WISDOM SEEDS
JF-Expert Member
- Jun 1, 2011
- 841
- 282
TURUFU YA MWISHO
Aliporejea Tanzania baada ya kuwa nje kwa miaka saba, alikuwa na matumaini makubwa ya kumkuta mdogo wake Celine akiendelea vyema na masomo. Hakuamini baada ya kugundua alichofanyiwa Celine ambacho kilimuweka katika hatari ya kifo. Licha ya kupambana kumwokoa, akajikuta katikati ya machozi na vipingamizi vingi. Pamoja na vitimbi vya kila aina na matukio yaliyohatarisha maisha yake, aliamua kurusha TURUFU YA MWISHO.
Imeandikwa na Hamisi Kibari, mtunzi wa riwaya na mashairi. Halikadhalika ni mwandishi wa habari mkongwe nchini. Kwa kipindi cha takribani miaka 20, amekuwa akiandika hadithi katika magazeti mbalimbali na baadhi kutumika katika filamu. Baadhi ya riwaya alizoandika ni pamoja na Sihusiki ambayo kitabu chake kipo madukani; Gerezala Kifo; Kizazaa cha Safia; Isiwe Nongwa; Machozi ya Suzana; Mtoto wa RPC; Nkurukumbi na Mzimu wa Annelisa.
SASA ENDELEA
BAADA ya kuweka mizigo yake sawia kwenye hoteli aliyofikia katikati ya mji wa Dodoma, masanduku mawili makubwa na begi, Marina alitoka akiwa na mkoba wake mdogo tayari kumtafuta rafiki yake kipenzi, Stella. Huyu ni mmoja wa watu wawili aliokuwa akiwaza sana njia nzima kukutana nao tangu alipoanza safari ya kutoka New York, Marekani kuja Tanzania, wa kwanza akiwa mdogo wake.
Kwa vile hakuwa na haja ya kujimwagia maji wala kula kwa sababu alikuwa ameshiba, hakuona sababu ya kuchelewa kumtafuta Stella. Alitoka nje na kusimama kwa muda akishangaa mabadiliko makubwa yaliyokuwa yamefikiwa katika mji wa Dodoma. Aliita teksi pale nje ya hoteli alikofikia na kumtaka dereva ampeleke mtaa wa Makole.
Miaka saba ni mingi, lakini aliamini hata kama Stella atakuwa amehama anaweza kupata taarifa zake kwenye nyumba aliyomwacha akiishi, pale Makole, nyumba ambayo hata yeye alipata kuishi pia. Pamoja na mabadiliko ya mji aliyoyaona toka amewasili Dodoma, maeneo ya katikati ya mji yalikuwa hayajabadilika sana kiasi cha kumpoteza.
Baada ya kutua na ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma mchana huo akitoka Dar es Salaam alikolala kwa siku moja akitokea Marekani, Marina hakupanga kwenda kijijini kwao, Mtakuja, Mayamaya, siku hiyo hiyo ili kupata muda wa kuongea na rafiki yake, Stella.
Pamoja na shauku kubwa aliyokuwa nayo ya kumwona mdogo wake, Marina alitaka jioni hiyo na hata siku ya pili yake ikiwezekana kuwa na rafiki yake kipenzi, Stella, wakiongea mengi na kukumbushana ya zamani baada ya kuachana kwa muda mrefu. Alitaka pia ajue anachokifanya kwa sasa na kuona namna ya kumsaidia. Mambo mengi yalikuwa kichwani mwake kuhusu namna ya kumsaidia Stella kama angemkuta kama alivyomwacha; je amfungulie duka la vipodozi, mgahawa, saluni ya kisasa ama chochote atakachotaka alimradi mtaji wake usiwe unavuka shilingi milioni 15.
Naam, hatimaye teksi ilisimama kwenye nyumba aliyomwelekeza dereva. Akashuka, akamlipa dereva ujira wake na kuchukua namba yake ya simu. "Nitakupigia uje unichukue unirudishe pale uliponitoa ama kunipeleka kwingine nikishamaliza mazungumzo yangu hapa... No, hebu tafadhali nisuburi kwanza pengine ninayemfuata hapa akawa keshahama."
"Hamna taabu sister, isipokuwa ukumbuke nitakuchaji kidogo gharama za kusubiria," akasema dereva. Bila shaka mwonekano wa binti huyo mrembo, pochi yake pamoja na mavazi yake nadhifu, suti ya kike ya rangi ya kahawia, viatu ambavyo dereva huyo alikuwa hajawahi kuviona na hata hoteli alimotokea vilionesha kwamba hawezi kukosa pesa ya kumwongezea kwa ajili ya kumsubiri. Kwa hakika mtu aliyemwona miaka saba iliyopita asingeweza kumtambua kwa jinsi alivyokuwa amebadilika.
"Usiwe na wasiwasi kaka," alijibu Marina akigeuka kujongea kwenye mlango wa nyumba ya kizamani iliyokuwa imesimama mbele yake, nyumba ambayo takribani miaka saba au minane iliyopita aliishi akiwa na Stella.
Pale nje kwenye msingi wa nyumba hiyo hakukuwa na watu tofauti na alivyozoea zamani. Ilikuwa ni kawaida muda kama huo wa baada ya chakula cha mchana kwa kaya nyingi, mama mwenye nyumba na mabinti zake kukaa hadi baadhi yao watakapoanza matayarisho ya chakula cha usiku. Hata ile stuli aliyozoea kuiona mbele ya nyumba hiyo ikiwa na sinia la karanga alizokuwa akikaanga mama mwenye nyumba haikuwepo.
