Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Haujafanikiwa kumshawishi naona kimya leohahahaa ngoja nimfate pm
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]kanitosaHaujafanikiwa kumshawishi naona kimya leo
🤭🤭🤭🤭haujatumia ushawishi mzuri[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]kanitosa
0621567672 nicheki kwa hiyo namba WhatsAppShukrani mkuu,naipataje yote na garama zake
Thanks so much brother for this love and big support, God bless you[emoji120]one of the sweet and thrilling story.unajiona ndani kabisa ya hii story.mimi nimemfata whatsapp kwa bei nzuri na rafiki nimeisoma yooote.hii story ipo mpaka ep 76 kwa humu inaweza malizika december.follow the guy, apreciate what he is doing(donate) and enjoy the story
Nooooma.aiseHADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
MTUNZI : Bux the story teller
WHATSAPP : 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 23
SEHEMU ILIYOPITA TULIPO ISHIA.............
“umejitahidi sana lakini sidhani kama una uwezo wa kupigana namimi, miaka kumi niliyo itumia ndani ya misitu ya kutisha sana ya Kongo ilinitosha kuwa mtu mwenye nguvu sana” yalikuwa maneno ya Brown huku akimfuata Victor pale alipokuwa amesimama. Victor aliona kama ni jeuri akajikusanya nguvu na kwenda kwa kasi ili kumvaa Brown lakini alirudishwa na mateke matatu mfululizo ya hatari sana kifuani yaliyo mpelekea kutoa damu ya kutosha mdomoni kwake akiwa hoi sana. Wakati mwanaume huyo mwenye mbavu za kutosha akiwa anaelekea alipo victor, Brown alishangaa wale wenzake wawili wanadondoka chini huku wakiwa wameshika shingo zao....................
ENDELEA................................
alishangaa ni nini kimetokea ikambidi aende kwa sasi kuwaangalia, alimshangaza kuona star ndizo zilizo ondoa uhai wa watu hao, akili ikaenda kasi kuwaza siku kadhaa za nyuma aina hiyo ya star ilimbaraza kwenye bega lake wakati anataka kumuua Veronica akagundua atakuwa ni huyo mtu yupo hayo maeneo. Ikambidi ageuke haraka sana wakati anageuka nyuma alishtuka anamkuta mtu amesimama kwa mbali kidogo, mara ya kwanza alijua ni Victor atakuwa kanyanyuka lakini alivyo angalia pembeni alimwona Victor akiwa amelala pale chini anagugumia kwa maumivu makali.
“nadhani ndiyo wewe nilikukosa siku ile maeneo ya kimara kule” Brown aliongea kwa kujiamini sana
“ahaaa kumbe ndo wewe kijana, nilikuwa natamani sana nikuone ulivyo kidogo unajitahidi kwenye urushaji wa risasi japo bado mikono yako ni mizito sana kiasi kwamba huwezi kumpiga mtu kama mimi na hizo risasi zako” Calvin alijibu kistaarabu kama kawaida yake bila papara yoyote.
“ni binadamu wachache sana huwa wanaishi pale ninapo amua kuinyanyua mikono yangu kuirusha risasi yangu una bahati tu ilikuwa usiku” alijibu Brown kwa majigambo
“ok nataka nijionee hilo leo hapa, usinipotezee muda sana hapa kakutuma nani na ulikuwa unataka nini kwa huyu bwana mdogo?, maana umempiga mwenzako vibaya mpaka unataka kumuua aisee” Calvin alikuwa akiongea huku anasogea. Lakini wakati anakaribia Brown alitoa bastola yake na kuachia risasi kwa haraka sana, lilikuwa jambo la haraka ambalo lilimshitua hadi yeye kwani Calvin alijirusha kwa sarakasi tatu akiwa juu na kuenda kutua pembeni.
“nimekwambia una mkono mzito sana kumpiga risasi mtu kama mimi ambaye ninaweza kusikia hata mtu akiwa anatembea kwa kunyata kwa zaidi ya mita miamoja, iangalie bastola yako hiyo” aliongea Calvin huku akitabasamu na wakati huo Brown alishtuka kuona bastola yake imekatwa na kitu kama panga, alivyo iangalia vizuri aligundua wakati mtu yule anaruka sarakasi Calvin alirusha star yake ambayo ndiyo imeikata bastola hiyo, aligundua huyo ni mtu mwenye uwezo mkubwa mno kiasi kwamba kitu kikitoka mkononi mwake kinatoka kwa kasi na nguvu kubwa sana kwa sababu kama angehitaji kumuua angemmaliza kwa star hiyo.
