Hadithi: Ulimwengu wa Watu Wabaya

Hadithi: Ulimwengu wa Watu Wabaya

HADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
MTUNZI : Bux the story teller
WHATSAPP : 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 31
SEHEMU ILIYOPITA TULIPO ISHIA.............

“nakuja mzee tutaongea vizuri siku tukikutana”, baada ya kushuhudia mauaji ya kaka yake kipenzi na wa pekee Samson alipata ukichaa pale pale, ni baada ya kuona unyama wa kutisha mno kwa mtu ambaye ndiye pekee aliyekuwa kama familia kwake, hakika alikuwa amelipwa ubaya wao waliokuwa wanaufanya kwa miaka mingi sana. Calvin aliunguruma kwa sauti kubwa sana na kupiga kelele kwa uchungu mno kama simba mwenye njaa kali sana, aliichukua simu yake mfukono na kumpigia mkuu wa idara ya usalama wa taifa.

ENDELEA.......................

“shikamoo mzee” Calvin alisalimia lakini akiwa bado sura yake ameikunja sana

“mhhhhhh kijana bado upo? Na namba yangu umeipatia wapi?” aliuliza mzee Kasisi Chacha kwa mshangao baada ya kuigundua sauti hiyo kwani hakudhania kama mtu huyo anaweza kumtafuta kwa njia ya simu

“hii dunia ni ndogo sana mzee wangu, tuachane na hilo ni kwanini umeamua kwenda kinyume na makubaliano yetu mzee? Huoni kama unaenda kusababisha madhara ambayo hayakuwa na msingi wowote ndani ya nchi hii”

“siwezi kukuacha raia wa kawaida sana kama wewe ujichukulie maamuzi unayo jisikia mwenyewe na sisi watu wa usalama tupo lazima ukamatwe na ukafungwe sehemu ambayo hautaweza kutoka tena kwenye maisha yako” alijibu mzee huyo

“sawa, kwa sababu umehitaji mwenyewe sitakuwa na lawama juu ya hili na haya maamuzi yako ya kipuuzi utayajutia sana baadae, waagize watu wako waje hapa Jangwani kuna miili ya watu njooni muichukue alafu mtamkuta kijana mmoja ambaye akili zimemruka kwa muda(Samson) mtibuni atawasaidia sana, nikimaliza mambo yangu nitakutafuta ili mimi nawewe tumalizane” mwanaume alikata simu huku akiongea kwa msisitizo

“hello, hello” alikuwa anaongea peke yake mzee huyu lakini simu ilikuwa imeshakatwa.

Upande wa pili mr Fabian Decco alikuwa amechanganyikiwa kwa kile alichokuwa amekiona kilimtisha mno, ilimpelekea kunyanyua simu yake na kupiga simu mahali

“nahitaji watu kumi walio bobea mno kwenye mapigano” aliongea mzee huyu akiwa anatokwa na jasho jingi sana wakati huo alikuwa ofisini kwake na kulikuwa na kiyoyozi kikali

“nimekupa vijana wengi sana kuna nini mpaka uhitaji vijana wengine mapema hivi?” sauti moja nzito sana yenye mikwaruzo ndiyo ilikuwa inasikika upande wa pili mwa simu hiyo

“mkuu ni suala la ghafla sana vijana wengi wameuawa na nimebakiwa na vijana wa uhakika watano tu nahitaji msaada wako haraka sana kabla mambo hayajaharibika” Mr Decco alionekana anaomba msaada kwenye simu yake hii inaonyesha kwamba mtu huyo alikuwa ni mtu mkubwa mno kwa sababu alikuwa anaongea nae kwa ustaarabu na unyenyekevu mkubwa ambao asingeweza kuuonyesha kwa mtu wa kawaida hata kidogo.

“ni kwa ajili ya huyo mtoto au kuna lingine?” Sauti ya upande wa pili iliuliza

“ndio, ila ni tofauti na tulivyokuwa tumemfikiria amekuwa binadamu wa kutisha sana, hata mali nadhani inabidi itumike njia nyingine kuzipata ila chaguo zuri ni kumuua alafu mali tunachukua kwa jina langu kwani akiendelea kubaki hai atatumaliza wote hizo nyaraka zenyewe hazitakuwa na umuhimu wowote” alijibu kwa uoga mkubwa sana

“usijali ni mtoto mdogo sana huyo na hii nchi nina mamlaka nayo makubwa sana hawezi kwenda popote, kesho jioni nakuagizia vijana wangu kumi ambao wapo kwenye kambi yangu ndogo ndani ya msitu wa kongo, ni makomando hao kwahiyo jiandae watafika jioni, sitaki unisumbue tena kuhusu suala la huyo mtoto mdogo, nazihitaji mno hizo mali nina kazi nazo kubwa mno ndani ya miaka mitatu ijayo, kama inahitajika ni kumuua ndipo zipatikane basi hakikisheni hazipiti siku tatu mnipe ripoti yake saivi nitakuwa busy na mambo ya muhimu sitaki usumbufu”. Aliongea mtu huyo kutoka kwenye hiyo simu na kuikata, alionekana kuwa na sauti na mamlaka makubwa sana kwa mr Decco.

NIFOLLOW Instagram @iamfebian Twitter #buxmsafi Tick-tock @buxmsafi LinkedIn FEBIANI BABUYA Facebook Bux the story teller WhatsApp 0621567672

Asubuhi na mapema sana ndani ya Kigamboni Thomas wakati anatoka chumbani kwenda mazoezini alishangaa nje kuna gari ambayo hakuwahi kuiona kabla ndani hapo aina ya V8 nyeusi, hakuelewa gari hiyo imefika hapo majira ya sangapi ikambidi kwenda kumuamsha Tomaso na Veronica ili kuwauliza kama kulikuwa na mtu mwenye taarifa na ujio wa gari hilo lakini wote walionekana kupigwa na butwaa mno basi ikawabidi wapandishe mpaka gorofa ya juu ambako ndiko kuna chumba cha Calvin, Veronica aligonga mlango huo ili kuona kama kuna mtu ndani yake, alitoka mwanaume akiwa kifua wazi kitu kilicho anza kumpa wakati mgumu sana Veronica na kumfanya aone aibu lakini alienda kumkumbatia hivyo hivyo.

“umerudi sangapi mbona tumechelewa sana kulala na hakukuwa dalili yoyote ya mtu kurudi na lile gari nje umekuja na mgeni gani?” Tomaso aliuliza kwani alishindwa kabisa kumuelewa mtu huyo

“nina gari nyingi sana ile ni mojawapo, kuhusu kurudi nimefika usiku wa manane sana sikutaka kuwasumbua, mnaweza kujiuliza nimeingiaje, hapa ni kwangu sina muda mrefu sana ila napajua kiundani kuliko mtu yeyote yule” alijibu Calvin akiwa na tabasamu tele kitu kilicho mfanya kuongezeka kuwa na mvuto mkubwa kupita kiasi. Aliwaelekeza kwamba awakute sebuleni wote watatu alikuwa na maongezi nao

“nahitaji muondoke hapa nchini wote watatu kisha mambo yakikaa sawa nitawafuata huko mnako enda” aliongea kiufupi

“tuondoke? Kivipi na kwanini? Yani hujatupa hata mrejesho kuhusu safari yako unatutaka tuondoke nchini tena shida nini?” Veronica aliuliza maswali mengi sana kwani alikereka sana na suala hilo kwa sababu alikuwa ashampenda sana mwanaume huyo suala la kumwambia aende nje ya nchi kwake lilikuwa gumu sana kukaa naye mbali.

“najua ni ghafla sana na huenda hamkujiandaa kwa hili, safari yangu imeenda vizuri sana ndio maana nimerudi tena nikiwa salama kabisa (mwanaume hakutaka kuelezea majeraha yake aliyo nayo japo bado mkononi alikuwa na plasta sehemu aliyopigwa risasi pamoja na kwenye paja sehemu aliyo zamishiwa kisu, alikuwa anajikaza kiasi kwamba hakuna aliyekuwa ametambua kwamba mwanaume huyo alikuwa na majeraha), siku chache zijazo kuna mambo yanaenda kutokea hapa nchini, na kwa nyie watu mnao nizunguka amani yenu inaweza kuwa shida sana na itanipa wakati mgumu kuwalinda kwani nina majukumu mazito sana mbele yangu. Wote watatu mlikuwa kwenye mikono ya wale watu wakihitaji kuwatumia, kupotea kwenu ghafla lazima kumewashtua sana kwahiyo watakuwa wanawatafuta usiku na mchana ili wawapate na siwezi kuruhusu hilo litokee nikiwa hai. Nilishawakatia tiketi za kwenda nchini Ufaransa katika jiji la Paris nina nyumba nimeinunua kule, mkifika airport kuna mtu atawapeleka mpaka mahali hapo” alihitimisha maelezo yake lakini alikuwa kama hajaeleweka japo walilazimika kumuelewa, ilikuwa ni ngumu mno kwa Veronica kuweza kuikubali hali hiyo mahali hapo lakini ilimbidi kwani uwepo wake ingempa wakati mgumu sana Calvin. Majira ya saa 10.30 za jioni walikuwa wapo kwenye ndege tayari watu hawa watatu ambapo ingewachukua masaa 9 na dakika zake 22 kuweza kufika kwenye jiji bora zaidi kwa raha na starehe duniani PARIS nchini Ufaransa.

