Jackal
JF-Expert Member
- Apr 10, 2012
- 9,971
- 13,608
NITAKUPA TU
SEHEMU YA 001
*********
Alihisi ilikuwa sauti ya mwanamke, sauti ambayo mwanzo alidhani haikuwa ya mwanamke kutoka na usiku ule kuwa vigumu. Lakini sauti ile bado ilikuwa ikisikika katika ngoma za masikio yake. Sauti ya mwanamke akilia na kuomba msaada, sauti ikipiga kelele za hali ya juu kuonyesha kwanba kunakitendo kiovu kinatendeka. Bado hakuijali sauti ile, alichukulia kwamba labda atakuwa ni malaya amekula pesa za watu sasa analazimishwa kulipa. Bado akapuuza akitembea kuelekea nyumbani kwake.
Licha ya kupuuza lakini safari hii, sauti ikasikika tena kwa karibu. Sauti ambayo ilipita masikioni na kwenda kuweka kituo ndani ya kina cha moyo wake. Sauti nayo ikazidi kuhanikiza, lakini safari hii kwa aina ambayo ili msisimua. Aina ambayo ilifanya kengele za hatari kugonga kichwani. Binti anayefukuzwa kulitaja jina lake usiku ule kulimpa mashaka makubwa. Kwa mara ya kwanza mkono wake ukashuka mpaka alipoihifadhi bastola yake. Kitendo cha kuitwa jina katika mazingira yale kulimpa hisia kuwa kulikuwa na namna, namna ambayo ilitengenezwa kwa aina fulani ya kutaka kitu kutoka kwake.
Wamejuaje niko hapa? Walijuaje nitapita njia hii tena katika muda huu? Yalikuwa maswali yaliokisumbua kichwa chake, yalikuwa maswali yaliomfanya aziamini hisia zake, hisia ambazo hazikuwahi kumuangusha. Sasa akatembea kwa umakini mkono ukiwa juu ya Bastola. Hakujali tena kelele za mwanadada yule. Licha ya kutokuwa na ulahai wowote katika sauti yake, lakini hakutaka kuliamini hilo, akaendelea kutembea.. lakini hakufika popote akausikia mlio wa bastola, mlio ambao uliambatana na yowe, yowe kutoka kwa mwanadada yule. Kwa mara ya kwanza akageuka nyuma, akageuka kukiangalia kilichotokea nyuma.. naam akamuona mwanadada amelala chini tena barabarani.
Hakuonekana kama alikuwa hai. Mbele kidogo ya ulipoangukia mwili wa binti yule, aliwaona wanaume wawili waliovalia makoti meusi wamesimama. Walikuwa wanaume hasa kwa kuwaangalia. Hakutaka kuupoteza muda, hakutaka kuupoteza muda kuwepo eneo lile. Akatokomea akiwaacha wanaume wale wamesimama wakimuangalia. Alitembea akijiuliza maswali mengi sana. Kama lengo lilikuwa ni yeye kwa nini wamemuua yule msichana? Walitaka nishuhudie kitu gani na kwa madhumuni yapi?
Haiwezekani watoke huko kisha waje wamuulie mtu mbele yangu harafu mimi wasinifanye kitu, kuna zaidi ya hili. Alijisemea peke yake akiufungua mlango wa nyumba yake, akaingia ndani moja kwa moja akaenda kujibweteka kwenye kiti. Sauti ya mwanamke yule bado ilikuwa ikijirudia kichwani mwake, bado aliisikia bado masikioni mwake. Akajaribu kuivuta kumbukumbu ya sauti ile kuona kama angeugundua ulahai katika sauti ya mwanamke yule, lakini hakukuwa na kitu chochote kilichoashiria kwamba mwanamke yule alikuwa akimrahai. Ilikuwa sauti iliokatika ukweli, haikuwa na hata shaka ndani yake.
Lakini sasa kwa nini mazingira yake yalikuwa ya kutilia mashaka? Hilo likamfanya ainuke na kuelekea bafuni ambapo alijimwagia maji kisha akarudi chumbani kwake. Akachagua mavazi ya kimichezo akavaa na baada ya hapo akachukua bastola yake na kutoka pale kuelekea kule alipoangukia yule mwanamke. Muda wote aliutamani ukweli wa jambo lile. Haikuwahi kutokea mtu kuuawa mbele ya macho yake. Hii ilikuwa mara ya kwanza na ilimtia mashaka sana. Alitaka kwenda kumuona marehemu, alitaka kumuona kwa kuwa aliamini angekipata kile ambacho kingemsaidia katika kumfahamu marehemu.
Akaurusisha mlango kisha akalifunga geti kwa ndani kisha yeye akauparamia ukuta na kuangukia upande wa nje. Hii ndio ilikuwa njia yake awapo katika shughuli ambayo alihisi ilikuwa na hatari mbele yake. Alipotua akachepuka na kutafuta njia mbadala tofauti na ile alioipita mwanzo. Alitembea usiku sambamba na vivuli vya miti, hata alipotokea sehemu ile bado palikuwa kimya na hata mwili wa mwanamke yule bado ulikuwepo ukionyesha kutokuwa na uhai. Macho yake yaliozoea giza yalikuwa yakizunguka maeneo yote, bado hakuiona dalili ya uwepo wa mtu katika eneo lile. Hakuiona dalili ya kufuatiliwa wala kuwekewa mtego. Mkono wake ulikuwa juu ya bastola akipiga hatua kuufuata mwili uliolala chini bila uhai. Damu ilikuwa imeunda dimbwi kubwa. Akaufikia mwili ule na kuanza kuuangalia kwa makini.
