Hadithi: Nitakupata Tu

NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 045
Ukimya ukachukua nafasi maeneo yale.
Hakuwa akisikia tena ile minong'ono.
Akausogelea mlango katika aina fulani
ya ukimya. Hata alipoufikia mlango
bado hapakuwa na kizuizi chochote.
Masimba akajaribu kutizama huku na
huko, lakini bado hapakuwa na kizuizi.
Bado hapakuwa na mtu. Mkono wake
ukashika kitasa na kukizungusha,
mlango ukamtii kama mfano wa mbwa
anapomtii chatu. Bastola ilikuwa
imetangulia Mbele tayari kumuondoa
mtu yoyote. Akaufungua zaidi kisha
kuingia. Alipoingia ndani alipokewa na
ukimya tena. Kuingia kwake tu hata ile
miguno ikapotea. Akaikamata bastola
zaidi na zaidi. Kidole bado kilisubiri
kuifanya kazi yake. Kazi ya kutoa tiketi
na hata usafiri. Usafiri wa kuwapeleka
watu kuzimu. Alitaka wakapumzike
sambamba na mama yake na hata Dee.
Alitaka wakajibu mashtaka yake mbele
ya Asteria na Familia yake. Kuingia
hapo akapokewa na harufu ya mipira
ya kiume. Harufu ya condom ilikuwa
imetawala katika nyumba ile.
Akaongeza hatua mbele kuwatafuta
wasafiri. Akaipita sebule bila kukutana
na kizuizi chochote. Aliposogea mbele
akasikia vishindo vya mtu vikionyesha
mtu kusogea kule alipo. Punde
akamuona mwanamume akitokea
katika giza lile. Giza ambalo alishindwa
kutambua kwa nini limeachwa
kutawala pale ndani. Mwanaume yule
akatembea na kupita karibu na
Masimba bila kumuona. Masimba
akamuacha apite, alivyopita
akamtokea kwa nyuma na kumkata
karate ya Shingo. Mtu yule akaanguka
kama mzigo. Baada ya kuhakikisha mtu
yule hayupo hai, akamsachi mifukoni.
Akamkuta na Bastola mbili sambamba
na vitamburisho kadhas. Vyote
akavichukua na kuvisunda mifukoni.
Baada ya kumaliza vyote akamshika na
kumuweka pembeni. Akasogea pale na
kuanzs kutembea kuingia ndani
alipotokea yule mtu. Wakati
anaukaribia mlango akasikia watu
wakiongea kwa ndani. Katika
mazungumzo yao akahisi walikuwa
watatu kutokana na mchanganyiko wa
Sauti zao.
"Mbona Fred harudi? Richie hembu
muangalie inawezekana amezima.
Aliisikia sauti ikitokea ndani. Masimba
akajua kuna mtu anakuja. Hivyo
akajibanza pembeni. Mara akauona
mlango ukifunguliwa kisha mtu tena
akatokea. Masimba akamuacha asogee
mpaka usawa wake. Hata alipoufika
usawa ule akajikuta akiguswa na kitu
cha barifi. Kisha sauti nzito ya
mwanaume ikanguruma. "Tulia kama
Ulivyo, ukifanya chochote sitasita
kukusafirisha kuzimu." " mtu yule
hakutarajia lile, akahamanika na kutaka
kupiga kelele. Masimba akamuwahi
kwa pigo moja ya kidogoni, mtu yule
akaanguka kama furushi. Masimba
akamuwahi na kumshindilia ngumi
kama tano. Mtu yule akatepeta kama
mlenda. Alimpekuwa mifukoni. Huyu
hakuwa na Silaha yoyote zaidi ya
paketi tano za condom. Akamuacha
sasa alikuwa akizama ndani kuwakabili
watu ambao walikuwa ndani.
Aliusukuma mlango taratibu na
kuchungulia kwa ndani. Watu wawili
walikuwa wamepakatana miguuni.
Kilichomshangaza huku ndani taa
hafifu zilikuwa zikiwaka. Nuru hiyo
ndio iliyofanya macho yake kutua kwa
watu wale wawili. Mwanaume na
mwanamke. Akaufungua mlango tena
na kupiga mluzi. Yule mwanaume
aliyekuwa amempakata mwanamke
akamuomva mwanamke asimame
kisha yeye kusogea pale mlangoni
huku akiuliza.
"Richie kuna nini? Aliuliza mtu yule
huku akiufungua mlango pasipo na
tahadgari. Akajikuta akikutana na
mapigo matatu ya kung fu. Mtu yule
akapepesuka na kwenda kumuangukia
mwanamke yule. Masimba hakuitoa
nafasi hiyo kwa mtu yule kuinuka.
Akawawahi wote pale chini huku
mdomo wa Bastola ukiwatizana sawa
sawia. Wote walikuwa wakitweta kwa
hofu. Kila mmoja alikuwa ameyatoa