Madam Luciana Mwaifupa alionekana akiwa ndani ya uwanja pembeni kidogo ya kambi yao ya siri akiwa anafanya mazoezi ya hatari akiwa mwingi wa hasira machoni pake, wakati huo Elia Mushi alikuwa amejibanza sehemu akimtazama mwanamke huyo mrembo sana lakini alikuwa anafanya vitu vya hatari kupita kiasi, akiwa hapo alimkumbuka sana moja ya wanawake ambao aliwahi kumpenda kupitiliza lakini mwanamke huyo alimkimbia kwa sababu hakuwa na pesa, ni stori iliyo muumiza kiasi chake, aliguswa bega na Felix Mgeni ambaye ndiye mtu pekee aliyekuwa anayatambua maumivu aliyo kuwa anayapitia mtu huyo

“ndugu yangu mapenzi ni fumbo zito sana, ni neno lenye herufi chache sana unapolitamka lakini lina maana kubwa sana ukianza kulichambua na bahati mbaya sana wengi huwa linawashinda kwenye matumizi na ndipo hapo maumivu huanza kuzalishwa na watu kuona mapenzi hayafai. Zamani kabla haya makaratasi hayajaanza kupambwa na kupewa jina la pesa haya maumivu ya mapenzi hayakuwa yanawasumbua watu, bibi zetu na babu zetu waliinjoi sana suala la mapenzi na nilitamani sana kama ningekuwa miongoni mwa wanaume ambao walibahatiba kuishi kwenye zama hizo bora sana. kizazi hiki usipokuwa na pesa wanawake wanakuona kama nawewe ni mvaa sketi mwenzao kwahiyo inakulazimu uwe mtu wa kujielezea sana ili uwapate, pesa sio kila kitu kwenye maisha ila ni muhimu sana kwenye maisha ya sasa ili uweze kuyaishi maisha ya ndoto zako hakikisha unayo pesa. Pole sana kaka najua kwa sasa unayo pesa ya kutosha lakini hauna furaha kwa kumkosa mwanamke wa ndoto zako, kwa sasa unaweza kusahihisha makosa kumtafuta mwanamke atakaye kupenda mwenyewe ila tu kuwa makini usije ukaishi na mwanamke ambaye wewe ndo umempenda sana narudia tena hakikisha yeye ndo anakupenda sana ndo unaweza kuishi nae” yalikuwa maneno ya busara sana kutoka kwa Felix Mgeni kwenda kwa rafiki yake Elia Mushi yaliyo onekana kumuweka sawa kwenye hali yake ya kawaida huku wakiendelea kupata kinywaji. Lakini walishtuka kutokumuona madam Luciana pale alipokuwa anafanyia mazoezi, walikimbilia eneo lile lakini hawakuona mtu, Elia aliangalia saa yake ilikuwa ni saa saba kasoro dakika mbili za usiku na alihisi kama nyuma yake kuna mtu amesimama alishtuka

“nani wewe?” Elia aliuliza haraka kwani kulikuwa na kiza mtu huyo alikuwa haonekani vizuri

“kiongozi wenu yuko wapi? nina mazungumzo nae” sauti nzito ya kukoroma iliuliza

“unamtaka madam wa nini? Kama una shida ya muhimu ongea hapa hapa alafu ueleze hapa umefika fika vipi bila taarifa” Elia alimkazia mtu huyo

“nina muda mchache mno wa kukaa hapa, niitie kiongizi wako tupeane maagizo” mwanaume aliendelea kusisitiza akiwa hana hata tone la wasi wasi, Elia alikunja ngumi haraka lakini kabla hajamfuata mtu huyo walisikia sauti ya kike ambayo ilimfanya atulie kwanza

“wewe ndiye Calvin Jackson sio?” Madam Luciana aliuliza akiwa anaruka kutoka juu ya paa la nyumba hiyo

“unaonekana ulikuwa unanisubiri kwa hamu sana?” Calvin aliuliza huku akimgeukia mtoto wa kike huyo mwenye haiba ya uanaume kwa mambo magumu na ya kutisha anayo yafanya

“sana nashukuru umejileta mwenyewe kazi ya kukukamata imekuwa rahisi sana” alijibu kwa ujasiri mkubwa mno madam huyo

“mhhhhhhh kumbuka wewe ni mtoto wa kike ni vyema ukawa na akiba ya maneno” Calvin wakati huo alikuwa anatabasamu, alivutiwa sana namna mwanamke huyo alivyo kuwa jasiri.

******************************
“hahahahhaa mwanamke sio kwahiyo hapa unaona kama nataka kukupa gemu kitandani unanichukulia poa sio?” Luciana aliona kama kadharauliwa sana kuonekana mlaini mbele ya mwanaume huyo ambaye alikuwa ni mzuri kwa sura na ungedhani ni kuku wa kisasa tu ukimuona (laini sana).Alikuwa ameikunja ngumi yake vyema akiwa anasogea bila wasi wasi wowote ule

“nitabadili maamuzi badaya ya kukukamata nikuue mpuuzi wewe kuwa na heshima” Luciana aliongeza kwa hasira bila kusubiri jibu la mara ya kwanza

“mna dakika mbili za kuniua kama mtahitaji hivyo, mkishindwa itabidi mnisikilize vyema, alafu uweke akilini kwamba mimi sipiganagi na watoto wa kike bora hata wanaume pale ndo wanaweza kujaribu” Calvin aliongea mikono yake ikiwa nyuma, mwanamke huyo aliona dharau zimezidi sana alikuja kwa hasira akirusha ngumu kali, ajabu Calvin alibaki vile vile, alimpiga ngumi nne, moja kwenye paji la uso, mbili tumboni na moja ya mbavu, mwanaume aliuma meno kuonyesha kwamba ngumi ya kwenye mbavu ilikuwa imemuingia bara bara. Madam Luciana alisimama kwa muda kumshangaa mtu huyo akiwa bado ameganda pale pale bila hata kutikisika

“narudia tena huwa sipigi wanawake nilikuwa namheshimu sana mama yangu usirudie tena huu upuuzi” Calvin aliongea akiwa ameikaza sauti yake vyema. Madam huyu hakuridhika alijirusha samba soti teke akilielekezea kwenye uso wa Calvin, mwanaume aliona teke hilo lingemletea madhara alilidaka kwa ukakamavu na kumrusha madam huyo mbali kidogo lakini alijigeuza haraka sana kama paka na kusimama wima kuonyesha alikuwa vyema mno mwanamke huyu. Alichomoa visu vyake viwili alivyokuwa anavitumia mara nyingi sana akiwa kwenye kazi zake za mhimu pindi anapo ona mambo yake hayapo vizuri sana na alikuwa akivihifadhi kwenye buti lake kubwa la mguuni wakati huo Felix na Elia walikuwa pembeni wakishuhudia kwani walimjua mwanamke huyo linapokuja suala la mapigano. Alitishia kama anarusha kisu cha mkono wa kulia Calvin alirudi hatua moja lakini mkono wa kushoto mwa mwanamke huyo ulirusha vyema sana kisu kingine kidogo ambacho Calvin alijitahidi sana kukikwepa lakini likimchana kidogo karibu na bega, alichukia sana akaikunja ngumi yake, wakati madamu huyo anakuja kwa kasi alimuacha apite kwa kumkwepa kidogo kisha akaikunjua ngumi yake kwenye bega la mwanamke huyo lililopelekea kupiga kelele ya maumivi makali, kisha likafuatia teke la mbavu na ngumi nzito ya tumbo iliyo mpelekea mwanamke huyo kwenda chini huku akilalamika sana kuhusu tumbo lake.

Kuona hivyo wanaume walikuwa wote wawili Elia na Felix baada ya kuona shughuli ya mtu huyo walirusha ngumi zao zilizo mpata vyema Calvin kwani hakukwepa lakini naye alikuwa amerusha ngumi zake mbili zilizo wapeleka mbali kidogo Felix na Elia waliokuwa wanatoa damu mdomoni kwani walihisi wamepigwa na vyuma vizito sana kwa namna ngumi ya mwanaume huyo ilivyokuwa imekomaa sana, wakati wananyanyuka Madam Luciana alishangaa watu wale wakidondoka chini huku wakishika shingo zao alivyo mwangalia vizuri Calvin aliona mkononi alikuwa na visindano vidogo sana akiwa anavirudisha kwenye mfuko wake, alijua hiyo itakuwa ni dawa ya usingizi lazima kisha mwanaume akamfuata madam Luciana pale chini na kuchuchumaa mahali hapo

“usipende kuanzisha vita ambayo unajua kabisa hauwezi kuishinda, kuna muda amani huwa ni bora zaidi kuliko ushindi. Sio jambo la busara kumuumiza mwanamke mrembo kama wewe hapo ambaye uzuri wako unafichwa na kazi ngumu unazo zifanya za kukesha na kulala muda mchache sana, sisi wote bado tuna safari ndefu sana ya maisha ya baadae sasa fikiria leo nikikufanyia kitu kibaya hata kukupa ukilema mwanamke mrembo kama wewe halafu baadae ukawa mke wangu hao watoto watanichukuliaje wakijua mimi ndiye niliye mpa mama yao ukilema wa maisha?, nadhani unaiona picha kabisa kwamba nitaonekana baba wa hovyo sana kwa familia yangu, jitahidi sana uwe na akiba ya maneno mama yangu usijisahau sana kwamba wewe ni mwanamke na unapaswa kuwa mama bora sana kwa baadae hata kama kwa sasa wewe ni mtu mkubwa sana ndani ya jeshi. ...........ukurasa wa 31 unafika tamati let's meet next time

Chao[emoji2768]

Bux the story teller

#ULIMWENGUWAWATUWABAYAView attachment 2332333
Shukrani mkuu
 
Mkuu Febian Leo tumepiga pass ndefu mpaka saizi, tulaze unono basi
 
HADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
MTUNZI : Bux the story teller
WHATSAPP : 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 33
SEHEMU ILIYOPITA TULIPO ISHIA.............
Saa mbili kasoro za usiku katika maeneo ya Tabata bima nje ya nyumba namba 750 kuna mwanaume anaonekana akiwa amevaa nguo za kininja lakini ajabu uso wake wote na kichwa chake havikufunikwa na chochote, kulikuwa kuko wazi kabisa kumaanisha kwamba mtu huyo sio ninja halisia kabisa, alikuwa amesimama akiukadiria ukuta mrefu wa nyumba hiyo huku mkononi alikuwa na ala ya upanga ambayo ilikuwa imekunjwa vyema kama pambo la kale lenye kuvutia sana.

ENDELEA................................................

Mwanaume huyo aliliweka panga lake mgongoni kwenye kamfuko kembamba ambako kalishonewa kwenye vazi hilo kisha akatoa star zake mbili, alizishika kwa ukakamavu mkubwa sana na kupanda kwa kasi kama vile paka, alikuwa anafanya haraka ili kuendana na kasi ya kamera mojawapo ambayo aliweza kuiona kwenye moja ya pembe za nyumba hiyo. Alitua bila kutoa kishindo kisha alikimbia kwa kasi ya ajabu kuelekea mbele mwa nyumba hiyo kiasi kwamba kama una macho mabovu ungehisi ni kivuli tu kimekatiza mahala hapo.

