Hadithi: Ulimwengu wa Watu Wabaya

Shusha shusha, kwani inatoka Kila baada ya muda gani?
 
HADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
MTUNZI : Bux the story teller
WHATSAPP : 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 14

UKURASA ULIOPITA TULIPO ISHIA.............

“kuhusu kutumia upanga sasa umeiva vyema kama nilivyokuwa nahitaji na nakuomba tu usikae ukalitumia panga wala kutembea nalo sehemu nyingi unazo enda kwani siku utakayo amua kuutumia upanga wako inawezekana ukawa mtu hatari sana kitu ambacho kitapelekea kuleta taharuki kubwa miongoni mwa watu mbali mbali, kwahiyo hii italeta kukosekana kwa amani miongoni mwa watu wanao kuzunguka. Leo nakupa huu upanga kama zawadi ya pekee, huu ni upanga ambao nimekuwa nikiutumia Kwa zaidi ya miaka thelathini sasa na kuulinda sana kwa miaka yangu yote na kwa nguvu zangu zote, huu upanga ni hazina kubwa sana ndani ya nchi ya Japan kwahiyo unapaswa uutumie vyema ikiwemo na kuulinda kama unavyo yalinda macho yako.
Chamwisho huu upanga utumie pale itakapo kubidi ila tu usiutumie vibaya kwa kuwadhuru watu wasio kuwa na hatia yoyote ile hiyo itapelekea nikuue kwa mikono yangu mwenyewe kitu ambacho hakitakiwi kutokea kwa sababu mimi ndiye ninaye takiwa kukulinda kwa namna yoyote ile.

ENDELEA...................

Baada ya siku mbili kupita Calvin alipelekwa kwenye moja ya vyumba ambavyo vilikuwa na ukimya mkubwa mno kiasi kwamba huwezi kusikia kitu chochote kile.
“zoezi la mwisho kwa hii miezi miwili na nusu iliyobakia ni hisia, una hiyo milango yako mikubwa ya fahamu mitano lakini usisahau hisia ndo kitu cha mhimu zaidi kwako, hayo maskio yako yanatakiwa yawe yanafanya kazi kuanzia umbali wa mita mia moja ili kuweza kusikia kitu chochote ambacho kinaendelea kwa umbali huo” aliongea master na mara moja utekelezaji ulianzia hapo, mazoezi haya yanahitaji utulivu mkubwa sana kuanzia mapigo ya moyo na namna mtu unavyokuwa unapumua, kwa kufuata maelekezo Calvin alikuwa anayafanya vyema sana kitu ambacho kilimpatia furaha sana master Haru .

Tarehe 12 mwezi wa 3 mwaka 2015 ikiwa imepita takribani miaka miwili na zaidi ya miezi 6, ndiyo siku rasmi ambayo YOUNG BILLIONAIRE Calvin Jackson alikuwa anakamilisha mafunzo yake ndani ya nchi ya Japan.

“kwa sasa naweza nikasema umekuwa miongoni mwa wanaume wa shoka sana lakini ili niweze kuliamini na kulithibitisha hilo bado una kazi moja ya kuifanya, nadhani unakumbuka vyema nilikuahidi ili niweze kukujibu maswali yako na kukuruhusu kuondoka kuna mtihani wa kuufanya, una dakika tatu tu pekee za kuufanya, unapaswa ufanikiwe kunipiga ngumi moja tu kwenye mwili wangu, hicho kitu ni rahisi sana kukitaja lakini utekelezaji wake ni mgumu sana, haya sitaki maelezo mengi kazi ni kwako kama uondoke au ubaki ila ukumbuke tu ukishindwa nafasi ya kuondoka tena itajitokeza baada ya miaka mingine miwili ijayo” ni maneno rahisi sana yalitoka kinywani mwa mzee huyu lakini yalikuwa ni magumu mno kwenye suala la kuyatekeleza.

