MUDA
SEHEMU YA SABA.
TUKIO LA AJABU KWA ANITHA
Wakati Nelson Akiangaika huku Anitha amechanganyikiwa mno, haelewi afanye nini
“Ni wapi hapa mzee wangu?”
Aliuliza Anitha Hata hivyo Mzee yule hakumjibu, mzee alikuwa bize akiudumia watu chai na maandazi.
Anitha alihisi labda Mzee yule amekataa kwasababu hakununua chochote kwake.
Anitha alichomoa noti ya elfu tano na kumpa mzee yule,
“Hii shilingi ya wapi?”
Aliuliza Mzee yule kwa Kiswahili kibovu.
Hata hivyo Anitha hakushangaa kwani rangi yake na mwonekano wake ulimwonyesha kuwa sio Mtanzania wa Asili. Alikuwa Mtu wa Asia hasa kutoka Masati.
Wateja walijikusanya kuona ile fedha ni ya nchi gani kusema kweli ilikuwa ya Tanzania ila ilitofautiana na pesa walio nayo.
“Leta kama hii”
Alisema yule Mzee, Anitha alipoitazama ilikuwa shilingi (50 ya zamani) Wakati Anitha anazidi kushangaa , Gari aina ya landrova iliyopakia Watu na Mizigo kwa pamoja ilisimama na konda alisema “kwa Azizi,Tumefika kwa Azizi Ally”
“Kwa Azizi Ally! Aliongea kwa mshtuko, Anitha Hali ya Hewa ilikuwa nzuri Hapakuwa na joto kali kama Eneo alilokuwepo majumba yalikuwa machache sana, tena ya hali ya chini ni kwa Azizi Ally tu ndiko kulikuwa na nyumba inayoeleweka, hakukuwa na kipande cha Barabara kinachotoka Temeke kuingia Barabara kuu,Barabara ilikuwa moja nayo ilikuwa ya vumbi ila ilionekana vizuri.
Anitha aliitazama Saa yake ya mkononi, ilikuwa inawaka mwanga wa Zambarau na mshale wake ulikuwa ukicheza chezasana kana kwamba imeishiwa moto kwenye Betri toka nipewe miaka nane iliyopita sasa imekuwaje? Anitha alijiuliza kisha akatumia kile kitufe cha ile saa kurudisha ule mshale sehemu yake.
Ajabu nyingine ilitikea alijikuta sebleni kwa Mama Nelson kilichomshangaza zaidi alijiona yeye akicheza Mziki na Mama Nelson.
Alibaki amewatazama huku ameduwaa bado hakuwa anaelewa chochote Mama Nelson na Anitha yule waliacha kucheza Walimgeukia na kumuuliza “Wewe ni nani?”Hakujibu chochote alikuwa amemtazama Nelson aliyekuwa amewatazama wanaocheza mziki usio sikika.
“Mimi ni .......Alishtushwa na Mtu aliyemshika mkono na kumburuta kwa nguvu. Alipo hamaki alimuona Nelson aliyekuwa akimvuta mkono kwa nguvu
“ Mbona sielewi!”
Alilalamika Anitha, Usijari wewe nifuate nimeshaelewa kinachoendelea.”
Alilalamika Nelson huku akimvuta kwa nguvu.
Walienda kwakukimbia mpaka lilipo Gari la Anitha , Anitha aliingia akiwa wa kwanza kwa woga kisha Nelson aliingia na kukaa upande wa pili wa Gari hilo. Anitha Aliwasha lile Gari walipofika mbele kidogo Nelson alitamka Anitha asimame naye Anitha alitii akiegesha lile Gari pembeni kisha waligeuka kutazama nyuma kwa maelezo ya Nelson.
Baada ya mda walimuona Nelson, Anitha na mama Nelson wakija lilipokuwa Gari walipofika walianza kuhamaki kwa kutoiona Gari , Hapo Nelson aliye kwenye Gari alibonyeza kitufe cha saa yake mpaka sehem flani kisha akimwambia Anitha afanye hivyo nae Anitha aliitazama Saa ya Nelson na kuona ule mshale uko wapi.