Nje kabisa ya nyumba hiyo walikuwa wamekaa makomando wawili mmoja akiwa anafanya mazoezi ya kupiga matofali ya simenti na kuyapasua huku mwenzake akiwa busy kuvuta sigara ambayo ilimfanya ajihisi yuko na hali ya ubora kupitiliza, komando huyo aliitupa sigara hiyo mbali kabisa kwenye kiza kiasi chake lakini haukupita muda aliona kuna kitu kimemlenga maeneo ya jichoni alikwepa kwa nguvu kikambaraza kwenye kope zake akakidaka haraka alishangaa ni kile kipisi kidogo cha sigara alichokuwa amekirusha sio muda mrefu, alihisi kuna mtu maeneo hayo huku mwenzake akiwa haelewi chochote anaendelea na mazoezi yake, haraka aliyainua macho yake juu ya ukuta karibu na geti la kuingilia akamwona mwanaume mwenye mwili wa kawaida ila umejengwa vizuri kwa mazoezi akiwa amejikumbata mikono kifuani huku amevaa nguo za kininja ajabu uso wake ulikuwa wazi kabisa. Mwanaume alijigeuza kwa sarakasi mbili na kutua chini bila kutoa aina yoyote ile ya kishindo, yule komando aliguna alijua vyema aina ya watu wa namna hiyo ambao wanaweza kuingia sehemu wakafanya wanacho kitaka bila kutoa aina yoyote ile ya kishindo huwa ni hatari kupitiliza na ni wepesi mno, mwenzake alishangaa kumuona jamaa yake kataharuki wakati anageuza macho Calvin alikuwa amewasogelea huku akichomeka panga lake vyema. Wanaume hao walicheka sana baada ya kuigundua sura ya mtu waliyekuwa wanamtafuta alikuwa amejileta kiwepesi sana kiasi kwamba kazi yao inaenda kuwa nyepesi kupita kiasi, aliyekuwa anafanya mazoezi alitaka kwenda kwa pupa lakini mwenzake alimshika mkono kumpa ishara kwamba mtu huyo ni hatari sana asiende kipuuzi, alipanga ngumi zake huku akiwa anamkimbilia Calvin mwanaume alikuwa amesimama tu akimsubiri mtu huyo afike hapo haraka , wakati anamfikia alipo aliruka juu kwa nguvu na kumfanya aende umbali mrefu kidogo hewani kitu ambacho kilikuwa ni kigumu mno kwa mwanadamu wa kawaida, alijigeuza na kushuka kwa nguvu huku akiwa amechomoa upanga wake, aliikata shingo ya mtu huyu huku akiwa ameangalia upande mwingine wala hakujisumbua kuhakikisha kama mtu huyo alikuwa tayari amekufa, yule aliyebaki alikuwa ni komando lakini ile ilimtisha sana haraka akakitupa kile kipisi cha sigara na kukanyaga chini kwa nguvu kujibetua na teke ambalo alikuwa na imani kama lingempata mwanaume huyo asingeweza kunyanyuka tena, alishtuka anahisi kama kitu cha baridi kimepita kwenye mguu wake wakati huo alikuwa anaenda chini, hakuamini anacho kiona mguu ulikuwa umekatwa kwa nguvu ulikuwa unaning’inia kiasi kwamba hata angekuja mtoto mdogo na kuuvuta mguu huo ulikuwa unatoka wote. Alikuwa kama amepigwa ganzi akiwa anaukadiria mguu wake kwa hisia za uchungu, sekunde kumi zilipita baada ya hapo kilifuata kilio kikali sana ambacho kiliwashtua wenzake ndani walio kuwa wapo kwenye mikakati ya kupanga namna ya kuweza kumpata Calvin, haraka sana bila kupoteza muda ili wakafanye kazi zao nyingine za kigaidi huko kwenye kambi yao nchini Kongo maeneo ya ndani ya msitu wa Kongo ambao unatisha kwa wanyama wakali na baadhi ya miujiza ambayo wengi huwa wananadai huenda ni mizimu ya mababu wa kale na kuna watu huwa wanaenda kuomba ikiwa wana imani kwamba watapata kila wanacho kihitaji.

NIFOLLOW Instagram @iamfebian Twitter #buxmsafi Tick-tock @buxmsafi LinkedIn FEBIANI BABUYA Facebook Bux the story teller WhatsApp 0621567672

Kelele zake hazikuweza kudumu baada ya kuzamishiwa kisu kwenye koromeo na kutokezea upande wa pili, wale wa ndani walikuwa wanakuja kwa kasi sana, aliyekuwa mbele hakuvaa hata shati alikuwa kifua wazi, aliufungua mlango kwa kasi wakati anatoka alirudishwa kwa kishindo ndani akiwa ameishika shingo yake kitu kilicho wafanya wenzake wasimame kwanza, ni star ilikuwa imezama shingoni na kumfanya mtu huyo apumue kwa shida kubwa hatimae akafumba macho yake na kutulia kimya pale chini. Mmoja wao alikimbilia mlangoni ili aufunge mlango baada ya kugundua huenda mtu huyo alikuwa anaona mahali walipokuwa na alifanya hivyo ili kuwatega waweze kutoka kichwa kichwa awamalize wote. Hata yeye alikuwa amechelewa sana wakati anafika mlangoni upanga ulizama kwenye tumbo lake na kuna mtu aliingia kwa kasi sana hapo ndani kisha akalichomoa panga lake taratibu kutoka kwenye tumbo la komando huyo, walikuwa wamebaki wanaume watano humo ndani. Aliwahesabu kwa upanga wake wakati huo mwanaume mmoja alichomoa bastora yake haraka ili afyatue risasi ila huenda alifanya kazi ya hatari kufanya hivyo, upanga ulizungushwa na kukikata kiganja cha mkono huo na mwanaume akamfuata pale kwa kasi mikononi mwake akiwa amezishika star mbili, alizipigiza kwa pamoja kwenye shingo ya yule jamaa, alitoa macho sana kwa namna shingo yake ilivyokuwa imebanwa kwa nguvu na star hizo zilizokuwa na makali kupita kiasi. Wale wanne walikuwa wanakuja kwa pamoja baada ya kuona wakifanya ujinga wanaisha wote mtu mwenyewe alikuwa hata haongei zaidi ya kuwachinja tu na kuwaua kikatili

Aliyafumba macho yake kwa haraka na kutulia, wakati huu alikuwa anapiga kwa hisia na ndio muda ambao alikuwa anakuwa kiumbe wa hatari kupita maelezo, walimfikia na kuanza kumrushia ngumi hakuikwepa hata moja zote zilimfikia vyema wakati huo alikuwa ameukaza mwili wake mpaka mishipa ilikuwa imejichora kuanzia shingoni mpaka mikononi, walikuwa wanapiga akiwa bado amesimama hapo hapo, akazikunja ngumi zake mbili zikiwa zote zina star (nyota), walirusha na kumpiga ngumi za mbavu wakati huo alikuwa akisikilizia ngumi zinakotokea aligeuka haraka na kurusha ngumi zake mbili kwa haraka na kasi kubwa sana, ziliwafikia wanaume wawili kwenye maeneo ya shingo star zilikuwa zimeshazamishwa hao wawili hakuwa na habari nao tena, mmoja alianza kurudi nyuma kwa uoga wakiwa wamebaki wawili tu, sasa Calvin aliyafumbua macho yake na kuuokota upanga wake chini pamoja na bastola ya yule aliyekuwa amemkata kiganja cha mkono, aliigeuza haraka na kumpiga mwanaume mmoja risasi tano za kichwa kilicho pasuka kwa sauti kubwa na ya kutisha sana, kuona hivyo yule komando mmoja aliyekuwa emebaki aliogopa na kutetemeka huku akiwa analia kama mtoto mdogo hivyo alianza kukimbia ili pengine ajinusuru na ukatili huo na moyoni mwake ni wazi alijiwekea nadhiri kwamba kama angefanikiwa kutoka hapo salama kabisa basi alikuwa anaenda kuokoka siku hiyo hiyo au kuwa mtu wa swala tano kila siku ya MUNGU lakini hakupewa hiyo nafasi kwani hakufika mahali mwanaume alijirusha sarakasi mbili na kumzuia mlangoni ilisikika tu sauti ya miguno kutoka kwa mtu huyo akiwa ameishika shingo yake, Calvin hakusimama wala kugeuka nyuma kumuangalia mtu huyo baada ya kuupitisha upanga huo kwenye eneo la shingo alijua hawezi kupona kwa namna yoyote ile, mwanaume taratibu alikuwa anaondoka mahali hapo kama sie yeye aliye sababisha mauaji ya kutisha sana katika eneo hilo

Saa tatu na robo za usiku maeneo ya Posta katika eneo inapopatikana maktaba kuu ya taifa yanaonekana magari mawili meusi ya kifahari sana, wanashuka wanaume watatu katika gari ya nyuma na kwenda kulizingira gari la mbele, kisha ndani ya gari la mbele wanashuka wanaume wawili wote wakiwa na suti nyeusi na wale wenzao watatu, mmoja anaufungua mlango wa nyuma wa gari hilo anashuka mzee mmoja wa makomo kidogo akiwa na suti yake ya blue iliyokuwa imempendeza sana, aliondoka na watu hao kuingia ndani ya maktaba hiyo hata walinzi hawakuonekana kumzuia kabisa mzee huyo ikimaanisha walikuwa wana taarifa juu ya ujio wake ndani ya eneo hilo Kwa maana alicho kuwa amekifuata hapo kiliwekwa majira ya saa moja za jioni.