Calvin alizikunja ngumi zake vizuri kisha akamwendea kwa spidi ambayo ilimfanya mzee huyu akubali kwamba bwanamdogo alikuwa ameiva haswa, Calvin alirusha ngumi nzito zaidi ya kumi na mbili kwa sekunde nane pekee lakini hakubahatika hata kumgusa mzee huyu, kabla hajarudi nyumba alirusha mateke kwa mkupuo kisha akiwa hewani akizunguka na double kick kwa kasi ya ajabu sana lakini alishangaa kumwona mzee huyu amesimama nyuma yake akiwa anamwangalia mikono yake iko nyuma, wakati anamwangalia mzee huyu alionyesha kusikitika tu na kuangalia upande wa saa, ilikuwa imebakia dakika moja tu pekee, Calvin jasho lilimtoka kwa maana alikuwa na sekunde sitini pekee za kumsaidia na kujitetea ili aweze kutoka nje ya kambi hiyo. Mzee haruto alimkumbusha tena “kuna muda unapaswa kutumia zaidi akili kuliko nguvu” kisha akapotea mzee huyu na kusimama upande wa pili Calvin aliogopa hii hakuwahi kuiona kabla alicho amua kukifanya ni kujaribu bahati yake kwa kutumia hisia, basi akayafumba vyema macho yake halafu alimfuata mzee huyo kwa kasi sana akatishia kama anarusha ngumi maeneo ya kichwani kisha akasimama ghafla, wakati ule mzee Haruto alikuwa amepotea ili kuikwepa ngumi ile lakini raundi hii alikuwa na bahati mbaya, kwani wakati anakwepa ngumi ya kwanza Calvin alikuwa tayari amesimama na kuzitumia vyema hisia zake, kwa mbali alisikia kama kuna upepo unapita karibu yake kwa kasi sana, alijibetua kwa teke moja safi sana ambalo lilimrudisha mzee Haruto kama hatua kumi nyuma. Ilikuwa ni mara ya kwanza kupigwa na binadamu na kusogezwa umbali mrefu kiasi hicho, alitabasmu na kuangalia saa ilikuwa sekunde ya hamsini na tisa dakika ya pili.

Alitamka “now you free to go (sasa uko huru kwenda) na nitakujibu maswali yako kuhusu mimi na baba yako”.

Bux the story teller

"Ni zaidi ya miaka thelathini iliyopita katika nchi ya Malaysia ndani ya jiji la QuaraRumpa, ni miongoni mwa majiji mazuri sana na majiji pendwa yaliyojengwa kwa ubora mkubwa sana hapa ulimwenguni. Ilikuwa ni mwishoni mwa mwaka kwahiyo ni muda ambao watu mbali mbali kutoka sehemu mbali mbali duniani huwa wanasafiri sehemu tofauti tofauti ulimwenguni kuweza kufurahia sikukuu za kufungia mwaka pamoja na likizo mbali mbali. Ni muda ambao nilikuwa kwenye mapenzi mazito sana na mwanamke mmoja ambae nilimpenda sana na ndiye alie nipatia mtoto wa pekee ambaye nae nimeishia kumpoteza, nilipewa likizo ya miezi sita baada ya kumaliza mafunzo yangu ya ukomando, basi niliichagua nchi ile ambayo nilikuwa naipenda sana kutoka moyoni.

Nakumbuka ilikuwa ni wikiendi majira ya usiku nilitoka na mpenzi wangu tukaenda hotelini kuweza kupata chakula cha usiku lakini kwa bahati mbaya sana baada ya kushuka kwenye tax niliyokuwa nimepanda nilidondosha waleti yenye pesa, kadi za bank na kila kitu kwenye ile tax bila hata kujua, tulifika hotelini na kuagiza chakula cha gharama sana kwa sababu sikuwa na shida kabisa ya pesa, tulivyo maliza kula chakula akaja mhudumu kudai malipo yake, lahaula ile naingiza mkono mfukoni nilishtuka sana sioni kitu chochote, hakuna alie weza kuniamini mle ndani wote walijua mimi ni mhuni na sikutaka nijitambulishe kama mimi ni komando kwa sababu nilikuwa ni mtu wa siri sana.
Mhudumu aliamua kuwaita walinzi ili wanikamate kwani walishahisi mimi ni mwizi, lakini kabla ya hilo kutokea kuna kijana mmoja alikuwa amekaa kwa muda kidogo na maeneo yale akiwa kavaa suti huku ameshika begi yake nyeusi, nilimuona tangu naingia mle ndani ila sikuwa hata na mpango nae kwani uwepo wake pale ulikuwa haunihusu kwa lolote, na kwa mwonekano wake haikuhitaji hata kujielezea kwamba ni mtu mwenye pesa za kutosha. Alinyanyuka taratibu kusogea upande ule ambao nilikuwa nimekaa na sikujua alikuwa na lengo gani.

Alivyofika pale hakutaka mambo mengi, aliwakataza watu wasifanye chochote kama tatizo ni pesa basi atalipa yeye pamoja na gharama za usumbufu, alikuwa kijana mpole na smati sana nilivutiwa naye, lakini niliipenda kauli yake moja “hata kama mnamdai mtu kiasi gani, mnapaswa kuelewa na kuuthamini utu wa mtu kwanza, sina imani kama mtu huyu alikurupuka kuja hapa lazima alijipanga lakini inawezekana kuna shida imetokea ndio maana akafikia kukosa pesa, mlipaswa kumsikiliza kwanza” kisha akalipa pesa milioni kumi taslimu akidai zingine ni za usumbufu, baada ya hapo akanipa pole na kuanza kuondoka, kwanza nilibaki nimeduwaa tu nisielewe cha kufanya.

