MY SOULMATE SEHEMU YA 11.
Produced by : Equatorstory Specials.
Stela : "Nickson unaitwa na boss ofisini kwake."Alisema wakati Nickson yupo ana shughulika na mambo yake ya kawaida.
Nickson : "Sawa naenda."
Nickson alisimama mara moja na kuelekea ofisini kwa Boss wake.
Boss : "Karibu kijana kaa." Boss alisema akimuonesha kiti cha kukaa.
Nickson : "Asante Boss."
Boss : "Sasa kijana unajua kwa nini nimekuita hapa!?".
Nickson : "Hapana Boss sijajua bado yamkini ni mrejesho kuhusu ile barua pepe niliokutumia kuhusu budget ya mradi mpya?"
Boss : "Hapana ilo tutaongea wakati mwigine"
Nickson : "Sawa boss."
Bosss : "Kijana unajua mimi ni mtu wa sheria sana sipendi mtu ambae ana pindisha sheria."
Nickson : "Ndio Boss najua."
Boss : "Na unajua kabisa nilikutoa mbali sana kijana!?".
Nickson : "Ndio boss najua!"
Boss : "Sasa hmmmm". Boss ali shusha pumzi.
Nickson : "Ndio Boss!."
Boss : "Sasa kijana sijui nikufanyaje!"
Nickson : "Kwa nini Boss!?"
Boss : "Hujui kosa lako!?"
Nickson : "Hapana."
Boss : "Una mahusiano gani na Stela!?"
Nickson : "Una maaana gani boss!?". Hapo moyo wa Nickson ulipasuka. Alijua yamkini boss ashagundua kuhusu hili penzi la siri.
Boss : "Hujaelewa ama hujasikia!?".
Nickson : "Stela si si...."
Boss : "Nini!? Kijana umevunja masharti na ushahidi ninao!."
Nickson : "Ushahidi gani boss." Nickson alianza kuhisi kizunguzungu kwa mbali.
Boss : "Ninayo video ya wewe na Stela mkikumbatiana na kupigana mabusu huko jikoni kwani hujui kina camera humo ama."
Nickson : "Hapana Boss niliju....."
Boss : "Sasa nini una fanya yerro!?"
Nickson : "Boss ni bahati mbaya". Nickson alianza kuishiwa na pumzi alishindwa kumalizia hata sentensi yake alianza kuona kama sakafu inasogea kushoto na kulia.
Boss : "Yerro jielezeee."
Nickson : "Boss ni ....." Nickson alianza kuangusha machozi akishindwa hata kuongea akijua tayari ameshapoteza kazi yake ataishije!?
Boss : "Kijana HUNA KAZI TENA." Boss alisema kwa msisitizo huku akimpatia barua ya kufutwa kazi.
Nickson alinyanyuka akapokea hiyo barua akatoka ofisini kwa boss wake.
Boss : "Kijana fanya kukabidhi kila kitu kwa boss wako Angela. Na nisikuone tena humu ndani mjinga kabisa.."
Nickson : "Sawa boss.". Nickson alienda kwenye chumba jiko la ofisi hiyo akiangusha macozi. Alie muona akiwa katika hali hiyo ni Angela naye akamfuata huko.
Angela : "Nickson nini shida!?."
Nickson ali toa barua aliyopewa akampa Angela ajisomee . Nickson akafuta machozi na kunawa uso akawa kawaida tu alijisemea moyoni yamkini ni ishara ya Mungu niache kweli hii kazi japokuwa itakua ngumu lakini Mungu yupo.
Angela : "Weweeeeee jamani pole."
Nicskon : "Asante!!.."
Angela : "Sasa mbona kwenye barua imesema kuwa uikuwa ume onekana ukiwa ki mahaba na mfanyakazi wa hii ofisi lakini hawajasema ni nani ama ni mimi!?. "
Nickson : "Ah wewe unajua mahaba sasa!?". Wakacheka wote.
Angela : "Nickson acha utani bhana mi nina maanisha bhana eti ni ile siku ambayo uli ni kiss mdomoni kama ndo hivyo sema!.."
Nickson : "Hapana wala sio hapo!."
Angela : "Sasa je!?".
Nickson : "Boss amegundua nilikuwa natoka na Stela."
Angela "Weweee."
Nickson akamuelezea kinaga ubaga kila kitu kilichotokea. Angela hakuamini lakini pia alielewa kwanini ile siku Stela alimfyonza kisa Nickson.
Angela : "Jamani pole."
Nickson : "Nishapoa asante."
Nickson akatoka akamkabidhi kila kitu boss wake mpya Angela vitu vyote alivyotakiwa kukabidhi. Wakati huo wote boss alikua ofisini kwake na Stela wakionekana wakiongea maongezi ya kina.
Angela : "Jamani kwaheri mchungaji!. Ukatuombee huko Mungu anapokupeleka."Nickson ali cheka haku amini kama Angela ni Boss wake wamekua na ukaribu sana kana kwamba sio mtu na boss wake.
Nickson : "Nitafunga na kuwaombea."Nckson alianza kuondoka Angela akamuita,
Angela : "Pole shika hii jamani itakusaidia huko mbele ya safari si amini amini kama ndo unaondoka moja kwa moja. Kama ni uongo utanirudishia hela zangu mara mbili."