macho yake akimtizama Masimba. Hofu
ilikuwa ikionekana machoni mwao.
Hofu ambayo haikufanana na
uonekanaji wa watu hawa. "Nimekuja
na tiketi zenu za kuzimu, nimekuja na
usafiri wa kuwapeleka huko. Lakini
mkinijibu maswali yangu naweza
kufikiria kuwaacha." Aliongea masimba
Akiwatizama watu wale pasipo
kuonyesha utani. "Usituue tutakujibu
maswali yako." Aliongea mwanamke
yule akitetemeka.
"Jimmy na suresh wako wapi? Akauliza
masimva.
"Mimi sijui unauliza nini. Alijibu yule
mwanaume akimuangalia masimba
usoni. "Narudia tena wako wapi Jimmy
na Suresh? Aliukiza tena safarii hii
akiuinua mkono ulioshika bastola.
"Unataka nikujibu mara ngapi?
Nimesema sijui.. akajibu tena yule
mwanaume. Muda ule ule mlipuko
mdogo ukatokea, bastola ya nasimba
ilikuwa imekohoa. Risasi ikatua
kwenye paja lake la kushoto. Akapiga
yoweee kubwa sana. "Utasema
hutasema? Akauliza masimba huku
bado bastola yake ameielekeza kwa
mtu yule aliyekuwa akigumia kwa
maumivu. Wakati mtu yule akiharibu
kujibu mlango ukasukumwa kwa
nguvu huku risasi kama mvua
zikimiminwa mle ndani. Masimba
akajivingirisha chini kisha kuchupa na
kuangukia pembeni. Risasi zikapita
muda ule ule akasikia yowee kutoka
pale alipowaacha wale majambazi.
Baada ya muda wa dakika tano. Risasi
zikakoma ukimya ukatawala Eneo lote.
Masimba Bado alikuwa amejificha pale
akiwaangalia wale watu. Hata wao
walionekana wakitafuta kitu. Hapo
akajua walikuwa wakimtafuta yeye.
Hakutaka kuwachelewesha, bastola
yake ikakohoa tena mfululizo. Watu
wanne walikuwa wakianguka mithili
ya magunia. Walikuwa tayari kwenye
safari ya kuzimu. Baada ya kuhakikisha
amewamaliza wote akainuka na
kusogea pale. Hapo akagundua hata
yule mateka wake wakiume alikuwa
ameuawa. Lakini kilichomshangaza ni
kutokumuona mwanamke yule. Wakati
akiendelea kutafuta akasikia kilio
kutoka chini ya kiti kikubwa . Punde
akamuona msichana yule akiinuka
huku akitetemeka. Bastola ya masimba
tayari ilikuwa ikimtizama. Lakini
alipomuangalia vizuri usoni..
Akajisemea malaika huyu hapaswi
kufa. "Nifuate tuondoke hapa kabla
polisi hawajaja." Aliongea Masimba
Huku akimvuta yule msicgana
waondoke mle ndani.
******
Walikuwa wawili tu ndani ya chumba
cha hoteli ile. Bastola ilikuwa bado
mkononi kwa masimba akuendelea
kumuangalia mwanadada yule
aliyekuwa akitetemeka kwa hofu.
"Unaitwa nani? Akauliza masimba
akiendelea kumtizama.
"Nani.!!!? Mimi au... aliuliza Binti huku
akitetemeka.
"Kwani hapa tuko wangapi?" Akauliza
Masimba akimuangalia tena.
"Tupo wawili." Akajibu tena Hofu
ikionekana machoni.
"Basi tambua nakuuliza wewe..
naomba unijibu kabla sijabadili
maamuzi." Aliongea Masimba.
"Naitwa SALHA ....." akajibu msichana
yule. "Umefikaje pale kwenye ile
nyumba na nani amekufikisha? Aliuliza
Masimba akiendelea kumuangalia.
"Nimeletwa pale na Jimmy. Wakati
ananileta aliniambia kuwa
amenitafutia kazi, lakini nilipofika
aliniweka pale kama Msimamizi wa
Biashara yao. Alijibu yule msichana. "JE
ni Biashara gani inafanywa pale? Na
kwa nini ulipogundua kazi ulioambiwa
haipo, wewe ukaendelea kukaa? Binti
yule akamuanglia Masimba kisha kwa
sauti yake ya upole akajibu. "Naogopa
kukwambia wataniua..... Maana
nishatishiwa kupigwa bastola. Baada ya
kumuuliza kwa nini ana muogopa mtu
mmoja aitwaye masimba.". " kwahiyo
una muogopa Jimmy lakini huniogopi
mimi? Tambua mimi ni israil nikiamua
ufe haufikishi sekunde moja. Naomba
nijibu maswali yangu kabla sijakupa
tiketi yako." Alinguruma Masimba
akimuangalia binti yule. Salha akainua
uso na kumwangalia masimba kisha
kwa Sauti dhaifu akasema ....
ITAENDELEA