Ng’ambo mwa barabara kutoka hapo alikuwa anaonekana mwanaume mmoja akiwa amejibanza kwenye ukuta akiwa anawatazama vyema sana watu hao, na mavazi yake ya kininja hakuwa na papara yoyote, baada ya kuona wameondoka alienda wenye lile gari la mbele akafungua buti na kukibana kifaa chake cha mawasiliano ambacho alijua kingeweza kumuonyesha ni wapi gari hilo litakuwa linaenda ili asije akalipoteza kisha akalifunga vyema sana buti hilo na kurudi sehemu aliyokuwa mwanzo. Dakika kumi mbele watu hao walikuwa wamesharudi tayari na safari yao ilikuwa ni kuelekea ufukweni mwa bahari. Dakika chache gari ziliweza kusimama mahali hapo kukawa na ukimya wa muda mrefu. Calvin alikuwa anakuja taratibu maeneo hayo kwa sababu gari zilikuwa zipo taratibu tu kwa kifaa chake kilivyo kuwa kinamuonyesha hivyo hakuwa na papara yoyote ile juu ya hilo jambo. Saa yake ilipiga alarm ndogo kumtaarifu kwamba gari hizo zilikuwa zimesimama basi akaongeza mwendo ili azifikie haraka, ila wakati anakatiza kona ya kuelekea kwenye fukwe hiyo ya bahari ambapo ndipo gari hizo zilikuwa zimesimama alipishana na piki piki moja ikiwa kwenye mwendokasi sana huku imewapakiza wanaume wawili waliokuwa wameziba sura zao, alitoka kwa kasi ili kama kuna hatari yoyote aweze kuikabili kwa usahihi kwani alihisi hakukuwa na usalama maeneo hayo, ilimshamgaza sana kuona hakuna watu mahali hapo kulikuwa kimya mno, gari zilikuwepo pale pale aliyafumba macho yake na kutuliza hisia zake sikio lake likiwa linafanya kazi kwa zaidi ya asilimia miamoja alisikia mtu akiwa anahema taratibu tena akionyesha kuwa na maumivu makali sana, aliyafumbua macho yake na kugeuka nyuma ndipo alipoweza kushangaa baada ya kuiona miili ya watu sita ikiwa chini ikivuja damu, alivyo waangalia wale watu aligundua ndo wale alio waona kule maktaba ya taifa, alishtuka baada ya kukumbuka miongoni mwa watu hao alikuwepo Fabian Decco na huyo ndiye alikuwa na shida naye kubwa mno amueleze kiundani mambo yako vipi na kwanini amfanyie ukatili wa namna hiyo baada ya kupewa msaada mkubwa na familia hiyo, alitoka kwenye mshangao na kumkimbilia mtu huyo aliyekuwa amechakaa kwa risasi nyingi sana huku wale walinzi wake wote wakiwa wameshakufa tayari.

Alikuwa anamuangalia mzee huyo kwa hasira mno kwani ndiye mtu aliyeweza kusababisha wazazi wake wote wapotee hapa duniani na alikuwa anamtafuta kwa hamu kubwa kupita kiasi. Baada ya kushikwa na kuwekwa kwenye mikono ya Calvin mr Fabian Decco aliyafumbua macho yake japo kwa taabu mno, alitabasamu baada ya kuona aliuekuwepo hapo ni Calvin Jackson mtoto wa binadamu ambaye aliyabadilisha maisha yake ya ulofa mtaani na kufanikiwa kuyaishi maisha ya ndoto ya wanadamu wengi sana. Alinyanyua mikono yake na kumpapasa usoni Calvin kwa tabasamu hafifu.

“mwanangu utakuwa unanichukia sana na unajutia sana kuweza kumjua mtu kama mimi kwenye maisha yako eeh? Najua unatamani niwe binadamu ambaye ninastahili kufa kifo kibaya sana eeh? Haya yote nayajua vizuri kijana wangu hilo litafanikiwa leo na nashukuru umefika kwenye dakika zangu za mwisho nikiwa kama mwanadamu niliye hai, nafurahi ni wewe mtoto wa mwanaume bora sana kuwahi kuishi kwenye dunia hii nikiwa nafia leo kwenye mikono yako na unaweza kuniwahisha kwenye safari yangu ili kidogo uweze kupunguza baadhi ya hasira na chuki ulizo nazo kwangu, asante kwa kuja muda mwafaka mwanangu” alikuwa anauliza na kuongea kwa sauti ya taabu mzee huyu akiwa yupo katikati ya hatima ya maisha yake akiwa anapigania pumzi yake ya mwisho ili kuushinda umauti ulio kuwa unamuita kwa kasi lakini hata hivyo Calvin hakumjibu chochote alikuwa akimtazama kwa hasira kupita kiasi baba yake mdogo huyo wa kufikia, mtu huyo alijikohoza kwa shida baada ya kuona Calvin hamjibu chochote.

******************************************
“miaka ishirini na minne iliyopita ulizaliwa kwenye familia bora sana na wote tulikupenda kwa mapenzi yetu yote hata wewe ulilijua hilo, nilikupenda mno kupita kiasi baada ya mimi kwenda hospitali na kuambiwa sikuwa na uwezo wa kuweza kumzalisha mwanamke kwahiyo nilikuwa nikikuona naona kama ni tumaini langu kama mwanangu, pia ulielewa namna nilivyokuwa nakujali ndio maana uliniheshimu mno, miaka ishirini na moja baadae ndipo ndoto za kuishi kwa furaha na familia ile zilipo anza kuyumba.

Nakumbuka siku moja nikiwa kwenye jumba langu la kifahari walikuja watu sita wenye suti nyeusi na sura zao zilikuwa ngeni kabisa kwenye sura yangu, watu wale walifika kwangu na kunichoma sindano ya usingizi kwa nguvu, nilivyo kuja kushtuka asubuhi nilishangaa nipo pale pale kwangu na watu hao hawakuwepo nilistaajabu sana kwani hawakubeba chochote, nilienda mpaka chumbani kama labda wamechukua hata pesa ambazo zilikuwa nyingi sana kwenye droo yangu lakini haikuwa hivyo kila kitu kilikuwepo hivyo sikuelewa kwangu walikuwa na lengo gani hasa.
Baada ya wiki moja kupita nilipigiwa simu na namba ngeni ikiniambia wiki moja baadae inabidi niende Kenya kwa gharama yoyote ile nilipuuzia na kukata simu lakini kesho yake ile namba ilipiga tena na kunitahadharisha kwamba nisije nikadharau kwani ningejutia sana kwa baadae. Niliamua kuiblock ile namba na kukawa kimya, ulipita mwezi mzima bila kutafutwa na mtu yeyote, wakati unaelekea mwezi wa pili walirudi tena wale watu wa mwanzo awamu hii walifika ofisini, walifanikiwa kunizimisha na kinibeba kwenye gari lao bila mtu yeyote yule kujua, nilifikishwa kwenye jumba moja kubwa sana ambapo ndo nilikuja kuzindukia hapo, nilikutana na mtu mmoja mwenye asili ya kiarabu lakini sura yake ilikuwa imekomaa sana akionyesha ni mtu wa mazoezi mno mtu huyo. Nilikalishwa chini na kupigwa sana kwa kukaidi maagizo, sikuwaelewa ni akina nani mpaka waseme mimi nimekaidi maagizo yao, jamaa aliniambia nafanya kitu cha hatari sana. Aliitoa laptop ndogo sana akaifungua moja ya file lililokuwa na video tano akaifungua moja, nilishangaa ni video ambayo watu wale walikuja kwangu siku ya kwanza kabisa, kuanzia walivyokuwa wanaingia, kunizimisha ila kilicho nishangaza ni sindano ambazo nilikuwa nachomwa, zilikuwa tatu moja shingoni , ya pili kifuani karibu na moyo na ya tatu nilichomwa mkononi baada ya kuchomwa sindano hiyo ilikuwa inaonyesha kwa ndani vitu vikiwa vinaingia kwenye mwili wangu.

“sxcd98 ni aina ya sumu ambayo umechomwa kwenye mwili wako, ni sumu mpya iliyotengenezwa nchini Japan na kwa bahati mbaya sana daktari aliye itengeneza amekufa ikiwa hajatengeneza chanjo za kutosha, inaanza kula sehemu ya ini lako taratibu alafu ndipo inahamia kwenye moyo, unakuwa mtu wa kuteseka sana mpaka siku unakuja kufa utapitia maumivu makali mno. Dawa ipo na unaweza kupona lakini hii itategemea na ufanyaji wako wa kazi utakayo pewa ndo itafanya upate dawa au usiipate, tuna shida na nyaraka za umiliki halali wa ndugu Jackson Aron nawewe ndiye mtu ambaye tuna imani una huo uwezo wa kuzipata kirahisi sana, zinahitajika mwa muda wa miezi kadhaa hivyo kuwa makini sana usije ukajiingiza kwenye matatizo makubwa ambayo hautaweza kuyaepuka tena” aliongea kwa sauti kavu sana na ya ukali mwanaume yule hakusubiri hata jibu langu akawa ameondoka. Kwangu ilikuwa ni kitu ambacho kilikuwa hakiwezekani kabisa kumsaliti ndugu yangu huyo niliyekuwa tayari hata kuyatoa maisha yangu kwa ajili yake. Nilipuuzia na kuona walikuwa wananitisha tu hakuna walicho kifanya kwenye mwili wangu lakini baada ya mwezi mmoja mbele mwili wangu ulianza kuona mabadiliko na kila nilipokuwa naenda hospitali niliambiwa sikuwa na tatizo lolote lile. Miezi mitatu baadae nilipigiwa simu na wale watu wakihitaji niwape mrejesho kama nimefikia wapi ila niliwaambia siwezi kufanya kitu kama hicho kwa ndugu yangu bora waniue ajabu hawakuhangaika namimi kabisa mpaka ilipoisha miezi sita, mwili wangu sasa ukawa una mabadiliko ya ajabu ikiwa kuna baadhi ya vinyweleo vya kutisha vikianza kunitoka kwenye sehemu zangu zote za siri pamoja na vidonda vilivyokuwa vinanuka sana na kutoa wadudu wa kutisha mno, wakati huo niliamua kujiweka mbali kidogo na familia yako ili msijue hali niliyokuwa naipitia, nilizunguka mahospitali mengi mpaka nje ya nchi lakini niliambiwa hakuna tatizo linalo onekana kwahiyo huenda ni mabadiliko ya mwili, nilijitahidi kutumia sana madawa lakini haikusaidia chochote. Siku moja usiku watu hao walifika kwangu wakiwa watatu tu kati ya wale sita mmoja alinichoma sindano nilishangaa vile vidonda na vinyweleo vyote vikapotea, niliogopa sana kuiona hali hiyo wakaniambia kama nikikubali nitapewa dawa ya kuniponyesha kwani hapo nilipewa kinga ya siku mbili tu, niliwaambia waende nijifikirie kwanza kwani lilikuwa ni jambo la kutisha sana.

