Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
KatutelekezaWe CK imekuwaje tenaaa
IPO vizuri11
“ kama mpo tayari basi tunaweza kuondoka nadhani mama mtu atakuwa anasubiri kwa hamu huko” alisema yule mama ambaye wakati wote alikuwa kimya.
“Sisi tumefurahi kumuona baba mzazi wa Angel” isaka hatimaye alisema.
Ilibidi nisogee pembeni na Angel ili kujua ratiba zikoje maana tayari hali ilishaanza kuwa tete
“Jimmy kwa mila za kwetu, hamuwezi kuja kwenye sherehe ya nyumbani, mzee wangu ni mtata sana, hapa kwenyewe amekubali kukusalimia kwasababu ya yule anti pale…”
“Angel, nimekuandalia sherehe sehemu pia , umeona nimekuja na “watu” kwa ajili yako D” nilimkatisha
“hapo ndio unakosea dear, hii ni siku kubwa sana kwangu unadhani wazazi wangu watakubali kirahisi hivyo hii siku ichukuliwe na mtu mwingine?”
Nielewe dear, niruhusu leo wazee wafurahi then soon nakuja Dar kwa ajili yako unifanye utakavyo!
Alisema angel huku akirudi nyuma taratibu kuelekea kule walipokuwepo wazee
“haya wifi, SHEM ISAKA, tutawasiliana ngoja sisi tywahi huko maana bi mkubwa keshaanza kusumbua” alisema Angel na kisha tukapeana mikono na wale wazee wakaingia kwenye gari moja ya kifahari iliyokuwepo mbele yao kisha wakaondoka!
“KAKA HII FAMILIA HII hahahahah! ” alisema dada yangu JENI huku akiangua kicheko
Basi hatukua na jinsi isipokuwa kucheka tu!
“aisee mbona kama MAJINI!” Grace alisema na sasa tukazidi kuangua kicheko,
Nami kukoleza zaidi nikatoa ile pete na sasa kila mtu akacheka mpaka watu wakaanza kutushangaa
“hey kumbukeni kuna ukumbi na vyakula kule tumetoa hela!” hatimaye ISAKA alisema
Na hapo nikawa kama nimekumbuka ,
Kwakuwa bado shughuli zilikuwa zinaendelea kule ndani niliwaomba wanipe dakika kadhaa na mimi nikarudi kule ndani mbio..
Niliangaza huko na huko kutafuta ambacho nilikuwa natafuta! Baada ya kuona nakosa wazo lilinijia na kuingia ndani kabisa ya chuo kule ukumbini ambapo wahitimu walikuwa wamekaa
Niliingia na kukuta wengine wakiwa wanaendelea kupiga picha kwenye mabango mbali mbali , wengine wakiwa wanatoka na baadhi wakiwa wanachati na simu zao..
Haraka niliruka mpaka alipokuwa MC wa ile shughuli nilimnong’oneza sikioni kwa dakika kadhaa kisha akaniruhusu kuchukua kipaza sauti! Tayari niliashaanza kutengeneza hali Fulani tulivu pale ndani kwani hata wale ambao walikuwa wanatoka walisimama kwanza kusilikizia tangazo gani linakuja..
“mabibi na mabwana!
Naitwa Jimmy John Lukas! Nilianza huku nikiwa sijui nasema nini,
“Niko hapa kufurahi na ninyi hivi leo! Hongereni sana kuhitimu! Niko hapa kushare hadithi fupi kuhusu Maisha yangu mimi binafsi na kwanini nimechukua kipaza sauti hiki sasa!
Mwaka 2016 nilikuwa mhitimu wa chuo kikuu , katika nchi mojawapo ya afrika mashariki, wazazi wangu hawakuwa na kipato kikubwa cha kuweza kusafiri kuja katika mahafali yangu, kwa hivi siku ile wakati wenzangu wanashangilia na kuruka ruka na wazazi wangu na ndugu zao mimi nilikuwa peke yanu kwenye pembe moja ya ukumbi nikilia!
Kwahiyo naamini leo kati yenu hapa kuna mtu mmoja au wawili ambaye anapitia hali hiyo leo, nimekuja kumtia moyo! Pengine mwingine hana wazazi kabisa kwa maana sio inshu ya kipato kama ilivyokuwa kwangu, lakini ni kwamba hawezi kabisa kufika, kwa maana hata iweje hawawezi kuwa hapa,
Lakini kuna wale ambao ni inshu ya kipato wameshindwa kufika…
Wakati naendelea na hotuba yangu niliona akina ISAKA wakiingia na sasa walikuwa wamepigwa na mshangao kuniona nahutubia pale “bila sababu za msingi”
“kwahiyo mimi na rafiki zangu tumeandaa kitu kidogo cha kufurahi na watu kama hao siku ya leo,
Ndugu zangu kama hamtajali tunaomba watu watano ambao kwa namna moja ama nyingine hawana ndugu au wazazi au rafiki wa kufurahi nao kwenye siku hii muhimu basi naomba tufuatane nasi sasa” nilisema huku nikiinamisha kichwa kwa staili ya kutoa heshima kwa kijapani.
Na sasa ukumbi mzima walipiga makofi na kushangilia,
“waoo that’s my brother” alisema Isaka huku akinipongeza
Ni kweli walisogea pale tulipokuwepo wadada watatu na mvulana mmoja na badala ya watano walikuwa wanne!
Tulisalimiana nao huku tukiwapa maneno ya Faraja na kisha tukafuata hatua zote muhimu ikiwemo kuacha nakala ya vitambulisho vyetu kwa uongozi wa chuo kisha tukaondoka nao!
Tulifika sehemu ambayo tayari ilikuwa imeandaliwa maalum kwa ajili ya “angel” lakini ikapata “ANGELS” wengine
Kwahiyo tukapata chakula kizuri na hakika kila mmoja wetu alifurahia na kusahau lile Sakata la Angel kwa muda
“sasa tunawaachaje hawa madogo” ISAKA aliuliza
“nadhani tukisema tuwasikilize story zao tutakesha hapa” nilisema
Hivyo tulitoa maneno kadhaa ya kuwashukuru kwa kukubali mualikowetu na wao walifurahi sana hakika siku yao ilikuwa imekwenda vizuri kabisa,
Baada ya kumaliza harakati zote siku ile tulipumzika kisha kesho yake tukaianza safari ya kurudi dar!