Kaka ningependa japo nizame kidogo nichungulie watu huko wanaishije nikajiandaa na tools na zana zote kuzama nikaingia sema nikagomewa kujiunga.
HAKUNA Fraud hapo!
Tafuta Black's Law Dictionary, au angalia kwenye encyclopedia Britannica uone maana ya neno "fraud" kisha utakuja kuniambia hapa kama kitendo cha kuwatumia watu wa ndani sio kujipatia advantage ambayo wengine hawana...kaangalie kwanza tafsiri kisha njoo tujadili mkuu.
Sehem nyingi za watu makini wanakuwa makini sana sku hizi na wageni wanaotaka kujiunga, scammers wamezidi, na wale jamaa zetu:cool2:!! Baadhi ya forums wanakuachia usome kama guest, nyingine wanaoweza kuziaccess ni members tu!
Naona wiki hii "mshahara" mapemaaa!...Mpwa wangu Elli tutafutane ijumaa palepaleee pa siku zote, siyo ndiyo uje na rundo la wanawake kama kawaida yako! hahahaa.
hebu nielekeze jinsi ya kuvua samaki na mie sio kila siku unipangie idadi ya wanawake wa kuja nao, nataka ikiwezekana nije na vibibi vyote vya JF hata na vigori, haya maujanja nataka niyajue aisee
Ok, iko hivi mkuu;
Hii mambo inahusiana na biashara ya hisa (sisi si wawekezaji, ni wajanja tu tunaotaka kununua kwa bei chini na kuuza kwa bei juu ndani ya muda mfupi)
1. Unakuwa na broker akaunti tayari kwa trading katika LSE
2. Kianzio at least 2000GBP
3. "Tipper" anakupa kampuni ya kununua hisa (yeye keshafanya research yake, he is an insider)
4. Unakaa unatulia tuliii, akisema UZA, unauza aster (unauza bei inapopanda, inaweza kuwa ndani ya dk chache au siku kadhaa, kwa hiyo unatakiwa kuwa attentive). Hapa kinachoangaliwa ni faida angalau ya 100% ili na yeye apate chambi.
5. Ukiuza unachukua faida halisi unagawa kwa mbili, fungu moja unamtumia mshkaji, fungu linalobaki unatia mfukoni, mtaji unabaki palepale unasubiri tena zamu yako ifike wakati akideal na washkaji wengine. Hapa ni suala la uaminifu, unaweza kuchagua kutomtumia cha kwake, lakini ndiyo unakuwa umejitoa na kujiondolea uaminifu.
Pia kuna hii ambayo mimi inanihakikishia vijisenti vya kula kila wiki
1. Unamtumia yeye kiasi cha pesa kuanzia 500GBP (mimi nimeanza na 800gbp)
2. Anatrade anavyojua yeye, kila wiki anakulipa 100gbp kwa kila 500 (hesabu yangu inasoma 160GBP/week)
Hapa uaminifu ni upande wake kwa sababu pesa anayo yeye.
Aisee haka kamchezo katamu ila hela za mawazo haziruhusiwi hapa. Kaka mkuu hii ni Internationally au hapa hapa DSE kaka?
Pesa ya mtaji usijaribu kuweka kaka, labda kwa option 2 ambayo ukiweka 500GBP ni guaranteed kupata 100GBP kila wiki! Hii ni LSE mkuu.