 
NITAKUPATA TU

SEHEMU YA 046

Binti akainua uso kisha kwa sauti
dhaifu akasema. "Biashara inayofanyika
pale ni uingizaji na usambazaji wa
madawa ya kulevya hapa nchini. Kuna
viongozi wengi wa serikali, wabunge
na mawaziri ni watu wenye hisa
kwenye biashara hiyo. Na wafanyakazi
wote tuliambiwa kwamba nilazima
tufumbe midomo yetu la sivyo
tutauawa. Wenzangu wengi
wameshauawa kutokana na kuivujisha
siri hii. Nadhani hata nami nipo njiani
kuwafuata. Kama usiponiua wewe basi
wataniua wao." Alijibu msichana yule
hofu ikionekana kwenye macho yake.
Masimba akamuangalia kwa nukta
kisha akamuuliza tena.
"Unaweza kunitajia majina ya mawaziri
watatu unaowajua? Swali hilo
lilionekana kuwa gumu kwake.
Akamuangalia Masimba kisha
akaonekana kufikiria kwa muda. Harafu
akashtuka kutoka huko na kutingisha
kichwa kabla ya kusema. "Hapana
siwezi kufanya hivyo, nitauawa.". Hilo
likaonyesha kumkwaza masimba.
Akamuangalia kwa muda huku mdomo
wa bastola ukimlenga msichana yule.
"Naomba unijibu maswali yangu, la
sivyo nitakusafirisha kuzimu sekunde
hii hii. Kama hujui mimi ndiye Masimba
ninayeogopewa na mabosi zako. Nina
uwezo wa kukufanya chochote. Sitaki
unilazimishe kufanya hili." Aliongea
huku akiendelea kumiangalia
mwanamke yule. Akausoma mshtuko
kutoka usoni kwa mwanamke yule.
Mshtuko uliotokea baada ya kulitaja
jina lake. Sasa akaiona hofu ikiyeyuka
katika uso wa mwanamke yule.
Tabasamu hafifu likaupamba uso wake.
Lakini ghafla akaliona tabasamu
likiyeyuka na kupotea ghafla kama
mshumaa kwenye upepo mkali. Sura
ikagubikwa na hofu tena. Ni hofu hiyo
iliyompumbaza masimba. Ni hofu hiyo
hiyo iliojenga maswali lukuki kichwani
kwa masimba. Tabasamu katika
sekunde tatu, lakini tabasamu
likapotea katika sekunde ya nne na ya
tano. Hofu ikamuingia tena mwanamke
huyu. Kwa nini hofu? Kwa nini aogope?
Anaogopa Jina langu ama anawahofia
watu wake? Yalikuwa maswali,
maswali ambayo hayakufanikiwa
kupata Jibu katika wakati ule ule.
Kwani ni muda ule aliokuwa akiongea
na Salha akauona mlango ukitingishwa
kisha kukasikika mlango kugongwa.
MASIMBA NA SALHA wakatizamana,
waliangaliana katika namna ya
kuulizana "Huyo ni nani" hakukuwa na
mwenye jibu. Lakini hapo hapo
akamuona Salha ikisimama na kuufuata
mlango. Hata hilo likamshangaza na
kumburudisha machoni na hata
Moyoni. Hakuburudika kwa utamu wa
mtikisiko wa Nyuma wa Binti huyu,
hakuburudika kwa kulitamani hilo, bali
aliutamani uamuzi wake na kujiamini
kwake. Huyu alikuwa kama Teddy
Harry Wake. Huyu alikuwa Teddy yule
wa kipindi kile. Teddy aliyekuwa
haogopi risasi na hata kifo. Hilo
likamkumbusha Syria. Kwenye mission
ngumu ambayo haikuwahi kutokea.
Salha alikuwa ni mfano huo. Licha ya
hilo lakini bado alikuwa makini na kila
