Hadithi ya pasaka

Hadithi ya pasaka

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
HADITHI YA PASAKA
KISA CHA YAHUDI JUDAH BEN HUR NA MRUMI MESSALA KATIKA MOVIE ‘’BEN HUR’’ THE STORY OF CHRIST

Mwandishi wa kitabu Ben Hur Lew Wallace alikuwa askari wa cheo cha juu katika jeshi la Unionists wakati wa American Civil War na aliandika kitabu hiki miaka hiyo ya 1860s

KItabu hiki kikapata umaarufu mkubwa pale kilipotengenezwa movie katika miaka ya mwishoni 1950s na wachezaji wake wakiwa waigizaji mabingwa wa nyakati hizo, Charlton Heston (Judah) na Steven Boyd (Messala) na wengineo

Lakini kivutio kikubwa katika movie hiyo ni kule kuwako kwa Yesu katika historia ya maisha ya Judah Ben Hur na Messala.

Marafiki wawili walikuja kugeuka kuwa maadui kwa sababu ya mmoja kuwa mtawala dhalimu na mwingine mtawaliwa asiye na sauti katika nchi yake mwenyewe.

Ndani ya movie hii kuna ‘’scenes,’’ nyingi nzuri za kumtuliza mtu kwenye kiti cha senema asitake hata kwenda msalani.

Mfano Judah Ben Hur, kijana kutoka ukoo tajiri na uliotukuka wa Kiyahudi akikamatwa kwa kosa ambalo hakufanya la kumtupia jiwe Emperor wa Rome na kuhukumiwa kwenda kutumika kama mtumwa katika manowari za vita za Kirumi akiwa mpiga makasia.

Scene nyingine ni kuzama kwa manowari aliyokuwamo Judah Ben Hur katika vita kati ya Warumi na Waajemi ambayo yeye alikuwa mtumwa mpiga makasia.

Kuokoka kwake na kumuokoa jemadari aliyekuwa ndani ya manowari ile.

Kuachiwa huru na safari yake kutoka Pwani ya Bahari ya Mediterranean na kurudi nchi kwake Palestine.

Mashidano ya mbio za magari ya farasi yaliyoshirikisha nchi zote za ulimwengu ule pamoja na Rome Judah Ben Hur akiwa mwakilisha wa nchi yake akishindana na Jemadari wa Majeshi ya Rome ndani ya Palestine.

Scene hii inajulikana kwa jina maarufu la ‘’Chariot Race.’’

Wanasema ilichukua miezi kadhaa kuipiga hadi kuipatia lakini katika movie inaonekana kwa dakika labda kama kumi hivi.

Hizi zote ni scene zilizotengenezwa kwa ufundi na ustadi mkubwa.
Lakini scene maarufu sana ziko tatu.

Ya kwanza wakati wakati Judah Ben Hur mtumwa yuko njiani katika msafara wa watumwa anakwenda utumwani.

Msafara ukapita nje ya nyumba ya Joseph wa Nazareth na mwanae Yesu fundi seremala yuko barazani anafanya kazi yake ya userelama.

Judah Ben Hur ameshikwa na kiu jua kali katika nchi ile ya jangwa anagombea maji na wenzake Yesu akiangalia kutoka kivuli cha nyumba yao.

Askari wa Kirumi anayamwaga maji huku anatembeza mjeledi wake kwenye migongo ya wale watumwa.

Yesu kijana mdogo labda wa miaka 17 hivi anachukua maji anapiga hatua kumwendea Judah Ben Hur amwenyeshe.

Askari wa Kirumi anachomoa mjeledi wake anauvuta nyuma anaunyanyua kutaka kumpiga Yesu.

Uso mpole wa Yesu unatazamana na uso wa wa askari katili wa Kirumi aliyeshiba sawasawa na yuko katika mavazi ya vita.

Ghafla askari wa Kirumi nguvu zinamwishia anashusha chini mjeledi wake kibri na ukatili wake wote umeyayuka mithili ya theluji kwenye jua kali.

Yesu anamwinamia Judah Ben Hur na kumpa maji.

Hapo wangozaji senema wa Hollywood na wapiga picha wao hapo ndipo wanapotengeneza sifa zao.

Camera inakwenda kwa Judah Ben Hur kisha inakuja kwa Yesu kisha inakwenda kwa askari kwa utulivu wa aina yake.

Watia muziki wanatia muziki wa simanzi unasikia ‘’strings,’’ tupu zinalia kwa mbali kwa key za ''minor.''

Ujumbe unaotolewa hapo ni kuwa Judah Ben Hur ameihifadhi vizuri sura ya Yesu kichwai kwake.

Scene ya pili ni siku Yesu keshahukumiwa kusulubiwa anapelekwa Golgotha amebebeshwa jisalaba kubwa zito linamwelea anatembea kalibeba huku anapepesuka.