Marina aligonga mlango. Baada ya muda mlango ukafunguliwa. Alikuwa ni mama mwenye nyumba aliyekuja kufungua.
"Shikamoo mama. Habari za masiku," alisalimia Marina akiachia tabasamu ikiwa ni mara ya kwanza kumwona mtu anayemfahamu tangu arejee Tanzania. Yule mama aliitikia huku akimwangalia usoni akitafakari yule ni nani. Marina akaona amwache tu yule dereva aondoke kwa sababu hata kama Stella alishahama nyumba hiyo alihitaji kuzungumza mawili matatu na mama huyo.
“Samahani kidogo mama. Nashukuru nimekukuta, ngoja kwanza nimuage huyu dereva,” alisema akigeuka kumfuata dereva teksi, akamwambia aondoke na kwamba atampigia simu baada ya kumaliza kilichomleta katika nyumba hiyo.
“Karibu ndani mwanangu,” alisema mwanamke yule mtu mzima, Khadija binti Zubeir maarufu pale mtaani kama Mama Siwema, bado akijiuliza ni wapi alipomwona binti huyo mrembo.
Wakaongozana hadi sebuleni kwake, sebule ambayo Marina aligundua kwamba ilikuwa imezidi kuchakaa na hakuna kilichokuwa kimeongezeka. Mama yule mjane wa miaka takribani 15 akamkaribisha aketi kwenye kochi mojawapo lililokuwa na afadhali kidogo. Mengine yalikuwa yamechanika, sponji zake zikiwa nje huku lile kochi kubwa likiwa limevunjika.
Kulikuwa na meza kuukuu pembeni kidogo mwa sebule hiyo ambayo bila shaka ilitengenezwa kwa ajili ya kulia lakini ilikuwa haitumiki kwa ajili hiyo badala yake ilijaa makorokoro kibao.
"Hebu nikumbushe binti. Sura inaniijia halafu inatoka."
"Mama umenisahau?"
"Yaani... uzee mwanangu. Ninajitahidi kukukumbuka bila mafanikio."
"Haiwezekani Mama Siwema."
"Kweli nimekusahau, macho nayo siku hizi sioni vizuri."
"Ulishapima macho ili wakupe miwani?"
"Bado mwanangu, pesa nitapata wapi miye."
"Basi nitakupa pesa, kesho ukapime. Siku nikija tena utaniambia gharama za miwani," alisema akitoa shilingi 30,000 na kumpatia.
"Nashukuru sana mwanangu."
"Mimi ni Marina, rafiki yake Stella mpangaji wako."
"Ah! Marina, umebadilika sana. Umependeza. Kweli Ulaya si mchezo. Nasikia uliolewa Ulaya eh!"
"Si Ulaya, ni Marekani mama."
"Ndo huko huko... Haya hebu niambie kuna habari gani mpya?"
"Hakuna jipya. Nimefika leo nikaona niwasalimie. Kwa kweli nimewakumbuka sana na nimefurahi sana kukuona."
"Kweli ni siku nyingi. Miaka 10 sasa eh?"
"Siyo 10, ni miaka saba tu."
"Hata hiyo mingi mwanangu."
"Yeah, vipi Stella, bado anaishi hapa?"
"Mh...." aliguna mama yule na kuinama huku uso wake ukibadilika. Alisita kidogo, akakohoa kisha akanyanyua tena uso. "Rafiki yako Stella hatunaye tena duniani. Alifariki dunia mwaka juzi... Lakini hadi anafariki alikuwa keshahama hapa. Alikuwa anaishi Kizota."
Maneno yale yalimkata Marina moyoni mithili ya upanga mkali. Akajikuta anabubujikwa na machozi ghafla licha ya kuyazuia bila mafanikio kiasi cha Mama Siwema kuanza kibarua cha kumbembeleza ili kunyamaza.
Baada ya kutulia Mama Siwema hakutaka kumficha. Akamwambia kwamba rafiki yake alifariki dunia baada ya kuugua ugonjwa aliouita wa 'kisasa'.
"Lakini yule kilichomuua ni kutofuata masharti na uoga wa kupima. Unajua alianza kuugua hapa akaonesha kila dalili. Aliugua Kifua Kikuu na baadaye mkanda wa jeshi. Lakini mbishi wa kwenda hospitali, msiri na hataki kuwa muwazi. Mimi kama mtu mzima nilimwita, nikamweleza awaone watalaamu badala ya kudai anarogwa na wenzake na kuanza kwenda kwa waganga wa jadi lakini mwanangu wahenga walisema kweli, sikio la kufa halisikii dawa. Hakunisikia," akasema Mama Siwema.
Akazidi kumwambia kwamba mke wa mdogo wake ambaye ni marehemu anaishi na ugonjwa huo kwa takriban miaka 15 sasa lakini ana afya njema na wala ukimwona huwezi kuamini kwamba ana tatizo hilo kwa sababu anafuata masharti na si msiri.
“Mdogo wangu ambaye ndiye alimletea huu ugonjwa alishakufa miaka mingi hata kabla rafiki yako hajaja kupanga hapa kwangu. Naye alikuwa kama huyo rafiki yako, anaogopa kupima na kuwa muwazi. Lakini wifi ni muwazi, hana wasiwasi na ndio maana huwezi kujua kwamba anaishi na huu ugonjwa mpaka akwambie au uambiwe. Na siku hizi kaolewa na mwenzake anayeishi na ugonjwa huo. Maisha yao mazuri kabisa.”
Inaendelea

Mh! Hatunaye tena duniani