Kwa kuwa hakutaka kuupoteza ushahidi, alichokifanya ni kutoa gloves na kuzivaa mikononi. Akaushika mwili wa binti yule na kuugeuza. Cha kwanza kukiona ni matundu matatu ya Risasi kifuani. Lakini kilichomchanganya katika matundu yale ni jinsi matundu yale yalivyo. Mpigaji alionekana kusimama kwa mbele na sio nyuma kama alivyokuwa akidhani. Hilo likampa picha, picha ya kuwa yeye ndie alikuwa mlengwa. Alikuwa mlengwa kutokana na ukweli kwamba marehemu alionekana hakuwa akikimbia. Bali alikuwa ameshikwa na alikuwa akilazimishwa kukifanya kitu.
Alikuwa akilazimishwa kumuita yeye. Hapo akapata picha nzima kuwa alikuwa akihitajika yeye na sio huyu msichana. Alichokifanya nikuupekua ule mwili, hapo akakutana na vitamburisho vitatu, pamoja na kadi moja kubwa ambayo hii iliikuta kwenye Mkoba, pamoja na Simu yake ya mkononi. Akavichukua vyote na kuvisunda mifukoni. Baada ya hapo akapata wasaa wa kuiangalia sura ya mwanadada huyu. Hapo akakutana na sura nzuri na yakuvutia.
"Watu wanaroho ngumu, ya nini kumuua mtoto mzuri kama huyu? Alinong'ona huku akiinuka tayari kwa kurudi kwake.
***********
Chumba chote kilikuwa kimya, kila mmoja alikuwa ametulia akitizama mbele kuliko na Tv kubwa. Walikuwa wakiangalia taarifa ya habari kutoka shirika la utangazaji nchini. Kila mmoja alikuwa akitarajia kutangazwa kwa habari fulani ambazo zingewafurahisha. Kila mmoja ndani ya chumba kile alikuwa akiisubiri taarifa hiyo kwa hamu. Alikuwa akisubiri kile ambacho kingewafanya wao wawe katika kiwango cha juu katika biashara zao. Lakini ilikuwa kinyume wa kile walichokitarajia.
Taarifa ambayo walikuwa wakiisubiri kwa hamu haikuja kama vile walivyotarajia. Bali vijana wao wanne walikuwa wamekamatwa wakiwa na mzigo wa madawa ya kulevya. Walikamatwa na maafisa wa usalama uwanjani hapo. Kila mmoja akapagawa, kila mmoja akahisi labda yupo ndotoni. Mzigo wao wenye thamani ya bilioni ishirini na mbili za kitanzania ulikuwa umekamatwa. Wakawaona vijana wao wakisukumwa kuelekea katika chumba maalum kwa ajili ya mahojiano zaidi. Chumba kikazizima kwa taharuki. Mmoja akaiendea simu yake na kupiga namba fulani. Muda mfupi simu ya upande wa pili ilikuwa ikiita. Iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa. Hata aliporudia bado hali ilikuwa pale pale.. hilo likawafanya watu wale watizamane.
"Haiwezekani!! Mmoja akanguruma.
"Kuna mchezo, huyu mwingine aliongea huku akishindwa kuuhimili presha. "Jimmy hawezi kutufanyia hivi!!!" Mwingine akaongeza. Lakini bado haikuondoa ukweli kwamba Mzigo wao ulikuwa umekamatwa na kulikuwa na uwezekano hata wao wenyewe wakatajwa. Bado simu haikupokelewa, bado iliendelea kuita kwa muda mrefu. Wajumbe wote wakazidi kushangazwa na hali ile. Lakini kabla hawajakaa sawa wakaisikia simu ikiita. Safari hii ilikuwa ikipigwa.
"Jimmy!!" Aliita.
"Jackson!!" Naye akaita..
"Atafutwe Teddy Harryson!!" Aliongea Jimmy kisha bila kusubiri maelezo yoyote akakata simu. Wajumbe wote wakaangaliana, hakuna alieamini maneno ya Jimmy. Kila mmoja alikuwa akiwaza mzigo wao uliokamatwa. Kitendo cha kuambiwa wamtafute Teddy Harryson bila kupewa maelezo yoyote kuliwakera baadhi ya wajumbe. Lakini wakiwa bado kwenye Mshangao wa kutokumuelewa Jimmy, simu ikatoa mliokuonyesha kuna ujumbe umeingia.
"Mpigie Teddy Mwambie akailete Roho ya Binti mmoja ambaye alikuwa chanzo cha kukamatwa kwa mzigo wetu. Nataka nikikupigia simu kwa mara nyingine unipe taarifa ya Roho Ya huyo Binti kuwasili hapo." Ulisomeka Ujumbe Ule.
ITAENDELEA