Hafla ya Tuzo za Ballon d'Or Oktoba 26, 2026; Harry Kane ashinda tuzo ya Ballon d'Or

hydroxo

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2015
Posts
6,772
Reaction score
15,651
Mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani na timu ya taifa ya England, Harry Kane, ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or ya Mchezaji Bora wa Dunia kwa mwaka 2026, katika hafla iliyofanyika Oktoba 26, 2026.

Katika tuzo hizo, nyota wa klabu ya FC Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Lamine Yamal, ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Kiume wa Mwaka 2026
========
Usiku wa leo pale jiji la London nchini Uingereza katika ukumbi wa Palladium theatre kutafanyika shughuli ya ugawaji wa tuzo za Ballon d'Or.

Nafasi mbalimbali za tuzo hizo zinazogombaniwa na wachezaji waliofanya vizuri zaidi katika ngazi ya klabu na nchi zao ni kama ifuatavyo;

Mchezaji bora wa kiume wa mwaka(men's ballon d'or)

Hapa kuna mchuano mkali kati ya wachezaji wafuatao.

1.Harry Kane(Buryen Munich/England)

2.Kylian Mbappe(Real Madrid/France)

3.Lamine Yamal(Barcelona/Spain)

4.Erling Haaland(Manchester City/Norway)

5.Rodri(Barcelona/Spain)


Mchezaji bora wa kike wa mwaka(Ballon d'or Feminin)

Hapa kuna mchuano mkali kati ya;

1.Alexia Putellas(Barcelona/Spain

2.Ewa Pajor(Barcelona/Poland)

3.Melchie Dummornay(OL Lyoness/Haiti)


Mbali na tuzo hizo za mchezaji bora wa kiume na kike wa mwaka pia kutakuwa na tuzo nyingine zifuatazo.

1.Mchezaji bora kijana chini ya miaka 21(kopa trophy)

2.Kipa bora wa mwaka(Yashin trophy)

3.Tuzo za kocha bora wa mwaka(Johan Cruyff trophy)

4.Klabu bora ya mwaka,na

5.Mfungaji bora(Gerd Muller trophy)


Kwa upande wa ballon d'or ya wanaume na wanawake vigezo vikuu vitatu vinavyotumika kumpata mshindi ni;

1.Kiwango cha mchzaji binafsi na uwezo uwanjani (Individual Performance & Decisive Impact):

Kigezo hiki kinahusu uwezo wa mchezaji uwanjani, takwimu zake za mabao, asisti, kiwango cha mara kwa mara katika mechi zote alizocheza, na jinsi alivyokuwa na mchango wa moja kwa moja wa kuamua matokeo ya timu yake.


2.Mafanikio ya Timu na Vikombe (Team Trophies & Collective Achievements):

Kigezo hiki kinaangalia mataji aliyoshinda mchezaji akiwa na klabu yake kama vile Ligi ya Mabingwa Ulaya, ligi za ndani, au vikombe vya FA pamoja na timu yake ya taifa hususani michuano mikubwa kama Kombe la dunia .

3.Uchezaji wa Haki na Heshima ya Kitaaluma (Fair Play & Career Class):

Hiki kinahusu nidhamu ya mchezaji uwanjani na nje ya uwanja, tabia yake ya kuonyesha uchezaji wa kiungwana (fair play), kuheshimu sheria za mchezo, wapinzani, na waamuzi, jambo ambalo linajenga picha nzuri ya mfano wa kuigwa katika soka.

Je nani kuibuka mshindi leo?

Updates...
Jude Bellingham ameshika nafasi ya 11, akiongoza orodha ya wachezaji walio kwenye nafasi za 11 hadi 15 katika Ballon d’Or 2026.

📌 11. Jude Bellingham
📌 12. Pau Cubarsí
📌 13. Achraf Hakimi
📌 14. Vitinha
📌 15. Declan Rice

Huku majina makubwa yakisubiriwa kwenye Top 10, macho ya dunia ya soka yanaelekezwa London Palladium, ambako hafla ya Ballon d’Or 2026 inafanyika leo usiku.

Nani ataibuka na tuzo kubwa zaidi ya mchezaji bora wa dunia?
========
Nyota wa Klabu ya FC Barcelona na Timu ya Taifa ya Hispania, Lamine Yamal ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Kiume wa Mwaka 2026 katika tuzo za Ballon d’Or zinazofanyika leo, Oktoba 26, Jijini London, Uingereza.

Yamal ametwaa tuzo hiyo kwa mwaka wa tatu mfululizo, baada ya kushinda mwaka 2024, 2025 na sasa 2026, akiendelea kuonesha ubora wake katika soka licha ya umri wake mdogo.
===========
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Hispania, Luis de la Fuente, ametangazwa kuwa Kocha Bora wa Mwaka kwa upande wa Soka la Wanaume katika tuzo za Ballon d’Or 2026 zilizofanyika Oktoba 26, Jijini London, Uingereza.