Leo tunafika mwisho na kalamu ya professor, ukurasa wa 33 unafika tamati mpaka wakati ujao.....

Chao[emoji2768]

Bux the story teller

#ULIMWENGUWAWATUWABAYA

Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
Siku ya tatu leo hujapost muendelezo tunaomba utupostie
 
HADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
MTUNZI : Bux the story teller
WHATSAPP : 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 34
SEHEMU ILIYOPITA TULIPO ISHIA.............

Siku moja usiku watu hao walifika kwangu wakiwa watatu tu kati ya wale sita mmoja alinichoma sindano nilishangaa vile vidonda na vinyweleo vyote vikapotea, niliogopa sana kuiona hali hiyo wakaniambia kama nikikubali nitapewa dawa ya kuniponyesha kwani hapo nilipewa kinga ya siku mbili tu, niliwaambia waende nijifikirie kwanza kwani lilikuwa ni jambo la kutisha sana.

ENDELEA..........................

Ni kweli baada ya siku mbili hali ilirudi kama mwanzo wakati huu nilikuwa nasikia maumivu makali sana kama moto unawaka kwenye mwili wangu, ilinilazimu kuwakubalia walicho kuwa wanakihitaji na nilipanga nichukue nyaraka niwape halafu baadae tuzirudishe kwa njia ya sheria, ndipo hapo walipo niambia nitafute watu wa kufanya nao kazi ili kukiwa na tatizo wawe wanalimaliza, niliunganishwa na Scot na watu hao pamoja na vijana wengine ambao walikuwa chini yangu kwa usimamizi wa Scot. Ulikuwa umekatika mwaka sasa tangu wanichome ile sindano nikiwa naishi kwa kutegemea kuchomwa sindano zao ili mwili wangu uweze kuwa sawa zilianza harakati za kuzipata nyaraka hizo ambazo kiukweli hata mimi sikuwa nikijua mahali zilipokuwa zinahifadhiwa, hivyo ilinilazimu nimtume Scot na baadhi ya vijana waje kumtishia mzee wako ili atoe nyaraka kwa hiari yake ili asije akauawa, usiku ule watu wale walikuwa nyumbani wakizisubiri nyaraka hizo lakini mambo yalienda tofauti na yalivyokuwa yamepangwa baada ya mzee wako kugoma kutoa nyaraka zile ule usiku na inadaiwa wewe haukuwepo eneo lile kwani huenda wangekutumia kama ngao ili kuzipata kwa urahisi kwa namna mzee wako alivyokuwa anakupenda, wakati Scot anapiga simu kuuliza afanyaje baada ya kushindwa kuzipata kuna mmoja ya wale watu alinipokonya simu na kumpelekea yule mwarabu na ndiye aliyetoa amri ya baba yako na mama yako wauawe na huo mzigo nikawa nimedondoshewa mimi.

Baada ya hapo ndipo rasmi nilipokuwa mtumwa wa hawa watu, nilikuwa kama mbwa kwao kwani nilikuwa nikijaribu kugoma chochote basi walikuwa wanaacha kunipatia dawa kitu kilichokuwa kinatishia amani sana ya maisha yangu na ndipo hapo nilipoamua kukutafuta sana ili upatikane umalizane nao niweze kupatiwa dawa lakini imekuwa ni ngumu sana kukupata na kwa sasa unaonekana umerudi na ni mtu wa hatari sana kwa namna unavyo yafanya mauaji hapa mjini. Natumiwa na watu hao lakini sijawahi hata siku moja kupata bahati ya kukutana wala kuonana na kiongozi wao zaidi ya kuishia kuongea nae kwenye simu tena siku moja pekee, wengi wanajua kama yule mwarabu ndiye kiongozi lakini sikweli kuna mtu yupo nyuma ya hili na ndo huyo nilibahatika kuongea nae kwa mara moja, katika kufuatilia kwangu anaonekana ni mtu mkubwa sana ndani ya nchii hii, huyo mwarabu ndiye mwenye taarifa kamili juu ya mtu huyo lakini kumpata sio rahisi sana kwa sababu akiwa anatoka nje hadharani kwa watu huwa ana sura anaivaa ambayo sio yake halisia kabisa na mara nyingi huwa anajificha ficha asijulikane, nakumbuka siku moja mzee Mgaya alitukuta nae pale Dar live ambayo ndo siku mzee huyo alimpoteza mke wake aliye uawa na Scot pamoja na kuingia kwenye matatizo yeye pamoja na mtoto wake niliyekuwa nimepanga kumuoa, yote ilikuwa ni kwa sababu tu ya kumuona yule mwarabu mahali pale na kusikia tulichokuwa tukikizungumza.

Imetumika pesa nyingi sana kuweza kumtengeneza Scot ikiwa ni pamoja na kumbadilisha sura ili afanye kazi ya kukutafuta na kukuua bila kujulikana lakini mambo yalibadilika baada ya Tomaso pamoja na Thomas kupotea. Hizo pesa wanazo zihitaji sana ni kwa ajili ya uchaguzi ujao, wanahitaji kuwekeza kwa watu wengi ili waweze kupita lakini bahati mbaya sana hawana pesa za kutosha kwahiyo waliona njia rahisi ya kufanikisha kushinda kwenye uchaguzi ni kutumia mali za baba yako mzazi na huu ulikuwa ni mpango wa muda mrefu sana. Ni watu walio jipanga sana na wana mipango ya kutisha sana ya kuweza kuiweka nchi hii kwenye mikono yao jambo ambalo ni la hatari kupita kiasi, nchi inaweza kupitia kipindi kigumu sana kwenye historia yake yote, sio kazi rahisi ila jitahidi kwa namna yoyote ile uweze kulimaliza hili utakuwa umelipa kisasi chako lakini pia utakuwa umeisaidia sana nchi hii kwa ajili ya vizazi vya baadae kutoka kwenye kuipeleka nchi kwa hao watu. Leo nimedanganywa ndio siku ambayo nakuja kuonana na kiongozi mkuu wao ndio maana nikawa nimeelekezwa hapa lakini kumbe walikuwa wanakuja kuniua na sijui wamefikiria nini kufanya hivi kwa sababu walisema wananitegemea sana kulikamilisha hili, kama nilivyo kwambia hawa watu ni hatari sana lazima watakuwa na njia nyingi sana za kuweza kulifanikisha jambo hili.Nastahili sana kufanyiwa hivi kwa haya yote kutokana na mambo niliyo yafanya huko nyuma” mr Fabian Decco alikohoa damu kwa nguvu kisha akamkabidhi Calvin Frash ndogo halafu akaendelea.

Instagram @iamfebian Twitter #buxmsafi Tick-tock @buxmsafi LinkedIn FEBIANI BABUYA Facebook Bux the story teller WhatsApp 0621567672

“humo ndani ya hiyo frash kuna taarifa ambazo zitakupa sehemu ya kuanzia ili kumfikia huyo mwarabu ambaye ndiye aliyekuwa anakuja kuonana namimi wakati wanafuatilia mali zako na ndiye mtu pekee wa kukufanya umjue aliye sabababisha yote haya. Ndani ya pemba katika enao moja lifahamikalo kama Kengeja Kuna gereza linaitwa ALL DEAD yaani wote huwa wanahesabiwa kwamba wamekufa, lipo pembezoni kabisa mwa bahari ya Hindi huko ndiko alikofungwa mwanaume mmoja ambaye nilimuona kwenye picha tu jina lake na picha yake vyote vipo humo, hilo gereza wanafungwa watu wenye makosa makubwa sana kama mauaji ya kutisha, kuasi nchi, majasusi wa kimataifa wanao kamatwa pamoja na magaidi, ni gereza la siri sana lipo chini ya ardhi na huko ndiko anako patikana mwanaume huyo. Unapaswa upewe kesi nzito mno ili uweze kupelekwa huko vinginevyo utakuwa hujafanya lolote na kamwe hautafanikiwa kuwapata watu hawa wako makini kuliko hata mhalifu anapokuwa anapita na bangi maeneo yenye kambi ya jeshi, huyo mwanaume unaye enda kumfuata huko ni gaidi aliye husishwa na kesi ya kuua watu mia tano kwa mabomu pamoja na gesi, alitakiwa kuuawa kwa aina ya kosa alilokuwa nalo lakini watu hawa waliudanganya uma kwa kusema mtu huyo alinyongwa mpaka kufa lakini haikuwa hivyo mtu huyo alienda kufichwa huko na wana mpango wa kumtumia sana kwenye uchaguzi kwani ni mtu hatari mno kwa taarifa zake zilizopo hata huko gerezani alidaiwa kuua majasusi watatu wa uingereza waliokuwa wamekamatwa hapa Tanzania, huyo ndiye mdogo wake na huyo mwarabu ambaye atakupa njia nzima ya kumjua mbaya wako ni nani ila ukicheza vibaya utakufa mapema sana hawa watu wanafanya majukumu yao kwa usahihi wa zaidi ya asilimia miamoja. Go and make me proud son nchi hii sasa ipo mikononi mwako ili iweze kupona bila hivyo itaingia kwenye machafuko makubwa sana yatakayo ondoka na damu za maelfu ya wanyonge wengi mno.

