Haftar ashutumiwa kuhusu mafuriko ya Derna

Haftar ashutumiwa kuhusu mafuriko ya Derna

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Shutuma zimeanza kuelekezwa kwa general Haftar na ukoo wake kuhusianan na mafuriko yasiyo kawaida yaliyosababisha watu 11,300 kufa na wengine zaidi ya 10000 wakiendelea kutafutwa chini ya vifusi vya majengo na baharini.

Meya wa mji huo Akram Abdul Aziz ambaye kwa sasa amesimamishwa amesema wakati kimbunga cha Daniel kikikaribia alishauriana na general Haftar kwa ajili ya kuwahamisha wakazi wa mji huo ambapo Haftar alikataa.

Wakati mvua zilipoongezeka sana wale waliotaka kuondoka kwa juhudi zao walitakiwa kila mmoja abaki nyumbani mwake.

Jeneral Haftari ambaye alikuwa mjjumbe wa siri wa CIA na ambaye bado ana uraia wa Marekani juzi Ijumaa ndipo kwa mara ya mwanzo alitembelea eneo hilo lililokubwa na janga hilo la mafuriko.

Kwa upande mwengine watoto wake wawili ambao ndio wanaotarajiwa kumrithi kiti chake wamekuwa ni kikwazo katika utoaji wa misaada kwa waathirika kwani wamelazimisha misaada yote itolewe kwa maelekezo yao.

Saddam Haftar ambaye ndiye mdogo mwenye umri wa mikaka 32 ndie ameonekana kutumia janga hilo kama fursa ya kujiweka wazi machoni pa jumuiya ya kimataifa.

Mwendesha mashtaka wa Libya generali al-Sediq al-Sour amesema karibuni ataanzisha uchunguzi ili kubaini nini chanzo hasa cha janga hilo na wapi kulikuwa na uzembe.

Kinachojulikana mpaka sasa ni kwamba mvua zilizonyesha mfululizo kutoka na kimbunga cha Derna zilifikia sentimita 40 na baadae mabwawa mawili makongwe yalibomoka na kuunda maji yaliyofikia mawimbi ya mita saba yaliyoteremka kwa kasi mlimani kuelekea baharini.

Njiani maji hayo yaliangusha majengo ya ghorofa hadi saba na kusomba majengo hayo na magari na watu wlaiokuwemo mpaka baharini.

Jambo jengine linalojulikana ni jenerali Haftari kutokuwa na imani na wakazi mji huo kutokana na historia yake japokuwa kwa misaada ya kutoka nje alifanikiwa kuuzingira mji huo na baadae kuupiga bila huruma kutoka angani na ardhini ili kuwaondoa wanamgambo waliokusudia kujitenga na kujitawala kiislamu.

1694969909242.png

1694970304074.png
 
Back
Top Bottom