Nickson : "Hahaha haya bhana. Kwaheri."
Angela alimkumbatia mara ya mwisho lakini pia wafanyakazi wengine hawa amini kama Nickson hayupo katika ofisi hiyo tena.
Nickson ali rudi nyumbani kila mmoja aki mshangaa bila kuamini kwamba Nickson amerudi mapema .
Dulla : "NI vipi kaka!?"
Nickson : "Salama tu kaka niambie."
Dulla : "Ah mbona mapema hivyo unaumwa nini? "
Nickson : "Hapana mkuu ni majanga tu ya kawaida ."
Dulla : "Majanga gaani?".
Nickson : "Ndugu yangu nimefukuzwa kazi."
Dulla: "Sasa kisa kazi unataka kulia . Aaaaah mkuu wacha zako mi najua wewe mpambanaji sana wewe kazi yoyote unashika."
Nickson : "Hiyo kweli.."
Dulla : "Sasa wewe usiogope wewe ni mwana eti!. Usiwaze wala nini kufukuzwa kazi mimi nimefukuzwa mara tano!. Mpaka nikaona huuu ujinga wa kuomba kazi sio huu."
Nickson : "Acha utani!!".
Dulla : "Aaaaah wewe unanionaje!??? Mimi nimepigika nimekula matusi kwenye gereji za watu mara zingine nimeacha kazi sijaipwa lakini napambana."
Nickson : "Dah ndio maisha yalivyo."
Dulla : "Wewe usiwe na shaka mwana hapa nitasimama mwana huta lala njaa nikiwa ninacho kaka!." Dulla aliendelea kusema hivyo akiwa ana malizia kuvuta sigara yake.
Nickson : "Sawa ngoja nika weke huu mkoba wangu ."
Wakati Nickson anaingia akasikia sauti ya Bertha .
Bertha : "Maajabu leo kuona mwezi mchana."
Nickson :"Kivipi!?."
Bertha: "Mbona mapema nini kimekusibu au ulipotea kwenda ofisini kwako umepa sahau ama!?"
Nickson : "Kumbe leo kidato cha nne wanafanya mitihani.... Sikujua ". Nickson na Bertha wakacheka maana hiyo haihusiani.
Bertha :"Hahahaha wewe kaka kwanini usiwe kwenye vichekesho vya TV."
Nickson : "Ah hawalipi vizuri yani millioni nne!? Sasa nina fanyia nini!?"
Bertha : "Kwema lakini mbona mapema jaman unaumwa au!?"
Nickson : "Hapana. Inaonekana umetoka kuoga nenda kavae kabla hiyo kanga haijakaukia mwilini alafu nitakuja nikupe simulizi nzima."
Bertha : "Haya nivaaajae!? Au twende tukapate na ka soda kama hutojali ili stori inoge?".
Nickson : "Yote mema!".
Bertha : "Sawa."
Nickson na bertha walitoka hapo na kuelekea pahali walipopataka . Nickson akaumuelezea jinsi alivyo fukuzwa kazi . Na bertha aliamuwa kumuelezea Nickson kinaga ubaga jinsi alivyo gombana na mumewe. Hii ni baada ya Bertha kuona anaweza kumuamini Nickson.
Walikaa sehemu hiyo mpaka ilipofikia jioni wakijadili mambo tofauti tofauti kuhusiana na mada mbalimbali za maisha.
Nickson alipokea ujumbe mfupi wa maaandishi kutoka kwa Stela ukisema "Naomba tuachane sasa hivi hauna kazi hutoweza kunihudumia au hata kunimudu lakini pia utanifanya nipoteze kazi.". Nickson alishindwa kuamini inakuwaje Stela hajafukuzwa kazi?. Hakutaka kuwaza sana aliona litampotezea muda. Lakini alimtumia ujumbe mfupi wa simu.
Nickson : "Stela jamani wewe si mpenzi wangu unatakiwa unishikee mkono na kunipa ushirikiano wako niweze kusonga mbele."
Stela : "Koma kuniita mpenzi wako huelewi ama!?".
Nickson : "Jamani Stela muda huu ndo nakuitaji zaidi katika maisha yangu!."
Stela : "Hapana siwezi nikawa na mpenzi asie na mbele wala nyuma. Huna lolote utanisaidia nini? Utaleta changamoto gani za kimaendeleo katika maisha? Tafadhali sana unikome."
Nickson aliamua kukaa kimya hakujibu tena ujumbe aliotumiwa.
Maisha yaliendelea huku 'urafiki ' wa Nickson na Bertha ukizidi na Nickson hakua mtu wa kuchagua kazi yeye alikua akifanya kazi zozote anazo itiwa iwe ni zege,kuchimba mitaro kubeba mizigo alimradi mdomo unaenda kinywani. Nickson aliendelea ku sambaza maombi ya kazi kwa kampuni kadhaa ambazo anaweza kupata kazi bila mafanikio.Pamoja na kuwa Nickson anao ndugu wengine ambao wanaweza kumsaidia kifedha haku diriki kuwa omba aliona ni kheri apambane na afe ki sabuni.
Mr Mandoto alionekana akiendelea kumtafuta mke wake alipo potelea bila mafanikio lakini hakati tamaa!
Itaendelea.....