Alikibonyeza kitufe cha Saa yake na kupeleka mshale mpaka eneo lilelile kama la Nelson. Hapo walijikuta eneo lile walimpungia Mama yao mkono nae mama yao alirudi nyumbani huku akifurahia.
Bado Anitha alikuwa hajaelewa jambo lolote, Anitha aliwasha Gari na kuondoka alipofika Mtoni kwa Azizi Ally alikuta foleni aliamua kuwasha Mziki hata hivyo Nelson alimkataza. Anitha aligeuka na kumtazama lakini alipomuona Nelsoni amekunja uso aliogopa kumkwaza tena, aliamua kuuzima Foleni iliruhusiwa, yeye kabla hajafikiwa “Nelson alimuona mama fulani akikimbia kuvuka Barabara alikuwa amemshika Mtoto mkononi ila Mtoto yule aliogopa Gari lililokuwa limeanza kuitawala Barabara, Aliuachia mkono wa Mama yake na kubaki nyuma , Hapo Nelson alimwambia Anitha “Mtazame mtoto yule ,Mama yake ni waajabu sana amemuacha peke yake”
Anitha alizima breki na kuwasha taa kama ishara ya kumruhusu apite, Mtoto yule alikimbia kwa woga lakini alifanikiwa kuvuka.
Aliushikilia Mtandio wa mama yake kwa nguvu. Baada ya Anitha kujihakikishia hilo aliruhusu Breki na kukanyaga mafuta na gari lilivuka sehemu ile kwa usalama,Anitha aligeuka na kumtazama Nelson , Nelson alikuwa na Tabasamu usoni mwake, Hapo Anitha nae alitabasamu pia Tabasamu lililo tafsiri huba,
Yote hayo yalitokea wakati anapiga kona ya uhasibu kuelekea Barabara ya kwenda Tazara.
Mkono wa Anitha ulikuwa ukiwashwa washwa kuwasha mziki ila alipogeuka kumtazama Nelson na kumuona yuko bize na kusoma alama zilizokuwa kwenye Saa yake aliacha na kuongeza mwendo.
Walifanikiwa kufika salama pale nyumbani kwa Anitha, Anitha alianza kumuita Jeni mfanyakazi wake, Jeni alitoka chumbani kwake kwa furaha na kumkumbatia Anitha “Ulikuwa wapi Dada? Ujue niliogopa siku zote hizo unaniacha peke yangu kazini kwenu wameisha kutafuta kila siku wanakuja hapa” Aliendelea kumwagia maneno bila kupumzika.
Ila kitu kilichomshangaza Anitha ni kuambiwa amemuacha Jeni kwa muda mrefu.
Yeye aliona ni Tukio la Saa chache lakini Jeni aliongea kana kwamba amemaliza mda mrefu, Tena sio wa Saa moja tu bali Siku kadhaa.
Ndipo alipoamua kumuuliza Jeni “Kwani sikuwepo kwa mda gani?” Hata sijui nisemeje Dada ila ni kama aah” Alionyesha kushindwa kuhesabu mda huo.
Hapo Nelson alimuomba amuonyeshe sehemu ya kuwashia Redio. Alipomuonyesha Nelson alisogea na kuwasha Redio hiyo, Mziki mtamu uliokuwa na mwendo wa Taratibu ulianza kusikika
“Tucheze basi”
Nelson alisema huku anajitikisa tikisa. Anitha alianza na Nelson alimfuatisha na hiyo ilikuwa Burudani ya bure kwa Jeni aliyekuwa amemzoea Anitha kwa staili zake.
Wakati wakiendelea kucheza taratibu Nelson alisema
“kuna kitu hujagundua bado”
“Kitu gani?
Aliuliza Anitha.
Baada ya kumkosakosa Mtoto mara ya kwanza ulijikuta wapi?
