- Thread starter
- #21
OG Sana mkali!Safi sana mkuu ,,tunasubiri next episode
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
OG Sana mkali!Safi sana mkuu ,,tunasubiri next episode
Na upload sasa hivi!Ile boss ya stella nayo ina ukakasi.. kavile nae anapita na the boss .
Uko vizuriii.. twasubir muendelezo please .
Sent using Jamii Forums mobile app
Kivipi mkuu?Nickson ni bonge la limbukeni
Kivipi mkuu?
Hahahh mapenzi upofu mkuu. Haswa haswa kama upo single ndugu ukipata mtu hutaki kusikia .Yaani poti demu anamlia pesa ye bado anaona anapendwa jinga sana
Na mdomo unamponza sana. Cheki keshagawa idea bure kabisa.Nickson ni bonge la limbukeni
Hahhahaaaa nice story twasubir next episodeMY SOULMATE SEHEMU YA 13.
Produced by : Equatorstory Specials.
Ni mida ya saa kumi na mmoja jioni Nickson anakutana na rafiki yake kipenzi walio soma wote tokea shule ya msingi.
Nickson : "Ahh Erick za kupotea kaka!".
Erick : "Aisee kaka umekuwa ndugu yangu". Waliongea huku wakikumbatiana.
Nickson : "Man nili kumiss sana!."
Erick : "Hata mimi kaka khaa ni kama mwaka na zaidi tokea tuonane mara ya mwisho tulipokuwa chuo!."
Nickson : "Ahh mambo ya hapa na pale tu mkuu."
Erick : "Vipi shemeji yetu anasemaje!?."
Nickson : "Ah shemeji yako pasua kichwa mkuu anapenda sana hela kama wallet."
Erick : "Hahahah wewe jamaa bado tu unahongaga!? Mimi siwezagi kuonga kabisa yani mwanamke ntampa hela kama ntapenda na sio kumuhonga."
Nickson :"Aisee kaka nataka nikiwa mkubwa niwe kama wewe!."
Erick : "Hahahahaahaah utaweza wewe? Wanawake ukiwa endekeza watakuja kukuletea madharau."
Nickson : "Lakini kwani si unampa hata ya vocha ama nayo hairuhusu kwenye kitabu cha wahuni?"
Erick : "Wewe uwape vocha si uta baki na kucha zako tu!? Mimi nina ma dem watano na wote siwapi hata mia. Ukisema uwape vocha wata taka za elfu 5 na mara 5 hiyo si elfu 25 nani anataka kufiliska!?"
Nickson : "Duhh hapo kaka umenishinda."
Erick : "We mzoeshe hela uone kuwa mgumu atakuomba mwishowe ata puuzia tu. Niambie lakini."
Nickson : "Ndugu yangu mimi nina mpango wa kufanya mradi bhana."
Erick : "Enhee leta maneno....".
Nicskon walikaaa na wakajadili kwa kina na Erick kuhusiana na huo mradi Nickson aliopanga na waka shauriana mambo mawili ma tatu.
Nickson : "Kwa hiyo sasa mkuu vipi utaniunga ama?"
Erick : "Ndugu hapa hakuna kulaza damu twende tukajisajili kabisa BRELA kama kampuni tuanze kuchapa kazi mkuu. Hapa kijana ume nena yani naweza hata nikakupa dada yangu umuoe yule hapendagi hela sana!. "
Nickson : "Sawa basi kesho tutaaanza michakato. Nadhani itakua vyema Kama tungemtafuta Damian tumpe ashulikie maswala haya sis tuendelee na mengine ama vipi?"
Erick : "We jamaa mbona mvivu hivyo?"
Nickson : "Mhh sasa wewe unataka kufatilia ama?".
Erick :"Haya sawa tumpe Damian si ndo kazi yake!."
Nickson :"Eeeh mkuu nitawasiliana nae!."
Erick : "Sawa mkuu kwa heri!."
Basi tokea wakati huo Nickson na Erick wali ingia katika makubaliano ya kazi na waka anza ku haingaika huku na huku kwa ajii ya kuhakikisha mradi unafanikiwa.
Bertha : "Mambo Nickson."
Nickson : "Poa mzima wewe?"
Bertha : "Hapa nimekufa hujui tu!"
Nickson : "Nini shida!?"
Bertha : "Nilikumiss tu ."
Nickson : "Aaaah sasa si ungenipigia simu?"
Bertha : "We mwenyewe saivi upo bize sana!."
Nickson : "Yani huu mradi ninao fanya unanifanya niwe bize."
Bertha : "Bhana mimi nina njaa twende tukale chipsi ile sehemu yetu."
Nickson : "Sawa twende leo nitalipia."
Bertha : "Aaaah nakuona umesha anza na kupata vi hela bhana eeeh?"
Nickson : "Usha anza nita ghairi mimi?"
