Haiba na michezo

Haiba na michezo

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Posts
11,478
Reaction score
3,659
Naomba kutoa maoni yangu.

kwa muda mrefu hapa TZ, baadhio ya michezo (soka, riadha, ngumi) imekuwa ikiachiwa kwa wale wanaoonekana kushindwa katika fani zingine ikiwa ni pamoja na taaluma, muziki, basket ball, n.k. Kwa nchi kama TZ na Afrika kwa ujumla, haiba ya mtu ( hapa nazungumzia muonekano) imekuwa kigezo kikubwa katika kuchagua fani ya kushiriki (bahati mbaya taaluma haina haiba). nadhani hii pia inatokana na ukweli kuwa michezo hapa kwetu ni kiburudisho zaidi kuliko kazi. Tazama muonekano wa wanamichezo toka ulaya na Amerika. kwa kuwatazama tu wanavutia, tangu wa kuogelea, riadha, mpira, n.k. tangu wanawake hadi wanaume. kwa TZ yetu kijjana akiwa na muonekano mzuri, na ikatokea hana elimu ya kutosha, kwa wale wa kikewanaona ni bora kujiingiza kwenye filamu, urembo na uchangudoa au kusubiri kuolewa kuliko kushiriki michezo kama riadha, netball na uogeleaji, n.k. kwa wale wa kiumenao hujiingiza katika filamu pia, umodel, muziki (hata kama sauti ya kuimba ni ziro), au kutafuta shugamami wa kuwalea ama 'kuolewa' na wanaume wenzao! kiujumla wanauza sura!

Jamii pia nayo inachangia kuwafanya hawa vijana kuonea haya hii michezo. utakuta watu wanasema, "binti mzuri kama wewe unaenda kukimbia?" Au "handsome kama wewe unaenda kupigana?" Jamii ibadili mitazamo. hivi sasa michezo ni ajira. Nimewaona mabondia wawili-tamimu na Ashraf. sijui walikuwa wamejificha wapi. pamoja na Kaseba. Hawa wana muonekano wa kimataifa. Tunataka wanamichezo wenye muonekano wa kimataifa zaidi kuliko mtu kuingia katika michezo kwa vile kakosa kitu kingine cha kufanya. Mbona warembo tunawachagua wenye muonekano wa kimatafa? Jamii tubadilike. Sura yako, umbo lako, muonekano wako, hata rangi yako visiwe kigezo cha kuchagua au kubagua baadhi ya michezo. Tjuindokana na hii kasumba, TZ tutapiga hatua mbele kimichezo
 
Back
Top Bottom