“Hata sielewi watu wenyewe haweleweki mavazi yao, hakukuwa na nyumba wala Barabara ya lami, ila nilisikia wakisema et kwa Azizi Ally! Alifafanua kwa mshangao Anitha.
“Bila shaka wewe ulirudi nyuma Anitha”
“Nilirudi nyuma?
Unamaanisha nini Nelson”
“Ndio! Wakati wewe unasema ulikuwa huko usipopafahamu, Mimi nilienda mbali kabisa, Mbele kabisa ya hapa tulipo ila Nyumba ilikuwa hii hii.
Wewe utakuwa na watoto mapacha wanaofanana sana. Hilo nililiona.”
Nelson alisita kumwambia kuwa kuwa ndiye atakuwa Baba wa wa Watoto hao. Aliziona wazi hisia za Anitha , hivyo kama angesema jambo hilo lingemfanya hashindwe kutimiza jambo Jipya lililokuwa akilini mwake.
“Sasa hilo liliwezekanaje?
Aah, halafu ulimuona Baba wa Watoto hao?
“Anitha aliendeleza maswali”
“Itazame Saa yako Anitha!”
Anitha alinyanyua mkono wake na kuitazama ilikuwa ikihesabu kawaida mda wake, aligeuza kichwa na kutazama iliyokuwa mkononi mwa Nelson, nayo vile vile, ilikuwa kama yake.
“Hii ndiyo inayofanya mambo yote, Mimi nilienda kununua Saa, Tukio flani lilitukia na kila kitu kilisimama, ila saa hii pekee ndio iliendelea kehesabu Wakati, Wewe hiyo uliipataje?
Aliuliza Nelson huku akiutazama uso wa Anitha uliokuwa umegubikwa na mshangao.
“Nilipewa Saa hii miaka nane ilyopita, Nilikuwa nimelazwa pale Hospitali ya Misseny, kipindi kile iliitwa Bunazi nadhani na sasa hivi inaitwa hivyo kama sijakosea, Daktari mmoja wa kiume ndiye aliyenipata Saa hii, Tena nayakumbuka maneno yake , alisema “Kati ya vitu ninavyopaswa kuvitunza Maishani mwangu ni Saa hii”
Tena aliongeza kuwa “Nikijua kuitumia Saa hii maisha yangu yatabadilika, tena nitakuwa na uwezo wa kufanya chochote nje na ndani ya mda” Ila mimi sikuelewa na wala sijawahi kuelewa maana ya maneno yake, nilichoamua kufanya ni kuitunza vizuri Saa hii.”
Alitua kidogo na kumtazama Nelson aliyekuwa akitetemeka kama mtu mwenye woga.
“Kila ninapoiona saa hii inanikumbusha kuwa nisije nikatamani kujiua tena”
Wakati anaongea maneno hayo machozi yalikuwa yakimlengalenga machoni mwake.
Bila kutarajia Nelsoni alimvuta kwa nguvu na kumkumbatia huku akisema .
“Kumbe ni wewe niliyekuokoa kwa Dakika 28?”
“Na hapo ndipo maisha yangu yalikoharibikia”
Alilalamika Nelson kwa uchungu huku akiruhusu machozi kutiririka Mashavuni.
“Nilijua ni wewe tu niliposikiliza simulizi lile, ni wewe Nelson, Neli ni wewe, nakumbuka unaniuliza , Tatizo nini? Bas niambie nitakusaidia,
Nilikuwa nimejichukia kuliko kitu kingine chochote hapa Duniani, sikutaka niishi tena , ni Daktari yule , Mwenye huruma kama wewe, ndiye aliyenisaidia kurudisha Akili yangu na alinisaidia nijione mwenye thamani tena.”
Wakati anaongea maneno hayo vilio vya kusigina vilikuwa vikisikika pale Sebleni.
Hapo Jeni alitoka chumbani kwake na kuja kuchungulia sebuleni , aliwaona wakilia huku kila mmoja akijaribu kumpoza mwenzake lakini kila mmoja alipouona uchungu uliokuwa usoni mwa mwenzake, kila mmoja ilishindwa kuzuia machozi yake.