hatua ya binti huyu. Hatua ya
mwanamke ambaye alionyesha kuwa
na vitu vingi. Hofu ikapotea usoni, hofu
ikapotea katika muda huu huu. Alikuwa
mfano wa kinyonga, alibadilika kila
wakati. Kila hatua yake ilikwenda
sambamba na mdomo wa bastola wa
Masimba. Hakumuacha ageuke akiwa
pekee. Ni pale alipoufikia mlango
ndipo likatokea la kutokea. Mlango
ukasukumwa wakaingia wanaume
katika aina ya kuburudisha na
kusisimua. Kila mmoja aliingia akiruka
hapa na kutua pale. Ilitia raha na hata
kuburudisha pia. Lakini wakati
akiliangalia hilo hata yeye alikuwa
ameshahama pale na kuangukia
pembeni. Ni wakati akitua hapo chini
akimuona mwanamke yule akifanya
kitu ambacho kilimfanya ashangae.
Binti alikuwa akionyesha burudani.
Alikuwa akihama hapa katika
kuwakabili watu wale. Alikuwa akipiga
mateke ngumi na hata vichwa. Alikuwa
akichanganya kung fu kareti na hata
martial combat. Ilikuwa burudani
kumtizama na ilikuwa burudani
kumuangalia. Haikupita hata dakika
mbili tayari wanaume wale walikuwa
wamelaliana wakiwa hawana uhai. Hilo
likikuwa jingine kwake. Licha ya uzuri
wake, licha ya urembo na muonekano
wake lakinikumbe alikuwa ni Hatari.
Binti yule akaufunga mlango tena na
kurudi pale alipokuwa Masimba
amesimama. "Nipo tayari kukujibu
maswali yako. Nipo tayari kukujibu
chochote kile utakacho." Aliongea
Salha akimuangalia Masimba. Masimba
naye akamtizama. Wakatizamana na
kutizamana. Kulikuwa na sumaku
machoni kwa mwanamke huyu wa
kichaga. Macho yalikuwa yakiongea
vitu vingi sana. "Nadhani lipo swali
langu hukunijibu." Akakumbusha, Kisha
akaongeza, "nataka kujua majina ya
mawaziri na hao wabunge. Pia nataka
kufagamu walipo Jimmy na Suresh."
Salha akamuangalia Masimba kisha
kwa sauti ambayo haikuwa na Hofu
Akajibu.
"Mawaziri ni Haji Mvula waziri wa
maliasili na utalii. Waziri Utajiju Nyuma
wa mambo ya Nje na mwingine
Alikuwa Waziri mkuu ambaye
amemuua wewe juzi. Wabunge ni
Hagare Maro wa jimbo la tarime.
Selestine pascal wa ukerewe na bibi
Grace Bwahama wa kigamboni. Akajibu
Salha.
"Jimmy na Suresh wako wapi?"
Akauliza tena Masimba. "Jimmy na Ben
Wamemfuatilia Teddy kwani
inasemekana ametoroka hapa jijini
akiwa na mtoto wako waliemchukua
baada ya kumuua mama yako mzazi.
Inasemekana Teddy aliomba likizo ya
ghafla kazini na alipokubaliwa jana
alionekana akitoka Airport na tokea
hapo hakuonekana tena mpaka muda
huu. Baada ya kufuatilia huku na huko
waligundua Teddy alikuwa ameelekea
Arusha akiwa na mwanao tayari kwa
kuihama Nchi. Wakapiga simu kwa
watu wetu kule kuwapa taarifa na
kuwataka wafuatilie hilo lakini majibu
yaliokuja ni kwanba Teddy
hakuonekana Airport wala kwenye
barabara yoyote. Ndipo jimmy na Ben
walipoamua kwenda arusha kuongeza
nguvu."
 