Bertha : "Ughairi una huo ubavu wewe?"
Nickson : "We twende bhana."
Nickson na Bertha walienda kula kama ilivyo kawaida yao wakienda wakicheka na kukombatiana na kushikana mikono kama mtu na mpenzi wake na jicho la Mpelelezi likiwa na wao bila wao kujua kuwa wanafuatiliwa kwa siku kadhaa na kila picha zao za furaha zinapokelewa na Mandoto akiwa huko alipo.
Upande mwingine Nyumbani kwa Mr Mandoto akiwa na dada yake ana angalia simu yake kwa hasira na kufyonza.
Mandoto : "Huyu mwanamke sijui nimfanyaje jamani."
Rose : "Kaka nini mbona una hasira sana?"
Mandoto : "Si huyo katuni naniliii mjinga huyu naniliii Bertha."
Rose : "Kwani kafanyaje kaka?"
Mandoto : "Bado yupo na yule mwanaume wake wapo barabarani wanacheka kama wajinga flani hivi."
Rose : "Kaka huyu mwanamke achana nae kalogwa huyo uyo mkaka atakuwa mchawi au kampa limbwata mwone anavyocheka cheka tu."
Mandoto : "Nitamuuuuuuuuuua mimi ngoja nitaenda huko Arusha watanijua mimi ni nani....."
Mara Mandoto simu yake ikaita akapokea aka gundua ni yule mchepuko wake waka anza kupiga story na aka anza kujisahau kuwa alikuwa amekasirika kuhusu Bertha na Nickson akaongea na kucheka na kulegeza macho na sauti kana kwamba sio mwanaume!.
Upande mwingine hotelini Bertha amefika na Nickson waka agiza walichokua wanataka kula.
Bertha : "Jamani Nickson saivi una mambo mengi Duuh"
Nickson : "Mradi najua utanipeleka mbali Mungu ata nijalia tu!."
Bertha : "Mmmmmh Sasa si bora uwe jambazi tu?."
Nickson : "Alafu nikuvamie wewe? Utanipa sh ngapi mimi naogopa kufa unaeza ukapigwa risasi ya kichwa ukafa wakati kuna mbinu zingine?"
Bertha : "Wapi wewe!!.... Sema tu ndo hivyo sina vifaa lakini ile meli ya kusafirshia pesa baharini ninge ivamia kama ningekua ni wale mabaharia wa bahari ya hindi."
Nickson : 'Hahaha kama uko serious si useme tuwape ramani afu watu tumie ka asilimia kidogo ile kitu unaeza vamia sawa lakini watakutafuta mpaka makaburini unacheza nini?."
Bertha : "Weewewe kwani tunawonesha sura? Si tunavaa maski bhana."
Nickson : "Eti eeeh afu unaifikiaje hiyo meli?"
Bertha : "Na mtumbwi..."
Nikcson : "Hahahah hahahahaha hahaha naona leo umeamua kunipa burudani..?"
Bertha : "Kwa nini."
Nickson : "Uvamie meli na mtumbwi si watailenga na jiwe izame!?"
Bertha : "Aaaah bhana sio kimtumbwi si tunatafuti boti nzuri."
Nickson : "Hiyo Idea nzuri lakini silaha hatuna pia hatuna vifaa labda tuwape hiyo idea."
Bertha : "Lakini kweli juzi bhana nilisikia wakisema wamefungua account mtandaoni labda tuwatumie ujumbe?"
Nickson : "Hahahah hao wapo na kazi nyingi sana ety wapate nafasi ya kukujibu?"
Bertha : "We tuwa andikie hivyo hivyo bhana sio mbaya hata tuwasiiane na watu wa huko nchi za nje."
Nickson : "Haya njoo tuwa andikie."
Nickson na Betha walikaaa wakiandika ujumbe huo kuwa shauri wa zamiaji wavamilie ile benki na wakiandika na mawazo yao hapa na pale wakijua hao wazamiaji wa meli hawa wezi kusoma sembuse kuwajibu walipo maliza walicheka na kuendelea na maakuli yao. Nickson aliendelea ku furahia wakati huo na kutokuwaza hata kuhusu Stela. ALikumbuka kwamba bila hela kwa hawezi ku fua dafu. Lakini mpelelezi bila kugundulika alikua anawanasa picha na akiwafatilia bila wao kujua. Yamkini Bertha hamjui mumewe vizuri ndio maaana hakuwa na hata wazo la mumewe kutumia wa pelelezi wa kujitegemea.
Upande mwingine tuna mwona Stela akiwa chumbani na Boss wake.
Stela : "Boss unajua Nickson anafanuya nini?"
Boss : "We nishakwambiaje kuhusu kuni ita ita Boss niite mpenzi bhana au unataka kunikera?"
Stela : "Aahhh wewe usiji chetue sana bhana."