​
================
Kipa wa Timu ya Taifa ya Hispania na Klabu ya Athletic Bilbao, Unai Simón ametangazwa kuwa Kipa Bora wa Mwaka 2026 kwa upande wa Soka la Wanaume katika tuzo za Ballon d’Or zilizofanyika Oktoba 26, 2026, Jijini London, Uingereza.
​
=========
Nyota wa Klabu ya Arsenal na Timu ya Taifa ya England, Bukayo Saka ametangazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Socrates katika hafla ya Ballon d’Or 2026 iliyofanyika Oktoba 26, 2026, Jijini London, Uingereza. Saka ametunukiwa tuzo hiyo kwa kutambua mchango wake katika Jamii kupitia shughuli za Kijamii na kuwa mfano bora nje ya uwanja wa soka.

Tuzo ya Socrates hutolewa kwa Mchezaji anayefanya mambo yenye manufaa kwa Jamii, ikiwemo kusaidia Watu wenye uhitaji, kuhamasisha usawa na kuonesha maadili mema nje
=========
Mshambuliaji wa Klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani na Timu ya Taifa ya England, Harry Kane ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or ya Mchezaji Bora wa Dunia kwa mwaka 2026.

Kane ametwaa tuzo hiyo katika hafla ya utoaji wa tuzo za Ballon d’Or 2026 iliyofanyika Oktoba 26, Jijini London, Uingereza. Ushindi huo ni wa kihistoria kwa Kane, ambaye ametwaa tuzo ya Ballon d’Or kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya soka, ikiwa ni hatua kubwa katika safari yake ya uchezaji.


Tupe maoni yako mdau.

secretarybird

Aleyn

Scars

Bufa

adriz

loose Nut

Kasongo yeeyee

​
 
Hizi tuzo tukiwa wakweli bila bias, ni tuzo ambazo zina ujanja ujanja sana na siasa nyingi ndani yake.

Mambo ya kibiashara (partnership kwa nominee) yana msukumo mkubwa kufanya upendeleo.

Nitakuja na hoja

Kama hii tuzo inaangalia zaidi performance ya last season katika michuano ya ndani na ya nje (club & national team)

Then kama ndio hivyo basi favourite wa kuwin hii tuzo alitakiwa kuonekana mapema.

Lakini kinachotokea ni kwamba graph ya namba za ushawishi za wachezaji ambao ni top kwenye nominee list zimekuwa zikipanda na kushuka kutokana na recently performance ya mchezaji husika.

Mfano kwenye games za mwanzoni za Laliga ambazo Lamine Yamal ali perform vizuri, chart ilionesha kuwa Lamine Yamal yupo juu ya Kylian Mbappe.



Na hata kampuni za Betting zilimpa odds ndogo Lamine Yamal ikiwa na maana yupo karibu zaidi kuchukua hii tuzo kuliko Mbappe ambaye kwa wakati huo alikuwa na odds 7

Lakini kufuatia Barcelona kupoteza games 2 in row, Yamal tayari kashuka nafasi 1 na nafasi yake imechukuliwa na Mbappe.

 
Naona hizi tuzo zimekuwa ngumu sana mwaka huu.

Pia kingine kukosekana extraordinary players like Messi na Ronaldo ambao ungeweza kuwapa bila kusita na watu wasikupigie kelele kunazidi kuifanya hii tuzo iwe ngumu sana kwa wanaume.

Ukiangalia uwezo na uchezaji wa wachezaji wengi unarandana hawapishani mbali sana.

Pia hata hiko kigezo cha makombe bado kunazidi kufanya mambo yawe magumu.

Mfano Kane hana world cup lakini ka win local trophies plus good performance.

Yamal kawin local Trophies na world cup lakini individually hayuko stable kama Kane yeye graph inapanda na kushuka.

Mbappe yeye hana local trophies lakini indivually kafanya vizuri zaidi.

Mfungaji bora UEFA,mfungaji bora La Liga na mfungaji bora World Cup.

Ukiangalia hapo mambo yanakuwa magumu sana kwenye kuamua.
 
Mimi nadhani tuzo inayomhusu mchezaji inatakiwa kuzingatia performance yake kama kipaumbele cha juu katika ugawaji tuzo.

Otherwise waongeze kipengele cha best team katika specific league au tournament ili kutenganisha kati ya mafanikio ya timu na mafanikio ya mchezaji.

Sasa mfano Mbappe yeye majukumu yake ya ufungaji anayetekeleza vizuri karibia kwenye kila mashindano aliyoshiriki amekuwa top scorer.

Then ubovu wa safu ya ulinzi wa timu yake kwenye kuruhusu mabao yanayofanya timu itolewe kwenye michuano, ubovu huo unaenda kumgharimu Mbappe kwenye individual award kwa hoja ya kwamba hajafanikiwa kuchukua kombe.
 
Vigezo sio indivudual performance pekee.

Ingekuwa iko ndio kigezo pekee no doubt angechukua.
Tafadhali elewa nilichokiandika hapo kabla.

Nilisema hivi;
If I had a chance to choose, I would have gone for Mbappe!
Ukauliza, kwa sababu gani Mbappe?

Nikakuambia kwa sababu ya individual performance.

Isivyo bahati, mimi si muhusika.

So, it's obviously known that individual performance isn't the only criteria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…