Brown akaamua kuitupa hiyo bastola kwa sababu ilikuwa haina kazi tena akaamua kuzipanga ngumi zake vyema sana, alikuja kwa kasi na kujiviringisha kama nyoka staili ambayo hata kwa Calvin ilikuwa ngeni, Calvin alipokea mateke mawili mazito sana yaliyo mpeleka mbali bahati nzuri kabla hajatua chini akashika mkono mmoja chini na kujibetua tena akasimama vizuri.
“mhhhhh unaonekana una uwezo mkubwa sana kama ukikubaliana namimi naweza nikakuacha hai ukanisaidia kwenye kazi zangu” Calvin aliongea akiwa bado kasimama pale pale, lakini wakati huo hakuna mtu ambaye aliweza kumsikiliza kwa lolote, Brown damu ilikuwa tayari inamchemka sana na alijiona mshindi akaja tena na kushambulia kwa nguvu kitu kilicho anza kumwelemea Calvin kwa sababu alikuwa anafanya kazi ya kupangua tu, alipokea teke kali la shingo lililo mfanya akajisikilizia kama sekunde thelethini hivi.
“khaaaa ndugu yangu mbona uko siriasi sana kiasi hiki mpaka unataka unitoe roho aisee, ebu tuongee kistaarabu kwanza, kakutuma nani kwa sababu huwa naogopa sana kuitoa roho ya mtu bila hatia yoyote, niambie ukweli nikuache uende zako” Calvin wakati huo alikuwa amesogea sana mahali alipokuwa Brown na kumwambia hayo maneno kwa mara nyingine tena akiendelea kuinyoosha shingo yake vyema kabisa, huku Victor akiwa kama mpenzi mtazamaji tu kwani alikuwa amepigwa vibaya sana na kwa wakati huo hakuwa hata na uwezo wa kusimama.
“kanituma mama yako mshenzi wewe” ni miongoni mwa makosa makubwa sana ambayo aliyafanya Brown Kasongo, ilimfanya Calvin akakumbuka siku ile miili ya wazazi wake ikiwa pale sakafuni aliumia sana kwa sababu ni moja ya matukio ambayo huwa hapendi kabisa kuyakumbuka alafu leo mtu kirahisi tu analitaja jina la mama yake hakika hakuwa na bahati binadamu huyu
“sawa nilitamani sana nikuache hai lakini kwa jeuri ya mdomo wako ngoja nikuonyeshe mama yangu alipo” Calvin wakati huo aliongea sura yake na macho yalibadilika mno, hakumsubiri Brown amfuate alikuja kama mzimu na kurusha ngumi zaidi ya 10 zilizo mpata vyema Brown kifuani kisha alirusha teke aina ya double kick lililo mpelekea Brown kujipigiza vibaya sana chini, lakini alijikongoja na kusimama, hakupewa hata nafasi ya kunywa maji mwanaume alikuwa amefika, Brown alijitahidi sana kurusha ngumi moja ya nguvu sana lakini Calvin aliiona vyema, nae hakukwepesha alirusha ngumi moja ambalo ndilo pigo lake la hatari mno ikitokea akakupiga , zilikutana ngumi kwa ngumi kisha Calvin akarudi nyuma hatua moja, hazikuisha hata sekunde kumi ilisikika sauti kali sana ya kilio kutoka kwa Brown, maskini mkono wake ulikuwa umevunjwa vibaya sana na mifupa ilikuwa imetokezea nje mpaka inaonekana.
Calvin alimsogelea kwa hasira alizunguka na kumshindilia teke moja maeneo yak kiuno, ilisikika tu sauti ya kh.kh,kh.kh,kh kumaanisha kwamba hicho kiuno kilikuwa hakina kazi tena kimeshavunjwa vibaya, hii ilimpelekea mpaka Victor kuogopa sana pale alipokuwa amekaa chini wakati huo nguvu zilikuwa zishaanza kumrudi kwani alipata muda wa kutosha wa kupumzika. Brown alipiga kelele za maumivu makali sana akiomba msaada.
