Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewatangazia wadau wa mpira wa miguu na umma kwa ujumla kuwa Hafla ya Tuzo za TFF 2025 itafanyika mwanzoni mwa mwezi Desemba.
Tarehe rasmi ya hafla hiyo, ambayo itatambua wanamichezo waliofanya vizuri katika maeneo mbalimbali kwa msimu wa 2024/2025, itatangazwa baada ya kukamilisha maandalizi yote muhimu, ikiwemo uteuzi wa ukumbi wa hafla.
Katika hafla hiyo, zitatolewa tuzo katika makundi yafuatayo:
Ligi Kuu ya NBC
Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB
Ligi Kuu ya Wanawake
Ligi ya NBC ya Championship
First League
Ligi ya U20 ya NBC
Tuzo za Utawala
Aidha, Mchezaji Bora (MVP) wa msimu wa 2024/2025 atajulikana usiku wa hafla, ambazo huchanganya wadau mbalimbali wa mpira wa miguu ikiwemo serikali na wadhamini.
Hizi tuzo zimeshapoteza mvuto. Siku zote ukitoa zawadi baada tu ya tukio kutokea, huwa na mvuto wa kipekee. Ukiitoa kwa kuchelewa, mvuto wake nao hupotea na kuonekana ni jambo tu la kawaida.