Wizara ya Maji
Govt Institution
- Oct 2, 2024
- 34
- 20
Waziri Wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amesema ujenzi wa bwawa la Farkwa ni mpango kabambe wa Serikali kuondosha changamoto ya maji kwa wakazi wa jiji la Dodoma na maeneo jirani.
Amesema hayo mwishoni mwa wiki katika hafla ya kusaini mkataba wa ujenzi wa bwawa la Farkwa katika kijiji cha Bubutole kata ya Farkwa Wilaya Chemba mkoani Dodoma.
Gharama ya mradi ni shilingi bilioni 163.43 mpaka kukamilika kwake, uhaba wa wa maji Jijini Dodoma utaondoshwa, bwawa likiwa na uwezo wa kuhifadhi lita za ujazo zaidi ya billion 400.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri amesema kuwa mradi huo utahusisha ujenzi wa bwawa kuu lenye mita 1300, kimo cha mita 32, pamoja na bwawa dogo lenye urefu wa mita 1600 na kimo cha mita 15 Ili kuzuia upotevu wa Maji.
Bwawa hilo likikamilika litakuwa na uwezo wa kutoa maji mita za ujazo 7236 kwa siku, aidha kutakuwa na mtambo wa kutibu maji wenye uwezo wa kuzalisha maji kwa siku mita za ujazo 128,000.
Fursa kwa wananchi zitakuwepo lukuki, sio tu kupata maji pekee bali pia kufungua pazia kwa kazi ya ufugaji wa samaki kuongeza usalama wa chakula na kipato kwa wananchi.
Mradi huo unatekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mkandarasi akiwa kampuni ya China Jiang Chi International ya China na muda wa kazi ukiwa kipindi cha miezi 22. Kazi inatekelezwa kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).