Kila mmoja aliachia kifua cha mwenzake na kuanza kumfuta machozi mwenzake.Wakati Nelson
Ana yafuta machozi ya Anitha, Anitha aliachia kicheko chenye mchanganyiko wa kilio, hapo Nelson aliwaza
“Huyu analia ama anacheka?”
Na jambo hilo lilimfanya kuachia kicheko kikavu na wote walikuwa wamerudia furaha yao ya awali.
Jeni alibanwa na kicheko baada ya kuona hali hiyo, Aliziba mdomo wake kwa nguvu na kukimbilia chumbani kwake aliofika aliufungua mlango wa chumba chake ili aweze kucheka , ila kicheko hicho hakikuwepo tena, aliishia Tabasamu tu.
Hata hivyo anitha alisikia mchakato wa mbio za Jeni na kutambua kuwa Jeni alikuwa akiwachungulia.
Sasa naomba unisikilize Anitha uliona nilichokifanya pale Mtangoni nilitumia Saa hizi tulizo nazo kuurudisha Wakati nyuma ,ili nirekebishe makosa tuliyoyafanya mpaka tunamgonga Mtoto na Madhara ya hilo, Wewe ungepalalaizi miguu na kutembelea kigari cha magurudumu Maisha yako yote. Lakini tulirekebisha na ndio maana tulipita salama, na mpaka sasa tuko hapa.
Mimi nafarijika kuuona uwepo wako mbele yangu ukiwa salama salimini. Aliongea hivyo huku akiipapasa miguu ya Anitha, Anitha alihisi mshtuko moyoni mwake na kuanza kucheka cheka bila mpangilio.
“Unajua nini Anitha , Tunapaswa turudi pale hospitalini ulikolazwa ili tukutane na yule Daktari, iliatufafanulie maana ya Saa hizi na kuna madhara yoyote yanayotokana na kuuchezea huu mda?
Anitha alinyanyua mkono wake na kuanza kugusa kile kitufe cha saa ili autafute mwako ule ukiwa hospitalini, hata hivyo Nelson alimzuia
“Unataka kufanya nini wewe?”.
Aliongea kwa kufoka hadi Anitha alishtuka.
“Si umesema turudi nyuma miaka nane?”
Sio hivyo Anitha ukirudisha mda nyuma utakuwa hapa hapa ila wakati wa nyuma, vipi ikiwa kutakuwa hakukuwa na usafiri imara wa kwenda Mkoa wa Kagera tena wilaya ya Missenyi,eeh! Inabidi tusafiri mpaka pale harafu tuweze kurudisha Wakati nyuma”
Anitha alifurahi sana na kuanza kuruka ruka kama mcheza Mziki aina ya Amapiano.
“Nina wazo sasa”
Alisema Anitha aliyekuwa amegubikwa na shangwe, Twende miaka kumi mbele alafu tuone usafiri yawezekana gharama za ndege zimeisha shuka, labda ni kama mabasi au treini za umeme zitakuwa zimeboreshwa, itakuwa rahisi kwetu kufika kule tunakotaka kwenda.”
Nelson alikuwa akimtazama Anitha aliyekuwa akionyesha shauku ya aina yake.
“Nikimzuia tena atajisikia vibaya acha nikubaliane nae tu, ila sio vizuri ni kutumia uwezo ulio nao bila sababu maalumu”.
Nelson alimkubalia na alimuomba waende miaka ishirini mbele , akilini mwake alitaka awaone Fobi na Robi kuna tatizo lolote litawapata, walikubaliana wote na kurudisha mshale wa Saa zao mpaka miaka ishirini ijayo, Rangi yenye mchanganyiko wa zambarau na njano ilianza kuonekana kwenye Saa hiyo.