NITAKUPATA TU

SEHEMU YA 047

Teddy ametoroka na mtoto na
inasemekana wameelekea Arusha.
Lakini tulipowasiliana na watu wetu
kule hawakumuona Teddy popote pale
licha ya kupekuwa viwanja vyote vya
ndege sambamba na kuangaliwa kwa
umakini kwa kila gari ambayo ilikuwa
ikiingia arusha na kutoka. Hivyo basi
Jimmy na Ben wameelekea huko
kumtafuta Teddy ili wamuue ili
wamchukue mtoto wako iwe chamba
cha kukufanya wewe urudishe mzigo
uliouchukua." Aliongea salha
akimtizama masimba kwa umakini.
Alitaka kugundua nini ambacho
angekishuhudia machoni kwake. Lakini
hakukutana na chochote kile,
hakukiona alichokuwa anakitafuta.
Licha ya masimba kutokushtuka kwa
taarifa ile, lakini moyoni na kichwani
hakuwa katika usawa. Hakuwa katika
utimamu wa kiakili na hata kimwili.
Alimuwaza france, alimuwaza
mwanaye aliempenda sana. Hakutaka
kukubali mwanawe kupotezwa.
Alinhitaji mwanawe akiwa hai.
Alimuhitaji france akiwa kwenye
tabasamu lake alilolizoea. Lakini
alipofikiria kuhusu Teddy kutoroka
bado mwanamke huyu aliiyumbisha
akili yake. Bado mwanamke huyu
hakueleweka upi msimamo wake.
Alifanya mauaji na usaliti wote sababu
ya Kundi lao. Hata kuuawa kwa mama
yake, Teddy alikuwa nyuma ya kifo cha
mama yake. Lakini leo hii tena Teddy
alikuwa akisakwa na Jimmy, teddy leo
alikuwa ametoroka tena akiwa kwepa
Jimmy na Kundi lake. Kwa nini
amekimbia? Kipi kimemfanya akimbie
Tena akiwa na france. Akaiona Hatari
mbele yake endapo atamuacha Jimmy
amfikie Teddy. Alitambua ungekuwa
nwisho wake sambamba na mwanawe
france. Hapo akaamua kufanya kitu.
Akarudisha macho kwa Salha.
Wakaangaliana kwa mara nyingine.
Kila mmoja akisoma kilicho ndani ya
macho ya Mwingine. Kila mmoja alijua
yupo na nani. Licha ya salha
kudanganya kuwa ni mfanyakazi wa
kawaida haikuwa hivyo. Huyu alikuwa
Jasusi. Alisomeka na Masimba
alilitambua hilo. "Naelekea Arusha
kumrudisha Teddy na France, nina
kisasi na teddy na nitapenda kumuua
kwa mikono yangu. Naomba tuondoke
hapa nikakuache sehemu salama.
Lakini kukuacha huko itabidi ufumbe
na usiufumbue Mdomo wako. Ukifanya
hivyo nilichomfanya mwamvita Muda
mfupi uliopita ndio nitakachokifanya
kwako." Alinguruma masimba huku
akianza kutembea kuelekea Nje. Licha
ya Masimba kutembea kuelekea nje,
lakini Salha bado alikuwa amekaa.
Alionyesha kupigwa na bumbuwazi.
Maneno yaliyotamkwa na Masimba
yalimuingia sawasawa. Kwamba
mwamvita amekufa? Kwamba
mwanamke yule katili ameuawa?
Kilikuwa kitu kigumu kukiamini.
Alijikuta akiwa kondoo mbele ya
Masimba. Alimfuata kwa nyuma
akihitaji kukijua kile alichokisia. Hata
alipomkaribia Masimba bado
aliilazimisha miguu yake kutembea.
Akamuangalia Tena masimba. Lakini
kabla hajaongea chochote simu yake
ikaonyesha uhai. Kuna mtu alikuwa
akimpigia. Akaitoa simu na Kuitizama.
Jimmy,neno pekee lililosomeka Juu ya
kioo. Akasita kisha kumuangalia Tena
Masimba. Kuangaliwa kule akatambua
kulikuwa kuna kitu. "Jimmy anapiga.!!
Ilikuwa sauti iliyomvuta Masimba
karibu na Salha. "Pokea, harafu
muulize yuko wapi na wamefikia
wapi." Ilikuwa amri kutoka kwa
Masimba, amri ambayo ilitekelezwa
muda ule ule.
********
Alikuwa juu ya kaburi la mama yake
Masimba akilia kwa uchungu katika
usiku ule. Moyo wake ulikuwa
umepondekapondeka. Alikuwa akijuta
na hata kulia kwa sauti. Hakuna baya
ambalo alifanyiwa na huyu mama. Siku
zote alimpenda kuliko hata mwanawe
Masimba. Alikuwa akisuluhisha
migogoro yao kwa upendo mkubwa.
"Nisamehe mama yangu, bila ujinga
wangu leo hii nisingekupoteza. Tamaa
ya pesa imenifanya niusahau utu wako.
Imenifanya nisahau mapenzi yangu
kwako. Nikafanya kitu ambacho sasa
nakiwaza. Mama nipo hapa