“nilikuuliza kistaarabu sana lakini jeuri yako imekuponza, kwa sasa sina haja na msaada wako tena, najua walio kutuma ndio hawa ambao nawatafuta, nakuhakikishia mtakufa mmoja mmoja, baada ya wewe anayefuata ni Samson Nelson pacha wa huyo mtu wangu ninaye mtafuta usiku na mchana alafu nitamalizana na huyo bosi wenu anaye wapa kiburi, ole wake siku nimjue ni nani, atakufa kifo kibaya sana” calvin aliongea na kumshangaza Brown kwani hakujua mtu huyo kajua vipi kihusu Samson ambaye anapatikana maeneo ya mbinga karibu na Songea kwa sababu mtu huyo alikuwa akiishi kwa siri mno na tangu arudishwe Tanzania ni watu wachache sana ambao walikuwa wanalijua hilo, wengi walikuwa wanajua bado yupo nje ya nchi. Bahati mbaya sana kwa Brown hali yake ilikuwa mbaya sana kutokana na kuvunjwa kiuno huku akiwa anaendelea kutoa damu nyingi sana puani na mdomoni. Kilicho fuata ni alama ya upanga kwenye shingo ya Brown, dakika moja mbele Calvin alikuwa ameshika upanga ukiwa na damu nyingi sana kumaanisha ndio ulio tumika kuyaondoa maisha ya Brown, wakati huo Victor alikuwa bado amefumba macho kwani mauaji hayo aliyo yashuhudia mtu akichinjwa yalikuwa yanaogopesha mno japokuwa alikuwa jasusi ambaye kaua watu wengi lakini hali hiyo haikuwa ya kawaida hata kidogo.
“nifate” calvin alimwambia Victor wakati huo alikuwa ameshaukunja upanga wake vyema, wakafika mpaka nyuma ya nyumba hiyo kwenye bustani nzuri ya maua.
“umejuaje kama huku nyuma kuna eneo la kukaa?” Victor aliuliza kwa mshangao mkubwa
“nimefika hapa dakika kumi na tano kabla ya wale watu kwahiyo nimezunguka na kungalia kwanza usalama wa hapa kwani nilikuwa nina mazungumzo nawewe, ila inasikitisha mtu mkubwa na komando mkubwa kama wewe unaishi bila ulinzi namna hii, ni hatari mno kwa maisha yako mtu mhimu sana kwenye taifa kama wewe” Calvin alielezea kwa ufupi
“huwa sipendi nijulikane, kuna wakati mkuu wangu alitaka kunipa wanajeshi wa kunilinda niligoma kabisa kwa sababu niliona najiweza kwa kila kitu lakini sikuwa sahihi hata kidogo sikuwahi kuwaza kwamba anaweza kutokea mtu mwenye uwezo wa kunizidi mimi mpaka siku ile nilipokutana nawewe baada ya kukutana kwa yule bwana mdogo niliye kuwa namfuatilia, na nashukuru sana kwa msaada wako wa leo maana kwa ngumi za yule jamaa ningekufa leo” victor alikuwa anampa sifa zake Calvin huku akiwa anacheka baada ya kugundua mwanaume huyu hakuwa na matatizo naye kabisa.
“usijali kusaidia ni jukumu langu lakini unaweza kuniambia siku ile kwa yule bwana mdogo Tomaso ulikuwa unataka nini?” Calvin alihitaji maelezo kwanini Tomaso alikuwa anafuatiliwa na watu kama hawa ambao ni majasusi kutoka ngazi za juu sana za serikali.