Boss : "Unataka tugombane tena?"
Stela : "Jamani mpenzi nakutania."
Boss : "Enhee unasema yule yerro anafanyaje?"
Stea : "Ana anzisha mradi wa kutengeneza aplikesheni ya notes"
Boss : "Anajisumbua tu huyo"
Stela : "Yani ana pambana sana kuhusu ili swala."
Boss : "Enhee embu nielezee."
Stela : "Anataka kutengeneza aplikesheni ya kutunza notes za chuo na una weza kuwa nazo mahali popote unapotaka."
Boss : "Etyy?? Ilo wazo zuri!".Boss alisema huku anasimama akiwaza mambo kichwani mwake.
Stela ; "Ndio una dhani anaeza akafanikiwa anapoteza muda wake bure."
Boss : "Hapana hapana anaweza akapata mamilioni mengi sana!"
Stela :"Boss hahahahah hahaha ndo unamtania hapo?"
Boss : "Hapana... hapana..... huyu yerro ana fanya kazi nzuri sana yani nimeipenda."Boss alionekana akiwa kwenye mawazo yalio mpata ghafla.
Stela : "Sasa tunafanyaje tumu ajiri?"
Boss : "Hapana tukitaka kumuajiri ata kataaa."
Stela : "Sasa tuna fanyaje?"
Boss : "Sasa mwambie Angela atafute vijana kama waaaaa.. Kwani Nickson anafanya kazi na watu wangapi?"
Stela : "Yupo na best wake tu kama sijakosea."
Boss : "So wapo wawili?"
Stela : "Bhana mi sijui lakini nadhani hivyo."
Boss : "Mwambie Angela andae vijana sita kwa ajili ya hii kazi "
Stela : "We unataka kushindana na hiyo haitofanikiwa bhana!"
Boss : "We huna akili sana kwenye haya maswala hili wazo lina hela sana tukimwachia afanye mwenyewe atafaidika sana."
Stela : "Eeeenh kumbe enh?"
Boss :"Huu mradi unaweza pata takribani millioni nane kwa mwezi."
Stela : "Jamani mpenzi si uta ni nunulia ka gari kangu nikawaoneshe ma rafiki zangu?"
Boss : "We unawaza tu kula hela."
Stela : "Kwa hyo hunitaki?"
Boss : "Mpenzi jamani mama yeyo wangu lazima niku nunulie wewe tena?"
Boss alikusanya kikundi cha vijana na waka anza huo mradi wa kumuiga Nickson bila kuwa ambia watu kuwa ni mradi wa kuiga.
Stela alipo ona kuwa mambo yanaweza kumuendea vizuri Nickson na anaweza kukosa nafasi ya kuya furahia maisha aka anza kujipendekeza kwa Nickson.Kwa kutumia ujumbe mfupi akamwambia.
Stela : "Baby mambo?"
Nickson : "Poa Mambo?"
Stela : "Jamani nimekumis."
Nickson : "Hata mimi nimekumis. Tukutane basi ile hotel tunayoipenda japo nikuone."
Stela : "Hapana sasa hivi kazi zimenibana."
Nickson : "Sawa haina neno."
Stela : "MImi nataka kukuambia tu kitu kimoja Nickson."
Nickson : "Kitu gani nakusikiliza."
Stela : "Sio kwamba siamini kuwa utafanikiwa nina amini. lakini"
Nickson : "Niambie"
Stela : "Nataka kukuambia kuwa yote ninayo fanya ni kukusukuma uende mbele zaidi."
Nickson : "Kweli mpenzi?"
Stela : "Ndio mpenzi ukifanikiwa usinisahau kwa juhudi za kukufanya uende mbele Nickson ama utaniacha ukale na wanawake wengine?"
Nickson : "Hapana mpenzi wangu siezi kukuasaliti."
Stela : "Sawa Nickson pambana mimi nakungojea."
Nickson alifurahi na alipata nguvu na kujua kumbe kuna mtu anampenda? Na alijua kumbe Stela alikuwa mgumu kwake ili apambane kusonga mbele.?Nickson alijiona kama mwanaume kwa matumaini aliopewa ya uongo na Stela.Alifurahi kuona kuna mtu ana msapoti afike mbali alifurahi sana.
Itaendelea..........
Comment yako tu! ya muhimu!
Yes sir!Iko poa sana,nimeipenda.
Next time unitag please...
Mkuu kitu hiyo inaendelea kunoga!Iko poa sana,nimeipenda.
Next time unitag please...
Hahahah huyo jamaa ni komedi! Lakini kweli huyo Mpelelezi sio mtu wa mchezo watu wakikwamulia watakutwanga mpaka ushangae!Nickson : "Hamna sikuzimia alinipiga ngumi nikajifanya nimezimia kujitetea ." 🙂 🙂 🙂 🙂