nikishindwa kujua wapi nitakwenda.
Masimba ananisaka aniue mama.
Masimba anitafuta anilete huko, sina
uwezo na ujasiri wa kusimama mbele
yake kumuomba msamaha. Sina ujasiri
hata wa kumuangalia Machoni. Mama
nakisubiri kifo changu hapa hapa Juu ya
kaburi lako. Nataka Risasi ya Masimba
Inilipue nikiwa hapa. Nitamwambiaje
mama na hata baba yangu? Vicky
atanielewaje katika hili niliofanya?
Ataniacha? Vipi mwanangu patra?
Hapana Nastahili kufa." Yalikuwa
maneno aliyotamka Teddy akiwa juu
ya kaburi. Alikuwa Tanga badala ya
Arusha. Alitambua asingeweza kufika
arusha bila kutiwa nguvuni. Kitu
alichoona ni kushinda juu ya kaburi ya
mama yake Masimba. Alishinda hapo
huku france akimuacha nyumbani
kwao kibugumo Nje kidogo ya Jiji la
Dar es Salaam.
*****
Alishuka Handeni Usiku wa Saa sita kwa
Usafiri wa kukodi. Baada ya kushuka
hapo akaongoza Moja kwa moja mpaka
nyumbani kwao ambapo bado watu
walikuwa wanalala Matanga. Aliwakuta
wengi wa watu wakiwa wamelala
huku wachache tu ndio waliokuwa
wakiota moto. Aliwasalimia wachache
waliokuwepo na kuanza kuongea nao.
Kufika hapo akakutana na vilio kutoka
nyumbani kwa mzee First wazo,. Hapo
akagundua kuwa tayari taarifa za kifo
cha Dee Plus zilikuwa zimefika hapo
kijijini. Wakaongea mpaka asubuhi
kulipokucha. Watu wakajiandaa kwa
sababu ya kwenda kuchimba kaburi la
kumhifadhi Dee plus. Wakiwa bado
wanajiandaa wakalisikia yowe kutoka
kwa mmoja wa watoto ambaye alipita
karibu na makaburi. Watu
waliokuwepo msibani wakageuka na
kutizama huko. Wengine walishaanza
kukimbia kuelekea kule wengine
wakibeba silaha tayari kwa lolote.
Masimba ndio aliyekuwa wa kwanza
kufika pale makaburini. Macho yake
yakatembea katika sekunde ile ile.
Macho yake yakatua juu ya kaburi la
mama yake. Akamuona mtu akiwa
amelala juu akionyesha kudhoofika
mwili. Hakushangazwa na kule
kudhoofika, bali alishangazwa na mtu
aliyejuu ya kaburi. Teddy alikuwa juu
ya kaburi la mama yake. Kaburi la
mwanamke ambaye alihusika katika
kumuondoa duniani. Alikuwa amelala
na alikuwa akionyesha kuchoka sana.
Wakati huo watu wengine nao
walikuwa wameshafika. Kila mmoja
alikuwa akikiangalia kile
kinachoendelea pale. Mwanamke
wanayemjua alikuwa akilia, akilia juu
ya kaburi la mama wa masimba. Kaka
yake Masimba aitwaye Samwebondo
ndiye aliyepiga hatua kuelekea pale
kaburini. Dada zake masimba naye
wakaungana naye kuelekea pale.
Sekunde hii walikuwa wakimbeba
Teddy akiendelea kulia. Licha ya ndugu
wote kufanya hivyo lakini kwa
Masimba haikuwa hivyo. Bado
alisimama akimuangalia Teddy Hasira
zikimchemka. Alitamani kuchomoa
bastola yake na kumlipua. Alitamani
kumuendea pale na kufanya lolote.
Lakini hakuweza hilo, kwa kuwa
macho ya watu yakaanza kumtizama
na minong'ono kuanza taratibu. Watu
walianza kuhoji katika hili. Walianza
kuhoji ulipo utu wa masimba.
Wakamlaumu tena na tena. Masimba
hakuwasikiliza. Akaondoka pale
akiwaza na kuwazua. Alitaka kumuua
Teddy, hakutaka alione Juaa la kesho,
lakini angemuuaje wakati tayari teddy
alikuwa mikono mwa ndugu zake tena
akiwa mwenyewe pasipo mtoto wake?
Kwa nini hakuelekea arusha na
kuamua kuja huku? Inamaana tokea
majuzi alikuwa pale juu ya kaburi.
Alijiuliza huku akijilazimisha kutembea
kurudi nyumbani. Hapo akakutana na
kitu kingine. Dada zake walikuwa
wamembadili nguo na sasa walikuwa
wakimpeleka bafuni kwa minajili ya
kumuogesha. Hapo akatamani
kuwaambia ukweli. Alitamani kupaza
sauti lakini hakuweza. Hawakuweza
kwa kuwa dada zake walimpenda na
Hawakujua kama alikuwa nyuma ya
kifo cha mama yao. LAITI WANGEJUAA!!
@@@??? SIDHANI KAMA KUNGEKUWA
NA HATA MMOJA ANGEMGUSA.
ITAENDELEA
 