“siku ile wakati umefanya mauaji kwa wale watu pale kimara, niliitwa na mkuu wangu wa idara ambaye kwangu ni kama baba pia, aliniomba ile kesi niisimamie mwenyewe kwani kwa watu wengine ilionekana kuwa nzito, basi ndipo nilipoamua kuja mahali pale lakini kwa siku ile tulifanikiwa tu kujua kwamba kulikuwa na wauaji wawili kwani mzee Ndipo Mwalemi yeye aliuawa kwa risasi. Baada ya kutoka pale baadae yake rafiki yangu mmoja ambaye nae yupo kwenye idara ya kijasusi ndani ya usalama wa taifa alinipigia simu na kuniambia kwamba polisi walimkuta na simu yule mzee ambapo walikuta amewasiliana na watu wawili pekee na ndizo namba zilizokuwa zipo kwenye hiyo simu, yakwanza haikujulikana lakini ya pili ilikuwa na jina la Tomaso, mtu huyu anaonekana ni mtaalamu sana wa mambo ya mitandao kwani location yake ilikuwa inabadilika kila sekunde kumi na kuonyesha nchi mia mbili duniani, ila kuna (kosa) mistake moja aliifanya wakati anawasiliana na mzee huyo kwa mara ya kwanza kabisa tuligundua alikuwa Goba ndipo nikaamua kwenda hapo ili nijue kama naweza kumpata. Lengo kubwa tulitaka kujua kama anajua chochote kutokana na kifo cha yule mzee, nadhani kabla hata sijakutana nae ulikuja pale ukaharibu kila kitu” Victor alielezea kwa urefu kidogo
“yule bwana mdogo nipo nae kwa sasa kwa sababu za usalama wake na kuna watu pia wanamtafuta mbali nanyinyi na hawa watu mimi nina shida nao kubwa sana, ni kweli wale watu mimi ndiye niliye waua na najua hilo mnalijua kwani siku ile nilisahau kuharibu mifumo ya cctv Camera alafu wewe mwenyewe siku ile nakuzimisha uliiona sura yangu kwa usahihi kabisa kitu ambacho ilikuwa ni rahisi kunifahamu hata kwa kutumia Sanaa ya uchoraji, ni kosa kubwa sana nililifanya”Calvin aliongea kwa kifupi
“yes, ni kweli sura yako imepatikana na idara yetu saivi wewe ndiye mtu inaye mtolea macho sana usiku na mchana uweze kupatikana kwa sababu hatuwezi kukuruhusu uendelee kumwaga damu na sisi tukakuangalia tu ni jambo la hatari sana kwa usalama wa taifa” Calvin aliinama baada ya kupewa maelekezo hayo na Victor kisha akamsimulia Victor stori nzima kilicho tokea mpaka sababu ya kwanini anafanya hayo yote kisha akamuuliza Victor “vipi kama wewe ungekuwa ndio mimi hawa watu ungewaacha?”
“kwanza pole sana na ni ngumu sana kuvumilia lakini nadhani ungeiachia sheria ifanye kazi yake na sio kuendelea na hayo mauaji ambayo yatazua taharuki” Victor alisisitiza tena.
“nadhani huwezi kuelewa chochote kuhusu maumivu nayo pitia kwa wakati huu, kingine upo kwenye sheria lakini huelewi chochote ni jinsi gani sheria inavyo endeshwa, hata hivi sikuja kwako kukuomba ushauri, kwa sasa labda nikuthibitishie tu kwamba hakuna roho ya mtu itaishi kama tu ilihusika kwa namna yoyote ile ya kuniondolea wazazi wangu duniani, na kama mnaweza kunizuia sawa kazi kwenu lakini kuweni makini sana kwa sababu sitaki kuua watu ambao hamhusiki kwa lolote ila mkinilazimisha nitakuwa sina namna tena”
“sawa nimekuelewa vizuri sana, lakini vipi kuhusu yule mzee mmiliki wa Decco Logistic imekuwaje upo hai na alitangaza kwamba umekufa?”
“mhhhhhhh ni kama baba yangu mdogo lakini nina wasi wasi nae sana mzee yule kwa sababu hata jana nimempigia simu kwa mara ya kwanza baada ya miaka miwili ameonekana kushtuka na kuogopa sana kitu kinacho nifanya nimtilie mashaka mno lakini bado sijui chochote kwahyo nitajua tu kama kuna kitu sio muda mrefu” Calvin alielezea kuhusu baba yake mdogo huyo
“yaah, jana hata sisi tulienda pale atuonyeshe mwili wako ulipo kwa sababu ilitushangaza mtu uliyetangazwa umekufa unaonekana kwenye video ukiwa unafanya mauaji mimi mwenyewe siku ile nimethibitisha kwa kukuona kwa macho yangu lilikuwa ni jambo la kusikitisha sana, lakini nilivyo muuliza kuhusu hilo alionekana kama mtu aliye changanyikiwa sana akadai hayuko sawa atatupigia akiwa sawa”
“binadamu hatupaswi kuaminiana sana kupita kiasi, kesho mwambie bosi wako nataka kukutana nae kwenye daraja ya Tanzanite majira ya saa saba kasoro dakika tano za usiku, mwambie asije kwa shali nahitaji kuzungumza naye mambo ya muhimu sana kwa amani tu, zingatia sana nilicho kwambia. Na hii ni namba yangu ya simu huwa inapatikana kila dakika tano za mwisho kwa kila saa nje na hapo huwezi kunipata, kama kukiwa na shida nipigie simu kwa hiyo namba” aliongea Calvin huku akimpatia namba Victor ambayo ilikuwa ni code maalumu, hakusubiri jibu akaamua kutoweka mahali hapo na kumuacha Victor kwenye mshangao mkubwa sana. Baada ya muda Victor alipiga simu polisi walikuja na kutoa miili ya watu walio kuwa wameuawa mahali hapo na kuondoka nao kwa ajili ya kufanya uchunguzi.