Kifo ni siri kubwa sana mwanangu, nimeyaishi maisha yangu ya kuhangaika kukikwepa kifo kwa zaidi ya miaka mitatu sasa nikiwa nimesababisha vifo vya watu wengi sana wasio kuwa na hatia yoyote ile lakini leo hii sina uwezo wowote wa kukikwepa kifo, najiona ni binadamu mpumbavu sana kuwahi kuishi kwenye ulimwengu huu kwa kukosa fadhila kwa watu walio nisaidia hata hapa naogopa sana naenda kumtazama vipi baba yako na mama yako huko nako elekea, MUNGU nitamjibu nini kwa haya niliyo yaishi kwa muda nilio bahatika, nikapendelewa kuupata hapa duniani, natamani ningepewa hata mwezi mmoja mwingine wa kuishi ili niyafute baadhi ya mabaya yote niliyo yafanya ikiwa ni pamoja na kuhubiri kwa watu ni namna gani watu wanapaswa kuyaishi maisha kwa usahihi sana kwa mfano wa baba yako marehemu Jackson Aron Mavunde, ila muda umeenda sana siwezi kuipata hiyo nafasi tena. Kama tutakuja kuonana tena kwenye maisha ya baadae tena basi kitu cha kwanza itakuwa ni kukuomba msamaha japo moyoni tu hata usiponijibu kwa mdomo “don’t live life wrong my son like I did” (usiyaishi maisha vibaya mwanangu kama nilivyo yaishi mimi), zingatia sana hilo na usisahau muda huwa haujirudi mara mbili kwenye maisha, binadamu tunakosa na kufanya makosa mengi lakini huwa tunajirudi na kubadilika baadae na kuwa watu wema ila kamwe muda haujawahi kukupa nafasi ya pili unavyo upoteza ndio jinsi unavyokuwa unaisogelea hali mbaya sana ya maisha yako, love you kid”. Aliongea kwa hisia mno mzee huyu wakati anaitoa simulizi ndefu ya mambo mazito aliyo yapitia mpaka kufika hatua ya kumsaliti mwanaume aliye mfichia aibu ya kudhalilika kwa sababu ya kuwa na maisha duni sana, Calvin alkuwa na hasira sana na mzee huyu na alikuwa ameahidi kumuua kikatili kupita kiasi lakini alijikuta akitoa machozi mengi sana ikiwa ni kuvunja kiapo alicho apa kwenye kaburi la baba yake kwamba hatatoa machozi tena mpaka siku atakayo weza kurudi tena pale akiwa amemaliza kisasi chake. Mr Fabian Decco alipitia mambo mengi sana magumu ambayo ilikuwa ni ngumu sana kwa binadamu mwenye moyo dhaifu unao weza kulainishwa kwa sauti nzuri ya mwanamke mrembo kuweza kuyavumilia mambo ya kutisha sana namna hiyo. Calvin hasira zote zilimuisha dhidi ya mzee huyu na kujikuta akimuonea huruma sana, alikuwa ametulia tuli kwenye mikono ya mwanaume huyu nafsi yake ikiwa imeuacha mwili tayari na hakuwa mtu hai tena alitangulia kwenda kuisubiri hukumu ya maisha ya mwisho, alifia kwenye mikono ya binadamu aliyekuwa anamtafuta sana kwenye haya maisha huenda kuliko hata anavyokuwa anaitafuta pesa siku za uhai wake lakini mtu huyo aliye mtafuta kwa gharama nyingi sana hakuwa na kauli tena mbele ya uso wa dunia. Inatukumbusha kwamba mwanadamu unatembea na kifo chako kwenye mifuko yako kwahiyo ukiitoa mikono yako vibaya utakuwa na mwisho mbaya sana, usije ukathubutu hata siku moja kumsahau MUNGU hata kama unajiona umefanikiwa vipi bado siku moja mafanikio yako hayatakuwa na uwezo wa kukufanya uwe na muda mrefu wa kuwa na sifa za kuifaidi pumzi ya bure hapa duniani. Calvin alilia kwa uchungu sana kwani alichelewa mno kulijua hili huenda wangejua tokea mwanzo wangeangalia namna ya kumsaidia mzee huyu, hakuwa na cha kubadilisha zaidi tu ya kubaki kuliheshimu neno “siri” kama alivyoweza kuitunza mr Decco kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.

**********************************
IKULU, DAR ES SALAAM

“Eneo tukufu na eneo lenye thamani zaidi ndani ya nchi yoyote ile duniani kwani ndiyo sehemu anayo ishi mtu wa mhimu zaidi ndani ya nchi yoyote ile hapa duniani kwa sababu mtu huyu ndiye anae amua mwenendo mzima wa maisha ya wananchi wake uweje, akili yake na maamuzi yake ya mwisho ndicho kitu kinacho amua hatima ya nchi nzima, kila siku ya MUNGU usije ukasahau kumuombea raisi wako hata kama una kinyongo kiasi gani kwani huyu mtu akifanya maamuzi ya hovyo yatakugharimu mpaka wewe hapo. Nasema mtu wa mhimu zaidi ndani ya nchi kwa sababu bila uwepo wa mtu huyo nchi haitambuliki sehemu yoyote ile na pia yeye ndiye mwenye maamuzi ya mwisho juu ya maisha ya wanadamu wote wanao patikana kwenye nchi husika. Huyu ndiye mtu anayepaswa kujua kila punje ya kitu kinacho endelea ndani ya nchi yake kwa gharama yoyote ile, huwa ni hatari na aibu kubwa sana kwa kiongozi mkubwa kuweza kumzunguka mkubwa wake wa nchi kwa hali yoyote maana yake hayupo tayari kumtii na anamuasi bosi wake” haya yalikuwa ni maneno ya raisi wa nchi ya Tanzania James Tomson, alikuwa akiyaongea huku amesimama dirishani akiangalia namna ndege walivyokuwa wanacheza na maji ya baharini, nyuma yake alikuwa amekaa mzee Kasisi Chacha mkuu huyu wa idara ya usalama wa taifa aliyekuwa akitokwa na jasho kila muda ilihali humo ndani hakukuwahi kuwa na joto hata siku moja, alijua kwa hayo maneno ambayo bosi wake anayaongea kulikuwa na hatari kubwa sana mbele yake.

“huwa sio rahisi sana uitwe na raisi wa nchi yako halafu akawa anakuongelea kwa mafumbo unatakiwa uuogope sana huo wakati kwenye maisha yako, yule ndiye bosi wa nchi na ndiye mwenye mamlaka na kila kitu ndani ya nchi akisema kesho hamuendi kazini basi hamuendi, hakikisha unamtii kwa kila kitu hata kama unaona anakosea, yule kuwa pale ni nguvu ya wananchi kwahiyo mheshimu sana siku zako zote za utumishi ndani ya ikulu yule ndiye raisi wa Tanzania usilisahau hilo” haya ni maneno ambayo mzee huyu alikuwa anayakumbuka vyema sana akiwa amekaa pale kwenye moja ya sofa ghali sana, alishawahi kuambiwa na mwalimu wake baada ya kuteuliwa kuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa TANZANIA INTELLIGENCE SECURITY SERVICE (TISS) akiwa na zaidi ya miaka ishirini sasa kwenye ngazi hiyo tangu amalize mafunzo ya juu sana ya ujasusi.

“kwanini unaamua kunificha mambo mazito yanayo endelea kwenye nchi yangu mimi mwenyewe?” lilikuwa ni swali la raisi huyu kwenda kwa mzee huyu ambae alishtuka sana alielewa alikuwa anamaanisha mauaji yanayo endelea kimya kimya hapa mjini.

“mkuu hili jambo nalishughulikia mwenyewe na nitalimaliza mapema sana iwezekanavyo nitakupatia majibu mazuri muda mchache ujao” alijibu kwa wasi wasi sana

“yani nchi yangu mwenyewe ndo unanambia huo upuuzi na wananchi wangu wanaingizwa kwenye wasi wasi na maisha ya shaka sana kwa kuhisi hakuna usalama wowote nchini na viongozi wakubwa mmekaa tu mnaota vitambi, kazi zenu ni zipi sasa kama hamuyaelewi hata majukumu yangu” raisi alikuwa akifoka kwa hasira sana kuonyesha amekerwa mno na hicho kitu kilicho kuwa kikiendelea ndani ya nchi yake bila yeye kupewa taarifa.

“samahani sana bosi kwa kukucheleweshea hii taarifa lakini mtu anaye yafanya haya yote ungemjua huenda usingeweza kuamini hata kidogo” Kasisi aliongea wakati huo raisi alikuwa anakaa ili kuweza kusikiliza kwa umakini kuhusu huyo mtu

“ni mtoto wa rafiki yako”

“unamaanisha nini?” raisi aliuliza kwa mshangao sana akipunguza hasira zake kwa utulivu mkubwa

“miaka miwili iliyopita nadhani unajua kwamba rafiki yako aliuawa na watu wasio julikana lakini kwenye mauaji yale mtoto wake aitwaye Calvin hakuwepo na inasemekana alitorokea nchi za nje huko, ilivyo isha hiyo miaka miwili sasa amerudi kwa ajili ya kulipa kisasi kwa hao watu ambao walimuulia familia yake, amekuwa ni mtu hatari kupita kiasi, nilimtumia komando wa kwanza akamshindwa nikaamua kumtumia kikosi maalumu cha siri sana cha THE RED SQUARD lakini mpaka sasa ndo wanapona majeraha na angeamua kuwaua angewaua wote ni mtu hatari kuliko hata ilivyo hatari yenyewe. Nilikutana nae siku moja baada ya kuniomba hilo na akanihitaji nimuache amalizane na watu wake kwani hana shida na watu wengine ila nikimlazimisha hatakuwa na namna, nilijaribu kumuuliza shida ni nini kwanini asiiachie sheria ifanye kazi yake, aliichukia sana hii sentensi yangu kwani alisema hii sheria ninayo isema mimi ndiyo hiyo hiyo ambayo imeshindwa kufanya chochote ndani ya miaka yote hii kwahiyo kwake haina umuhimu wowote ule. Licha ya hivyo mimi kama kiongozi mkuu wa usalama nchini siwezi kumwacha raia wa kawaida ajichukulie maamuzi anayo yataka yeye mwenyewe lazima nimkamate akafungwe kwenye gereza la siri maisha yake yote ili asije akasababisha maelfu ya maafa nchini” alieleza kwa ufasaha sana mzee huyu akiwa anameza mate Kwa wasi wasi.