NITAKUPATA TU

SEHEMU YA 048

Hawakujua chochote kuhusu kuhusika
kwa teddy katika kifo cha mama yao.
Walimpenda Teddy kama wifi yao.
Hawakujali hali ambayo alikuwa nayo
Masimba. Masimba bado alikuwa
amejiinamia mahali akifikiria.
Hakuonyesha kujali katika kile
ambacho kilikuwa kikiendelea.
Alimpoteza Dee plus kwa sababu ya
Teddy, kama sio Teddy kumsaliti leo hii
mama yake mzazi asingekufa. Lakini
usaliti wa teddy umesababisha
madhara makubwa sana kwake. Leo hii
teddy alikuwa mbele yake katika
nyumba ya mwanamke yule yule
aliyemuua? Alikuwa amepokewa kama
malkia. Mwanamke aliyemuua mama
yake alikuwa akifurahiwa na ndugu
zake wote. Sasa alikuwa akienda
kuogeshwa kama mwali ama mtu
maalum. Moyo ukampasuka hasira
zikiendelea kupanda. Muda huu
alikuwa akijipapasa bastola yake. Ni
jana tu aliachana na Dee katika aina ya
kazi yao. Ikimpa Dee kazi ya kumtafuta
Teddy.. lakini leo hii Dee alikuwa
marehemu. Alikuwa amepigwa risasi
zisizo na Idadi. Akatamani ainuke ili
aondoke zake arudi dar es salaam,
lakini angeondoka vipi bila kumzika
Rafikiki yake? Kuliwaza hilo kulimfanya
Masimba Atulie. Punde akawaona
ndugu zake wakimfuata pale alipo
wakiwa wameongozana na Teddy.
Wamemshika huku na huko. Hilo
hakulitegemea na Hata kuliwaza. Hilo
hakuliamini na hakutaka iwe. Lakini
ulishakuwa. Teddy alikuwa mbele ya
miguu yake akiwa amepiga magoti
akilia. Alikuwa katika kuuomba
msamaha kwa kile kilichotokea.
Ingawa asingeweza kurudisha uhai wa
mama lakini bado aliliona kosa lake.
Akaanguka miguu kwa Masimba akilia
na kulia. Masimba bado alikuwa kimya
akimtizama. Akimtizama teddy huku
fundo kubwa likiwa kooni. Ni teddy
huyu huyu aliyemuondoa Asteria,
Mwamvua na Hata familia ya Asteria. Ni
teddy aliyemleta Mwamvita kwao
mpaka kumuua mama yake. Ni Teddy
aliyewapiga watoto katika mapigo
ambayo haya stahili. Teddy leo alikuwa
miguuni mwake akagalagala. Teddy
leo alikuwa akihitaji kusamehewa. Ni
msamaha gani angeweza kutoa? Je
akiutoa huu msamaha roho za watu
waliouawa kwa kushiriki kwake
zitarudi? Yalikuwa maswali yaliohitaji
Majibu, yalikuwa maswali yaliohitaji
ufumbuzi kwa wakati ule ule. Ni
ufumbuzi gani angeupata pale kwa
wakati ule? Hakujua!! Na kamwe
asingejua. Alipoinua uso kutizama
mbele yake, akakutana na macho ya
ndugu zake yakimtizama katika namna
ya kuumuuliza. "Hana mbwani hano,
mbona hachikuelewa" (kuna nini hapa
mbona hatuelewi).. Kila mmoja
alikuwa akihitaji Majibu kutoka kwake.
Angejibu nini wakati akijibu kutatokea
jingine tena kubwa.
"Welewe chigambile ichindeni,
mwanangwa kumtenda zeze? Aliuliza
mjomba wake aitwae kilango
almaarufu kwa Jina la kabanza.
Akimaanisha kutaka kujua ukweli nini
ambacho amemtenda Mtoto wa watu.
Masimba hakuweza kujibu. Bado
alikuwa akikumbuka tukio la
mwamvita. Mwili wa Mama yake
ulipotupwa juu baada kupigwa risasi.
Mama anauma na mama anaumiza.
Akainama tena kisha kumuangalia
mjomba wake. Machozi yakashuka
mpaka mashavuni. Masimba alikuwa
akilia mbele ya ndugu zake. Wote
walikuwa kimya wakiwatizama
wapenzi hawa. Hawakuijua siri ambayo
ilikuwa mioyoni mwao. Bado alikuwa
akilia machozi. Punde mikono yake
ilishuka na kushika mabega ya Teddy.
Teddy akaacha kulia na kuinua uso
kisha kumtizama Masimba. Macho yao
yaliojaa machozi yakiangaliana kwa
zaidi ya dakika mbili. "Mapenzi" ndio
kitu kilichoonekana machoni mwao.
Ndio kitu kilichozungumzwa katika
macho yao. Punde walikuwa
wakikumbatiana kwa nguvu kila
mmoja akilia. Teddy ndiye
aliyeonekana akilia na kujutia zaidi.
Ndugu wakaungana nao katika kilio,
kilio ambacho mara hii kikageuka na
kuwa msiba. Wote walikuwa
wakimkumbuka mama yao.
******
Walikuwa wawili tu chumbani
wakitizamana. Safari hapakuonekana
mapenzi machoni kwa huyu kijana wa
kiume. Uso wake ulikuwa
umekunjamana kwa hasira. Alikuwa
akimtizama mpenzi wake kwa hasira.
Bastola ilikuwa mkononi akimuangalia
Teddy. "Kabla ya yote nahitaji kujua
alipo mwanangu France. Aliongea
Masimba huku macho yake
yakimuangalia Teddy. "Yupo Nyumbani