“alfajiri sana ndani ya casino kubwa la Seven World ambalo linamilikiwa na mzee Kasisi Chacha mkurugenzi wa TISS (Tanzania Intelligence Security Service) wanaonekana wanaume watatu wakiwa wameizunguka meza moja na Victor ndiye aliye weza kuwakutanisha watu hao wawili pamoja na yeye mwenyewe.
“leo usiku nimekutana na mtuhumiwa wetu namba moja” Victor aliongea kirahisi sana kitu kilicho pelekea Alex pamoja na Mkuu huyu wa idara ya usalama wa taifa wabaki wanamshangaa tu kwani walidhani labda amechanganyikiwa.
“vipi umekesha club?” lilikuwa swali kutoka kwa Alex akimhoji rafiki yake huyo kwa mshangao
“nimewaita hapa sio kutaniana huyo mtu nimekutana naye tena amekuja kwangu, hiyo inamaanisha alinifuatilia kwa muda mrefu mpaka ameweza kujua hata nyumbani kwangu” Victor alimjibu rafiki yake
“alikuwa anahitaji nini na kwako alikuwa amefuata nini?” ni sauti nzito kutoka kwa mzee Kasisi Chacha iliingilia maongezi
“amedai kwamba alikuwa amepotea kwa miaka miwili na sasa amerudi kuwatafuta wabaya wake wote ambao walikuwa wamehusika kwenye mauaji ya wazazi wake, nimejaribu kumuonya kwamba asithubutu kufanya hiki kitu ni hatari sana kwani hatutamvumilia kumuona anaendelea lazima atakumbana na mikono yetu, yeye amesema hana shida kabisa nasisi na hawezi kukifanya hicho tunacho kitaka sisi na amenitahadhalisha tu kwamba iwapo tutazidi kumuwekea vikwazo katika hili atakuwa hana namna itamlazimu kuanza kudili nasisi pia. Kuhusu yeye kuja kwangu alihitaji kujua kwamba siku ile pale kwa yule Tomaso nilikuwa nimefuata nini, kaniambia pia tusihangaike kumtafuta yule bwana mdogo kwa sasa yupo naye kamhifadhi kwa ajili ya usalama wake kwani inaonekana kuna watu wanamtafuta ili waweze kumuua. Hata hivi ujio wake umenisaidia sana kwa sababu nilivamiwa na watu ambao wanaonekana ni wataalamu mno kwenye masuala ya mapigano, angechelewa dakika hata tatu tu nilikuwa nakufa, kuwahi kwake kumenifanya niendelee kuifaidi hii hewa ya bure kabisa duniani hapa. Chamwisho anahitaji kuonana nawewe mkuu siku ya leo majira ya saa saba kasoro dakika tano za usiku pale kwenye daraja la Tanzanite na kasisitiza kwamba ana mazungumzo ya amani nawewe kwahiyo usiende pale kwa nia mbaya ana jambo la mhimu sana la kuongea nawewe na uende pekeako.” Victor alikuwa mehitimisha maelezo yake.
Unahisi Victor anahitaji nini kwa mzee huyu ambaye ni mkuu wa idara ya taifa nchini? Ukurasa wa 23 unafika mwisho tukutane wakati ujao.
Chao [emoji996]
Bux the story teller
#ULIMWENGUWAWATUWABAYAView attachment 2318761
Hahahahha haya mimi niko wapi calvin jackson aronMimi ndio CALVIN sasa naisoma vzuri historia yangu..nikiwa hapa kwenye mjengo wangu mpya kigamboni.
[emoji28][emoji28] hongera sana tajiriMimi ndio CALVIN sasa naisoma vzuri historia yangu..nikiwa hapa kwenye mjengo wangu mpya kigamboni.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Hahahahha haya mimi niko wapi calvin jackson aron