Walipobonyeza walijikuta kwenye Nyumba kubwa yenye gholofa tatu kwenda juu, madirisha yote yalikuwa vioo vitupu walipotupa macho nje waliona Magari yamepangana yenye rangi za aina mbili tu. Wakati wakiendelea kustaajabu, Walisikia kelele za ugovi kule gholofa ya juu, Mara moja Nelson alimshika mkono Anitha na kuanza kumvuta waelekee huko juu kadri walivyosonga ndivyo kelele zilvyozidi kuongezeka.
Kuingia tu ndani Fobi na Robi walikuwa wamekamatana kabala ya nguvu huku maneno
“Ni wangu! Ulijua ni wa kwangu!”
Yalikuwa yakiendelea.
Huku Baba yao akiwa anajaribu kumnyanyua Mama yao ambaye alikuwa amesukumwa kwa nguvu na kujigonga kwenye sakafu baada ya kuingilia ugomvi ule.
“Mnafanya nini Rafiki zangu?”Mama yenu mnakaribia kumuua nyie bado mnaendelea na ugomvi?
Alitamka Nelson.
“ Ni huyu Robi na ugomvi wake, amempiga Mama yangu”Aliongea kwa kufoka Fobi”Bas achianeni Rafiki zangu” Alizidi kusisitiza Nelson, Hawakumshangaa Nelson wanamfaham ila mshangao ulikuwa kwa Anitha, kwani kitendo cha kujua Mtoto wake atampiga kiasi hicho, kilimfanya afadhaike sana.
“Tatizo nini wanangu”?
Alihoji kwa masikitiko Anitha,Lakini ni kama swali lake lilihamsha asira zao.Kusema kweli hawakuweza kuona utofauti wowote kati yao na mtu huyo anaye waita wanae.
“Wewe ni nani hadi utuhite sie wanao?”
Alihoji Robi,Kusema kweli Robi alikuwa mtu anaye ongozwa na hasira katika maamuzi yake.
“Unataka kuleta balaa linguine Robi”?
Alitamka yule mzee aliye kuwa akijitahidi kumnyanyua mke wake aliye kuwa akiugulia maumivu makali.
“Niambie tatizo lenu tafadhari,tumesikia purukushani zenutukasemezana,ngoja tuwasaidie” Aliongea kwa kusihi Nelson.
Fobi alisogea na kuanza kufafanua kwa hisia yenye uchungu.
“Rafiki zetu, matatizo yote yanasababishwa na Robi,Mimi nina mchumba wangu na tunaendana sana. Ila Robi amekuwa akitumia kigezo cha kufanana na mimi na kumchanganya mchumba wangu. Hii leo nimemuona akimlaghai na kumpeleka katika hoteli bora hapa jijini.Nimemuo nimemuona kwa macho yangu”
Alitua Fobi huku kifua chake kikipanga na kushuka mithili ya gari la Suzuki la kizamani.
“Eti umefanyaje Robi?”
Alihoji kwa hasira Nelson.
“Tatizo siyo mimi ni yeye na mama yake,Wao wamekuwa wakinitenga hawaendezwi na mafanikio yangu.Kila mara wanazungumza wao wenyewe,Ila mimi uniona kama kivuruge tu ninaye wavuruga. Hemu mpigie msichana huyo aje hapa!”Aliamrisha Nelson, na Fobi alinyanyua simu yake na kumpigia . Haikuchukua mda aligonga kengele ya nyumba yao Fobi na Robi walinyanyua sim zao na kuzitazama walimuona msichana huyo akiwa mlangoni, Fobi alibonyeza namba fulani katika simu yake na milango ilifunguka kwa kufuatana na yule msichana aliingia ndani .
Alionesha kustaajabu kwa mshangao mkubwa “Usiogope Dora we sogea tu hapa”
Dora alikuwa akiona kama maajabu ndani ya jumba hilo la kifahari. Alimtazama Fobi na Robi wanavyofanana utadhani ni mtu mmoja, ila jambo lililomshangaza zaidi ni kumuona Nelson na Anitha huku Baba yake Fobi na Mama yake nao wakiwa wamekaa ni umri tu ulio watofautisha.
“Sasa Fobi ni yupi?”