Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Makomandoo hao ambao ni Walinzi wa Freeman Mbowe kwa kinachoitwa ( VIP PROTECTION ), waliokamatwa na kuwekwa Gerezani kwa miezi mingi, leo wamefika Hai Mkoani Kilimanjaro pamoja na Mtuhumiwa mwenzao Mbowe, aliyeenda huko kutoa Sadaka ya Shukrani kwenye Kanisa la KKKT Nshala Machame.
Pamoja na kuzawadiwa ng'ombe dume wakubwa kabisa kila mmoja, pia wamepewa BAHASHA NZITO NZITO SANA kila mmoja , ambazo ndani yake haifahamiki mmewekwa nini.
Zawadi hizo zote zimetolewa na Wazee wa Machame kama sehemu ya Shukrani zao kwa Makomandoo hao kwa Uaminifu wao kwa Mbowe kutokana na kinachoitwa Kukataa kutoa Ushahidi wa Uongo ili ionekane Mbowe ni Gaidi hata baada ya kuteswa sana kuliko karibia kifo , uaminifu wa Makomandoo hawa umewapa heshima kubwa sana mbele ya Jamii.