Mimi ni komando nimezunguka sehemu nyingi sana duniani na nimekutana na watu wa kila aina lakini sikuwahi kufikiria kwamba watu wema wa namna hii bado wapo duniani wakiendelea kuishi. Kwenye maisha yako unapaswa kumheshimu sana mwanadamu ambaye anakusaidia wakati una uhitaji mkubwa sana wa hicho kitu na ulikuwa huna namna ya kukipata alafu mtu huyo anakusaidia na hana hata shida na hiyo asante yako, mwalimu wangu jeshini aliwahi kuniambia siku moja kwamba mtu anae kusaidia shilingi miatano ukiwa una uhitaji nayo ni mtu muhimu na wa thamani zaidi kuliko mtu anae kuja kukupa milioni mia moja ukiwa hauna shida na hiyo pesa, siku ile nililithibitisha hilo kwani nina pesa nyingi sana lakini siku ile nilikuwa nahitaji pesa ya kawaida tu ili nilipie bili lakini sikuwa nayo kwa muda ule, wanadamu wa hivi wamebaki wachache mno ukizingatia na kiwango alicho kitoa pale angeweza hata kununulia gari ndogo au kwenda kufurahi nchi yoyote ile, siku ukimpata mtu wa aina hii haupaswi kumpoteza kwa namna yoyote ile hata Kama ni kwa gharama ni wachache mno kwenye hiki kizazi.

Basi haraka sana nilimkimbilia kabla hajaingia kwenye gari ili niweze angalau kumfahamu hata jina

“hey bro” nilimuita akageuka

“oooh ni wewe mr nilijua unaendelea kula ndiyo maana sikutaka kukusumbua”

“no kula nishamaliza, hivi wewe ni nani na umetoka wapi?”

“Jackson Aron, natokea Tanzania” alinijibu kifupi

“daaah aisee nafikiri nchi yako inastahili heshima kubwa sana, mtu hata hunijui lakini umeamua kunisaidia kwa kunitolea pesa nyingi kiasi kile alafu ajabu hutaki hata asante yangu nimeshidwa hata kukuelewa ndugu yangu”

Alitabasamu kijana yule kisha akanijibu “pesa ni muhimu sana lakini pesa ni watu, pesa inatengenezwa na watu, pesa inatumiwa na watu hiyo inamaanisha bila pesa mtu unaweza ukaishi hata kama ni kwa shida lakini pesa haiwezi kuwepo bila watu. Hiyo inatukumbusha kwamba ubinadamu na utu ndio msingi mkubwa wa haya maisha mafupi tunayo yaishi kila siku kwa sababu kuna siku sitakuwa na pesa ila nitasaidiwa na kuzikwa na watu, na unapaswa uishi ukielewa kwamba ukipata nafasi ya kumsaidia mtu usisubiri malipo wala asante kutoka kwake ila tu kupitia msaada wako nayeye ataenda kusaidia wengine nao wengine watasaidia wengine, na hivyo ndivyo mimi ninavyoishi na nilivyo lelewa na wazazi wangu kwahiyo usijali kabisa kwa kilicho tokea pale japo unapaswa tu kuwa makini na siku nyingine”.

*********************************

Tangu nianze kuyaishi maisha yangu yote kwenye dunia hii iliyo jaa dhuluma na dharau, baba yako mzee Jackson ndiye binadamu wa kwanza kunihakikishia kwamba hata kuwe na watu wabaya kiasi gani ila kwenye hilo kundi watu wema huwa wanakuwepo japokuwa ni wachache mno, yule ndiye mwanadamu wa kwanza mimi kunivutia kwa maelezo yake hapa duniani.

Tangu siku ile sikuhitaji kumpoteza miongoni mwa wanadamu wachache sana ambao walikuwa ni bora sana kuwahi kuishi kwenye uso wa dunia hii, nilimuomba tukakae sehemu bahati nzuri hakuwa mbishi akakubali, niliamua kumuelezea uhalisia wa maisha yangu, nilimwamini na kumpatia siri zangu haraka kwa sababu maelezo yake yalikuwa yapo tofauti na wanadamu wengine. Nayeye aliniweka wazi kwamba yupo pale kibiashara aliagizwa na baba yake Aron Mavunde,alikuwa na mkutano na tajiri mmoja kwenye lile jiji ameshamaliza na kesho yake alikuwa anatarajia kurudi nchini Tanzania.