“shiiiiiiiiit….tumemkosea sana, baba yake ni mtu pekee aliye niweka kwenye hiki kiti wakati watu wote walipo nikataa nahitaji kukutana naye huyu mtoto haraka sana” alikuwa anajiwazia raisi huyu baada ya kusikia hiyo stori ya mtoto wa rafiki yake ambaye kwa asilimia nyingi ndiye aliye mfanya aingie ikulu kwa kutumia fedha zake nyingi sana kwenye uchaguzi wa James Tomson.

Ukurasa wa 34 unafika tamati ungana nami wakati ujao.

Chao[emoji2768]

Bux the story teller

#ULIMWENGUWAWATUWABAYA

Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
Umetisha sana mkuu ,hii kitu imesimama kinyama
 
HADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
MTUNZI : Bux the story teller
WHATSAPP : 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 36
SEHEMU ILIYOPITA TULIPO ISHIA.............

“hahahah nawewe na siasa aisee naona unataka uje uanze kutupitishia sheria unazo zipenda mwenyewe maana nakijua vizuri sana kichwa chako rafiki yangu” Jackson alimtania rafiki yake huyo wakiwa ni watu wenye furaha sana, wakaelekea zao kulala.

ENDELEA...........................

Walifanikiwa kumaliza masomo yao na kwenda kujiunga chuo pamoja, huko ndiko kila mtu aliko enda kuanza kuziishi ndoto zake, James Tomson alijiingiza taratibu kwenye siasa huku Jackson akianza kujiwekeza kwenye biashara mbali mbali. Katika harakati zao zote za utafutaji walikuwa watu ambao walishirikiana sana na hawakuwahi kuachana, walimaliza masomo yao ya chuo kila mtu rasmi akijiingiza zaidi sehemu aliyo iona atatimiza ndoto zake. James Tomson jina lake lilianza kuvuma sana hasa kutokana na sera zake kama kijana lakini ilikuwa ni ngumu sana kuweza kupita kutokana na aina wa wapinzani alio kuwa akipambana nao.

“daah rafiki yangu siasa ni ngumu sana tofauti na unavyoweza kuifikiria unapokuwa upo nje” Tomson alikuwa akiongea na rafiki yake wa siku nyingi sana wakiwa kwenye moja ya hoteli kubwa maeneo ya Mbezi beach.

“lakini ndicho kitu unachokipenda kwahiyo hauna namna zaidi ya kupambana nacho, unajua shida inayo wafanya wanasiasa wengi mnafeli kwenye harakati zenu hizo hamjui namna ya kuishi na hawa wananchi” Jackson alielezea huku akishushia juice za baridi.

“hatujui kivipi” aliuliza akiwa na hamu ya kujua rafiki yake alikuwa akimaanisha kitu gani mpaka amwambie hivyo.

“kwenye kichwa chako kabla hata haujaingia kwenye siasa ulipaswa ujue kwamba wewe maisha yako muda wote yatakuwa yanategemea watu ambao ndo wananchi wanao kupigia kura, kwahiyo unapaswa uzishinde kwanza nafsi zao ili ziweke mawazo kwako wakupime kama unawafaa, unaweza ukawa haujanielewa namaanisha kwa sasa wekeza kwa watu kwanza kabla hujaanza kushindana na wapinzani wako kumbuka mpinzani wako sio mtu wa kukupigia kura zaidi nayeye anatetea tu maslahi yake” Jackson alimwelewesha vizuri rafiki yake huyo aweze kuzichanga karata zake upya kwa kuwekeza kwa watu.

“nadhani ungekuwa mwana siasa hakuna mtu ambaye angeweza kushindana nawewe unawaza mbali sana, lakini hata hivyo inahitajika pesa nyingi sana ili kuweza kuwekeza kwa hao watu” Tomson alikuwa ameufurahia sana ushauri wa rafiki yake lakini alikuja kunyong’onyea baada ya kukumbuka kwamba hayo yote yanahitaji pesa nyingi kuweza kuyakamilisha.

“kuhusu pesa usijali sio tatizo hilo nitalishughulikia mwenyewe wewe andaa mipango yako vizuri halafu utanipa mrejesho uianze kazi yako ila kuna vitu viwili unapaswa uvizingatie sana na uviweke akilini, kwanza sitaki pesa zangu ninazo zitoa zije kutumika kutesea wananchi maana utanifanya nisikutambue tena kama rafiki yangu tuliye toka mbali sana, chamwisho sitaki kabisa familia yangu ihusishwe na uwepo wako kwenye siasa yaani nataka iwe mbali sana na hayan mambo naijua vizuri sana michezo ya siasa inaweza kuniingizia familia yangu kwenye hali ya hatari mno. Nitakupatia chochote unacho hitaji ila mimi najiweke pembeni juu ya hili sitaki nijulikane kama nakupatia misaada hata kukutana kwetu saivi itakuwa ni kwa siri na sio kila muda, nahitaji familia yangu iwe salama” Jackson aliongea huku akiwa anampungia mkono rafiki yake huyo wa damu. Hapo ndipo rasmi James Tomson alipoanza kuvuma kila sehemu kwa sababu pesa ya kuwashawishi wananchi ilikuwepo kwanza hiyo ilimfanya aonekane ni kiongozi asiye na njaa ya madaraka kwa sababu pesa kwake haikuwa tatizo. Miaka kadhaa mbele alikuwa amefanikiwa kukibeba kiti cha uraisi nchini Tanzania kwa msaada mkubwa sana wa Jackson aliyekuwa kama kivuli kwani hakutaka kufahamika zaidi tu walimjua watu wachache wa karibu na raisi waliokuwa wanaelewa mchango wa mtu huyo kwenye hayo maendeleo. Hii ndio sababu familia ya Jackson Aron hususani mtoto wake Calvin hakuwahi kabisa kujua uhusiano ulio kuwepo kati ya raisi na baba yake.
Mheshimiwa raisi alivuta pumzi ndefu sana baada ya kutoka kwenye kumbu kumbu ndefu sana iliyo mrudisha miaka mingi iliyopita wakati yupo na rafiki yake huyo waliye pendana sana na kusaidiana kwa kila hali lakini leo hii hakuwa kwenye uso wa dunia tena, kilichokuwa kinamuuma ni kushindwa kumsaidia mtoto wa rafiki yake huyo ambaye ajabu kwa sasa ndiye mtu aliyekuwa anafanya mauaji ya kutisha sana na sheria ilikuwa ishaanza kumsakama mtu huyu kwa udi na uvumba.

“inatakiwa nikutane na huyu mtoto haraka sana” aliongea huku akiwa anaingia zake ndani muda ulikuwa umeenda sana.

Calvin alikuwa bado hayaamini macho yake alidhani yatakuwa yanamdanganya pengine alidhani ilikuwa ni ndoto ya kutisha huenda angeshtuka usingizini lakini haikuwa hivyo kila kitu kilikuwa ni cha kweli, midomo yake ilikuwa mizito sana kutamka chochote kile mbele ya mtu huyo aliye weza kumuona mbele yake hali kadhalika kwa mtu huyo naye ilikuwa hivyo alitaharuki mno kuweza kumwona mwanaume huyo maeneo hayo. Aliyekuwa mbele yake Calvin alikuwa ni mwanamke aliye mhusudu mno kwenye maisha yake, ni mwanamke aliyekuwa amemfanya ahisi dunia ni nzuri sana kuiishi pale anapokuwa karibu yake, alimpenda mno mwanamke huyu, ilikuwa imepita miaka mitatu sasa tangu aweze kumtia machoni mrembo huyo ambaye asili yake ilikuwa ni katika nchi ya marekani, huyu alikuwa ni mrembo Jackline. Jackline wakati huo alikuwa akitiririsha machozi kama mvua huku akimkimbilia mwanaume na kumkumbatia kwa nguvu sana mwilini, Calvin bado alikuwa ameduwaa hakuwa anaamini kama kweli ni uhalisia wenyewe kwa sababu ni mtu ambaye alimtafuta mno ajabu kumbe muda wote yupo dar hapa hapa maeneo ya Tegeta tena akiwa mzima wa afya kabisa. Calvin aliunyanyua mdomo wake kwa mara ya kwanza na kumuuliza

Instagram @iamfebian Twitter #buxmsafi Tick-tock @buxmsafi LinkedIn FEBIANI BABUYA Facebook Bux the story teller WhatsApp 0621567672

“umeolewa?” Jackline alijitoa mwilini mwa Calvin na kujibu kwa kichwa akimaanisha kwamba alikuwa hajaolewa.

“kwanini ulifanya haya?” Calvin alimuuliza tena huku akiwa kamkazia macho. Basi ilimbidi Jack amchukue Calvin mpaka ndani ya nyumba hiyo mpaka kwenye sebule moja ya kisasa sana kupita maelezo, bibie huku akiendelea kutoa machozi aliufungua mdomo wake kwa mara ya kwanza.

“nilivyokupata wewe niliamini nimepata mume wa maisha yangu ndio sababu nilikupatia upendo wangu wote, nilitamani niwe mwanamke wa kipekee sana wa kuweza kuyatibu maradhi ya moyo wako ili popote uendapo uwe unaniona mimi tu, haya yote niliyafanya kwa zaidi ya asilimia mia moja lakini hizi ndoto zangu zilikuja kuyeyushwa na baba yangu aitwae Haruto Hinata Haru, mzee wangu hajanizaa yeye lakini ndiye baba ninaye mtambua hapa duniani kwangu, ananipa kila nacho kihitaji kwa muda wowote ule hata kiwe na gharama kiasi gani, ni mzazi wa kipekee sana kwangu kwahiyo huwa nina msikiliza kuliko ninavyo msikiliza binadamu yeyote yule. Miaka mitatu iliyopita siku moja nikiwa npo chuo nakumbuka tulipanga usiku ule mimi nawewe tutoke pamoja na tukalale huko pamoja, huo ndio usiku ulio nifanya nikaishi kwa kuulaumu sana moyo wangu, baba yangu ni jasusi mkubwa sana ambaye anatafutwa kila kona ya dunia ili viongozi wakubwa wamtumie kwa manufaa yao nayeye amekuwa akikipinga sana hicho kitu na ndio sababu ya kunileta mimi kuja kusoma Tanzania ambako ndiko niliko kuja kukutana nawewe.

