Hadithi nahadithia leo

Hadithi nahadithia leo

hii hadithi ni ya kutunga na si ya kweli kabisa, hapo kwenye "red" inaonyesha kuwa ulianza na story ukitafuta muunganiko ili mwisho ulete radha kwa hadhira ila umekosea sana kuleta story ambayo inakinzana kimaana na mwisho wa hadithi, kuumwa homa, malaria, tumbo na kuhara wala havihusiani na kutembea na h/girl,

Issue ya kuumwa na kukwambia umchukulie dawa na kukukuta umelala fofofo na h/girl pia haiingii akilini kwa great thinker funzadume

Kwenye "blue" ndio utata sana unasema uligonga geti mpaka ukachoka bila kupata response na kumwita kijana aje kufungua hapo kuna utata kwani ukigonga sana geti watu kama wako ndani wanachinja kobe lazima wajistukie na kuchukua taadhari (hii nimeongea kutokana na uzoefu mbalimbali) pia unasema ulipoingia ulikuwa na wasiwasi uenda mme wako amezidiwa ila pamoja na wasiwasi wako badala ya kuanzia chumbani kwenu ukaenda kwa house girl, kisha kwa watoto na mwisho ndio ukaenda kwako hii haiingii akilini kabisa maana ulitakiwa kwenda straight chumbani kwenu kujua mmeo anaendeleaje na sio kupitia kote huko as if ulikuwa umejiandaa kufumania

Kingine kwenye "blue" ni issue ya kuingia chumbani na kukuta wamelala fofofo mpka ukawaona na kuamua kutoka kwenda kuita jirani aje kushuhudia wakati huo bado tu wamelala fofofo hiyo kwa kweli aiingii akilini hata siku moja

UJUMBE kwa mwandishi:
Kutunga story ni kipaji tena cha kuzaliwa na kusomea pia usione kina Shigongo wanatunga hadithi ukadhani ni kitu rahisi tu, kile ni kipaji tena unatakiwa uwe genius kuweza kuuteka moyo wa msomaji kwa kupangilia story toka mwanzo mpk mwisho kwa umakini uliotukuka

Mkuu heshima mbelee, kwa hili umenisemea na mimi kama ulivyowasilisha.
 
yaani after all that drama na pipi inalika?kweli ndimi zinatofautiana,hebu nipe namba ya kungwi wako.I need ur craziness!:mod:😛ound:

Nililia, nikajuta, nikalalamika. Mwenzangu aliomba radhi na kusema ni shetani alimpitia. Msichana kaondoka bila kufukuzwa.

Kwa upande wangu nilipewa pipi nikatulia, leo nashare kitanda na huyu bwana, tena. Naconnet dots uhusiano huu ulianza lini, na hatua gani nichukue. Sijijui sijielewi sijutambui.
 
wifi,yaani hata ww ukimfumania braza afu ukabembelezewa pipi nitakuona kichaa kama sio mwehu!ww ukimfumania tu leta kesi hapa,manake nitamla nyama aisee!kwani na ww mwehu kama lewinsky,nifunde kidogo manake nna hasira za kikurya!
Wifi ndo unanifunza nini hivi????[/QUOTE
 
Siku za karibuni mume wangu kipenzi, al aziz, nuru ya macho yangu kwa siku tofauti amekuwa akisumbuliwa na magonjwa kama vile tumbo, homa, kichwa, malaria na siku nyingine uchovu uliopindukia. Haya yote yalisababisha dia wangu arudi nyumbani kupumzika. Pamoja na hayo ufanisi wake kiunyumba ulikuwa umelegalega. Pia amebadilika tabia na kuwa mtulivu nyumbani, hata kutoka toka weekends au nyakati za jioni anapokuwa fit, amepunguza kama sio kuacha kabisaaa. Nilimshukuru Mungu kwa kumtuliza mwenzangu huyu nyumbani, kwani kutokatoka nako kuna mengi.

Jana majira ya saa saba mchana nilipokea simu toka kwa mume wangu, barafu wa moyo wangu kuniarifu kuwa anaumwa sana, na amekwenda hospitali kapimwa na kugundulika ana malaria. Kwa jinsi anavyojisikia vibaya inambidi arudi nyumbani mida ile ile nyumbani kupumzika. Aliniambia nipitie duka la dawa nimnunulie dawa alizonitajia. Nilisikitika sana na hizi homa zinazomsumbua baba watoto wangu, ikanibidi niondoke kazini muda ule ule, nipitie duka la dawa na kuanza safari ya kurudi nyumbani kumliwaza.

Nilipofika nyumbani, niligonga sana geti, halikufunguliwa. Niliomba msaada kwa kijana wa jirani akapanda ukuta na kunisaidia kufungua geti kwa ndani. Nyumbani palikuwa kimya mno, gari ya mwenzangu ilikuwepo, na msaidizi wa kike wa kazi za nyumbani sikumuona kama nilivyotarajia na nyumba ilikuwa imefugwa. Jasho lilinitoka kuwa labda mpenzi baba wa watoto wangu kazidiwa na kupelekwa hospitali au hata ameshaaga dunia nikirejea alivyokuwa akilalamika kuumwa sana. Nilipiga simu yake ya mkononi haikupokelewa, ya msichana wa kazi haikupokelewa pia.

Nikazidi kuchanganyikiwa nianze kufanya nini na nianzie wapi. Nifungua nyumba kwa funguo zangu, nikaenda chumbani kwa binti hayupo, kwa watoto hakuna mtu. Mwisho nikaingia chumbani kwangu. Nikaingia chumbani kwangu......nilichokiona sikuamini. Nikatoka na kwenda kumwita jirani yangu alisaidie kuangalia pengine angeelewa. Jirani yangu kidogo azimie.... mume wangu na msaidizi wangu wa nyumbani walikuwa wamelala fofofo kitandani kwetu, wakiwa kama walivyozaliwa!

Naomba niishie hapa.

hadithi hii kakufundisha nani? Na inatufundisha nini?
Haya makofi matatu kwa mwenzetu.........
Hongera.......... Imara.......... Waaaaaaaaaaaa
 
hadithi hii kakufundisha nani? Na inatufundisha nini?
Haya makofi matatu kwa mwenzetu.........
Hongera.......... Imara.......... Waaaaaaaaaaaa
jamani labda kweli Bujibuji
 
Back
Top Bottom