Hadithi ya Del Piero na Totti kuhusu jezi namba 10

Hadithi ya Del Piero na Totti kuhusu jezi namba 10

Gang Chomba

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Posts
20,649
Reaction score
4,786
Ilikuwa Kabla ya Kombe la Dunia Mwaka 2002 kule Korea na Japan, pale Del Piero alipokuwa akivaa Jezi namba 10 huku Totti akiwa anavaa namba 20.

Siku moja baada ya mazoezi ya nguvu huku kila Mchezaji akiwa full kwa ajili ya kulitumikia Taifa, wachezaji waliitwa waliitwa ili wachague namba za Jezi zao Mgongoni na Pajani kabla ya kwenda kupata Mlo wa Mchana.

Kila Mmoja alikwenda kasoro Simba Dume Mwamba Paolo Maldini ambae jezi nambari 3 ilikuwa maalum kwa ajili yake na hakukuwa na Mtu alieitaka kwa wakati huo.

Basi kila mmoja alichagua namba yake lakini kwa mshtuko zaidi Totti alikwenda mbele ya rafiki yake kipenzi na kumwambia “AISEE KUANZIA LEO NATAKA KUVAA JEZI NAMBARI 10 NA HAITOKUWA YAKO TENA”.

Lakini pasipo dhaniwa na kila Mmoja Del Piero alijibu na kumwambia “HONGERA, MIMI SIJALI KUHUSU NAMBA, ILA NINACHO JALI NI KUMALIZA MAZOEZI HARAKA NA KWENDA KUPATA MLO ILI KUIMARISHA AFYA YANGU KISHA KWENDA PUMZIKA NA YULE MREMBO”
Baada ya Jibu hilo Totti alikunja sura na kisha akaichukua ile Jezi na kuondoka kabisa eneo hilo kiasi kila aliekuwepo hapo aliangua kicheko.

Wawili hawa walikuwa marafiki wakubwa lakini hawakuwahi kucheza Milan.
Story zaidi zina tanabaisha kwamba kuna muda katika urafiki wao Totti alikuwa na kinyongo na Del Piero kwa kuwa mwenzie alikuwa na Nyota zaidi na warembo wakali wa Kitaliano na Duniani kwa ujumla.

@acmilan_swahili

a1f5d313-cc6b-40dc-91b8-21948842a8bc.jpeg
 
Del piero aliwahi kufunga magoli 3 ndani ya dakika 3 tena zile za nyongeza na aliingia wakati huo huo wa lala salama akitokea benchi akaikoa timu yake kwenye mtoano

Ila mechi iliyofuata park ji sung akawalaza na viatu wataliano kwa kuwapa kichapo wakawa wametoka kwenye mashindano wakati huo park alikuwa anacjezea klabu ya huko italia ligi ya serie A akafukuzwa kazi usiku huo huo

Ni kumbu kumbu zangu mwaka 2002 sijui zipo sawa
 
Aliefukuzwa kazi alikuwa anaitwa Anh
 
Back
Top Bottom