Siku ile majira ya jioni nikiwa naelekea kujiandaa ili nije kuonana nawewe wakati natoka tu nje ya chuo nilishangaa namuona baba kwenye gari akionekana kunisubiri kwa hamu sana, nilishtuka na niliogopa mno kwani haikuwa kawaida yeye kutoka Japan na kuja Tanzania bila kunambia kwahiyo nilihisi huenda kutakuwa kuna tatizo. Nilipanda kwenye gari na kuondoka naye mahali pale mpaka kwenye hii nyumba ambayo kwa wakati ule kwangu ilikuwa ni ngeni kabisa na sikujua kanileta kufanya nini.

“dady tunafanya nini hapa na kwanini umekuja Tanzania ghafla sana namna hii?” nilimuuliza kwa mshangao kwa sababu nilikuwa naogopa sana moyoni

“im sorry my daughter I have to do this” (samahani binti yangu lazima nifanye hivi). Nadhani unaelewa ni kazi gani nilikuwa nazifanya ndio sababu ya kukuleta Tanzania kwa kigezo cha kudai umekuja kusoma wakati tayari wewe ni msomi mkubwa tu, kwa hali ya kawaida inaweza kuwa kama kitu cha kushangaza kukuleta huku lakini niliona ndiyo sehemu sahihi sana yawewe kuweza kuishi kwa amani kumbuka wewe ndio tumaini langu la pekee kabisa kwenye maisha yangu.

“ndiyo baba hilo najua lakini bado hujanijibu swali langu vizuri, kwanini umekuja ghafla hivi

“nahitaji kuanzia leo usiendelee na chuo tena” alinijibu kiufupi mzee wangu.

“kwanini imekuwa ghafla hivi?” niliuliza huku nikiwa nimehamaki

“sogea binti yangu(akiwa ananikumbatia), dunia ya sasa imebadilika sana mwanangu kila mtu anajali maslahi yake tu bila kujali kuhusu usalama wa watu wengine, mimi ninatafutwa sana kuliko hata pesa inavyo tafutwa, sio kwamba nina makosa mpaka nitafutwe hapana lakini kuna baadhi ya watu wanahitaji wanipate ili wanitumie kujinufaisha kitu ambacho siwezi kukifanya kwa sababu naweza nikayaumiza maisha ya watu wengi sana wasiokuwa na hatia yoyote ile. Kuna walinzi wa siri sana ambao nimewaweka ili waweze kuhakikisha usalama wako popote pale unapokuwepo, hawa watu wameanza kuona dalili za baadhi ya watu kutaka kukuchunguza ili wakujue kiundani sasa hicho ni kitu cha hatari mno kwa sababu kama wakikujua tu watakutumia wewe kama ngao yamimi kuwafanyia kazi zao kiwepesi sana, na pia nimepata taarifa umenitafutia mkwe(Baba akitabasamu) nimemuona ni kijana mzuri sana lakini kuanzia leo yule kijana haupaswi kumuona tena mwanangu” mzee wangu aliongea yale maneno kiwepesi kupita kiasi bila hata kuwaza kama mimi ningeyachukulia vipi.

“sitaki kujua umejua jua vipi, ila suala la kuacha kumuona huyo mwanaume mimi siwezi nampenda sana” nililia sana mbele ya baba yangu huyu wa kunilea.

*****************************************
“huyo kijana kama utaendelea kumuona basi mapema sana anaenda kupotea kwenye uso wa dunia kwa sababu ukigundulika tu wataanza kwanza na watu wako wa karibu na mtu wako wa karibu sana hapa Tanzani ni huyo mpenzi wako pamoja na familia yake hao ndio watapata matatizo makubwa sana kwa ajili yako, mimi sikulazimishi juu ya hilo na najua ni kiasi gani unavyo jisikia kukaa mbali na huyo mtu unaye mpenda ila kama unampenda kweli unaweza kumlinda kwa kufanya hivyo” hayo maneno ya baba yangu kilikuwa kama kisu kikali sana kilichokuwa kikiuchoma moyo wangu vibaya sana, nililia na kuumia sana lakini hiyo haikubadilisha uhalisia kwamba mimi sikupaswa kuja kukuona tena. maisha yangu ya shida yalianzia hapo kazi yangu ikawa ni kucheza na komputa tu ndani na ndicho kitu nilicho kisomea tangu nikiwa binti mdogo kwahiyo naijua komputa kuliko hata navyo lijua jina langu. Jackline alimaliza stori yake iliyo mfanya akae mbali na mwanaume huyo kwa zaidi ya miaka mitatu huku akiwa analia kwa hisia sana. Calvin alinyanyuka alipokuwa amekaa kisha akamfuata Jackline na kumkumbatia kwa hisia kubwa sana.

“nimekusubiri kwa miaka mitatu sasa lakini moyo wangu haukukata tamaa, nilijaribu kukusahau japo niyaanze maisha ya furaha lakini nilishindwa, miaka miwili iliyopita niliwapoteza wazazi wangu wote wawili ambao waliuawa kikatili sana, ule ndio muda ambao nilikuwa natamani sana uwepo wako kuliko wakati wowote ule kwenye maisha yangu ila ulikuwa mbali sana kiasi kwamba usingeweza hata kusikia kilio changu, nilikuwa mpweke sana, nimepitia wakati mgumu sana kumbe malikia wangu upo huku” Calvin aliongea kwa hisia sana huku akimkumbatia tena mwanamke wake huyo.

“pole sana mume wangu” walikumbatiana kwa furaha sana utadhani ni watu ambao siku zao zote walikuwa pamoja, mapenzi huwa ni matamu sana pale wapendanao wanapo amua kuzipotezea kabisa tofauti zao na kuziacha hisia za mapenzi ziongee kwa niaba ya mioyo yao, hakuna mwanaume mkorofi mbele ya mwanamke mnyenyekevu, ni maneno ambayo niliwahi kuambiwa na babu yangu siku moja wakati nipo chumbani kwake tukiwa tunapata mtindi safi sana na ndicho kilichokuwa kinatokea kwa wawili hawa aliamini mwanamke huyu kwa sasa anaenda kuichukua nafasi ya mama yake kwake. Ikawabidi wakae chini sasa Calvin akamsimulia kila kitu kuanzia siku ya kwanza ya matatizo yake, jinsi alivyoweza kusaidiwa na master Haru mpaka anarudi Tanzania kwa mara nyingine tena.

“baba yangu umejuana naye vipi?” Jackline alishangaa sana mtu huyo kusema aliye msaidia ni baba yake

“mimi mwenyewe sikuwahi kumjua kabla mpaka siku niliyokuja kukutana naye na akanielezea uhalisia wote, huyo baba yako ni rafiki wa baba yangu wa miaka mingi sana kabla hata baba yangu hajaweza kuwa na familia, na waliwekeana ahadi kwamba kama kuna kitu kitatokea basi yeye ndiye mtu ambaye atanipa uangalizi ndio maana mzee wangu kauli yake ya mwisho alinitaka niende kwa mtu huyu kuweza kupata msaada, amefanya kazi kubwa sana ya kunitengeneza kwa sasa nimekuwa moja ya viumbe hatari sana kuweza kuishi kwenye uso wa dunia ninapo amua kubadilika”. Calvin aliielezea stori yale

(kumbe ndio maana baba alinitaka nikae mbali na mtu huyu kwa kuogopa angepata matatizo ina maana anamjua tangu zamani sana) bibie alikuwa anajiwazia kichwani pekeyake kisha akauliza “
“usiniambie haya mauaji nayo sikia watu wanauawa kikatili sana niwewe ndo unahusika na yote”

“sina namna ya kufanya nimeshakula kiapo kwa yeyote aliye husika na haya hatopona mtu ndipo nitakapo weza kupumzika kwa amani nje na hivyo ni bora nife mimi” mwanaume alijibu kwa ujasiri sana lakini kitu hicho kiliweza kumuumiza sana Jackline kuona mtu aliyekuwa akimpenda hajali chochote kuhusu maisha yake.

“unaweza kuacha hili lipite ili tuende mbali na hapa tukaishi wote?” Jackline aliongea huku akiwa amejikatia tamaa kufuatia kauli ya mwanaume aliyo itamka mwanzo lakini alipigwa jicho kali ambalo hata yeye mwenyewe alijishitukia na kuangalia pembeni.

“nilikula kiapo mbele ya miili ya wazazi wangu, hata mwalimu wangu alinipa baraka zake, ningeweza kuachana na hilo kama tu nisingeutumia upanga ule nilio kabidhiwa lakini bahati mbaya sana ule upanga ulishaonja damu hivyo haiwezekani kabisa kuacha hiki kitu ni labda kiishe au mimi ndiye nife vinginevyo damu itamwagika sana” Calvin alijibu huku akimrushia mrembo huyo frash kwani mwanaume alikuwa siriasi sana baada ya mrembo huyo kujaribu kumshawishi aache hicho kitu alichokuwa anaendelea nacho, Jackline hakuwa mbishi alimchukua Calvin wakaenda kwenye chumba chake kikubwa cha kulala alibonyeza bembeni mwa kitanda na kuweka nywila zilizokuwa zinabadilika kwa kasi sana pamoja na kutumia jicho lake, chini palifunguka na kulikuwa na ngazi za kushuka chini Calvin alibaki ametoa macho kwa hali aloyo iona hapo ilimfanya amheshimu mwanamke huyu kwani hakuwa wa kawaida kama yeye alivyokuwa akimchukulia. Walifika chini kabisa na juu palijifunga, mbele yao kulikuwa na chumba kikubwa kilicho kuwa kama maabara nzuri sana lakini ndani yake kulikuwa na makomputa ya kisasa mno, Jackline alibonyeza kwenye kioo kimoja na komputa zote zikawaka ikiwemo kubwa moja ambayo ndiyo ilikuwa ikitumika kuongozea zingine.

Ukurasa wa 36 unafika mwisho kalamu yangu haina wino kwa Leo inshanlah tukutane wakati ujao.

Chao[emoji2768]

Bux the story teller

#ULIMWENGUWAWATUWABAYA

Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
Tunashukuru sana Febian kwa simulizi kali ya kusisimua mungu akubariki
 
Back
Top Bottom