Toangoma. Nilimuacha kwa kuwa
nilikuwa na maamuzi magumu."alijibu
Teddy huku akimuangalia masimba
zaidi na Zaidi. "Mpigie Vicky niongee na
France, ole wako unidanganye
nitakuua kwa mikono Yangu..." teddy
hakujibu, alichokifanya nikuchukua
Simu ya Masimba na kuingiza namba
ya Vicky, kisha akaipeleka sikioni. Muda
mfupi simu ilikuwa ikiita. "Hellow
Mume mambo?" Alisikika sauti ya
upande wa pili kutoka kwa Vicky
ambaye ni mdogo wa Teddy. "Safi
mke, naomba Kuongea na Mwanao
mkubwa.." aliongea Masimba. "Yupi
patra au nani? Akauliza Vicky huku
akionyesha kushangaa. MASIMBA NA
TEDDY wakatizamana. Haikuwa
kawaida kwa vicky kutokumjua Mtoto
mkubwa.
"Hapana sio Cleopatra, nataka
kuzungumza na France." Alijibu
masimba. Ukimya wa ghafla ukatokea
upande wa pili. Mshangao na kengele
za hatari zikagonga vichwani mwao.
Ukimya wa ghafla wa Vicky
uliwashangaza.
"Vicky bado upo hewani bado?."
Akauliza Masimba. "Ndio nipo hewani
mume. Lakini nimeshangaa kwa simu
yako kumhitaji France. Wakati kuna
mtu amekuja hapa akadai mmemtuma
amchukue France awaletee? Aliongea
Vicky huku naye akianza kuhisi hali
kutokuwa sawa. Kengele ya Hatari
ikalia. Pale pale Teddy akaichukua simu
kisha kwa sauti ya kupagawa akasema.
"Ni nani amekuja hapo nyumbani?
Niambie Vicky!!" Huku vicky
akionyesha kuchanganyikiwa akamjibu
"alikuja rafiki yako yule wa kike
akaniambia umemtuma mtoto..." jibu
hilo likakifanya kichwa cha Teddy
kufanyakazi kwa Haraka. "Mwamvita
utanikoma nikikukamata." Aliongea
teddy bila kujua kuwa mwamvita
hakuwa hai. Alishasafirishwa kuzimu.
"Mwamvita hawezi kufufuka kwenda
kumchukua France. Huyu Atakuwa
Salha. Mwamvita nilishaamuua na
kilichokuwa kikifuata ni kifo chako."
Alijibu Masimba akimuacha teddy
kwenye mshangao. "Salha umemjuaje
salha?" Akauliza teddy sasa
akimuangalia Usoni kwa makini.
"Hatuna muda wa kujibizana na
kuukizana. Naamini unazijua njia zote
wanazopitia watu hawa. Nimekupa hii
kama nafasi ya Mwisho. Ukingengeuka
na nikahisi chochote nitakuua Teddy.
Naomba Ubaki hapa nyumbani. Sitaki
uwaambie chochote. Nasikitika
kuondoka nikiacha mazishi ya Dee plus.
Lakini hakuna namna ngoja niwahi.
Tutaonana Dar es salaam." Aliongea
masimba huku akisimama na kuanza
kupiga hatua. Teddy akamuwahi na
kumkumbatia. Punde ndimi
zikagusana. Nahitaji tuongozane
masimba. Nahitaji kupambana kufidia
damu yote nilioshiriki kuimwaga.
Nitakupeleka kila ngome ninayoijua na
tutafanya kile ambacho unakitaka."
Akaongea Teddy huku akimuangalia
Masimba. Hata masimba akamtizama.
Safari ya Dar es salaam ikaanza huku
masimba akiwa makini sana juu ya
Teddy.
*******
Kilikuwa kikao kidogo kilichokuwa
kikifanyika nje kidogo ya Jiji la Dar es
salaam. Kilikuwa kikao kidogo
kilichowakutanisha washirika wote wa
biashara ya kulevya hapa nchini.
Viongozi wa serikali, wabunge na
maafisa na wakurugenzi wa mashirika
mbalimbali ya kigeni. Ni kati ya watu
waliokusanyika katika kikao hiki. Kila
mmoja alikuwa kimya akitega sikio
kusikia lolote kutoka kwa
mwanamkakati wa kuingiza biashara
hiyo bwana Jimmy Lambert. Kila
mmoja alikuwa akimuangalia
mwenyekiti wengi wakishangazwa na
ule uonekanaji wake katika siku ya leo.
Jimmy alikuwa mpole sana. Alikuwa
amejiinamia akiitizama picha ya
mwamvita. Picha ya mpiganaji wake
alieuawa usiku uliopita. Akainua uso
wake na kuwatizama wajumbe
wenzake....
 
Mtunzi wa hii riwaya.. ...kwani yupo hai?!

Pumu Ni ugonjwa mbaya Sana!
 
Tuendelee na tulipoishia weekend hii..... Mtunzi karibu
 
Si vyema kuiipost mali ya marehemu Ibrah Mwasimba huku ukiwa umetoa hadi jina lake, tulikuwa naye humu mwandishi ibra87 ambaye hivi sasa katangulia mbele za haki na kazi hiyo alishaitumia humu yeye mwwnyewe


Moderator
 
Mkuu, sijaandika mimi. Naenzi kile alichokua anafanya ni kwa nia nzuri tu. Samahani kama umekwazika. Hivi aliimaliziaga yote?
Haitakiwi kutuma kazi ya mwingine kwanza na kama humu ipo uzi wake haikuwa na maana ya kufanya hibyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…