hii hadithi ni ya kutunga na si ya kweli kabisa, hapo kwenye "red" inaonyesha kuwa ulianza na story ukitafuta muunganiko ili mwisho ulete radha kwa hadhira ila umekosea sana kuleta story ambayo inakinzana kimaana na mwisho wa hadithi, kuumwa homa, malaria, tumbo na kuhara wala havihusiani na kutembea na h/girl,
Issue ya kuumwa na kukwambia umchukulie dawa na kukukuta umelala fofofo na h/girl pia haiingii akilini kwa great thinker funzadume
Kwenye "blue" ndio utata sana unasema uligonga geti mpaka ukachoka bila kupata response na kumwita kijana aje kufungua hapo kuna utata kwani ukigonga sana geti watu kama wako ndani wanachinja kobe lazima wajistukie na kuchukua taadhari (hii nimeongea kutokana na uzoefu mbalimbali) pia unasema ulipoingia ulikuwa na wasiwasi uenda mme wako amezidiwa ila pamoja na wasiwasi wako badala ya kuanzia chumbani kwenu ukaenda kwa house girl, kisha kwa watoto na mwisho ndio ukaenda kwako hii haiingii akilini kabisa maana ulitakiwa kwenda straight chumbani kwenu kujua mmeo anaendeleaje na sio kupitia kote huko as if ulikuwa umejiandaa kufumania
Kingine kwenye "blue" ni issue ya kuingia chumbani na kukuta wamelala fofofo mpka ukawaona na kuamua kutoka kwenda kuita jirani aje kushuhudia wakati huo bado tu wamelala fofofo hiyo kwa kweli aiingii akilini hata siku moja
UJUMBE kwa mwandishi:
Kutunga story ni kipaji tena cha kuzaliwa na kusomea pia usione kina Shigongo wanatunga hadithi ukadhani ni kitu rahisi tu, kile ni kipaji tena unatakiwa uwe genius kuweza kuuteka moyo wa msomaji kwa kupangilia story toka mwanzo mpk mwisho kwa umakini uliotukuka
Mkuu heshima mbelee, kwa hili umenisemea na mimi kama ulivyowasilisha.