Basi kuanzia siku ile tulikuwa watu wa karibu sana kiasi kwamba tulianza kutembeleana kuna muda alikuwa anakuja Japan na nilifanikiwa kumuunganisha na matajiri wengi sana ndani ya Osaka kwa sababu alikuwa anapenda sana biashara lakini hata yeye pia aliweza kuniheshimisha kwenye familia yao, ilikuwa ni kama familia yangu pia na babu yako mzee Mavunde, alikuwa ananiita mimi ni pacha wa baba yako. Nilikuwa mpweke sana lakini nilivyo ipata familia ile maisha yangu yalikuja kuwa ya furaha kubwa sana.

Unaweza ukajiuliza kwamba ni kwanini nilikuwa karibu na familia yako alafu wewe haukuwahi hata kunifahamu. Baada ya kuimarisha urafiki mkubwa baina yangu na baba yako, nilikuja baadae kuhisi kwamba kuna watu wananifuatilia kwa sababu nilikuwa jasusi, baadae nilifikiria sana ninaweza kuiingiza familia ile matatizoni, niliamua kuanza kuishi kwa siri sana na sikuhitaji kuwa karibu sana na familia ile, nilimuita baba yako kwa siri nikamweleza kila kitu na akanielewa. Tangu hapo nilikuwa nakuja Tanzania kwa siri sana na mara nyingi nilikuwa nikitumia sura bandia kila napokuja, pale kwenu nilikuwa ninakuja kama mfanyabiashara na usingeweza kunijua kwani nilikuwa kila nikija nadadilisha sura ila wewe nakujua tangu mama yako ana mimba yako na mpaka siku unazaliwa nilikuwa kwenu.

Nimekuwa nikiishi hivyo kwa siri sana kwani nchi nyingi sana zinanihitaji ili zinitumie kwa mambo yao kwa sababu ya uwezo nilio nao, bahati mbaya sana kwao siwezi kuruhusu hicho kitu kitokee kamwe ni bora nife, hata siku baba yako anauawa ilitakiwa nije nikuchukue haraka sana lakini nilichelewa kupata taarifa mapema na ndiyo sababu hukuona msaada wowote wa haraka, hata hivyo baba yako alitumia akili kubwa sana kukuelekeza kwangu kabla hajafa sababu kubwa alijua hakuna mwanadamu aliye hai ambaye anaweza kukugusa hata kucha yako tu unapokuwa kwenye mikono yangu, hii nyumba yangu ni miongoni mwa sehemu chache sana duniani zenye ulinzi mkubwa sana , siku nimemtuma Akio akufuate Tanzania kabla hajafika airport ndio muda ulio nipigia simu ikawa rahisi sana kukupata, ukiachana na hilo nilifurahi kwa ujasiri wako wa kuweza kufika mpaka japani pekeako bila msaada wowote.

Kule Tanzania kuna binti yangu ambae naye sitaki atambulike kabisa ndio maana huwa tunaonana mara chache sana, binti huyu ni mtaalamu sana wa mambo ya mitandao, nilimpeleka Tanzania kwa sababu najua kule ni salama kwake kwahiyo nikaamua awe anasoma chuo kule, alikuwa anasoma chuo kama tu sehemu ya kutoa upweke kwa sababu alichokuwa anakisoma tayari alikuwa anakijua sana miaka mingi hivyo niliamua kumuachisha kabisa masomo. Jina lake anaitwa Yevada, hili ni jina ambalo nilihitaji awe analitumia kwa sababu za kiusalama ila pia ana jina lake la shule hilo sitakutajia ila kama ukibahatika kukutana nae atakueleza mwenyewe, ni binti mzuri sana na kama utafanikiwa kuwa nae karibu basi jukumu la kumlinda ni juu yako na uhakikishe hakutwi na tatizo lolote lile, code zake za kumpata ni T9M79, akikuuliza nani mjibu M45Haru atajua umeagizwa namimi, kwenye suala la kuonana mtajuana wenyewe ila hakikisha anakuwa salama huyo binti.

Nini kimejificha nyuma ya hili? iweje mzee huyu Haru adai kwamba ana mtoto wa kike ambae yupo Tanzania ingali sisi tunajua kwamba alikuwa na mtoto mmoja wa kiume ambae alifariki? Je Calvin atafanikiwa kumpata Yevada?.. .......

Kwa Leo natundika Daruga katika ukurasa wa 14 sina la ziada tena tukutane wakati ujao kwenye kalamu ya professor.

Chao [emoji996]

Bux the story teller

#ULIMWENGUWAWATUWABAYA
 
Mmmj hadth naona inatoka mara moja Kwa mwezi
 
No, JM nilikuwa nimeitoa kwenye cm hivyo nikabase sana WhatsApp, then hii hadithi ilisha isha so nikawa sina application hii
Pole Sana, Kwahiyo unatuahidi Nini wapenzi wasomaji baada ya kurejea tena hewani
 
Imefika patamu sana, shukrani mkuu endelea kubaki kwenye kutimiza ahadi Yako hivi si ulisema kimoja Kwa siku eee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…