Wayahudi wamejipanga njia nzima wanamzomea na kumkejeli.

Shughuli za mji mzima zimesimama watu wamejipanga barabarani watoto kwa wakubwa zogo ni kubwa na kelele zisizo na kifani.

Judah Ben Hur anasikia kelele zile anatoka kuangalia kulikoni?
Anamwangalia mtu yule anaezomewa na huku kabeba msalaba mkubwa mzito haumudu uzito wake.

Anamwangalia vizuri.

Sura ile keshapata kuiona mahali ingawa ni miaka mingi nyuma.

Miaka imepita mingi lakini anaikumbuka sura ile ni yule kijana aliyempa maji Nazareth wakati anakwenda utumwani.

Hiki kipande kikiwatoa machozi wengi ndani ya kumbi za senema.

Tulikuwa enzi hizo za utoto tukienda senema na dada zetu.
Utasikia vilio vya chini chini.

Hapa waongozaji senema wanamaliza ufundi wao kwa kubadilisha ‘’angle’’ za camera na camera ipige nini.

Camera inakwenda kwenye msalaba kwenye bega la Yesu kisha inakwenda kwenye taji la miba alilovishwa kichwani.

Yesu anavuja damu usoni.
Camera ikitoka hapo inahamia kwenye sura ya Judah Ben Hur ambae ni Charlton Heston bingwa wa kuigiza.

Tunaweza tukakesha hapa.
Ngoja nihitimishe.

Judah Ben Hur anaingia chini ya msalaba pembeni ya Yesu anuchukua uzito wa msalaba kwenye mabega yake.

Hatua kwa hatua Wayahudi wawili, Yesu na Judah Ben Hur wanaubeba msalaba kuelekea Golgotha.

View attachment 1743579
 
Ben-Hur is a story of a fictional hero named Judah Ben-Hur, a Jewish nobleman who was falsely accused and convicted of an attempted assassination of the Roman governor of Judaea and consequently enslaved by the Romans. He becomes a successful charioteer.[4][5] The story's revenge plot becomes a story of compassion and forgiveness.[6]

The novel is divided into eight books, or parts, each with its own subchapters. Book one opens with the story of the three magi, who arrive in Bethlehem to hear the news of Christ’s birth. Readers meet the fictional character of Judah for the first time in book two, when his childhood friend Messala, also a fictional character, returns to Jerusalem as an ambitious commanding officer of the Roman legions. The teen-aged boys come to realize that they have changed and hold very different views and aspirations. When a loose tile is accidentally dislodged from the roof of Judah's house during a military parade and strikes the Roman governor, knocking him from his horse, Messala falsely accuses Judah of attempted assassination. Although Judah is not guilty and receives no trial, he is sent to the Roman galleys for life, his mother and sister are imprisoned in a Roman jail where they contract leprosy, and all the family property is confiscated. Judah first encounters Jesus, who offers him a drink of water and encouragement, as Judah is being marched to a galley to be a slave. Their lives continue to intersect as the story unfolds.[6]

In book three, Judah survives his ordeal as a galley slave through good fortune, which includes befriending and saving the commander of his ship, who later adopts him. Judah goes on to become a trained soldier and charioteer. In books four and five, Judah returns home to Jerusalem to seek revenge and redemption for his family.

After witnessing the Crucifixion, Judah recognizes that Christ's life stands for a goal quite different from revenge. Judah becomes Christian, inspired by love and the talk of keys to a kingdom greater than any on Earth. The novel concludes with Judah's decision to finance the Catacomb of San Calixto in Rome, where Christian martyrs are to be buried and venerated.[
 
Da...
Ahsante sana.
 
Aliyekufa ni Kristo sio Yesu

Yesu Kristo yu hai 🔥🔥🔥
 
Aliyekufa ni Kristo sio Yesu

Yesu Kristo yu hai 🔥🔥🔥
Yesu ni wengi ila Kristo ni mmoja so aliyekufa kwa ni yesu "wao' ila Yesu Kristo alikufa siku ya tatu akafufuka.
Mwandishi wa simulizi hii mzee Said kasahau kusema kwamba hichi ni kisa cha kubuni.. Kama nilivyoonyesha palw bolded
 
"Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani." Isaya 9:6

"18 Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho;
19 yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho.
20 Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu." 2Korintho5:18-20
 
Yesu ni wengi ila Kristo ni mmoja so aliyekufa kwa ni yesu "wao' ila Yesu Kristo alikufa siku ya tatu akafufuka.
Mwandishi wa simulizi hii mzee Said kasahau kusema kwamba hichi ni kisa cha kubuni.. Kama nilivyoonyesha palw bolded
Da...
Hii ni riwaya.
 
Back
Top Bottom