Hadithi ya Yona

Hadithi ya Yona

kweleakwelea

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2010
Posts
3,072
Reaction score
1,545
nakumbuka nilivyokuwa mdogo nilisoma hadithi ya Yona kwenye biblia...

ya kwamba alitumwa na Mungu akawafundishe watu wa nchi nyingine NINAWI neno lake kisha wakiri na wamrudie mola wao,,,,,

ya kwamba watubu maana walipitiliza kwa uovu..

yona kumbe bado anayapenda maisha....akatoroka vijana wa sasa hivi wanasema akalala mbele....akapanda meli aende mitaa mingine akayakoboe maisha.....that means alikuwa na dinari za kutosha.....alikozipata sijui...... maana shetani naye ana akili...mungu akiagiza ufanye jambo naye anajiinua hapo hapo.....

meli ilipokuwa safarini mara ikakubwa na gharika kuu.....ikawa vurumai karibu kuanguka..

yona akajikaza weeeee mwisho akaona hakuna namna ... maana walianza hojiana mle ndani kwani haikuwa kawaida...

yona mwishowe akashindwa kuvumilia ... akaishia kujitaja kuwa yeye ndio mleta shida kwani amelala mbele kinyume na agizo la mungu....

kisha wale mabaharia na watu kwene meli wakamtupa yona baharini na gharika ikaisha mara.....

watu wasio na makosa wakasalimika mara na safari ikaendelea wakafika salama...

yona akamezwa na samaki mkuuuubwa anaitwa changu.....ambaye alienda kumtapika kwenye ufukwe wa NINAWI...

YONA AKAMSHUKURU MUNGU,,,,,AKATII NENO NA AKAFANYA KAZI ALIYOTUMWA NA MUNGU...KUHUBIRI NENO LAKE NA KUWATAKA WAMTII NA KUTUBU DHAMBI ZAO..

na huo ndio mwisho wa hadithi yangu....

je hadithi hii inatufundisha nini?
 
Back
Top Bottom