zaidi ya dakika tano huku kila moja akishindwa namna ya kuanza mpaka pale mzee Tupa lipovunja ukimya
“usishangae Gift, damu ni nzito kuliko maji, yaliyotokea yametokea, hawa ni dada zako!” alisema mzee Lukas akiwaangalia akina Joan ambao walisimama tena kukumbatiana huku machozi yakiwatoka kisha wakamkumbatia na Esta pia
Baada ya maongezi kiasi sasa waliaga na kusimama
“sasa nataka kuja tena kucheza na wajukuu hapa Gift, wajukuu!” alisema mzee Lukas kwa utani huku akipanda gari na kuondoka
Hakika ilikua siku ya furaha sana kwa Gift na Esta siku hiyo alirudi ndani haraka na kumshika mkono mke wake na kumvuta
“nini tena Gift!’ alisema Esta
“hujamsikia Mzee anasema anataka wajukuu!’’
Alisema Gift huku wote wakiangua kicheko.
MWISHO_____
Asanteni sana kwa uvumilivu wenu na kusoma hadithi hii!
Siwez kuwataja wote lakini niseme mmenitia moyo sana, ni hadithi yangu ya 3 kuleta humu baada ya Kesi ya Mzee Mnyoka na Madam president,
Kwasasa nitaweka pozi kidogo kwakuwa kifaa nilichokua natumia (laptop) nimekisukuma! Kutokana na sababu za hapa na pale!
Basi niseme Tena nawashukuru sana na in shall Allah tutaonana Tena kwenye MZAHA WA DAMU, Huko mbeleni , panapo majaaliwa
Wabilah towfiq
CK Allan
0746 266 267
Asante sana kwa kuturudisha ,,,ni mtunzi pekee unaye mwaga story mwanzo mwishooo
 
Sabuskraibudi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika unautendea haki muda!
 
Back
Top Bottom